Monday, November 25, 2019

MWEKEZAJI KUTOKA MALAYSIA ANATARAJIA KUWEKEZA MRADI WA DOLA BILIONI 2.5 PORI LA AKIBA LA KIJERESHI SIMIYU

Mwekezaji Azhar Malik kutoka Nchini Malaysia ameonesha nia ya kuwekeza kiasi cha Dola za kimarekani bilioni 2.5 katika mradi mkubwa eneo la pori la akiba la Kijereshi na Ziwa Victoria wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, sehemu ya uwekezaji huo ikiwa ni katika ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji, utamaduni na maeneo mengine yatakayoimarisha utalii na kutoa ajira kwa wananchi.

Mwekezaji ambaye amefuatana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Mhe. Dkt. Ramadhan Dau amesema ikiwa kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa ikiwemo mradi huo unatarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia mwezi Januari 2020, huku akisisitiza kuwa utatekelezwa bila kuathiri ikolojia na mazingira ya uhifadhi.

“Nashukuru kwa ushirikiano nilioupata kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu, pia namshukuru Balozi Dau kwa namna alivyolisimamia jambo hili tangu likiwa wazo mpaka sasa tunapoelekea kwenye utekelezaji niwaahidi tu kuwa pale pande zote zitakapofanya maamuzi mikataba ikisainiwa kwa mujibu wa sheria, mwakani mwezi Januari tutaanza utekelezaji,”alisema Malik

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Mhe. Dkt. Ramadhan Dau amepongeza uongozi wa Chama na Serikali kwa utayari walioonesha, akisisitiza ushirikiano wa viongozi hao na taasisi zote za Serikali zinazohusika, ili mambo yote muhimu yanayohitajika kufanikisha uwekezaji huo yafanyike mapema  kuanzia mwezi Januari kazi ianze.

“Kwa kasi na namna tulivyoanza lile lengo tulilojiwekea kwamba ikifika Januari 2020 mambo yote yanayohusiana na taratibu na  kusaini mikataba, yanapaswa yawe yamekamilika na wataalam waje site (eneo la mradi) waanze survey (utafiti) watengeneze master plan(mpango kabambe), ili kabla ya mwezi Juni 2020 hili jambo liwe limeanza,” alisema Balozi Dau.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema Uwekezaji huu utaupambanua Mkoa wa Simiyu, Kanda ya Ziwa na kuupambanua utalii kwenye uso wa dunia, ambapo amebainisha kuwa mradi huu utajibu mahitaji mengi kwenye ajira na kukua kwa maendeleo ya ukanda huo.
Kwa upande wao Wizara ya Maliasili na Utalii na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) wameahidi kutoa ushirikiano ili kuhakikisha mradi huu unafanikiwa.
Mradi huu wa uwekezaji katika sekta ya utalii wilayani Busega utatekelezwa kwa awamu, ambapo awamu ya kwanza inatarajiwa kugharimu takribani dola bilioni 500 na mpaka kukamilika kwake utagharimu dola za Kimarekani bilioni 2.5.
MWISHO

Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik(kulia) akiwasilisha taarifa yake ya uwekezaji katika sekta ya Utalii kwenye Pori la Akiba la Kijereshi  wilayani Busega kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu na watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, wakati wa Ziara yake jana akiwa amefuatana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau aliyofanya kwa lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji
 Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau akizungumza na viongozi wa mkoa wa Simiyu baada ya kuwasili mjini Bariadi akiwa na Malik(kulia) ambaye amekubali kuwekeza katika mradi mkubwa kwenye sekta ya utalii katika Pori la Akiba la Kijereshi wilayani Busega utakaojumuisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine yenye kutoa ajira kwa wananchi wakati wa ziara yake jana mkoani Simiyu,


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kulia) akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau akiwa amefuatana na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik ambaye amekubali kuwekeza katika mradi mkubwa kwenye sekta ya utalii katika Pori la Akiba la Kijereshi  wilayani Busega utakaojumuisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine yenye kutoa ajira kwa wananchi mkoani Simiyu.

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera (kulia) akitoa neon la shukrani mara baada ya kumalizika kwa  ziara ya Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau akifuatana  na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik ambaye amekubali kuwekeza katika mradi mkubwa kwenye sekta ya utalii katika Pori la Akiba la Kijereshi  wilayani Busega utakaojumuisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine yenye kutoa ajira kwa wananchi mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifafanua jambo katika kikao kati ya viongozi wa mkoa, Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau  na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik ambaye amekubali kuwekeza katika mradi mkubwa kwenye sekta ya utalii katika Pori la Akiba la Kijereshi  wilayani Busega utakaojumuisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine yenye kutoa ajira kwa wananchi mkoani Simiyu

 Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau(wa tano kulia) akizungumza na viongozi wa mkoa wa Simiyu baada ya kuwasili mjini Bariadi akiwa na Mwekezaji kutoka Malaysia Azhar Malik(wa pili kushoto), ambaye amekubali kuwekeza katika mradi mkubwa kwenye sekta ya utalii katika Pori la Akiba la Kijereshi wilayani Busega utakaojumuisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine kwenye Utalii yenye kutoa ajira kwa wananchi wakati wa ziara yake jana mkoani Simiyu.


Mkuu wa  Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua  kikao kati ya viongozi wa mkoa, Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau  na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik ambaye amekubali kuwekeza katika mradi mkubwa kwenye sekta ya utalii katika Pori la Akiba la Kijereshi  wilayani Busega utakaojumuisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine kwenye Utalii yenye kutoa ajira kwa wananchi  wilayani Busega mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kulia) akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau (katikati) na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik(kushoto) mara baada  ya kuwapokea katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza  jana, kwa ajili ya kuanza ziara ya kuangalia mazingira ya uwekezaji katika sekta ya utalii mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kulia) akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau (katikati) na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik(kushoto) mara baada  ya kuwapokea katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza  jana, kwa ajili ya kuanza ziara ya kuangalia mazingira ya uwekezaji katika sekta ya utalii mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akiteta jambo na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik wakati wa ziara yake katika Pori la Akiba la kijereshi wilayai Busega  jana ambapo amekubai kuwekeza katika mradi mkubwa utakaohusisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine ya kuinua utalii na ajira kwa wananchi.
Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau (katikati) akifurahia jambo na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu, wataalam kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik(kushoto)mara baada ya ziara ya balozi na mwekezaji huyo katika Pori la Akiba la Kijereshi wilayani Busega  jana,  iliyofanyika kwa lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji katika sekta ya utalii.

Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau (katikati) akifurahia jambo na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu, wataalam kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik(kushoto)mara baada ya ziara ya balozi na mwekezaji huyo katika Pori la Akiba la Kijereshi wilayani Busega  jana,  iliyofanyika kwa lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji katika sekta ya utalii.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  na viongozi wengine wakifurahia jambo wakati wakiagana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau (wa tatu kulia) Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik,mara baada ya ziara ya balozi na mwekezaji huyo katika Pori la Akiba la Kijereshi wilayani Busega  jana,  iliyofanyika kwa lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji katika sekta ya utalii.
Mkurugenzi wa Utalii kutoka wizara ya maliasili na utalii akieleza mchango wa wizara hiyo katika kufanikisha mradi utakaotekelezwa na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik, katika Pori la Akiba la Kijereshi wilayani Busega  jana ambapo amekubali kuwekeza katika mradi mkubwa utakaohusisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine ya kuinua utalii na ajira kwa wananchi.
Kutoka kushoto Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini, Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakimsikiliza :- Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau, wakati wa ziara yake katika Pori la Akiba la kijereshi wilayani Busega  jana ambapo amekubali kuwekeza katika mradi mkubwa utakaohusisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine ya kuinua utalii na ajira kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  na viongozi wengine wakifurahia jambo wakati wakiagana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau (wa tatu kulia) Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik,mara baada ya ziara ya balozi na mwekezaji huyo katika Pori la Akiba la kijereshi wilayani Busega  jana,  iliyofanyika kwa lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji katika sekta ya utalii.


Baadhi ya wataalam wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa ya Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik(hayupo pichani), katika sekta ya Utalii kwenye Pori la Akiba la Kijereshi  wilayani Busega aliyoiwasilisha kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu na watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, wakati wa Ziara yake jana akiwa amefuatana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau aliyofanya kwa lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji.

Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik(kulia) akiwasilisha taarifa yake ya uwekezaji katika sekta ya Utalii kwenye Pori la Akiba la Kijereshi  wilayani Busega kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu na watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, wakati wa Ziara yake jana akiwa amefuatana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau aliyofanya kwa lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji .

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kulia) akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau akiwa amefuatana na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik ambaye amekubali kuwekeza katika mradi mkubwa kwenye sekta ya utalii katika Pori la Akiba la Kijereshi  wilayani Busega utakaojumuisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine yenye kutoa ajira kwa wananchi mkoani Simiyu.
Baadhi ya wataalam wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa ya Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik(hayupo pichani) , katika sekta ya Utalii kwenye Pori la Akiba la Kijereshi  wilayani Busega aliyoiwasilisha kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu na watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, wakati wa Ziara yake jana akiwa amefuatana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau aliyofanya kwa lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji .
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifafanua jambo (wa tatu kushoto) wakati wa ziara ya Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau akiwa amefuatana na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik ambaye amekubali kuwekeza katika mradi mkubwa kwenye sekta ya utalii katika Pori la Akiba la Kijereshi  wilayani Busega utakaojumuisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine yenye kutoa ajira kwa wananchi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  na viongozi wengine wakifurahia jambo wakati wakiagana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau (wa tatu kulia) Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik,mara baada ya ziara ya balozi na mwekezaji huyo katika Pori la Akiba la kijereshi wilayani Busega  jana,  iliyofanyika kwa lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji katika sekta ya utalii.
Kutoka kushoto Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo wakiteta jambo wakati wa ziara ya Balozi na Mwekezaji huyo , ambaye amekubali kuwekeza katika mradi mkubwa kwenye sekta ya utalii katika Pori la Akiba la Kijereshi  wilayani Busega utakaojumuisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine yenye kutoa ajira kwa wananchi mkoani Simiyu.
Kutoka kushoto Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini, Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa ya Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik(hayupo pichani) , katika sekta ya Utalii kwenye Pori la Akiba la Kijereshi  wilayani Busega aliyoiwasilisha kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu na watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, wakati wa Ziara yake jana akiwa amefuatana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau.

Baadhi ya viongozi wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa ya Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik(hayupo pichani) ,amabye amekubali kuwekeza katika sekta ya Utalii kwenye Pori la Akiba la Kijereshi  wilayani Busega aliyoiwasilisha kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu na watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, wakati wa Ziara yake jana akiwa amefuatana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau(kulia).
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kulia) akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau akiwa amefuatana na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik ambaye amekubali kuwekeza katika mradi mkubwa kwenye sekta ya utalii katika Pori la Akiba la Kijereshi  wilayani Busega utakaojumuisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine yenye kutoa ajira kwa wananchi mkoani Simiyu.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kulia) akizungumza na akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau (wa pili kulia) na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar  Malik(kushoto) mara baada  ya kuwapokea katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza  jana, kwa ajili ya kuanza ziara ya kuangalia mazingira ya uwekezaji katika sekta ya utalii mkoani Simiyu, wengine ni wataalam walioambatana na mwekezaji huyo.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!