Friday, December 31, 2021

Tuesday, December 28, 2021

RC KAFULILA ALIA NA KAMPUNI YA UJENZI YA CHICCO .

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.David Kafulila akizungumza wakati wa kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika leo Katika Ukumbi wa Bariadi Conference Centre, mjini Bariadi- Simiyu. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu Bi. Shamsa Mohamed.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila, akieleza kutokuridhishwa kwake na wakandarasi na hivyo kuagiza kufutwa kwa zabuni zilizotolewa kwa kampuni 7
Aliyesimama ni Mbunge wa Itilima Mhe. Njalu Silanga akichangia jambo, Kushoto Mbunge wa Vijana Mkoa wa Simiyu Mhe.Lucy Sabu. Kulia Mbunge wa Maswa Mashariki Mhe. Stanlaus Nyongo.

Aliyesimama Mbunge wa Maswa Mashariki Stanslaus Nyongo, akichangia hoja , aliyekaa kulia Mbunge wa Meatu, Mhe.Leah Komanya

Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa,Eng.John Mkumbo, akitoa  taarifa ya Mtandao wa Barabara na jinsi ujenzi wa barabara unavyoendelea mkoani Simiyu, kwenye kikao cha barabara kichofanyika leo mjini Bariadi

MKUU wa Mkoa wa Simiyu,David Kafulila ameonyesha kutoridhishwa na kitendo cha Kampuni ya ujenzi wa barabara ya CHICCO ya nchini China kupewa kandarasi ya ujenzi wa barabara ya lami ya Mchepuko(By Pass)ya Km 11 ya mjini Maswa.

Akizungumza leo kwenye kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa huo kilichofanyika mjini Bariadi,amesema kuwa atawasiliana na Waziri wa ujenzi na Uchukuzi, Mhe.Prof. Makame Mbarawa kupata maelezo kuhusu uhalali wa kampuni ya Ukandarasi wa Barabara CHICCO kupewa kandarasi ya ujenzi huo.

Amesema kampuni hiyo awali  ilipewa kandarasi ya ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa Km 57 kutoka Mwighumbi hadi Maswa kwa gharama ya Sh Bilioni 75 lakini wakajenga chini ya kiwango na kutakiwa kuirudia upya kipande cha barabara chenye urefu  wa Kilomita 15.Mwisho.

 RC.Kafulila alibaini kujengwa kwa kiwango cha chini barabara hiyo mara baada ya kutembelea ujenzi huo Mwezi Juni mwaka huu na kuagiza maeneo yote ambayo ujenzi haukukidhi viwango kurudiwa na hadi sasa mkandarasi anaendelea na kazi ambayo inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.Mwisho.

Thursday, December 23, 2021

WAKANDARASI TEKELEZENI MIRADI YA MAJI KWA UADILIFU NA KWA WAKATI-RC KAFULILA

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amewataka Wakandarasi na Local fundi wa miradi ya maji mkoa wa Simiyu  kutekeleza miradi ya maji kwa uadilifu na wakati. Mhe. Kafulila ameyasema hayo wakati wa hafla ya kusaini mikataba 24 kati ya RUWASA na wakandarasi na RUWASA na Local Fundi.

Akizungumza katika hafla hiyo meneja wa RUWASA- Simiyu Eng. Mariam Majala amesema kuwa baada ya kuanzishwa kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini,mkoa wa Simiyu unaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maji 53 katika Wilaya za Busega, Meatu, Maswa, Itilima na Bariadi, aidha kati ya miradi 53, miradi 31 ni mipya, miradi 10 ya upanuzi, miradi 9 ya ukarabati na miradi 3 ya ukamilishaji. Eng Mariam ameeleza kuwa miradi yoye hiyo 53 inatekelezwa kwa kutumia wataalam wa ndani (Force Account).

Akieleza kuhusu usainishaji wa mikataba mipya 24, Eng.Mariamu ameeleza kuwa "Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA) leo tunatarajia kutia saini ya mikataba 24 kati ya 36 yenye gharama ya Tsh. 6.9bln. Mikataba 12 ni ya Wakandarasi na mikataba 12 ni ya Local fund. Aidha mikataba ya miradi 4 inatarajiwa kusainiwa na RUWASA makao makuu na mikataba ya miradi 8 itasainiwa katika awamu ya pili mara baada ya taratibu za ununuzi kukamilika". Meneja RUWASA Simiyu amebainisha kuwa mikataba yote iliyosainiwa 22/12/2021 itafanya kazi kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Januari, 2022 hadi June 2022. Baada ya kukamilika kwa miradi hiyo Mkoa wa Simiyu unatarajia kuongeza vituo vya kuchotea maji 143 ambavyo vitahudumia wananchi wapatao 35,750 na kufanya idadi ya wananchi wanaopata huduma ya maji safi na salama kwa maeneo ya vijijini mkoani humo kufikia 1,185,035 sawa na asilimia 73.6. 

Akizungumza, changamoto zinazowakabili Watanzania,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila, ameeleza kuwa utafiti uliofanywa 2008 kupitia kura za maoni,ulionyesha kuwa kati ya matatizo makunbwa manne yanayowasumbua Watanzania, tatizo la pili lilikuwa maji, wakati tatizo la nne likiwa rushwa.Hii inaonyesha kuwa suala la maji ni suala ni suala muhimu sana. Hivyo uamuzi wa kuanzisha RUWASA ulikuwa uamuzi sahihi. 

 Mkoa wa Simiyu una idadi ya watu wapatao 1.9ml, kati ya hao ni watu 1.14 mln sawa na 67.22% ndio wanaopata maji safi na salama. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 ongezeko la upatikanaji wa maji ni lita 1,833,400 sawa na 6.4%. Ni imani yangu kuwa kwa kusaini hii mikataba ya miradi 24 yenye thamani ya 6.9bln.Upatikanaji wa maji katika mkoa wa Simiyu utaongezeka kutoka 67.22% kufikia 73.6%.Lengo letu ni kufikia 85%.Hali hii inaonyesha waziwazi kuwa fedha za maji sio tatizo bali utekelezaji ndio mgogoro.

 "Wito wangu kwa wakandarasi na Local Fundi, tekelezeni miradi hii kwa uadilifu na kwa wakati.Kwani kwa kufanya kazi kwa wakati au hata chini ya wakati na kwa ubora mtakuwa mmejitangaza zaidi. Halmashauri taarifa kuhusu masuala ya maji, umeme, Pamba,ni taarifa muhimu kwenye vikao na ziwe zinatolewa kwenye kila kikao cha madiwani. Madiwani wanatakiwa kuwa nazo, na hii itaongeza umaarufu wa RUWASA". Amesisitiza Mhe.Kafulila.

 Maji ni kitu muhimu sana katika mfumo mzima wa maisha ya mwanadamu.Miaka miwili iliyopita upatikanaji wa maji Mkoani Simiyu ulikuwa 40.5%, Kufikia June 2022 upatikanaji wa maji Simiyu utakuwa 73.6%. Hii inaonyesha wazi kuwa tunaweza tukafika zaidi ya 90%. Pongezi kwa kazi nzuri mnayofanya RUWASA. Hongera Meneja RUWASA kwa uwazi. Hii inaongoza uwajibikaji. Ni imani yangu kuwa upatikanaji wa watoa huduma ulizangatia mchakato,sheria, kanuni na taratibu.Hivyo nendeni mkapige kazi na kazi iwe kwenye moyo na kiganja chako.

 Kwenye hii Tsh.6.9bln,toeni hata misaada kwa jamii (CSR) kwani nyie ni wawekezaji. Mkalipe Kodi  zote mnazotakiwa kulipa kwa mujibu wa sheria hii ni pamoja na Service levy,malipo ya service levy yalipwe kwa Halmashauri husika.Ushuru ni vitu ambayo vipo kisheria na vilipwe. Simiyu ni yetu pamoja hivyo ni lazima tuijenge.Nawakumbusha wajibu wenu na muende mkatende, kafanyeni kazi.Lengo ni moja kumtua mama ndoo kichwani.

Nae, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu Bi. Shamsa Mohamed, aliwapongeza RUWASA kwa kazi nzuri na kuwakumbusha wakandarasi na Local Fundi kuwa kazi waliyopewa ni ya miezi 6 tu."Kama Chama tutaanza kukagua miradi yote mwezi 3.Miradi hii ikamilike kwa wakati. Ni matarajio yetu kuwa kama ahadi iliyotolewa kwenye Ilani ya chama kuwa ili ifikapo 2025, 85% ya watu wote kutumia maji safi na salama itimie

Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Njalu Silanga, amesema, kikao hiki kimehusisha Waheshimiwa wabunge, viongozi wote wa Chama na Serikali, hivyo makandarasi kumbukeni kwamba mmesaini mikataba mbele yetu na tunatarajia mtafanya kazi vizuri, tutawapa ushirikiano, hatuhitaji malalamiko, tunataka kazi ifanyike.

Aidha, Mbunge wa Meatu Mhe. Leah Komanya, alitoa shukrani kwa tukio hili la usainishaji mikataba kwani ni la mara ya kwanza na kubwa zaidi yote mikataba 24 kusainiwa Mara moja. Mhe.Komanya aliwafahamisha washiriki wa hafla hiyo kuwa Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan akiwa Makamu wa Rais alianzisha kampeni ya kumtua mwanamke ndoo kichwani, kampeni ambayo akiwa Rais ameitekeleza kwa kuagiza 20% fedha za UVIKO-19 ziende kwenye miradi ya maji.Mhe Komanya amewataka wananchi wote kulinda miundo mbinu na vyanzo vya maji

Wakizungumza, Wakuu wa Wilaya ya Maswa, Itilima na Busega waliishukuru RUWASA kwa huduma ya maji inayopatikana katika halmashauri zao, na kueleza kuwa kuna baadhi ya maeneo upatikanaji wa maji ni wa 65% tu, na hivyo ni matumaini yao kuwa kwa usainishaji huu wa mikataba 24 ya maji kati ya RUWASA na Wakandarasi pamoja RUWASA na Local Fundi,upatikanaji wa maji utaongezeka na utekelezaji wa miradi hiyo utafanyika kwa mujibu wa ratiba, huku wakizingatia ubora, kwani kiasi cha fedha zilizoelekezwa kwenye miradi hiyo si ndogo.Wakuu wa Wilaya hizo waliwahakikishia wakandarasi na Local Fundi kuwa wako pamoja nao na kuwahakikishia ushirikiano wao.
Mwisho



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akizungumza na washiriki wa hafla ya kusaini mikata 24 ya RUWASA,.Kulia KUU ya Mkoa na baadi ya wafanyakazi wa RUWASA Simiyu



Meneje wa RUWASA , Eng. Mariam Majala, akisaini mikataba ya utendaji kazi kati ya RUWASA na Wakandarasi, pamoja na RUWASA na Local Fundi, Jumla ya mikatata 24, yenye thatamani ya Tsh. 6.9bln ilisainiwa.

Mbunge wa Itilima Mhe. Njalu Silanga akichangia jambo



Mbunge wa Meatu Mhe. Leah Komanya akichangia jambo
Mwenyekiti wa chama cgha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu Bi. Shamsa Mohamed akisisituiza jambo wakati wa hafla ya kusaini mikataba 24 ya RUWASA
Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Gabriel Zakaria akichangia hoja

Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Faiza Seleman alichangia hoja kulia kwake,ni Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge
Wakandarasi na Local Fundi wakisikiliza yanayojiri wakati wa hafla ya kuaini mikataba 24 ya RUWASA

Wednesday, December 22, 2021

MIKOA YOTE IGENI SIMIYU MIKATABA YA UWAJIBIKAJI




Naibu Waziri- TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange, leo amepongeza  Mkoa wa Simiyu kwa ubunifu wa kuanzisha mikataba ya uwajibikaji ambapo Mkuu wa Mkoa David Kafulila amesaini na wakuu wote wa wilaya na kisha Katibu Tawala Mkoa kusaini na wakurugenzi wote wa Halmashauri ambao nao wamesaini na wasimamizi wa sekta ya afya ngazi ya wilaya mpaka vijiji kwa lengo la kupima ufanisi wa kila Kiongozi na mtendaji kuanzia ngazi ya mkoa ( performance contract ) na kutaka mikoa mingine kuiga ili kuongeza tija katika usimamizi majukumu ya Serikali.  

Naibu waziri amesema hayo baada ya kupokea taarifa ya Mkoa wa Simiyu leo kuhusu masuala ya elimu na afya katika ziara yake ya siku moja mkoani simiyu, ambapo imelezwa kuwa ndani ya nusu mwaka  mifumo ya ya mapato GOTHOMICS imeboreshwa na kusababisha ongezeko la mapato kwa asilimia zaidi ya 300%, kutoka makusanyo ya takribani  milioni 200 mpaka zaidi ya milioni 600. 

Aidha mafanikio makubwa ktk usimamizi wa afya za lishe hata kufikia asilimia 92 mwezi Novemba , kiwango ambacho kinategemea kuipaisha simiyu katika tathimini ijayo itakayofanyika Januari 2022. " kwa ufanisi wa asilimia 92% sasa ni wazi tathimini ijayo Januari mkoa utakuwa 3 bora kutoka nafasi ya 23 kitaifa katika tathimini ya mwisho alisisitiza Kafulila. Mwisho.

Mikoa yote igeni Simiyu Uwajibikaji- Naibu Waziri TAMISEMI( Afya)

 Wito huo umetolewa leo na Mhe.Dkt.Festo Dungage- Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serilkali za Mitaa (TAMISEMI-AFYA), mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya uviko 19 Mkoa wa Simiyu.

Mhe.Dugange,amepongeza Sekretarieti ya Mkoa,Mamlaka za Serikali za Mitaa na viongozi wote wa Mkoa wa Simiyu,kwa kazi nzuri wanayofanya.

"Hongera kwa kazi nzuri sana mnayofanya mkoa wa Simiyu.Hatua ya  ujenzi wa madarasa kufikia 85%, hiyo ni hatua kubwa sana. Lengo la Serikali ya awamu ya Sita ni kuhakikisha kwamba watoto wetu wanaoingia kidato cha kwanza 2022, wote wanaingia darasani kwa pamoja,na  hivyo kutokuwa na uchaguzi wa mara ya pili kwa ajili ya kuingia kidato cha kwanza yaani  (second Selection).

Serikali ya Awamu ya sita imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 15000 kati ya hayo  madarsa 12000 ni kwa ajili ya shule za sekondari na  madarasa 3000  kwa ajili ya shule za msigi. Mkoa wa Simiyu umepatiwa shule 380.

Kuhusa sekta ya afya pongezi kwako Mkuu wa Mkoa, RHMT na RMO,kwani sekta hii ilikuwa na changamoto sana, mikataba ambayo inatoa viwango vya upimaji  utendaji kazi (Key Performance Indicator - KPI) na vikao vya kila robo mwaka ni ubunifu wa hali ya juu kwani inaleta uwajibikaji.Kabla ya kuwa Naibu Waziri nilikuwa Mwanasimiyu/mganga Mkuu wa Mkoa na hivyo namba yangu ya simu ilitumika kupokea malamiko mbalimbali ya wanasimiyu. Kipindi cha nyuma kulikuwa na malalamiko  mengi sana ila ndani ya miezi 6 sijapata malalamiko yeyote.

"Asilimia 95 ya huduma za afya hutolewa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo zipo chini ya TAMISEMI.

 Niwapongeze sana Mkoa wa Simiyu kwani kwa kipindi cha miezi sita  mlianza matumizi ya mfumo wa GoThomis, na   65% ya vituo vyenu vya afya vinatumia mfumo huo  kwa  ajili ya kukusanya mapato. Kama aliyoeleza mkuu wa Mkoa  mfumo huo umewasaidia kuongeza mapato kutoka kiasi cha Tsh.200mln–600mln. Makusanyo haya yanasaidia sana kuacha utegemezi toka Serikali kuu au wafadhili. Hivyo ni vyema Halmashauri zote ziige mkoa wa Simiyuamesema Mhe. Dugange .


Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila amemshukuru Mhe.Dugange kwa kutembelea mkoa wa Simiyu,na kumhakikishia kuwa ujenzi wa madarasa ambao umefikia  85% utamalizika kwa wakati. Kwa upande wa sekta ya afya Mhe. Kafulia amemfahamisha Naibu Waziri Tamisemi /afya kuwa mafanikio katika sekta ya afya yametokana na utendaji kazi mzuri wa Mganga mkuu wa mkoa pamoja na timu yake,kwani kwa kipindi cha miezi sita mapato yameongezeka kwa asilimia 300."Nimesaini mkataba wa utendaji kazi kati yangu na  Wakuu wa wilaya.Niwapongeze  wakuu wa Wilaya kuwa sasa tunasomana" amesema Kafulila.

Akiwasilisha taarifa ya hali ya utekelezaji mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 mkoa wa Simiyu, Kaimu Katibu Tawala,Injinia Mashaka Luhamba alieleza kuwa Mkoa wa Simiyu umetengewa jumla ya Tshs 20,476,951,633.30 kwa ajili ya kutekeleza miradi inayolenga kuimarisha miundombinu ya Sekta za Elimu na Afya na mapambano dhidi ya UVIKO 19. Fedha hizo zimetolewa kwa taasisi mbalimbali za Serikali zikiwemo Shule za Sekondari,Shule Shikizi,Hospitali za Wilaya katika ngazi za Halmashauri za Wilaya, Miji ,Manispaa na Majiji. Aidha, fedha zingine zimepelekwa kutekeleza miradi ya kipaumbele katika Hospitali ya Rufaa za Mkoa na Mamlaka za maji.

Kuhusu miradi ya ujenzi wa madarasa mkoani Simiyu,Injinia Luhamba amesema, hadi sasa miradi iliyoanza kutekelezwa ni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 380 vya shule za Sekondari na vyumba vya madarasa 69 vya Shule Shikizi.Mpaka sasa ujenzi huo umefikia  85% ya utekelezaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa. Injinia Mashaka Luhamba ameeleza kuwa, pamoja na mafanikio haya katika ujenzi wa madarasa Mkoa umekuwa ukikabiliwa na  changamoto mbalimbali hususani katika halmashauri ya wilaya ya Maswa na Itilima ambapo changamoto kubwa imekuwa upatikanaji wa vifaa.Vifaa vya viwandani kama vile bati na saruji kuchelewa kufika katika maeneo husika hasa kwa Halmashauri ambazo zilitumia mfumo wa manunuzi ya pamoja. Bei ya vifaa kupanda ghafla mara tu miradi ilipoanza na hivyo kusababisha gharama ya mradi kuongezeka.Shule ambazo ziliomba kibali cha kuhamisha fedha kwenda katika maeneo mengine kwa ajili ya ujenzi zilichelewa kupata kibali na hivyo kusababisha kuchelewa kuanza kwa mradi.

Kuhusu sekta ya afya,mganga Mkuu Mkoa wa Simiyu Dkt. Boniface Marwa, ameeleza kuwa kwa kipindi cha miezi tisa kumekuwa na mafanikio makubwa sana katika sekta ya afya Mkoani Simiyu.Awali kulikuwa na vituo vya afya 218 lakini sasa kuna vituo vya afya 221.Aidha upatikanaji wa dawa nao umeongezeka kufikia asilimia 91.

 Dkt. Marwa amesema mafanikio yote haya yamepatikana kutokana ushirikiano uliopo baina ya wafanyakazi wa Sekta ya Afya, uongozi bora toka kwa mkuu wa mkoa na menejimenti yake. DKt Marwa amemfahamisha Naibu Waziri kuwa moja ya siri kubwa ya mafanikio haya ni usainishaji wa mikataba ya utendaji kazi katika sekta ya afya kati ya Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya ambao nao walisainishana na maafisa tarafa,Katibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmashauri zote ambao nao wamesainishana na waganga wakuu wa halmashauri.

"Lengo la kusaini mikataba hii ni kuhakikisha utendaji kazi katika sekta ya afya unafanyika kwa weledi zaidi. Aidha ripoti za utendaji kazi zimekuwa zikitolewa kila robo mwaka na kwa kweli kumekuwa na mafaniko makubwa sana.Lengo letu ni kutaka kuwe na usimamizi na utendaji wa pamoja katika mkoa"amesema.Dkt Marwa.

Akijibu hoja kuhusu changamoto ya uhaba wa watumishi sekya ya afya Mhe. Dugange amekiri kuwa mkoa wa Simiyu ni mmoja kati ya mikoa inayokabiliwa na changamoto  kubwa ya uhaba wa Watumishi wa  sekta ya afya. Serikali imeliona hilo na  inafanyia kazi kwa  kuendesha zoezi la kujua daktari na N esi ikilinganishwa na idadi ya wagonjwa wanaopaswa kuhudumiwa na dakkati /nesi mmoja ( Doctor/Nurse Patient ratio).Lengo la Serkali ni kuhakikisha kuwa kila mkoa uwe na watumishi angalau si chini ya  60% ya mahitaji yao. Akizungumzia 40% ya mapato ya ndani baada ya kutoa mapato lindwa, Mhe. Dugange amesema kuwa lazima fedha hizo ziende kwenye miradi ya maendeleo.

 Naibu Waziri TAMISEMI (Afya) 


Mhe. Festo Dugange yupo ziara Mkoani Simiyu kwa lengo la kupitia miradi ya ujenzi wa madarasa ya Uviko na vituo vya afya,ili kuona shughuli zinazoendelea na Changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo, katika utekelezaji wa shughuli





Naibu Waziri TAMISEMI( Afya) Mhe.Dkt. Festo Dugange akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.
Kaimu Katibu Tawala Mds. Mashaka Luhamba akiwasilisha taarifa ya Mkoa kuhusu utekelezaji wa Miradi ya Uviko-19,aliyekaa wa kwanza Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.David Kafulila 

Naibu Waziri TAMISEMI( Afya) Mhe. Festo Dugange, akimpongeza mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe Kafulila kwa utendaji kazi mzuri


Naibu Waziri TAMISEMI- AFYA Mhe. Festo Dugange akizungumza na kutoa wito wa Halmashauri zote kuiga Mkoa wa Simiyu

Washiriki wa Kutoka hospitali ya mkoa wa Simiyu pamoja na Makatibu Tawala wasaidizi wakifuatilia kwa makini maelezo ya viongozi mbalimbali wakati wa kikao hichoo.

Tuesday, December 14, 2021

RC Kafulila Aagiza Wazawa Malampaka Wapewe Kipaumbele














Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akizungumza na Wananchi wa Malampaka- Maswa

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila ameagiza wazawa wa Malampaka wapewe kipaumbele kwenye ajira ya Ujenzi wa reli ya kisasa(SGR), Mwanza/ Isaka.

Maagizo hayo yametolewa, mara baada ya mamia ya wananchi wa  mji wa Malampaka wilaya ya Maswa, kumlilia mkuu wa mkoa awasaidie kupata ajira kwenye kituo cha ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Mwanza kwenda Isaka kilichopo kwenye mji huo, inayojengwa na kampuni ya CCECC ya nchini China.

Wananchi hao walitoa kilio chao katika mkutano wa hadhara uliondaliwa na Mkuu wa mkoa kwa ajili ya kusikiliza malalamiko yao kuhusu kubaguliwa kwao katika masuala ya ajira pamoja na kuwepo kwa vitendo vya rushwa kwenye mradi huo unaofanyika mjini Malampaka.

Wananchi  hao walimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa wakati mradi huo unatambulishwa kwa mara ya kwanza kwao na viongozi wa serikali walielezwa kuwa wakazi wa eneo hilo ambapo panajengwa bandari ya nchi kavu watapatiwa kipaumbele kwenye masuala ya ajira.

Walisema kuwa kwa sasa shughuli zimekwisha anza lakini waliopatiwa ajira ni watu wachache tu ambao hawazidi 15 kulinganishwa na idadi watu 300 walioko kwenye kambi hiyo. Ambapo wengi wao wametoka nje ya mkoa wa Simiyu.

'Mwanzoni tulielezwa kuwa mradi utakapoanza kipaumbele kitatolewa kwa wananchi ambao wanaishi katika eneo ambalo mradi unatekelezwa lakini cha kushangaza mambo yamekwenda kinyume kabisa wengi wa waajiriwa wanatoka nje kabisa ya mkoa wa Simiyu,"

"Sisi tumekuwa tukibaguliwa katika masuala ya ajira na jambo baya zaidi katika kupata ajira hizo vitendo vya rushwa vimeshamiri sana,"alisema Juma. 

Kutokana na malalamiko hayo Mkuu wa Mkoa ameagiza vyombo vya dola kufutailia suala la rushwa kama lipo na kutaka wahusika watakaobainika kuchukuliwa hatua za kusheria.

Aidha ametaka kupelekewa majina ya watu walioajiriwa kama wanatoka mkoa wa Simiyu au la kwani Serikali imekuwa ikitaka wanufaika wa kwanza wawe wanaoishi kwenye eneo la mradi.

MWISHO.



Thursday, December 9, 2021

Kuna Watu Wengi wa Maana Kaburini Kuliko Tuliobaki



“Kipo wapi kizazi kile ambacho kijana alihitaji kuwa na jembe, panga na shoka kuvamia msitu kuanza kuzalisha? 
Leo wazee wanataka kuwezeshwa kwasababu ni wazee, kina mama wanataka kuwezeshwa kwasababu ni wanawake, sasa na vijana nguvu kazi inazungumza kuwezeshwa vilevile kama wazee na kina mama. 

Ukiangalia majengo yaliyojengwa miaka 20 ya kwanza ya uhuru tukiwa na wahandisi wachache bado yapo, yanafanyiwa usafi tu lakini kuta bado imara.Lakini zama hizi za milenia ambazo tuna wahandisi wengi mpaka wanakosa kazi, kuna majengo hayafiki miaka 10 kabla ya kuanza kupasuka.Kifupi tuna watu wengi wa maana kaburini kuliko tuliobaki na maisha.Na hii ndio changamoto ya kizazi cha milenia leo.

Raia kwenye nchi masikini tunapumzika saa nyingi kuliko wa nchi tajiri.." RC - Kafulila akizungumza na wanachuo miaka 60 ya Uhuru.


Thursday, December 2, 2021

Simiyu Yafanya Vizuri Viashiria vya UKIMWI, Kitaifa na Kimataifa-RC KAFULILA

 Mhe. Kafulila ameyasema hayo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani  yaliyofanyika kimkooa katika Viwanja Vya Halmashauri Bariadi, Mkoani Simiyu.

 Akizungumza Mhe Kafulila alieleza kuwa Siku ya Ukimwi Duniani ni siku muhimu sana kwani ni siku ambayo tathmini ya jinsi gani janga la ukimwi lilivyoleta na linavyoendelea kuleta athari kubwa kuanzia mtu mmoja, familia hadi Taifa kwa ujumla hufanyika. Aidha siku hii ni muhimu kwa Dunia na kwetu wana Simiyu kwani hutoa fursa ya kuhamasisha Watanzania na Wana Simiyu na kuwaeleimisha jinsi gani wanavyoweza kupambana na maambukizi mapya ya VVU na UKIMWI..

Aidha Mhe. Kafulila amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutilia mkazo  agenda ya afya, kwani  afya imekuwa kipaumbele kikubwa sana katika Serikali ya Awamu ya Sita.Toka miaka ya 1980 wakati janga la UKIMWI lilipoikumba Dunia,Dunia imefanikisha kwa kiasi kikubwa kupambana na janga la hili, ili hali Changamoto kubwa ikiwa  imebakia katika nchi zilizopo kusini mwa Jangwani la Sahara .

Dunia Inaendelea kupambana na jangwa la UKIMWI kwa Sababu  athari zake ni kubwa,nazo huathiiri mtu mmoja mmoja, familia na hadi Taifa. Mkoani Simiyu  idadi ya maambukizi ya UKIMWI ni asilimia  3.9%  ambayo ni chini ya kiwango cha Kimataifa ambacho ni asilimia 5.1%,hii inaonyesha kwamba kazi imefanyika.Pamoja na mafanikio haya hii haimaniishi kwamba tulane badala yake tuzidishe mapambano, na iwe agenda kwenye vikao vyetu kuanzia ngazi ya kata.

"Vikao vya kamati ya maendeleo ni vyema vikajadili suala hili. Mabaraza ya Madiwani RMO,kwenye vikao vyote vya RCC,DCC na vikao vya Madiwani mada kuhusu magonjwa ya UKIMWI na UVIKO namna na  jinsi ya kujikinga ni lazima ziwe agenda za mawasiliano" Tukijenga uelewa mzuri kuhusu magonjwa haya tuna uwezo mkubwa wa kujikinga na hatimaye kuepukana  magonjwa yote ".Alisisitiza Mhe.Kafulila.

Ujumbe wa Mwaka huu wa Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani  unasema "ZINGATIA USAWA, TOKOMEZA UKIMWI, TOKOMEZA MAGONJWA YA MLIPUKO". Kauli mbiu hii ni pana na inabeba mambo mengi.Kama viongozi tunapaswa kuzungumzia magonjwa haya ya mlipuko.

I" Asilimia 43% ya maambukizi mapya Tanzania, yanatokea kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15-24,  hii ndio nguvu kazi ya nchi .Hali hii inaonyesha kuwa tusipochukua hatua, tutabaki na Taifa dhaifu sana, kwani huwezi kujenga Taifa lenye nguvu kama  lina vijana wenye afya dhaifu. Ukubwa wa Taifa ni rasilimali watu ambao hupimwa kwa mambo matatu,afya,uadilifu na maarifa. Nitoe wito "pale ambapo itakuwa umeathirika huo sio mwisho wa maisha yako.Kupata ukimwi haimaanishi ni mwisho wa maisha yako na mwisho wa kufanya kazi,hivyo tujitahidi  kukabiliana na janga hili.Tuwahi kupima ili tujue afya zetu,kwani kwa kuwahi kutumia dawa sahihi na kwa usahihi kutafubaza  wadudu wa UKIMWI" Amesema Kafulila.

Aidha Mhe. Kafulika alionya tabia ya wanaume kutegemea wake zao kupima VVU na kuamini kwamba majibu ya mke wake ni majibu ya wote."Hii ni dhana potofu na wanaume tunatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kujua afya zetu".

 Mhe. Kafulila alitaja baadhi ya mambo  yanayochochea UKIMWI mkoani Simiyu,kuwa ni kuwa na wenza wengi, Kurithi wajane,kuanza ngono katika umri mdogo, kujihusisha na makundi hatarishi,kulewa kupindukia,kutumia Dawa za kulevya, idadi ndogo ya wanaume wenye tohara na biashara ya ngono. Mkuu wa Mkoa alieza kuwa amepata taarifa kuwa baadhi ya wadada wanajiuza maeneo mmbalimbali na hivyo akatoa maelekezo kwa  wakuu wote wa  Wilaya kuhakikisha maeneo yote yanayotumika kwa biashara ya ngono yanadhibitiwa, kwani hiyo sio biashara halali, na sio utamaduni wetu. Mkuu wa Mkoa aliziagiza Kamati za Amani na kamati za Usalama kukutana  mara kwa Mara na kuhakikisha zinashirikiana katika kudumisha maadili.

 Akitaja  malengo matatu ya kidunia ya kupambana na maambukizi ya VVU na UKIMWI na uhalisia katika mkoa wa Simiyu Mhe. Kafulila ameeleza kuwa katika   95% ya kwanza ifikapo mwaka 2030 wananchi wenye maambukizi wawe wanafahamu hali zao, Mkoani Simiyu wananchi asilimia 84 wanatambua hali zao za maambukizi ya VVU. Katika 95% ya pili  dunia ilikubaliana kuwa ifikapo mwaka 2030, asilimia 95 ya wale wanaobainika  kuwa na maambukizi ya VVU, asilima 95 waanzishwe dawa za ARV kwa ajili ya kufubaza VVU. Katika lengo hili Mkoa wa Simiyu tumefikia 99% hii ni hatua kubwa sana inayohitaji Pongezi. Asilimia 95 ya tatu, wale wote walioko kwenye dawa baada ya miezi 6 virusi viwe vimefubaa kwa 95% kwa mkoa wa Simiyu tumefikia 96%. 

Nichukue fursa hii kuwakumbusha wananchi wote wa mkoa wa Simiyu wanaotumia dawa za kufubaza VVU, kuendelea kuzitumia kwa usahihi kama inavyoshauriwa na wataalam wetu ili tufikie 100%. Mashuhuda Wawili wa Kike na Kiume walitoa ushuhuda kuhusu jinsi ambavyo wameweza kuishi na VVU na UKIMWI kwa zaidi ya miaka 10, kiasi cha kupata watoto ambao hawajaathirika na  hivyo kuwahamasisha wananchi kupima afya zao,kujikubali, kisha kunywa dawa sahihi zinazotolewa na vituo vya afya kama zinavyoshauriwa na wataalam.

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, kimkoa yamefanyika Wilayani  Bariadi, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe.Lupakisyo Kapange alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kukubali kuwa mgeni rasmi.Akizungumzia Ujenzi wa Madarasa ya Uviko-19 Mhe. Kapange amemweleza Mkuu wa Mkoa kuwa "tumefikia  mwisho/finishing.

Mwisho





Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani

Mufti wa Mkoa wa Simiyu akisali wakati wa Maadhimisho ya UKIMWI Duniani

Mhe. David Kafulila akisoma risala ya Waathirika wa UKIMWI,Katika Viwanja vya Halmashauri  Bariadi

Wanakwaya ya AICC Simiyu ikitumbuiza wakati wa Maadhimisho

Kutoka kulia RAS wa Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo, akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Lupakisyo Kapange pamoja na DAS- Bariadi Bw.Shirima wakielekea kwenye jukwaa kuu.




Mhe. Kafulila akiwa ameambatana na viongozi wengine wakikagua mabanda ya maonesho katika viwanja vya Halmashauri Bariadi



Mkuu wa Mkoa  wa Simiyu Mhe. David Kafulila pamoja na  Katibu Tawala Mkoa wakifuatilia jambo.


Wajumbe wa Kamati ya Usalama wakifuatilia jambo wakati wa maadhimisho ya UKIMWI  Duniani

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo(kulia), Mhe. David Kafulila(RC) na Mhe. Lupakisyo Kapange(DC- Bariadi) wakiondoka viwanja vya Halmashauri Bariadi mara baada ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani

 

.

 

 

 

 

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!