Wednesday, April 14, 2021

WANAFUNZI SIMIYU WAOMBA KAMBI ZA KITAALUMA ZIWE ENDELEVU

Wanafunzi wa shule ya sekondari Bariadi mkoani Simiyu wameomba viongozi wa mkoa na wadau wote wa elimu kuwa kambi za kitaaluma ziwe endelevu kwa kuwa zina matokeo chanya kwa katika ufaulu wa wanafunzi na ili mkoa uendelee kufanya vizuri katika mitihani yote ya Kitaifa. 

Ombi hilo limetolewa tarehe 14 Aprili 2021 wakati wanafunzi hao walipopokea msaada wa chakula, shajala na taulo za kike kutoka Benki ya TPB vyote vikiwa na thamani ya shilingi 4,550,000/= ambavyo vimetolewa kwa jili ya wanafunzi wa kambi za kitaaluma kwa kidato cha sita mkoani hapa.

“Tunaomba kambi hizi ziwe endelevu maana zina mchango chanya kwenye ufaulu wa masomo yetu, miaka ya nyuma tulikuwa tukishika nafasi za mwisho kabisa lakini sasa hivi tumekuwa wa tatu Kitaifa; pia tuwaahidi tu kwamba kidato cha sita mwaka huu  hatutawaangusa tutashika nafasi ya kwanza,” alisema Godfrey Andrew mwanafunzi wa kidato cha sita.

“Tunashukuru kwa msaada huu wa vitu tulivyopewa lakini pia tunashukuru kwa jitihada za mkoa kuanzisha kambi ambazo zimetusaidia kuongeza ufaulu wetu, pamoja na ufaulu kambi hizi zimesaidia wanafunzi wengi kumaliza masomo yao pasipo kukatishwa na sababu za kijamii kwani muda mwingi wanakuwa shuleni,” Minza Kija mwanafunzi wa kidato cha nne

Awali akitoa taarifa ya elimu ya mkoa Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema mkoa una mkakati wa taaluma wenye vipengele 12 na kimojawapo kikiwa kambi za kitaaluma ambazo zimechangia kuuweka mkoa katika mikoa kumi bora katika mitihani yote ya Kitaifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya TPB, Bw. Henry Bwogi akikabidhi msaada wa chakula, shajala na taulo za kike kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPB Benki amesema benki imetoa msaada huo kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika elimu.

Aidha, Bwogi ametoa rai kwa wanafunzi kujisomea kwa bidii ili waweze kufanya vizuri na kufikia ndoto zao ikiwa ni njia moja wapo ya kuthamini juhudi za viongozi wa Mkoa wa Simiyu na wadau mbalimbali katika elimu.

Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa Mkoa, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Ekwabi Mujungu ameishukuru Benki ya TPB kutoa msaada huo ambao umeonesha ni namna gani wadau wa elimu wanatambua kazi inayofanywa na viongozi na wananchi wa mkoa wa Simiyu katika sekta ya elimu ambapo amewahakikishia kuwa msaada huo utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Vile vile Mujungu amewapongeza viongozi na watendaji wa idara ya elimu mkoa wa Simiyu kwa jitihada wanazofanya katika elimu ambazo zimechangia kuuweka mkoa wa Simiyu katika nafasi nzuri ya ufaulu kwa mitihani yote ya Kitaifa, huku akiwataka wanafunzi wasome kwa bidii ili waweze kufanya vizuri na kufikia lengo la mkoa la kushika nafasi ya kwanza katika mitihani yote.

MWISHO

Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya TPB, Bw. Henry Bwogi(mwenye suti nyeusi) akikabidhi msaada wa chakula, shajala, taulo za kike kwa uongozi wa Mkoa wa Simiyu, kwa ajili ya kambi za kitaaluma za kidato cha sita na kidato cha nne, ambao ulikabidhiwa katika Shule ya Sekondari ya Bariadi, tarehe 14 Aprili 2021.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Bariadi wakishuhudia makabidhiano ya msaada wa vyakula na mahitaji mengine muhimu kwa wanafunzi wa kidato cha nne na cha sita walio katika kambi za kitaaluma katika shule zao, msaada ambao umetolewa na benki ya TPB tarehe 14 Aprili 2021.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Bariadi wakishuhudia makabidhiano ya msaada wa vyakula na mahitaji mengine muhimu kwa wanafunzi wa kidato cha nne na cha sita walio katika kambi za kitaaluma katika shule zao, msaada ambao umetolewa na benki ya TPB tarehe 14 Aprili 2021.
Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw.  Ekwabi Mujungu akizungumza na walimu na wanafunzi wa Shule ya sekondari Bariadi wakati wa makabidhiano ya vyakula, shajala na taulo za kike kati ya Benki ya TBP na Uongozi wa Mkoa ambapo umepokelewa shuleni hapo tarehe 14 Aprili 2021 kwa , kwa niaba ya shule nyingine.
Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya TPB, Bw. Henry Bwogi akizungumza na baadhi ya viongozi na watumishi wa Mkoa wa Simiyu, walimu na wanafunzi wa Shule ya sekondari Bariadi wakati wa makabidhiano ya vyakula, shajala na taulo za kike kati ya Benki ya TBP na Uongozi wa Mkoa ambapo umepokelewa shuleni hapo tarehe 14 Aprili 2021 kwa , kwa niaba ya shule nyingine kwa ajili ya kutumika katika kambi za kitaaluma.
Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya TPB, Henry Bwogi (mwenye suti nyeusi) akikabidhi msaada wa chakula, shajala, taulo za kike kwa uongozi wa Mkoa wa Simiyu, kwa ajili ya kambi za kitaaluma za kidato cha sita na kidato cha nne, ambao ulikabidhiwa katika Shule ya Sekondari ya Bariadi, tarehe 14 Aprili 2021.
Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya TPB, Henry Bwogi (mwenye suti nyeusi) akikabidhi msaada wa chakula, shajala, taulo za kike kwa uongozi wa Mkoa wa Simiyu, kwa ajili ya kambi za kitaaluma za kidato cha sita na kidato cha nne, ambao ulikabidhiwa katika Shule ya Sekondari ya Bariadi, tarehe 14 Aprili 2021.

Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya TPB , Bw. Henry Bwogi mwenye suti nyeusi) akikabidhi msaada wa taulo za kike kwa uongozi wa Mkoa wa Simiyu, kwa ajili ya kambi za kitaaluma za kidato cha sita na kidato cha nne, ambao ulikabidhiwa katika Shule ya Sekondari ya Bariadi, tarehe 14 Aprili 2021.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Bariadi wakishangilia jambo wakati wa makabidhiano ya msaada wa vyakula na mahitaji mengine muhimu kwa wanafunzi wa kidato cha nne na cha sita walio katika kambi za kitaaluma katika shule zao, msaada ambao umetolewa na benki ya TPB tarehe 14 Aprili 2021.

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya TPB, Henry Bwogi,  Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw.  Ekwabi Mujungu na Afisa Elimu wa Mkoa, Mwl. Ernest Hinju wakiteta jambo mara baada ya Mkurugenzi huyo kukabidhi msaada wa vyakula, shajala na taulo za kike kwa wanafunzi wa kidato cha nne na kidato cha sita katika kambi za kitaaluma kwa shule za mkoa wa Simiyu, ambao ulikabidhiwa katika shule ya sekondari Bariadi, tarehe Aprili 14, 2021.
Baadhi ya vitu vilivyotolewa msaada na Benki ya TPB Bank kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi walio katika kambi za kitaaluma kwa kidato cha nne na cha sita, tarehe 14 Aprili 2021.
Baadhi ya vyakula vilivyotolewa msaada na Benki ya TPB Bank kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi walio katika kambi za kitaaluma kwa kidato cha nne na cha sita, tarehe 14 Aprili 2021.

Baadhi ya watendaji katika idara ya elimu mkoa wa Simiyu na Halmashauri ya Mji wa Bariadi  wakishuhudia makabidhiano ya msaada wa vyakula na mahitaji mengine muhimu kwa wanafunzi wa kidato cha nne na cha sita walio katika kambi za kitaaluma katika shule zao, msaada ambao umetolewa na benki ya TPB tarehe 14 Aprili 2021.









WASTAAFU WAWAASA WATUMISHI KUFANYA KAZI KWA KUJITUMA

        Watumishi waliostaafu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wamewaasa watumishi wa Umma kufanya kazi kwa bidii, uaminifu na kujituma ili waweze kutekeleza majukumu yao vizuri na kumaliza salama safari yao ya utumishi wa Umma. 

Rai hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti katika hafla ya kuwaaga iliyoandaliwa na Katibu Tawala wa Mkoa ambayo iliyofanyika Aprili 13, 2021 Mjini Bariadi.

“Nawasihi Watumishi wenzangu mfanye kazi kwa kujituma na muwe makini katika utendaji kazi wenu ili mtoe huduma inayotakiwa kwa watu mnaowahudumia,” alisema Dkt. Mugune Maeka ambaye alistaafu utumishi wa Umma akiwa Daktari msaidizi Mkuu

“Ninawashukuru kwa ushirikiano mlionionesha siku zote nilizofanya kazi nanyi, nawaomba watumishi mtimize wajibu wenu na muwe na subira mnapokutana na changamoto mbalimbali katika utumishi wao,” alisema Gamitwe Mahaza ambaye amestaafu utumishi wa Umma akiwa Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na uzalishaji 

“Ninawashukuru sana viongozi wetu kuona umuhimu wa kutuaga baada ya kukoma kwa utumishi wetu, niwaombe watumishi mfanye kazi kwa utii na uaminifu ili muweze kumaliza vema safari yenu ya Utumishi wa Umma,” alisema Joseph Milando ambaye amestaafu watumishi wa umma akiwa Mlinzi.

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimali watu, Bw. Ekwabi Mujungu amewapongeza wastaafu hao kwa utumishi wao uliotukuka kwa kuwa wakati wakiwa watumishi hawajawahi kuwa rekodi yoyote ya utovu wa nidhamu wala tuhuma zozote na kuwataka watumishi wengine kuiga mfano wao. 

Naye Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Donatus Weginah amewashukuru wastaafu hao kwa kuwa na mchango mkubwa katika kufikia ndoto ya mkoa huku akiwapongeza kwa kuwa watumishi wa mfano wenye utumishi uliotukuka. 

Wastaafu hao ni pamoja na Bw. Rauden Mwamwaja ambaye amekuwa mtumishi wa Umma kwa miaka 38 amestaafu akiwa dereva mwandamizi, Dkt. Mugune Maeka amekuwa mtumishi wa Umma kwa miaka 37 amestaafu akiwa Daktari Mkuu msaidizi, Dkt. Gamitwe Mahaza ametumikia Umma kwa miaka 36 amestaafu akiwa Katibu Tawala msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji, Bw. Joseph Milando ametumika miaka 21 kama mlinzi na Bw. Leonard Malulu ambaye amefanya kazi kwa miaka 34 na amestaafu akiwa Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi. 

Katika hafla hiyo kila mstaafu alikabidhiwa cheti cha utumishi uliotukuka pamoja na fedha taslimu shilingi milioni moja (1,000,000/=), zawadi ambazo zimetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa kwa lengo la kuwapongeza na kutambua mchango wao wakati wa utumishi wao.

MWISHO

Bw. Rauden Mwamwaja (kulia) ambaye amekuwa mtumishi wa Umma kwa miaka 38 amestaafu akiwa dereva mwandamizi, akipokea cheti cha utumishi uliotukuka na zawadi ya shilingi 1,000,000/= kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah katika hafla ya kuwapongeza wastaafu, Aprili 13, Mjini Bariadi.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Donatus Weginah akizungumza na watumishi katika hafla ya kuwaaga wastaafu iliyofanyika Aprili 13, 2021 Mjini Bariadi.

Bw. Joseph Milando ametumika miaka 21 kama mlinzi (wa pili kulia) aakipokea cheti cha utumishi uliotukuka na zawadi ya shilingi 1,000,000/= kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah (wa pili kushoto) katika hafla ya kuwapongeza wastaafu, Aprili 13, Mjini Bariadi.

Dkt. Mugune Maeka (katikati) ambaye amekuwa mtumishi wa Umma kwa miaka 37 amestaafu akiwa Daktari Mkuu msaidizi, akipokea  zawadi ya shilingi 1,000,000/= kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah katika hafla ya kuwapongeza wastaafu, Aprili 13, Mjini Bariadi.

Dkt. Gamitwe Mahaza(wa pili kushoto) ambaye  ametumikia Umma kwa miaka 36 amestaafu akiwa Katibu Tawala msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji, akipokea  zawadi ya shilingi 1,000,000/= kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah katika hafla ya kuwapongeza wastaafu, Aprili 13, Mjini Bariadi.

Bw. Leonard Malulu ambaye amefanya kazi kwa miaka 34 na amestaafu akiwa Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi, akipokea cheti cha utumishi uliotukuka na zawadi ya shilingi 1,000,000/= kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah katika hafla ya kuwapongeza wastaafu, Aprili 13, Mjini Bariadi.

Bw. Leonard Malulu ambaye amefanya kazi kwa miaka 34 na amestaafu akiwa Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi, akipokea cheti cha utumishi uliotukuka na zawadi ya shilingi 1,000,000/= kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah katika hafla ya kuwapongeza wastaafu, Aprili 13, Mjini Bariadi.

Bw. Leonard Malulu ambaye amefanya kazi kwa miaka 34 na amestaafu akiwa Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi, akipokea cheti cha utumishi uliotukuka na zawadi ya shilingi 1,000,000/= kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah katika hafla ya kuwapongeza wastaafu, Aprili 13, Mjini Bariadi.

Bw. Joseph Milando ametumika miaka 21 kama mlinzi(Mstaafu) aliyesimama, akizungumza katika katika hafla ya kuwapongeza wastaafu, Aprili 13, Mjini Bariadi.
Baadhi ya watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakiwa katika hafla ya kuwapongeza wastaafu, Aprili 13, Mjini Bariadi

TAZAMA PICHA MBALIMBALI KATIKA HAFLA YA KUWAPONGEZA WASTAAFU ILIYOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA OFISI YA MKUU WA MKOA, APRILI 13, 2021 MJINI BARIADI.



















Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!