Saturday, January 30, 2021

WATU WENYE ULEMAVU WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA MIKOPO YA ASILIMIA MBILI KUTOKA HALMASHAURI

 

Na Stella Kalinga, Simiyu RS

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe.Ummy Nderiananga amewataka watu wenye ulemavu nchini kujitokeza kuchukua mikopo inayotolewa na halmashauri bila riba kutoka katika asilimia mbili ya mapato ya ndani ili waweze kujipatia kipato na kuondokana na adha ya kutumikishwa kama omba omba. 

Mhe. Nderiananga ametoa wito huo jana Januari 29, Mjini Bariadi wakati alipokutana na kuzungumza na viongozi wa makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu akiwa katika ziara yake ya siku moja mkoani Simiyu, iliyolenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu..

" Licha ya baadhi ya Halmashauri kufanya vizuri katika kutenga fedha kwa ajili ya watu wenye ulemavu, kuna taarifa kuwa baadhi yenu mmekuwa waoga kukopa fedha zinazotengwa kwa ajili yenu, nitoe rai kwenu tumieni fursa hiyo kopeni ili mpate mitaji ya kuwasaidia kufanya shughuli za kuwaingizia kipato, fedha hizi ni kwa ajili yenu na Serikali imefanya kazi kubwa sana ili mpate fedha hizi,” alisema Nderiananga. 

Katika hatua nyingine Nderiananga amewaasa watu wenye ulemavu wanaochukua mikopo hiyo kurejesha kwa wakati kwa mujibu wa miongozo na taratibu za utoaji wa mikopo hiyo ili kutoa fursa kwa kila mmoja anayehitaji  mikopo hiyo kuipata kwa wakati. 

“Natoa wito kwa watu wenye ulemavu ambao mmekuwa mkikopeshwa fedha itokanayo na asilimia mbili ya mapato ya ndani ya halmashauri kurejesha nawaomba msile, mkila mtafanya watu wenye ulemavu wasiaminike,” alisema Nderiananga 

Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu wa viungo (CHAWATA) Mkoa wa Simiyu, Bw Gera Makasi ameomba Viongozi na wataalam kutoka Serikalini waendelee kutoa elimu juu ya mikopo hiyo ili watu wenye ulemavu wapate uelewa mpana juu ya namna mikopo hiyo inavyotolewa, inavyorejeshwa na namna sahihi ya kuitumia kwa manufaa. 

Naye  Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema Mkoa wa Simiyu unawajali sana watu wenye ulemavu  huku akibainisha kuwa Simiyu imejipanga kuanzisha namna ya tofauti (unique model) ya utoaji wa mikopo kwa watu wenye ulemavu, wanawake na vijana ili mikopo itolewayo kutoka katika asilimia kumi ya mapato ya Halmashauri iwe na tija kwa makundi lengwa ( watu wenye ulemavu asilimia mbili, vijana asilimia nne na wanawake asilimia nne)

Akitoa taarifa ya mkoa kwa Naibu Waziri, Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu amesema watu wenye uemavu mkoani hapa wamekuwa wakishirikishwa katika shughuli za kijamii na uhamasishaji unaendelea kufanyika ili waweze kuunda vikundi kurahisisha upatikanaji wa mikopo, ambapo  mpaka sasa takribani vikundi 45 vya watu wenye ulemavu vimeshaundwa.

Aidha , Mujungu ameongeza kuwa katika bajeti ya mwaka 2020/2021  kiasi cha shilingi milioni mia mbili na laki sita kimetengwa katika halmashauri zote sita za mkoa wa Simiyu (Bariadi Mjini, Bariadi Vijijini, Busega, Itilima, Maswa na Meatu)  kwa ajili ya kutoa mikopo kwa watu wenye ulemavu.

MWISHO 

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza na baadhi ya viongozi na watendaji wa mkoa wa Simiyu mara baada ya kuwasili jana Januari 29, 2021 Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara yake ya siku moja mkoani hapa iliyolenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu.

Mmoja wa wakalimani wa lugha ya alama mkoani Simiyu akitafsiri hotuba ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga kwa viziwi wakati akizungumza na viongozi wa makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu jana Januari 29, 2021 Mjini Bariadi akiwa katika  ziara yake ya siku moja mkoani hapa iliyolenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi , Mhe. Festo Kiswaga akizungumza katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga na viongozi wa makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu jana Januari 29, 2021 Mjini Bariadi, wakati wa  ziara ya Naibu waziri huyo  mkoani hapa iliyolenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu(kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa watu wenye Ulemavu kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Jacob Mwinula katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga na viongozi wa makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu jana Januari 29, 2021 Mjini Bariadi, wakati wa  ziara ya Naibu waziri huyo  mkoani hapa iliyolenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA)  Mkoa wa Simiyu, Bi. Josephine Shimula akitoa taarifa ya shirikisho hilo katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga na viongozi wa makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu jana Januari 29, 2021 Mjini Bariadi, wakati wa  ziara ya Naibu waziri huyo  mkoani hapa iliyolenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu.

Bi. Rachel Buluba kutoka wilayani Bariadi akiwasiliha hoja yake katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga na viongozi wa makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu jana Januari 29, 2021 Mjini Bariadi, wakati wa  ziara ya Naibu waziri huyo  mkoani hapa iliyolenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu(kulia) akimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga katika kikao cha Naibu waziri huyo na viongozi wa makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu jana Januari 29, 2021 Mjini Bariadi, wakati wa  ziara ya Naibu waziri huyo  mkoani hapa iliyolenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu.

Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Bariadi , Mhe. Festo Kiswaga, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakifuatilia kikao cha Naibu waziri huyo na viongozi wa makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu jana Januari 29, 2021 Mjini Bariadi, wakati wa  ziara ya Naibu waziri huyo  mkoani hapa iliyolenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu mara baada kuhitimisha ziara yake jana Januari 29, 2021 mjini Bariadi ambayo ililenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga(mwenye mtandio wa njano) akifurahia jambona baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na badhi ya watu wenye ulemavu mara baada ya kuhitimisha ziara yake jana Januari 29, 2021 mjini Bariadi ambayo ililenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ule

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu, baadhi ya maafisa na baadhi ya watu wenye ulemavu mara baada kuhitimisha ziara yake jana Januari 29, 2021 mjini Bariadi ambayo ililenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu.

PICHA ZAIDI KATIKA ZIARA YA NAIBU WAZIRI NDERIANANGA

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!