Thursday, October 22, 2020

KIDATO CHA NNE SIMIYU KUANZA KAMBI ZA KITAALUMA OKTOBA 30

 Wanafunzi wa Kidato cha nne mkoani Simiyu wanatarajia kuanza kambi za kitaaluma tarehe 30 Oktoba 2020, kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa Taifa unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 23 Novemba 2020 hadi tarehe  11 Desemba, 2020. 

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati akizungumza na Maafisa Elimu, wakuu wa shule na baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne baada ya kufunga kikao maalum cha kutangaza na kutathmini  matokeo ya Mtihani wa Utimilifu (Mock)  kilichofanyika jana Mjini Bariadi. 

Mtaka amesema wanafunzi wote wa kidato cha nne waliopata daraja la I (division one) daraja la IV (division four), daraja la sifuri (division zero) katika Mtihani wa Mock mwaka 2020 na wale wanaotoka katika shule zenye watahiniwa  pungufu ya 30 Serikali imeandaa utaratibu kwa ajili yao, hivyo tarehe 30 Oktoba wanapaswa kufika katika vituo vilivyoandaliwa ambavyo ni Shule ya Sekondari Simiyu na Shule ya Msingi Ndekeja. 

“Mwaka huu kumekuwa na majanga  mengi ya moto, majanga ya moto dawa yake si kufunga kambi za shule na ndiyo maana shule za bweni hazijafungwa, tumekuwa na utaratibu wa kambi za kitaaluma kwa watoto wote wa kidato cha nne wa Mkoa wa Simiyu wa shule za Serikali; maelekezo yangu, kambi za kitaaluma kwenye maandalizi ya kidato cha nne zianze na ziendelee mpaka tutakapoanza mtihani wa Taifa,” alisema Mtaka. 

Mtaka amezitaka Kamati za Ulinzi na Usalama za wilaya zote mkoani Simiyu kuendelea kuchukua tahadhari na kinga zote za majanga ya moto, huku akibainisha kuwa elimu ya tahadhari ya majanga ya moto imeshatolewa katika shule zote na vifaa vya kuzimia moto vimefungwa  katika baadhi ya shule ikiwemo shule ya Sekondari Simiyu ambacho ni kituo cha kambi hizo.

 

Akizungumzia suala la motisha kwa walimu na wanafunzi watakaofanya vizuri katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne amesema mwalimu atapewa shilingi 30,000/= kwa kila alama A itakayopatikana kwenye somo lake na shilingi 10,000/= kwa alama B.

Ameongeza kuwa mwanafunzi atakayepata daraja la kwanza pointi saba atapewa shilingi 1,000,000/= na ikiwa atakuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora Kitaifa ataongezewa shilingi 1,000,000/=na kumfanya apate shilingi 2,000,000/=, ambapo amesisitiza kuwa mwanafunzi wa kike atakayefanya vizuri kuliko wenzake wote atapewa shilingi 500,000/= na ikitokea msichana aliyeongoza amepata daraja la kwanza pointi saba atapewa shilingi 1,500,000/=

Shule ya Serikali ya Sekondari ya Mkoa wa Simiyu itakayoingia katika shule 10 bora Kitaifa itapewa zawadi ya shilingi 5,000,000/= huku akiahidi kuwapeleka walimu wote ambao Halmashauri yao itafanya vizuri na kuingia katika nafasi kumi bora Kitaifa kwenda kufanya utalii wa ndani katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu Mw. Ernest Hinju amesema katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka 2019 Simiyu ilishika nafasi ya tano Kitaifa na matarajio ya mwaka huu ni kushika nafasi ya kwanza Kitaifa, huku akibainisha kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na wazazi wamehamasika kuwachangia wanafunzi chakula.

Kwa upande wao walimu na wanafunzi wameshukuru Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kuruhusu kambi za kitaaluma kwa kuwa kambi hizo zimekuwa msaada sana kwa wanafunzi hususani wale ambao wanatoka katika mazingira magumu ambayo hawawezi kujisomea kwa uhuru.

“Awali tuliposikia kambi zimeahirishwa tulisononeka sana maana kambi zimekuwa msaada hasa kwa watoto wanaotoka katika mazingira magumu, hata walimu tunabadilishana utaalamu na mbinu za ufundishaji; tunamshukuru Mhe.RC kuruhusu kambi maana miaka ya nyuma Simiyu ilikuwa nyuma sana kwa ufaulu; lakini sasa hivi tumetoka huko tumepanda mfano matokeo ya kidato cha sita mwaka huu tumeshika nafasi ya tatu na kidato cha nne mwaka 2019 tulishika nafasi ya tano Kitaifa,” Mwl. Khamis Lubugwa.

“Kambi za kitaaluma zimekuwa na msaada sana hususani kwa watoto wa kike, tunapokuwa kambi tunapata muda mwingi wa kujisomea kuliko tunapokuwa nyumbani lakini vile vile tunapokuwa kambi inatusaidia kuepukana na vishawishi mbalimbali maana miongoni mwetu wako wanaotoka mbali, tumejisikia vizuri kufunguliwa kwa kambi na tunatarajia kufanya vizuri sana,” Nshoma Joseph mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Bariadi.

MWISHO

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya Maafisa Elimu, wakuu wa shule na na baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Bariadi baada ya kufunga kikao cha kutangaza na kutathmini  matokeo ya Mtihani wa Utimilifu (Mock)  kilichofanyika jana Mjini Bariadi.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Bariadi wakishangilia mara baada  ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akitangaza kuanza kwa kambi za kitaaluma kwa wanafunzi hao Oktoba 30, 2020 baada ya kufunga kikao cha kutangaza na kutathmini  matokeo ya Mtihani wa Utimilifu (Mock)  kilichofanyika jana Mjini Bariadi.

Baadhi ya wanafunzi, walimu, Maafisa Elimu, wakuu wa shule wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani)  baada ya kufunga kikao cha kutangaza na kutathmini  matokeo ya Mtihani wa Utimilifu (Mock)  kilichofanyika jana Mjini Bariadi.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akitangaza kufunguliwa kwa kambi za kitaaluma kwa wanafunzi hao Oktoba 30, 2020 baada ya kufunga kikao cha kutangaza na kutathmini  matokeo ya Mtihani wa Utimilifu (Mock)  kilichofanyika jana Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi na walimu na Maafisa Elimu, wakuu wa shule na baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne baada ya kufunga kikao cha kutangaza na kutathmini  matokeo ya Mtihani wa Utimilifu (Mock)  kilichofanyika jana Mjini Bariadi.
Baadhi ya Makamu Wakurugenzi, Maafisa Elimu, wakuu wa shule wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani)  akitangaza kuanza kwa kambi za kitaaluma za kidato cha nne mwishoni mwa mwezi huu baada ya kufunga kikao cha kutangaza na kutathmini  matokeo ya Mtihani wa Utimilifu (Mock)  kilichofanyika jana Mjini Bariadi.

Wednesday, October 21, 2020

SERIKALI YATOA BILIONI 1.2 KULIPA WAKULIMA WA PAMBA SIMIYU

Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya kukamilisha malipo ya madeni ya wakulima wa pamba kwa msimu wa mwaka 2019 mkoani Simiyu, ambapo kufikia tarehe 21 Oktoba 2020 wakulima wote waliokuwa wanadai fedha watakuwa wameshalipwa fedha zao. 

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka jana tarehe 19 Oktoba 2020 katika kikao cha wadau wa pamba kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa mpango mkakati wa mageuzi ya kilimo cha zao la pamba kwa mwaka 2019/2020 na mpango wa uzalishaji kwa mwaka 2020/2021. 

" Tulishafanya uhakiki wa wakulima wetu wote, kufikia Jumatano wakulima wote waliokuwa wanadai malipo ya pamba kwa mwaka 2019 watakuwa wamelipwa fedha zao; vyama vya ushirika hakikisheni kila mkulima anapata fedha yake, ole wenu wakulima walalamike kuwa hawajapaya fedha zao au fedha zao zimekatwa mtakuwa hamjipendi," alisema Mtaka. 

Aidha, Mtaka amewakata Maafisa Ushirika wa Halmashauri waandae taarifa ya malipo ya pamba kwa wakulima kwa malipo ya awamu ya kwanza yaliyofanyika Septemba na malipo yanayofanyika sasa ili kupata takwimu za wakulima waliolipwa, kilo zilizolipwa na fedha zilizolipwa kwa kila mkulima ifikapo Oktoba 22, 2020. 

Naye Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe amesisitiza umuhimu wa Vyama vya msingi vya Ushirika (AMCOS) vipatavyo 70 vya mfano kuingia mkataba na makampuni ya ununuzi wa pamba ili Bodi ya pamba itakapotoa leseni za ununuzi wa pamba isitoe leseni kwa wanunuzi wengine kununua katika AMCOS hizo. 

“Ninataka hizi AMCOS 70 kwa kupitia Bodi ya pamba, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mrajisi wa Vyama vya Ushirika mtambue kampuni ambayo itaingia mikataba na hizi AMCOS moja kwa moja ili Bodi ya pamba itakapotoa leseni isitoe leseni kwa mnunuzi mwingine kwenda kwenye hizo AMCOS,” alisema Bashe.

Katika hatua nyingine Bashe amesema ni vema wakulima wenye mashamba ya pamba yaliyosajiliwa wapewe hati za kimila wapewe hati za kimila ili waweze kukopesheka, huku akitoa wito kwa taasisi za fedha kutoka kwenye mifumo za kizamani ya biashara (utoaji mikopo) ili mifumo ya mikopo iwe na uhusiano wa moja kwa moja na sekta ya kilimo. 

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba, Bw. Marco Mtunga amesema ipo haja kwa wadau wa pamba kuona namna ya kuwasaidia wakulima kuongeza tija katika uzalishaji wa pamba kwa kuwa kumekuwa na dhana kwamba bei ya pamba ndiyo tatizo, ambapo amebainisha kuwa changamoto kubwa katika uzalishaji wa pamba ni tija ndogo. 

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Gatsby Tanzania ambalo limeshiriki kuandaa mkakati wa mageuzi ya uzalishaji wa zao la pamba mkoani Simiyu, Bw. Samwel Kilua amesema kama wadau muhimu wamejipanga kufanikisha mkoa wa Simiyu kuwa mfano wa maeneo mengine yanayozalisha pamba.

Akiwasilisha taarifa ya tathmini ya utekelezaji wa mpango mkakati wa mageuzi ya kilimo cha zao la pamba kwa mwaka 2019/2020 na mpango wa uzalishaji kwa mwaka 2020/2021, Afisa Kilimo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Kija Kayenze amesema katika msimu wa ununuzi wa pamba wa mwaka 2020/2021 unaoendelea hadi kufikia tarehe 04 Oktoba 2020 kilo 111,610,227 zimeshanunuliwa. 

Aidha, Kayenze amesema Mkoa wa Simiyu unaongoza kwa kilo 62,822,941 za pamba mbegu ambazo kati yake kilo 4,479,117 ni pamba kilimo hai.

MWISHO  

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na viongozi na wadau mbalimbali wa zao la pamba katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa mageuzi ya uzalishaji wa zao la pamba mwaka 2020/2021 Mkoani Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na wadau mbalimbali wa zao la pamba wakifuatilia kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa mageuzi ya uzalishaji wa zao la pamba mwaka 2020/2021 Mkoani Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe akizungumza na viongozi na wadau mbalimbali wa zao la pamba katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa mageuzi ya uzalishaji wa zao la pamba mwaka 2020/2021 Mkoani Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akielezea jambo katika kikao cha viongozi na na wadau mbalimbali wa zao la pamba katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa mageuzi ya uzalishaji wa zao la pamba mwaka 2020/2021 Mkoani Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) wakifuatilia kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa mageuzi ya uzalishaji wa zao la pamba mwaka 2020/2021 Mkoani Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi kikiwahusisha viongozi na wadau mbalimbali wa zao la pamba .

Baadhi ya viongozi na wadau mbalimbali wa zao la pamba wakifuatilia kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa mageuzi ya uzalishaji wa zao la pamba mwaka 2020/2021 Mkoani  Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mkuu wa Gatsby Africa Bw. Samwel Kilua akiwasilisha mada katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Mkakati wa Mageuzi ya uzalishaji wa zao la Pamba mwaka 2020/2021 Mkoani Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadiambapo Gatsby ilishirikiana na Ofisi ya mkuu wa Mkoa kuandaa mkakati huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania, Bw. Marco Mtunga akitoa ufafanuzi wa jambo katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Mkakati wa Mageuzi ya uzalishaji wa zao la Pamba mwaka 2020/2021 Mkoani  Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi.
Afisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Kija Kayenze akiwasilisha taarifa ya tathmini ya utekelezaji wa Mkakati wa Mageuzi ya uzalishaji wa zao la Pamba mwaka 2020/2021 Mkoani Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akichangia hoja katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Mkakati wa Mageuzi ya uzalishaji wa zao la Pamba mwaka 2020/2021 Mkoani  Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia hoja katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Mkakati wa Mageuzi ya uzalishaji wa zao la Pamba mwaka 2020/2021 Mkoani  Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Aswege Kaminyoge  akichangia hoja katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Mkakati wa Mageuzi ya uzalishaji wa zao la Pamba mwaka 2020/2021 Mkoani  Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera akichangia hoja katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Mkakati wa Mageuzi ya uzalishaji wa zao la Pamba mwaka 2020/2021 Mkoani  Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi

Baadhi ya viongozi na wadau mbalimbali wa zao la pamba wakifuatilia kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa mageuzi ya uzalishaji wa zao la pamba mwaka 2020/2021 Mkoani Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi.


Baadhi ya viongozi na wadau mbalimbali wa zao la pamba wakifuatilia kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa mageuzi ya uzalishaji wa zao la pamba mwaka 2020/2021 Mkoani Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi.




Saturday, October 10, 2020

WAZAZI, WALEZI WAPUNGUZIENI KAZI WANAFUNZI WA MADARASA YA MITIHANI: RC MTAKA

    Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwapunguzia kazi  wanafunzi wenye madarasa ya mitihani ya Taifa ya darasa la nne, kidato cha pili na kidato cha nne ambayo inatarajiwa kufanyika mwezi Novemba ili waweze kujipatia muda mwingi wa kujisomea kujiandaa na mitihani hiyo. 

Mtaka ameyasema hayo jana  wakati makabidhiano ya Chuo cha Ufundi Kasoli katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi kilichojengwa na mwekezaji Alliance Ginnery Limited na kukabidhiwa kwa Serikali na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Maduhu Kazi kwa niaba ya kampuni hiyo na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa niaba ya wananchi. 

“Darasa la saba wameshafanya mtihani wao, watoto wa darasa la nne, kidato cha pili na kidato cha nne waendelee kufanya maandalizi, wazazi na walezi wapunguzieni kazi watoto wote walio kwenye madarasa haya na wakiwa nyumbani wafanye majadiliano ya pamoja,” alisema Mtaka. 

Aidha, Mtaka amewaonya wazazi na walezi wenye nia ya kuwaozesha wanafunzi wa kike waliohitimu elimu ya msingi na kutoa wito kwa jamii yote kuwa walinzi wa watoto wa kike ili waweze kutimiza ndoto zao. 

Mtaka ameishukuru Kampuni ya Allience Ginnery kujenga chuo cha ufundi Kasoli na kutoa wito kwa wasichana na wanawake kijiji cha Kasoli kujitokeza kupata mafunzo ya ushonaji bila malipo katika chuo hicho katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba, kabla ya kuanza kwa mafunzo yatakayoanza mwakani kwa mtaala wa Serikali na kuahidi kutoa vyerehani 25. 

Meneja Mkuu wa Alliance Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola amesema Kampuni hiyo imekuwa inajihusisha sana na maendeleo ya jamii katika sekta ya elimu, afya na maji kwa kuwa wao ni sehemu ya jamii, ni wajibu wao  kufanya hivyo na ni sehemu ya maelekezo ya TIC wanayopewa wawekezaji wote.

“Tunashiriki kwenye masuala ya jamii kwa sababu sisi ni sehemu ya jamii, sisi tunashughulika na wakulima na wanaotulimia pamba na kutuuzia kutuwezesha kuendesha kiwanda chetu, siku za nyuma tulijikita kwenye afya, maji na elimu ya msingi na sekondari; tumeona haja ya kujenga chuo cha ufundi ili wanafunzi watakaoshindwa kuendelea na masomo, wapate mafunzo  ya ufundi ili waweze kujitegemea,” alisema Ogola.

Aidha, Ogola amesema pamoja na mafunzo ya ufundi mipango ya baadaye ya kampuni ya Alliance Ginnery kuongeza darasa moja la wakulima kwa lengo la kutoa warsha na mafunzo kwa wakulima ili waweze kulima kilimo chenye tija ili kampuni hiyo iweze kupata malighafi bora kwa ajili ya kiwanda chake cha kuchambua pamba..

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Maduhu Kazi ameipongeza na kuishukuru Kampuni ya Alliance Ginnery kujenga chuo cha Ufundi na kutoa wito kwa wawekezaji wengine kuona umuhimu wa kuwafikia wananchi walio katika maeneo yao huku akiahidi kuwa TIC itahakikisha kinakuwa mstari wa mbele kutatua changamoto zinazowakabili wawekezaji. 

“TIC inashirikiana na Serikali hata ngazi ya mikoa na tumejielekeza zaidi kuongeza ufanisi katika shughuli zetu za kuwasaidia wawekezaji masuala ya vibali kwa kushirikiana na Taasisi zinazohusika; pia tumejipanga hata kuwafikia wawekezaji wadogo Watanzania maana baada ya tathmini tumeona eneo hilo kuna mapungufu maana wengi wanadhani sisi tunahusika na wawekezaji wa kigeni tu,” alisema Dkt. Kazi.

Naye Mkazi wa Kijiji cha Kasoli Shamsa Abdallah amesema anaishukuru Kampuni ya Alliance Ginnery kwa kuwajengea chuo cha ufundi na anaamini kuwa kitawasadia kwenye mafunzo ya ushonaji  na mafunzo yanayohusiana na kilimo yatakayowasaidia kujikwamua kiuchumi.

Kampuni ya Alliance Ginnery Limited imejenga majengo ya chuo cha ufundi kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 180, kuchimba kisima cha maji chenye uwezo wa kutoa lita 5000 kwa saa pamoja na kuweka vifaa kama vyerehani, majiko ya gesi  na vifaa mbalimbali vya kujifunzia upishi,vifaa vya kujifunzia uashi na useremala meza na viti vya ofisi.

MWISHO

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi (wa tatu kulia) akikata utepe kufungua chuo cha  ufundi Kasoli  iliyojengwa  kwa msaada na Mwekezaji wa Kampuni ya Alliance Ginnery na baadaye kukabidhiwa kwa Serikali jana  katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

Sehemu ya majengo ya chuo cha  ufundi Kasoli  iliyojengwa  kwa msaada na Mwekezaji wa Kampuni ya Alliance Ginnery na baadaye kukabidhiwa kwa Serikali iliyopo  katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

Meneja Mkuu wa Alliance Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola akitoa maelezo  kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi  (mwenye skafu) juu ya shule ya ufundi Kasoli iliyojengwa na kampuni hiyo kwa msaada na kuikabidhi kwa serikali, baada ya kukifungua chuo hicho jana katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi akiyaangalia maji yanayotoka katika kisima kilichochimbwa kwenye shule ya ufundi ya Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni Alliance Ginnery na kuikabidhi kwa serikali, baada ya kuifungua chuo hicho jana katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi, Meneja Mkuu wa Alliance Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakifurahia na wananchi katika kijiji cha Kasoli baada ya ufunguzi wa  chuo cha ufundi Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni Alliance Ginnery na kuikabidhi kwa serikali jana kijijini hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto ) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi mara baada ya makabidhiano ya chuo cha ufundi Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni ya Alliance Ginnery na kuikabidhi kwa serikali, katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Meneja Mkuu wa Alliance Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola akiwaongoza Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi  (mwenye skafu) na viongozi wengine kukagua chuo cha ufundi ya Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni Alliance Ginnery na kuikabidhi kwa serikali, baada ya kuifungua shule hiyo jana katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

Meneja Mkuu wa Alliance Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola akitoa maelezo  kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi  (mwenye skafu) juu ya vifaa mbalimbali vilivyopo katika  chuo cha ufundi Kasoli iliyojengwa na kampuni hiyo kwa msaada na kuikabidhi kwa serikali, baada ya kuifungua chuo hicho jana katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Kutoka kulia Meneja Mkuu wa Alliance Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga wakuteta jambo baada ya makabidhiano ya chuo cha ufundi Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni ya Alliance Ginnery na kuikabidhi kwa serikali, katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Kutoka kulia Meneja Mkuu wa Alliance Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga wakiwa katika picha ya pamoja jana baada ya makabidhiano ya chuo cha ufundi Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni ya Alliance Ginnery na kuikabidhi kwa serikali, katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Wasanii wa kundi la FUTUHI kutoka jijini Mwanza wakitoa burudani katika hafla ya makabidhiano ya shule ya ufundi ya Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni ya Alliance Ginnery na kukikabidhi kwa serikali, katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

Meneja Mkuu wa Alliance Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola akiwaongoza Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi  (mwenye skafu) na viongozi wengine kukagua chuo cha ufundi ya Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni Alliance Ginnery na kukikabidhi kwa serikali, baada ya kukifungua chuo hicho jana katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.


Meneja Mkuu wa Alliance Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola akitoa maelezo  kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi  (mwenye skafu) juu ya chuo cha  ufundi Kasoli iliyojengwa na kampuni hiyo kwa msaada na kuikabidhi kwa serikali, baada ya kuifungua chuo hicho  jana katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto ) akiagana na na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi mara baada ya makabidhiano ya chuo cha ufundi Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni ya Alliance Ginnery na kuikabidhi kwa serikali, katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

Meneja Mkuu wa Alliance Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola akitoa maelezo  kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi  (mwenye skafu) na viongozi wengine  juu ya maeneo mbalimbali ya  shule ya ufundi Kasoli iliyojengwa na kampuni hiyo kwa msaada na kukikabidhi kwa serikali, baada ya kukifungua chuo hicho jana katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi (mwenye skafu) akifurahia burudani ya nyimbo kutoka kwa msaani Elizabeth Maliganya (mwenye kipaza sauti) wakati wa ufunguzi wa chuo cha ufundi Kasoli 


Sehemu ya majengo ya chuo cha ufundi Kasoli  iliyojengwa  kwa msaada na Mwekezaji wa Kampuni ya Alliance Ginnery na baadaye kukabidhiwa kwa Serikali iliyopo  katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.



Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kasoli wakifuatilia hafla ya makabidhiano ya shule ya ufundi Kasoli iliyojengwa na mwekezaji kampuni ya Alliance Ginnery  kwa msaada na kuikabidhi kwa serikali, baada ya kukifungua chuo hicho jana katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Simiyu wakishangilia baada ya  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi (wa tatu kulia) kufungua chuo cha ufundi Kasoli  iliyojengwa  kwa msaada na Mwekezaji wa Kampuni ya Alliance Ginnery na baadaye kukabidhiwa kwa Serikali jana  katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi (wa tatu kulia) akipanda mti wa kumbukumbu mara baada ya  kufungua shule ya ufundi Kasoli  iliyojengwa  kwa msaada na Mwekezaji wa Kampuni ya Alliance Ginnery na baadaye kukabidhiwa kwa Serikali jana  katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto ) katika picha ya pamoja  na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi mara baada ya makabidhiano ya chuo cha ufundi Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni ya Alliance Ginnery na kukikabidhi kwa serikali, katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi, Meneja Mkuu wa Alliance Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakifurahia na wananchi katika kijiji cha Kasoli baada ya ufunguzi wa  chuo cha ufundi Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni Alliance Ginnery na kukikabidhi kwa serikali jana kijijini hapo.
Meneja Mkuu wa Alliance Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola(kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika hafla ya makabidhiano ya Chuo cha ufundi Kasoli iliyojengwa kwa msaada na mwekezaji kampuni ya Alliance Ginnery  na kukikabidhi kwa serikali, baada ya kukifungua shule hiyo jana katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiyaangalia maji yanayotoka katika kisima kilichochimbwa kwenye shule ya ufundi ya Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni Alliance Ginnery na kuikabidhi kwa serikali, baada ya kuifungua chuo hicho jana katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu

Monday, October 5, 2020

DARASA LA SABA SIMIYU WAAHIDI KUONGOZA MTIHANI WA TAIFA MWAKA 2020

Zikiwa zimebaki siku mbili kufanya mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba, wanafunzi wa darasa la saba mkoani Simiyu wamesema wamedhamiria kushika nafasi ya kwanza Kitaifa  katika mtihani huo kutokana na mikakati ya taaluma iliyopo na maandalizi yaliyofanyika, huku wakiahidi kutoa wanafunzi kumi bora Kitaifa. 

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wanafunzi wa Shule za msingi Somanda A, Somanda B, Sima A na Sima B za mjini Bariadi wakati wa ziara ya Viongozi wa Mkoa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika shule hizo iliyokuwa na lengo la kujiridhisha na maandalizi na kuwatakia heri wanafunzi watakaofanya mtihani huo.

“Tumejiandaa vizuri na mtihani wa Taifa utakaofanyika tarehe 07 na 08 mwezi huu, walimu wetu wametuandaa vizuri tunawashukuru sana walimu kwa kutufundisha vizuri, tulifanya vizuri mtihani wa Mkock na tumejipanga kufanya vizuri zaidi mtihani wa Taifa, tunaahidi kutoa wanafunzi watano katika  kumi bora Kitaifa,”Kija Masunga mwanafunzi wa darasa la Saba Somanda B.

“Nawashukuru walimu kwa kutufundisha kutoka chekechea mpaka darasa la saba pia tunashukuru uwepo wa kambi za kitaaluma zimetusaidia sana, baadhi ya wanafunzi katika shule za serikali wanadanganywa na wazazi wao wakaandike majibu yasiyo sahihi ili wakaozeshwe lakini kupitia kambi wanafunzi tunalindwa na tunajiamini,”Edina Meshaki kutoka Sima A.

Aidha, wanafunzi hao wameomba Serikali iendelee kuboresha miundombinu ya kujifunzia ikiwa ni pamoja na uwekaji wa nishati ya umeme katika vyumba vyote vya madarasa ili waweze kujisomea nyakati zote hususani wakati wa kambi za kitaaluma.

Mwalimu Monica Silayo kutoka Shule ya Msingi Somanda B amesema wamewaandaa wanafunzi vizuri ambapo amebainisha kuwa hata wakiletewa mtihani sasa hivi wako tayari kufanya mtihani huo wa Taifa.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sima A, Hamza Hamis amesema “sisi si watu wa maneno ni watu wa vitendo hatuzungumzi mambo mengi lakini tunaahidi kuwa tumejipanga,  hili suala la kuwa namba moja tumeliwekea mikakati toka mwaka jana tunafanya mwendelezo wa mikakati yetu mwaka huu Simiyu hatukamatiki”.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewashukuru walimu wote wa mkoa wa  Simiyu kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwataka viongozi na watumishi wengine kutoa kipaumbele kwa walimu katika maeneo ya huduma ili wapata nafasi ya kuwafundisha wanafunzi wao .

Kuhusu zawadi kwa wanafunzi na walimu watakaofanya vizuri katika mtihani waTaifa wa Darasa la Saba mwaka 2020 Mtaka amesema, “wanafunzi watakaoingia 10 Bora kitaifa kila mmoja atapewa shilingi 500,000/= mwalimu atakayeongoza kwa ufaulu wa A nyingi kimkoa kwa kila somo , atapewa shilingi 500,000/=, shule itakayoingia 10 bora Kitaifa itapewas hilingi milioni tatu, wilaya itakayoingia 10 bora walimu wake wataenda kufanya utalii wa ndani katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.”

Katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Darasa la saba mwaka 2019 wanafunzi mkoa wa Simiyu ulitoa wanafunzi wanne walioingia katika 10 bora Kitaifa kwa shule za Serikali na kila mwanafunzi aliepwa zawadi ya shilingi 300,000/=

Kwa mujibu wa Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju jumla ya wanafunzi 30,779 wanatarajia kufanya mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba, huku akibainisha kuwa maandalizi yako vizuri ambayo yamechangiwa na walimu, wazazi, viongozi na wadau wote wa elimu katika kufikia azma ya mkoa ya kushika nambari moja Kitaifa.

MWISHO

 

Wanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Somanda A na Somanda B Mjini Bariadi wakipokea mkono wa heri kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati alipowatembelea shuleni hapo kwa ajili ya kujiridhisha na maandalizi na kuwatakia heri wakati wakielekea katika  Mtihani wa Taifa wanaotarajia kuufanya Oktoba 7-8, 2020.


Mmoja wa Wanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Sima A Mjini  akiwaongoza wanafunzi wenzake kwa dua maalum kwa ajili ya kuombe Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba unaotarajiwa kufanyika tarehe 7-8 Oktoba, 2020; (kulia)  waliosimama juu ya meza ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka akiungana nao katika dua wakati alipowatembelea shuleni hapo Oktoba 05, 2020 kujionea maandalizi na kuwatakia heri katika mtihani huo.


Mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Sima B Mjini Bariadi, akizungumza namna walivyojiandaa na mtihani wa Taifa unatarajiwa kufanyika Oktoba 07-08, 2020 wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka iliyolenga kujionea maandalizi yaliyofanyika na kutakia kila la heri katika mtihani huo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Shule ya Msingi Sima A Mjini Bariadi Mwl. Hamza Hamis akieleza hali ya maandalizi ya mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba  katika shule yak,  wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka Oktoba 05, 2020  iliyolenga kujionea maandalizi yaliyofanyika na kuwatakia kila la heri wanafunzi wa darasa la saba katika mtihani huo.
Wanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi  Sima A na Sima B Mjini Bariadi wakipokea mkono wa heri kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati alipowatembelea shuleni hapo kwa ajili ya kujiridhisha na maandalizi na kuwatakia heri wakati wakielekea katika  Mtihani wa Taifa wanaotarajia kuufanya Oktoba 7-8, 2020.
Mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Sima B Mjini Bariadi, akizungumza namna walivyojiandaa na mtihani wa Taifa unatarajiwa kufanyika Oktoba 07-08, 2020 wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka iliyolenga kujionea maandalizi yaliyofanyika na kutakia kila la heri katika mtihani huo.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Sima A na Sima B wakati alipotembelea shule hiyo akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi kwa lengo la kijiridhisha na hali ya maandalizi ya mtihani wa Taifa na kuwatakia kila la heri katika mtihani huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 07-08, 2020.Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Somanda A na Somanda B wakati alipotembelea shule hiyo akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi kwa lengo la kijiridhisha na hali ya maandalizi ya mtihani wa Taifa na kuwatakia kila la heri katika mtihani huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 07-08, 2020.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Somanda A na Somanda B wakati alipotembelea shule hiyo akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi kwa lengo la kijiridhisha na hali ya maandalizi ya mtihani wa Taifa na kuwatakia kila la heri katika mtihani huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 07-08, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifurahia jambo na wanafunzi  wa Darasa la Saba katika  Shule ya Msingi Sima A na Sima B na Mwalimu Mkuu wa Sima A baada ya kukamilisha ziara yake katika shule hizo ikiwa na lengo la kujiridhisha na maandalizi ya Mtihani wa Darasa la Saba na kuwatakia heri wanafunzi wa Darasa la Saba wanaotarajia kuafanya  mtihani huo Oktoba 07-08, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifurahia jambo na  Samson Robert mwanafunzi  wa Darasa la Saba katika  Shule ya Msingi Sima B, baada ya kukamilisha ziara yake katika shule hiyo ikiwa na lengo la kujiridhisha na maandalizi ya Mtihani wa Darasa la Saba na kuwatakia heri wanafunzi wa Darasa la Saba wanaotarajia kuafanya  mtihani huo Oktoba 07-08, 2020.
Mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Somanda  B Mjini Bariadi, akizungumza namna walivyojiandaa na mtihani wa Taifa unatarajiwa kufanyika Oktoba 07-08, 2020 wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka iliyolenga kujionea maandalizi yaliyofanyika na kutakia kila la heri katika mtihani huo.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Somanda A na Somanda B wakati alipotembelea shule hiyo akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi kwa lengo la kijiridhisha na hali ya maandalizi ya mtihani wa Taifa na kuwatakia kila la heri katika mtihani huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 07-08, 2020.
Wanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Somanda A na Somanda B Mjini Bariadi wakipokea mkono wa heri kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati alipowatembelea shuleni hapo kwa ajili ya kujiridhisha na maandalizi na kuwatakia heri wakati wakielekea katika  Mtihani wa Taifa wanaotarajia kuufanya Oktoba 7-8, 2020.

Mmoja wa Wanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Sima A Mjini  akiwaongoza wanafunzi wenzake kwa dua maalum kwa ajili ya kuombe Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba unaotarajiwa kufanyika tarehe 7-8 Oktoba, 2020; (kulia)  waliosimama juu ya meza ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka akiungana nao katika dua wakati alipowatembelea shuleni hapo Oktoba 05, 2020 kujionea maandalizi na kuwatakia heri katika mtihani huo


Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Sima A na Sima B wakifurahia jambo


Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!