Sunday, July 14, 2019

WAZIRI JAFO AAGIZA HOSPITALI ZA WILAYA KUKAMILIKA JULAI 30, 2019

Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo ametoa agizo kuwa ifikapo Julai 30, 2019  hospitali zote za wilaya zinazojengwa nchini ziwe zimekamilika .

Jafo ameyasema hayo   akiwa kwenye ziara ya siku moja  mkoani Simiyu ambapo alitembelea miradi mbalimbali ukiwemo wa ujenzi wa  hospitali ya wilaya ya Itilima,. ujenzi wa barabara  ,ujenzi wa kiwanda cha chaki na ujenzi wa kituo cha mabasi(stendi) cha kisasa, huku akipongeza ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Itilima kwa kizingatia viwango, mahitaji na ubora katika ujenzi.

Aidha amesema kuwa hakuna sababu za fedha kuongezwa kiasi kilichotolewa awali kwa ajili ya ujenzi wa majengo saba ya awali kinatosha kukamilisha huku akitolea mifano ya hospitali ambazo zimeshakamilika kwa kiasi hicho kilichotolewa awali.

Akiwa wilaya za Meatu na Maswa waziri Jafo amekagua  na kuridhishwa na ujenzi wa barabara zilizojengwa na mkandarasi CHICO kwa kiwango cha lami ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli aliyoitoa akiwa ziarani mkoani hapo zenye urefu wa kilometa tatu( kilometa moja na nusu kwa kila wilaya)

“Nikupongeze sana  mratibu wa TARURA Mhandisi Dkt Philimon Msomba kwa kazi hii nzuri kikubwa wananchi  muutunze mradi huu ,kwanza nimefarijika sana kukuta hadi taa za barabarani zipo hongereni sana ”alisema waziri Jafo.

Kwa upande wake Mbunge wa Maswa Mashariki ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini Mhe.Stanslaus Nyongo amemuomba Waziri Jafo kabla mkandarasi hajaondoa vifaa vyake eneo la ujenzi wa barabara ni bora ukafanyika mchakato wa kuongeza kiasi kingine cha pesa kwa ajili ya kilometa 1.5 zilizobaki.

Katika hatua nyingine akiwa Mjini Bariadi Waziri Jafo ameridhishwa na ujenzi wa kituo cha mabasi kinajengwa Mjini hapo na kumtaka mkandarasi Kampuni ya Halem and Kings Builders Co Ltd kutoka Dar es salaam kukamilisha ujenzi  ifikapo Septemba 2, 2019  ambapo kwa sasa umefikia asilimia 87 na mpaka kukamilika kwake ujenzi utagharimu   kiasi cha shilingi bilioni 7.2

Pamoja na hayo waziri Jafo alitembelea ujenzi wa kiwanda cha chaki na kiwanda cha vifungashio unaoendelea wilayani Maswa na kupata taarifa ya ujenzi huo ambao ulipaswa kukamilika Augost 7  lakini mkandarasi SUMA JKT kaomba kuongezewa muda hadi sept 22 ,2019 kwa kile alichodai awali walipata changamoto zilizopelekea kuchelewa kuanza .

“kwenye taarifa yenu ujenzi huu ulipaswa kukamilika lakini hapa mnasema muongezewe muda ,mradi una lengo maalum na mkakati kiwanda kikamilike kianze kutoa products(bidhaa), mimi niwahakikishie ntakuja  hapa tarehe 22 au 23 kujihakikishia kama kweli ujenzi huo umekamilika ” alisema waziri  Jafo


Wakiongea kwa niaba ya wananchi Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinguzi (CCM) wilaya ya Maswa Mhandisi. Paul Jidayi na Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Chilongani wameishukuru Serikali kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza ahadi ya Mhe. Rais na kubainisha kuwa watashirikiana na wananchi kuhakikisha kuwa miundombinu hiyo inatunzwa.
MWISHO
Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akizungumza na viongozi wa wilaya ya Itilima baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo, Julai 13, 2019.
Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya Itilima wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo, Julai 13, 2019.
Baadhi ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Itilima ambayo ujenzi wake umemridhisha Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo wkati alipoyakagua jana Julai 13, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Chilongani(mwenye suti ya kijivu) akimongoza Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo katika ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya kilometa moja na nusu ambao ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli aliyoitoa akiwa ziarani mkoani Simiyu, Septemba 2018.
Mratibu wa TARURA katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, mhandisi. Mathias Mugolozi (aliyenyosha mkono) akitoa maelezo kwa Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kuhusu ujenzi wa kituo cha mabasi(stendi) Mjini Bariadi wakati alipotembelea na kukagua mradi huo Julai 13, 2019.
Mratibu wa TARURA katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, mhandisi. Mathias Mugolozi (aliyenyosha mkono) akitoa maelezo kwa Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kuhusu ujenzi wa kituo cha mabasi(stendi) Mjini Bariadi wakati alipotembelea na kukagua mradi huo Julai 13, 2019.
Sehemu ya jengo la abiria lililopo katika kituo cha mabasi(stendi) Mjini Bariadi ambacho kinaendelea kujengwa na kinatarajia kukamilika Septemba 02, 2019.
 Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo( wa tatu kulia) akiwa na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Maswa katika ziara yake ya kukagua ujenzi wa  barabara ya lami kilometa 1.5 ambao ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli aliyoitoa akiwa ziarani mkoani Simiyu, Septemba 2018.
Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akitoa maelekezo kuhusu ujenzi wa kituo cha mabasi(stendi) Mjini Bariadi mara baada ya kuitembelea na kukagua mradi huo Julai 13, 2019.
Sehemu ya barabara ya lami kilometa 1.5 inayojengwa wilayani Maswa ambayo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli aliyoitoa akiwa ziarani mkoani Simiyu, Septemba 2018.
Sehemu ya barabara ya lami kilometa 1.5 inayojengwa wilayani Meatu. ambayo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli aliyoitoa akiwa ziarani mkoani Simiyu, Septemba 2018.
Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo(kulia) akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Simiyu alipomtembelea ofisini kwake wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Simiyu jana Julai 13, 2019.
Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo(kulia) akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Simiyu alipomtembelea ofisini kwake wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Simiyu jana Julai 13, 2019.
Sehemu ya eneo la Kituo cha Mabasi(stendi) cha mjini Bariadi.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!