Sunday, April 28, 2019

RC MTAKA: KAMBI ZA KITAALUMA SIMIYU ZITAKUWA ENDELEVU


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Kambi za Kitaaluma mkoani Simiyu kwa wanafunzi wa darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha Sita, ambayo ni madarasa yanayofanya Mitihani ya Taifa ya kuhitimu elimu ya Msingi na Sekondari zitakuwa endelevu.

Mtaka amesema hayo Aprili 28, 2019 wakati akihitimisha Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha sita iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, iliyohusisha wanafunzi 1166 kutoka katika shule 12 mkoani hapa.

Amesema Mkoa utaendelea kufanya jitihada na kuboresha zaidi kambi hizo huku akieleza kuwa ameshawaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo kutenga fedha kwa ajili ya motisha kwa walimu na wanafunzi watakaokuwa wakifanya vizuri.

“Kambi za kitaaluma  zitaendelea kuwepo katika kipindi chote nitakacho kuwepo na tutaendelea kuboresha; mwaka huu nimewaambia Wakurugenzi ni lazima kila Halmashauri itenge fedha kwa ajili ya motisha katika elimu, motisha kwa walimu na wanafunzi wanaofanya vizuri” alisema Mtaka.
Katika hatua nyingine Mtaka amewashukuru walimu, wanafunzi na wadau mbalimbali waliochangia kufanikisha kambi ya kidato cha sita, huku akiwasisitiza wanafunzi wa hao kuendeleza juhudi walizozionesha wakiwa kambini na kutumia mbinu walizopewa na walimu mahiri ili waweze kufanya vizuri mitihani yao ya mwisho.
Naye Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato kutoka Jijini Mwanza, Nicodemo Ntabindi amewaonya wanafunzi wa Kidato cha sita kutojihusisha na masuala ya mapenzi badala yake wajikite katika masomo tu kwa sasa ili waweze kufikia ndoto zao.

Kwa upande wao wanafunzi waliokuwepo katika kambi hiyo ya Kitaaluma wamesema kambi hiyo imekuwa msaada kwa wanafunzi kwa kuwa imechangia kuwasaidia kupata ufumbuzi wa mada ngumu zilizokuwa zinawapa shida na kuahidi kufanya vizuri katika mtihani wa Taifa kutokana na namna walivyoandaliwa vema.

“Tunashukuru uwepo wa kambi hii maana imetusaidia kupata maarifa ya namna ya kujibu maswali kwenye mitihani, lakini tumeweza kusaidiwa na walimu kutatua mada ngumu ambazo zilikuwa zinatushinda, ninaamini kwa namna tulivyoandaliwa hatutamuangusha Mkuu wetu wa Mkoa” alisema mwanafunzi Farida Omary.

“Kambi hizi hazijafanyika popote hapa nchini tunamshukuru sana Mkuu wa Mkoa kwa kuja na wazo la kuwa na kambi kwa sababu tumejifunza mengi, tumekutana na wenzetu wa shule mbalimbali hapa mkoani kwetu na tukapata maarifa ambayo awali hatukuwa nayo, tuna imani tufanya vizuri “ alisema mwanafunzi Casto Nyakarungu.

Katika kambi hii Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu, imetoa shilingi milioni 12 kwa ajili ya motisha kwa walimu waliokuwa wakifundisha kambini hapo na imeahidi kutoa shilingi milioni nne kwa mwanafunzi atakayepata ‘division one, pointi tatu’ na kuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora Kitaifa.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa.wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa Kidato Cha Sita Mkoani humo, wakati wa kufunga Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019.
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato Cha Sita Mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kufunga Kambi ya Kitaaluma ya Wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo.
Aliyekuwa mlezi(Patron) wa kambi ya kitaaluma ya kidato cha sita kwa wanafunzi wa kidato cha Sita mkoani Simiyu, Mwl.Pimbili Chalya kutoka Mwandoya, akitoa tathmini ya kambi hiyo , iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka.
Joseph Mathias Mwanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Bariadi akitoa tathmini ya kambi ya kitaaluma ya kidato cha sita mkoani Simiyu, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka.
Mwanafunzi wa kidato cha Sita Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, akitoa burudani ya wimbo, wakati wa kufunga Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka.


 Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato kutoka Mkoani Mwanza, Nicodemo Ntabindi akizungumza na wanafunzi wa Kidato Cha Sita Mkoani Simiyu, wakati wa kufunga Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka.


 Mwalimu Dennis Wasagara ambaye pia ni mzazi akizungumza na wanafunzi wa Kidato Cha Sita Mkoani Simiyu, wakati wa kufunga Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka.


Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Mwl. Kuyunga Jackson akitoa tathmini ya kambi ya kitaaluma ya kidato cha sita mkoani Simiyu, wakati wa kufunga kambi hiyo , iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka.
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato kutoka Mkoani Mwanza, Nicodemo Ntabindi (wa pili kushoto) akiongoza maombi kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha sita mkoani Simiyu wanaotarajia kuanza Mtihani wao wa taifa Mei 06, 2019 wakati wa kufunga Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka.
Wakuu wa Shule za Sekondari za Kidato cha Sita mkoani Simiyu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao  pamoja na wanafunzi wa kidato cha sita , wakati wa kufunga Kambi ya Kitaaluma ya Wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo.




Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita mkoani Simiyu wakiimba wimbo wa kuwapongeza viongozi, walimu na wanafunzi wenzao mkoani humo kwa kufanikisha Kambi ya Kitaaluma ya Wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo.

Baadhi ya wanafunzi wa Kidato Cha Sita Mkoani Simiyu wakinyosha mikonoyao juu kukubali kuwa watafanya vizuri mara baada ya kuhojiwa na  Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) ikiwa wako tayari kufanya vizuri  alipokuwa akizungumza nao wakati wa kufunga Kambi ya Kitaaluma ya Wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 .
Vijana wa Skauti wakimvisha skafu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  kabla ya Mkuu huyo wa Mkoa kuhitimisha Kambi ya Kitaaluma ya Wanafunzi wa Kidato cha Sita Aprili 28, 2019  , iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.




 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi cheti cha shukrani Katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu,  Bw. Samwel Mwanga, ikiwa ni kutambua mchango wa waandishi wa habari katika kuripoti habari za Kambi ya Kitaaluma ya Wanafunzi wa Kidato cha Sita, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019.




Mmoja wa walimu mahiri akitoa tathmini ya kambi ya kitaaluma ya kidato cha sita mkoani Simiyu wakati wa kufunga kambi hiyo , iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka.
Wanafunzi wa Kidato cha Sita mkoani Simiyu, wakiwa katika maombi maalum wakati wa kufunga kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi hao , iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka.




 Mkuu wa Mkoa.wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa Kidato Cha Sita Mkoani humo, wakati wa kufunga Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019.
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato Cha Sita Mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kufunga Kambi ya Kitaaluma ya Wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi cheti cha pongezi kwa mmoja wa walimu Mwl. Makame Makame ikiwa ni kutambua mchango wake katika kuwafundisha wanafunzi kwenye Kambi ya Kitaaluma ya Wanafunzi wa Kidato cha Sita, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019.


0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!