Sunday, March 1, 2020

RC MTAKA APIGA MARUFUKU WATOA MIKOPO KUSHIKILIA KADI ZA BENKI KAMA DHAMANA

Na Stella Kalinga, Simiyu RS

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amepiga marufuku wakopeshaji wanaowakopesha walimu,  kushikilia kadi zao za kutolea fedha  benki (ATM) na vyeti vya taaluma kama dhamana ya mkopo.
Mtaka ametoa marufuku hiyo wilayani Itilima wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu kwa kufanya vizuri katika  mitihani ya kitaifa mwaka 2019.

“Walimu jiepusheni na mikopo isiyo na ulazima, benki yenu ipo itumieni; imefika wakati  walimu wanaweka kadi zao za  ATM kama dhamana wengine wanaweka mpaka vyeti vya taaluma; hii biashara hapana, kitambulisho cha benki na vyeti ni mali mwalimu,”alisema Mtaka.

Aidha, amewapongeza walimu kwa kazi nzuri wanayofanya na kuwaeleza kuwa wana nafasi kubwa ya kuufanya mkoa kufanya vizuri  zaidi katika mitihani yote ya Kitaifa  ambapo ameeleza kuwa lengo la Mkoa ni kutoka kwenye nafasi kumi bora na kushika nafasi tatu bora kwa mitihani yote ya Kitaifa kwa shule za msingi na sekondari.

Katika hatua nyingine Mtaka ameendelea kusisitiza utekelezaji wa agizo la walimu kupewa kiupaumbele kuhudumiwa katika taasisi za Umma ili wapate muda wa kwenda kuwafundisha wanafunzi wanaowaacha shuleni wakati wanapoenda kupata huduma.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wialya ya Itilima, Bi. Elizabeth Gumbo amesema hali ya ufaulu katika Halmashauri hiyo imekuwa ikipanda kila mwaka, kutoka asilimia 56.2 mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 78.52 mwaka 2019.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini ametoa wito kwa walimu na wadau wengine wa elimu kutekeleza mkakati wa elimu wa mkoa kila mmoja kwa nafasi yake ili mkoa uweze kufikia lengo la kuwa miongoni mwa mikoa mitatu bora.

Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe. Njalu Silanga amewapongeza walimu kwa kazi nzuri waliyofanya na kuahidi kuwa Wilaya hiyo itaendela kufanya vizuri kimkoa na Kitaifa huku akieleza  mpango wa Wilaya ya Itilima kuwa ni kuhakikisha kila shule ya sekondari wilayani humo inakuwa na bweni.

Nao walimu wa Wilaya ya Itilima wamesema kuwa wataendelea kufanya kazi kwa bidii huku wakiahidi kutekeleza ikakati yote inayowekwa katika ngazi ya Mkoa, wilaya mpaka ngazi ya shule ili waweze kufikia azma ya kuufikisha mkoa katika mikoa tatu bora nchini katika mitihani yote ya Kitaifa.

“Kutokana na mikakati ambayo mkoa umeweka ukiwemo wa kambi za kitaaluma na wanafunzi kupata chakula cha machana shuleni itasaidia sana kuinua ufaulu kwa shule za msingi na sekondari,” alisema mwalimu Bindi Busagala.

Shule na walimu waliofanya vizuri katika mitihani ya Kitaifa wamepewa zawadi ya vyeti na fedha taslimu.
MWISHO

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na walimu wa wilaya ya Itilima katika hafla ya kuwapongeza walimu Shule ya Msingi na Sekondari kutokana na kufanya vizuri katika Mitihani ya Taifa mwaka 2019, iliyofanyika Februari 28, 2020 katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.
 Baadhi ya walimu wa Wilaya ya Itilima wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akizungumza nao katika hafla ya kuwapongeza kutokana na ufaulu mzuri katika Mitihani ya Taifa mwaka 2019, iliyofanyika Februari 28, 2020 katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.


 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe. Njalu Silanga katika hafla ya kuwapongeza walimu wa Shule ya Msingi na Sekondari wilayani Itilima kutokana na kufanya vizuri katika Mitihani ya Taifa mwaka 2019, iliyofanyika Februari 28, 2020 katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.


 Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na wilaya ya Itilima wakicheza pamoja na walimu wa Wilaya ya Itilima, katika hafla ya kuwapongeza walimu wa  Shule ya Msingi na Sekondari  wilayani Itilima kutokana na kufanya vizuri katika Mitihani ya Taifa mwaka 2019,iliyofanyika Februari 28, 2020 katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.


 Kutoka kushoto Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya itilima, Mhe. Mahamoud Mabula, Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe. Njalu Silanga wakicheza pamoja na baadhi ya viongozi na walimu wa Wilaya ya Itilima, katika hafla ya kuwapongeza walimu  wa Shule ya Msingi na Sekondari  wilayani Itilima kutokana na kufanya vizuri katika Mitihani ya Taifa mwaka 2019, iliyofanyika Februari 28, 2020 katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bi. Elizabeth Gumbo akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya elimu ya wilaya hiyo, katika hafla ya kuwapongeza walimu  wa Shule ya Msingi na Sekondari  wilayani Itilima kutokana na kufanya vizuri katika Mitihani ya Taifa mwaka 2019, iliyofanyika Februari 28, 2020 katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.


 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na walimu wa wilaya ya Itilima katika hafla ya kuwapongeza walimu Shule ya Msingi na Sekondari kutokana na kufanya vizuri katika Mitihani ya Taifa mwaka 2019,iliyofanyika Februari 28, 2020 katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.


 Baadhi ya walimu wa Wilaya ya Itilima wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akizungumza nao katika hafla ya kuwapongeza kutokana na ufaulu mzuri katika Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba na Kidato cha Nne mwaka 2019, iliyofanyika Februari 28, 2020 katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.


 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi cheti na fedha taslimu Mmoja wa Walimu wa Wakuu, katika hafla ya kuwapongeza walimu Shule ya Msingi na Sekondari kutokana na kufanya vizuri katika Mitihani ya Taifa mwaka 2019, iliyofanyika Februari 28, 2020 katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.


 Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga akizungumza na walimu wa wilaya ya Itilima katika hafla ya kuwapongeza walimu Shule ya Msingi na Sekondari kutokana na kufanya vizuri katika Mitihani ya Taifa mwaka 2019, iliyofanyika Februari 28, 2020 katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.


Vijana wa Skauti wa Wilaya ya Itilima wakimvika skafu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika hafla ya kuwapongeza walimu Shule ya Msingi na Sekondari kutokana na kufanya vizuri katika Mitihani ya Taifa mwaka 2019, iliyofanyika Februari 28, 2020 katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!