Saturday, February 27, 2021

KILA MTUMISHI ITILIMA ASHIRIKI KIKAMILIFU UKUSANYAJI WA MAPATO: RAS SIMIYU

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amewataka watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu kuwa sehemu ya Halmashauri hiyo katika ukusanyaji wa mapato ili Halmashauri hiyo iweze kupanda katika ukusanyaji mapato na  kupata uwezo wa kujiendesha.

 

Mmbaga ameyasema hayo wakati akizungumza na baadhi ya watumishi wa tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.

‘Halmashauri yetu haifanyi vizuri katika ukusanyaji wa mapato, kutokana na hali hii ya ukusanyaji baadi ya masuala yenu muhimu kama watumishi mnaweza msiyapate kwa wakati hivyo kila mtumishi ajulikane kama afisa mapato wa halmashauri, hili si jukumu la Mkurugenzi na Mtunza Hazina wa Halmashauri pekee, wote mshirikiane kukusanaya mapato kwa uadilifu,” alisema Mmbaga.

Aidha, Mmbaga amewataka watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima kuwa waangalifu katika matumizi ya mapato yanayokusanywa kwa kuhakikisha wanawekeza katika maeneo yenye tija na matokeo.

Sambamba na hilo Mmbaga amewataka watumishi hao kuziba mianya yote ya ubadhilifu na kumwataka viongozi kuwachukulia hatua watumishi watakaothibitika pasipo shaka kuwa wamefanya ubadhilifu wa mali za umma na katu wasiwafumbie macho.

Kwa upande wao watumishi wa lioshiriki katika kikao hicho walipata fursa fursa ya kuwasilisha changamoto zao ikiwa ni pamoja na kuomba Katibu Tawala wa Mkoa kama Mkuu wa Utumishi wa Umma ndani ya Mkoa aweze kuzipatia ufumbuzi ambazo ni kulipwa stahiki zao ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya mishahara, madai ya fedha za kujikimu na nauli kwa watumishi wapya, upandishwaji wa madaraja na suala la uhamisho.

Katika kuyapatia ufumbuzi masuala haya Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amesema ni vema wakuu wa taasisi wapewe taarifa sahihi juu ya upandishwaji wa madaraja na uhamisho wa watumishi ili waweze kuwaelimisha na kuwapa taarifa sahihi za masuala hayo watumishi walio chini yao.

Aidha, Mmbaga amemtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya itilima kuweka mpango mkakati wa kulipa madai mbalimbali ya watumishi ikiwa ni pamoja na nauli na fedha za kujikimu ili waweze kulipwa kulingana na halmashauri itakavyopata fedha.

Naye Afisa Utumishi wa Halmashauri amesema suala la kupandishwa madaraja kwa watumishi walioajiriwa kuanzia mwaka 2014 halijafanyika kwa nchi nzima si kwa Itilima peke yake hivyo amewasihi watumishi hao kuendelea kuwa watulivu mpaka yatakapotolewa maelekezo na Ofisi ya Rais Utumishi juu ya upandishaji wa vyeo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Itilima, Bi. Elizabeth Gumbo amewataka wakuu wa shule na wakuu wa Vituo vya kutolea huduma za afya wilayani humo kuyawekea mipaka asili maeneo yaliyo chini yao ili kuepusha maeneo hayo kuvamiwa na wananchi ambapo uvamizi huo unaweza kuleta migogoro katika jamii inayozunguka taasisi hizo.

MWISHO

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akizungumza na baadhi ya watumishi wa tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.


Baadhi ya watumishi wa tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akiwa katika kikao pamoja nao wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bi. Elizabeth Gumbo akifafanua jambo katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya watumishi wa  tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.

Mmoja wa watumishi wa tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Miriam Mmbaga na watumishi hao, wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.

Mmoja wa watumishi wa tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Miriam Mmbaga na watumishi hao, wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.

Kaimu Katibu Tawala Msaidizi wa Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji, Bi. Kija Kayenze akifafanua jambo katika katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya watumishi wa  tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.

Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bi. Upendo Haule akifafanua jambo katika katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya watumishi wa  tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.

Baadhi ya watumishi wa tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akiwa katika kikao pamoja nao wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021

Mmoja wa watumishi wa tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Miriam Mmbaga na watumishi hao, wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.

Mmoja wa watumishi wa tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Miriam Mmbaga na watumishi hao, wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.

Mmoja wa watumishi wa tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Miriam Mmbaga na watumishi hao, wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.


RAS SIMIYU AWAASA VIONGOZI WA DINI, WAGANGA WA TIBA ASILI KUSHIRIKI KUPUNGUZA VIFO VYA WAKINAMAMA NA WATOTO

 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ametoa wito kwa viongozi wa dini na waganga wa tiba asili mkoani Simiyu kushirikiana na Serikali katika juhudi mbalimbali za kupunguza vifo vya wakina mama wajawazito  na watoto vitokanavyo na uzazi. 

Mmbaga ameyasema hayo katika kikao chake na viongozi wa dini na waganga wa tiba asili wilayani Itilima, kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya wilaya hiyo Lagangabilili.

“Sisi kama mkoa tunasema hatutaki kuona mwanamke yeyote anapoteza maisha wakati akijifungua na mtoto akipoteza maisha wakati anazaliwa tunasema waliokufa sasa basi, ni muhimu viongozi wa dini na waganga wa jadi wakashirikiana na Serikali katika kueleimisha jamii juu ya umuhimu wanawake wajawazito  kupata huduma stahiki za afya kwa wakati,  tunajua haya makundi yanakutana na yanawahudumia watu wengi,” alisema Mmbaga.

Aidha, Mmbaga amesema Serikali inatambua mchango na kazi nzuri inayofanywa na viongozi wa dini kupitia kamati za amani huku akisisitiza kamati hizo ziendelee kutekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazokutana na taasisi wanazozisimamia (madhehebu ya dini).

Wakati huo huo Mmbaga ametoa rai kwa waganga wa tiba asili mkoani Simiyu kuchagua viongozi waadilifu watakaowaunganisha pamoja na kuwa msaada kwao katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, miongozo, kanuni na taratibu za nchi zilizowekwa.

Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi amewapongeza waganga wa tiba asili kwa kuwa wadau muhimu wa maendeleo katika wilaya hiyo kwa kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa, kutoa chakula kwa ajili ya wanafunzi wanaokuwa katika kambi za kitaaluma; huku akiwaomba waimarishe umoja wao na kuwa na uongozi imara ili waweze kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili.

Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lagangabilili ameomba Serikali ione uwezekano wa kuunda chombo kitakachowasaidia viongozi wa dini na waganga wa tiba asili ili makundi hayo yaweze kutekeleza majukumu yao kwa misingi ya sheria, kanuni, taratibu na miongozo inayotolewa na serikali, huku Padri Ivo Komba akitoa wito kwa viongozi wa dini kuwaongoza waumini wao katika imani ya kweli iliyo thabiti mbele za Mwenyezi Mungu.

Kwa upande wake Bw. Tandala Shuri Mganga wa asili kutoka kata ya Nkoma ameomba waganga wa tiba asili washirikiane na viongozi wa dini kufanya kazi kwa kufuata taratibu huku akieleza kuwa baadhi ya waganga wa tiba asili siyo waaminifu wamekuwa wakikiuka taratibu zilizowekwa hivyo akaiomba serikali isisite kuwachukulia hatua waganga wote watakaokwenda kinyume cha sheria zilizopo.

“Tunaomba serikali ishughulike na waganga wahalifu na sisi waganga ndiyo tuwe mstari wa mbele kuwafichua wahalifu hao ili uhalifua wao usituchafue waganga wote, tufuate utaratibu unatakiwa na serikali katika kufanya kazi zetu tusitafute kugombana na serikali,” alisema Tandala Shauri.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Dkt. Anold Musiba amesema waganga wote wanapaswa kuomba leseni za kuendesha shughuli zao ili waweze kutambulika kisheria ambapo mpaka sasa jumla ya waganga wa tiba asili 1387 wametambuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Itilima. 

Aidha, Dkt. Musiba ametumia fursa hiyo kuwaomba waganga hao kuwaelekeza wakina mama wajawazito, wakina mama wenye watoto wenye utapiamlo mkali na matatizo yote ya lishe kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya mapema.

MWISHO

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akizungumza na baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa tiba  asili wa wilaya ya Itilima, katika kikao kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.

Baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa tiba asili  wa wilaya ya Itilima, wakiwa katika kikao na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga, kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.

Baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa tiba asili wa wilaya ya Itilima, wakiwa katika kikao na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (hayupo pichani) , kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.

Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi akizungumza katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa tiba asili  wa wilaya ya Itilima kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Itilima, Mhe. Mahamoud Mahamoud akizungumza katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa tiba asili wa wilaya ya Itilima kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.

Tandala Shauri Mmoja wa waganga wa tiba asili akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa tiba asili wa wilaya ya Itilima kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.

Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Lagangabilili Itilima akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa tiba asili wa wilaya ya Itilima kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.

Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe. Njalu Silanga akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa tiba asili wa wilaya ya Itilima kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Dkt. Anold Musiba akifafanua jambo katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa tiba asili wa wilaya ya Itilima kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.

Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Kilulu wilayani Itilima akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa tiba asili wa wilaya ya Itilima kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.

Mmoja wa Waganga wa tiba asili wilayani Itilima akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa tiba asili wa wilaya ya Itilima kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.

Mmoja wa Waganga wa tiba asili wilayani Itilima akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa tiba asili wa wilaya ya Itilima kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.

Baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa tiba asili  wa wilaya ya Itilima, wakiwa katika kikao na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga, kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.

Baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa tiba asili  wa wilaya ya Itilima, wakiwa katika kikao na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga, kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.

 

Wednesday, February 17, 2021

 

WIZARA YA ELIMU YAAHIDI KUTOA FEDHA UJENZI WA CHUO VETA SIMIYU

Na Stella Kalinga, Simiyu RS

Naibu waziri wa Elimu, sayansi na teknolojia, Mhe.Omary Kipanga amesema Wizara hiyo itahakikisha inatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha VETA cha mkoa wa Simiyu ili kutimiza azma ya serikali ya kila mkoa na wilaya kuwa na chuo cha Mafunzo ya ufundi stadi (VETA).

Kipanga ameyasema hayo Februari 16, 2021 wakati wa ziara yake iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyuo vya VETA ambapo kwa mkoa wa Simiyu alipata fursa ya kutembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha VETA cha mkoa katika Mtaa wa Bunamhala Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omari Juma Kipanga (katikati) akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wakati alipotembelea Chuo cha Maendelea ya Jamii Bariadi kilichopo Mtaa wa Bunamhala Februari 16, 2021 wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani Simiyu.


Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!