Friday, July 19, 2019

MAANDALIZI YA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA 2019 SIMIYU YAFIKIA ASILIMIA 75

Naibu waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba ametembelea Viwanja vya Nyakabindi kujionea maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakatofanyika kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019 katika Viwanja Vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu, ambapo ameridhishwa na maaandalizi hayo ambayo amesema kwa sasa yamefikia zaidi ya asilimia 75.

Amesema maandalizi ya mwaka huu ni tofauti na mwaka jana kutokana na mwaka jana kwa sababu mwaka jana yalikuwa ya dharura lakini mwaka huu  taasisi zimejipanga na baadhi ya zimeanza kujenga majengo ya kudumu katika Viwanja vya Maonesho.

“ Maandalizi ya mwaka huu ni tofauti na mwaka jana kwa sababu mwaka jana yalikuwa ni ya dharura lakini kwa udharura ule ule tulifanikiwa kufanya vizuri lakini mwaka huu, maandalizi yamekuwa tofauti kwa sababu majengo ya kudumu yameongezeka na niwahakikishie watu wote watakaokuja kwenye maonesho mwaka huu kupata vitu vizuri” alisema  Mgumba.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wakulima, wafugaji, wavuvi na wadua wengine kushiriki katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 huku akiwahakikishia kuwa maonesho hayo yatakuwa makubwa sana hivyo wategemee matokeo makubwa pia.

Kwa upande wake Mratibu wa Nanenane kutoka Wizara ya Kilimo, Dkt. Kissa Kajigili amesema barabara zinazozunguka uwanja zenye urefu wa kilometa sita zimeshachongwa na visima vinne vya maji vinachimbwa kuongeza idadi ya viwili vilivyopo ili kuboresha  huduma ya maji katika viwanja vya  Nyakabindi.

Ameongeza kuwa Halmashauri zote 21 za Mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga inayounda Kanda ya Nanenane ya Ziwa Mashariki na taasisi nyingine zimepanda vipando vya mazao mbalimbali kwa ajili ya kuwaelimisha wakaulima, wafugaji na wavuvi  ambavyo  vinaendelea vizuri.

Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yataanza tarehe 28 Julai, 2018 na yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan Agosti 01, 2019  na kufungwa Agosti 08, 2019 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
MWISHO
Naibu Waziri wa kilimo, Mhe. Omary Mgumba (wa pili kushoto) akikagua vipando vya mazao ya kilimo ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa maandalizi ya maoensho ya nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019..

Naibu Waziri wa kilimo, Mhe. Omary Mgumba (wa pili kushoto) akipewa maelezo kuhusu vipando vya mazao ya kilimo ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa maandalizi ya maoensho ya nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019.
Naibu Waziri wa kilimo, Mhe. Omary Mgumba (wa nne kulia) akiwa na baadhi ya  viongozi na wataalam wa Mkoa wa Simiyu na Wizara ya kilimo  katika  ukaguzi wa maandalizi ya maoensho ya nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019..
Naibu Waziri wa kilimo, Mhe. Omary Mgumba kushoto akiangalia baadhi ya mazao yliyopandwa katika Kitalu nyumba kilichopo Nyakabindi  wakati wa ziara yake ya kukagua maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akimuongoza Naibu Waziri wa kilimo, Mhe. Omary Mgumba kwenye moja ya majengo ya kudumu yanayojengwa na Jeshi la kujenga Taifa(JKT) katika Viwanja vya Nanenane Nyakabindi Bariadi, wakati wa ziara yake ya kukagua maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019.
Mmoja wa Maafisa wa JKT(wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa kilimo, Mhe. Omary Mgumba alipotembekea moja ya majengo ya kudumu yanayojengwa na Jeshi hilo  katika Viwanja vya Nanenane Nyakabindi Bariadi, wakati wa ziara yake ya kukagua maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019.

Moja ya majengo ya kudumu yanayojengwa na Jeshi la kujenga Taifa(JKT) katika Viwanja vya Nanenane Nyakabindi Bariadi, ambalo litatumika katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019.
Baadhi ya mazao yaliyo kwenye vipando ambayo yameandaliwa kwa ajili ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akimuonesha kitu Naibu Waziri wa kilimo, Mhe. Omary Mgumba(kulia)wakati wa ziara yake ya kukagua maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019.
Baadhi ya mazao yaliyo kwenye vipando ambayo yameandaliwa kwa ajili ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019.


0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!