Friday, October 25, 2019

WANANCHI ZAIDI YA 1000 WAPATIWA MSAADA WA KISHERIA MKOANI SIMIYU

Msajili wa Taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Felistas Mushi amesema  takribani wananchi 1018  wamepata huduma ya msaada wa kisheria katika maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria tangu Oktoba 21, 2019 mpaka Oktoba 25, 2019, yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Mushi ametoa taarifa hiyo katika Kilele cha Maadhimisho hayo, Oktoba 25, 2019 ambapo amebainisha kuwa asilimia kubwa ya matatizo ya kisheria yalihusu migogoro ya ardhi na yameshafikishwa mahakamani  na yako katika hatua mbalimbali.

Amesema huduma walizopata wananchi katika wiki ya msaada wa kisheria ni pamoja na huduma za usuluhishi, ushauri wa kisheria, kuandaa nyaraka na maelekezo ya sehemu  sahihi ya kwenda pindi wanapopata migogoro.

“Mbali na huduma kwa wananchi mafunzo yametolewa kwa makundi mbalimbali ya watumishi wa umma wapatao 1300 wakiwemo, wajumbe wa menejimenti ya sekretarieti ya mkoa, wajumbe wa kamati ya parole, wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya kata na vijiji, wajumbe wa kamati ya maadili ya mahakimu, askari polisi na magereza, wajumbe wa kamati za shule na watendaji wa vijiji na kata, “ alisema Mushi.

Kwa upande wake Hakimu Mary Nyangusi akimwakilisha Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio, ametoa wito kwa wananchi kuandika wosia ili kupunguza migogoro ya ardhi ambayo mingi inatokea mara nyingi wanaume(baba) wanapofariki na wake(mke) na watoto kudhulumiwa haki zao.

Adam Kisinza ni Mmoja wa wananchi waliofika kupata msaada wa kisheria katika maadhimisho hayo amesema, “nashukuru nimeelewesha ninachotakiwa kufanya maana kule kwetu baba mwenye mji anapokuwa amefariki wakabaki watoto na mama, wanakuwa hawana mamlaka juu ya mali iliyoachwa maana kila mtu anataka achukue chake wakati mzee hakuacha hata  wosia”.

Akifunga Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema ni vema wizara ya katiba na sheria ikaona umuhimu wa kupeleka maadhimisho ya wiki ya msaada wa huduma za kisheria katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo, ili wananchi wapate uelewa wa masuala ya kisheria na kupata matokeo yatakayoonekana.

Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Kitaifa mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu:- “Msaada wa Kisheria kwa Maendeleo Endelevu”ambapo kilele cha maadhimisho haya kimeenda sambamba na uzinduzi wa Jarida la Msaada wa Kisheria, ambalo limezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) na viongozi wengine wakionesha nakala ya Jarida la Msaada wa Kisheria lililozinduliwa katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akiteta jambo na Msajili wa Taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Felistas Mushi, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa Katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa mkoa mkoa huo(hawapo pichani), katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani), katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jarida la msaada wa kisheria katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Baadhi ya wataalam wa sheria na watoa huduma za kisheria  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani), katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja  na baadhi ya viongozi wa Mkoa huo na wataalam wa Sheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na taasisi za watoa huduma za kisheria, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktioba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati walioketi) akiwa katika picha na baadhi ya viongozi wa Mkoa huo, wataalam wa Sheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na wawakilishi wa taasisi za watoa huduma za kisheria, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkurugenzi wa Taasisi inayotoa huduma ya msaada wa kisheria ya Mama’s Hope Organisation for Legal Assistant (MHOLA),Bw. Saulo Malauri (kulia) akipokea nakala ya Jarida la Msaada wa Kisheria kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi Msajili wa Taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Felistas Mushi, nakala ya Jarida la Msaada wa Kisheria, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani), katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, nakala ya Jarida la Msaada wa Kisheria, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera, nakala ya Jarida la Msaada wa Kisheria, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkurugenzi wa Taasisi inayotoa huduma ya msaada wa kisheria ya Mama’s Hope Organisation for Legal Assistant (MHOLA),Bw. Saulo Malauri (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) na viongozi wengine wakionesha nakala ya Jarida la Msaada wa Kisheria lililozinduliwa katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akitoa salamu za wilaya ya Bariadi, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mwakilishi wa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio akitoa taarifa katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, mhe. Tano Mwera akitoa salamu, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Msajili wa Taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Felistas Mushi, akitoa taarifa ya namna wananchi wa Mkoa wa Simiyu walivyohudumiwa katika masuala ya kisheria wakati wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria,  katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa Katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Baadhi ya viongozi na watoa msaada wa huduma ya kisheria wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani), katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Baadhi ya viongozi na watoa msaada wa huduma ya kisheria wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani), katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mwanasheria kutoka Wizara ya Mambo ya ndani, akipokea cheti cha pongezi kwa kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria yaliyoadhimishwa Kitaifa Katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019 cheti hicho kimekabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika kilele cha maadhimisho hayo Oktoba 25, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa  tatu kushoto) na viongozi wengine wakishuhudia burudani kutoka kwa Eliza Band wakati wa  Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Wasanii wa Eliza Band ya mkoani Simiyu, wakitoa burudani katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) na viongozi wengine wakisikiliza jambo kwa makini wakati wa  Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Afisa Uhusiano wa Shule ya Sheria Tanzania(LST), Bi. Scholastica Njozi akipokea cheti cha pongezi kwa kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria yaliyoadhimishwa Kitaifa Katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019 cheti hicho kimekabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika kilele cha maadhimisho hayo Oktoba 25, 2019.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!