SEKTA YA VIWANDA,
BIASHARA NA UWEKEZAJI MKOA WA SIMIYU
Sekta
ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Simiyu inashughulika na shughuli
mbalimbali zinazohusu Viwanda, Biashara, Masoko na Uwekezaji kwa kuzingatia
Sera ya Taifa ya Biashara, Sera ya Taifa ya Uwekezaji, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mpango wa
Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2011/12-2015/16, Mkakati wa Kupunguza na
Kuondoa Umasikini Awamu ya Pili (MKUKUTA II) na Sera ya Maendeleo Endelevu ya
Viwanda 1996-2020.
Shughuli
zinazofanywa ni kusimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa kuweza kufanikisha Sera,
Sheria na Mipango mbalimbali ya kitaifa, kusimamia utekelezaji wa Sheria za
Biashara na Viwanda, Kutoa ushauri wa kibiashara kwa wadau mbalimbali, Kuratibu
shughuli za usajili wa Leseni za Biashara, Kusimamia mwenendo wa Masoko,
Kuhamasisha shughuli za Wajasiriamali, Biashara Ndogo, Kati na Viwanda Vidogo
(SME’s), Kuhamasisha na kuvutia Uwekezaji katika maeneo ya Kilimo, Madini,
Utalii na Viwanda hususani viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na
mifugo.
1.
VIWANDA
Idadi ya Viwanda vilivyopo
katika Mkoa wa Simiyu
Mkoa
wa Simiyu una takribani ya viwanda 14 ambavyo vingi vinajishughulisha na
uchambuzi wa Pamba ghafi na usindikaji wa mafuta ya pamba mbegu. Pia kuna viwanda
vidogo (mashine za usindikaji mazao) zaidi ya 1,021 vinavyojishughulisha na
usindikaji wa mafuta yatokanayo na zao la Alizeti, kukoboa na kusaga mazao ya mpunga na mahindi. Ifuatayo ni orodha ya idadi ya
viwanda vya kati na vidogo vilivyopo Mkoani Simiyu.
Idadi
ya Viwanda
IDADI YA VIWANDA VYA
KATI NA VIWANDA VIDOGO MKOANI SIMIYU
|
||||||
Na.
|
HALMASHAURI
|
VIWANDA VYA KATI
|
VIWANDA VIDOGO
|
|||
Aina ya
uzalishaji
|
Aina ya
uzalishaji/usindikaji
|
|||||
Pamba ghafi &
mafuta
|
Mpunga
|
Mahindi
|
Mafuta
|
Jumla
|
||
1
|
MASWA DC
|
6
|
123
|
73
|
18
|
220
|
2
|
BUSEGA DC
|
3
|
70
|
165
|
0
|
238
|
3
|
ITILIMA DC
|
0
|
44
|
44
|
23
|
111
|
4
|
MEATU DC
|
1
|
20
|
60
|
13
|
94
|
5
|
BARIADI DC
|
1
|
71
|
199
|
4
|
275
|
6
|
BARIADI TC
|
3
|
31
|
56
|
7
|
97
|
JUMLA
|
14
|
359
|
597
|
65
|
1035
|
Chanzo:
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa (2016)
BIASHARA NA
MASOKO
UTARATIBU WA KUTOA LESENI YA BIASHARA
Leseni ya Biashara
Hiki ni kibali maalum cha Serikali
kinachotolewa kwa mfanyabiashara yeyote anapotaka kufanya biashara hapa nchini.
Sheria ya Leseni za Biashara Na. 25 ya 1972 – Kifungu cha 3(a) kimeweka bayana
kuwa, Kibali hicho maalumu kinaitwa Leseni ya Biashara. Kwa hiyo basi, kufanya
biashara yoyote bila kuwa na kibali hiki ni kosa la jinai.
Ili Mwombaji Apate Leseni Ya Biashara Anapaswa Kumbatanisha
Nyaraka Zifuatazo:
- Nakala ya hati ya kuandikisha jina la Biashara au Kampuni (Photocopy of Certificate of Incorporation or Registration & Extract);
- “Memorandum, and Articles of Association” ambazo zitaonyesha kuwa Kampuni imeruhusiwa kisheria kufanya biashara inayoombwa, pamoja na majina ya wamiliki wa kampuni, hisa zao na utaifa wao;
- Uthibitisho wa uraia kwa kuwasilisha, nakala ya hati ya kusafiri nje ya nchi ya Tanzania au hati ya kusafiri katika nchi za Afrika Mashariki, cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo (Affidavit) kuonyesha kuwa ni Mtanzania, na kama mgeni alete hati ya kuishi nchini daraja la kwanza (Residence Permit Class A).
- Endapo wenye hisa wote wapo nje ya nchi itabidi maombi yaambatane na hati ya kiwakili (Power of Attorney) ya kumpa mamlaka raia wa Tanzania, raia wa kigeni mwenye hati ya kuishi nchini daraja “A” au hati ya kufanya kazi nchini daraja “B” zinazoainisha kuwa anasimamia kampuni husika.
- Nakala ya ushahidi wa maandishi kuwa ana mahali pa kufanyia biashara (lease agreement, Title deed, Certificate of occupancy, e.t.c);
- Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi (Tax Payer Identification Number - TIN).
- . Hati ya uthibitisho wa ulipaji kodi (Tax Clearance Certificate)
Utaratibu Wa Kupata Leseni:
- Mamlaka za Serikali za Mitaa(Halmashauri) zinahusika na utoaji wa Leseni za Biashara ambazo zinatambulika kama Leseni za Biashara za kundi B(Makundi yameainishwa katika Sheria ya Fedha na. 2 ya mwaka 2014). Ili kupata Leseni inatakiwa ufike Halmashauri ambayo unataka kufanyia biashara yako na kuwasilisha maombi yako pamoja na kupata maelekezo mengine ya taratibu za usajili wa Leseni ya Biashara.
- Jaza fomu ya maombi ya Leseni (TFN 211 ya 2004)
- Ambatisha nyaraka kama ilivyoainishwa hapo juu kwa ajili ya ukaguzi (assessment) na kujulishwa kiasi cha ada cha kulipia;
- Kwa biashara za Kundi A (Sheria ya Fedha na. 2 ya mwaka 2014), utapata maelekezo kutoka kwa Afisa Biashara aliyepo eneo lako na baada ya maombi yako kukubaliwa malipo yafanyike kupitia Benki ya CRDB mahali popote kwa kutumia Akaunti Namba 0150413356300; Jina Revenue Collection Trading Licence – MIT;
- Kisha utafika Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ambapo utawasilisha “pay in slip” ya Benki Barua na Fomu(TFN 211 ya 2004) kutoka katika Halmashauri yako ili kupata risiti halali ya Serikali na Leseni ya Biashara;
USAJILI
WA MAKAMPUNI
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
inatoa ushauri wa usajili wa Majina ya Biashara na Makampuni kwa kushirikiana
na Taasisi ya Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA). Wananchi wote mnakaribishwa
kupata ushauri wa usajili wa majina na makampuni ili muweze kuwa na biashara
zinazotambulika kisheria ambayo itakuwezesha kupata masoko ya Kitaifa na Kimataifa
katika Bidhaa na Huduma.Pia unaweza kwenda kwenda moja kwa moja kwenye wavuti
ya BRELA kwa ajili ya kusajili Majina ya Biashara na Makampuni www.brela.go.tz
MASOKO
Mkoa
wa Simiyu una masoko ya kila siku ya bidhaa katika kila Halmashauri, vilevile kuna
masoko ya minada na magurio ipatayo 16 ambayo huendesha biashara ya uuzaji wa
mifugo mbalimbali hasa ng’ombe, mbuzi na kondoo. Pia katika minada hiyo kuna
magurio ambayo wafanyabiashara na wachuuzi huuza bidhaa na mazao mbalimbali.
Jedwali
5: Orodha ya Masoko ya Minada na Magurio
NO.
|
HALMASHAURI
|
JINA LA MNADA
|
SIKU YA MNADA
KWA WIKI
|
1.
|
BARIADI
|
Dutwa
|
Alhamisi
|
2.
|
BARIADI
MJI
|
Bariadi
Mji
|
Jumanne
|
3.
|
BUSEGA
|
Nyang’hange
|
Jumapili
|
Mwasamba
|
Jumamosi
|
||
4.
|
ITILIMA
|
Migato
|
Jumapili
|
Laini
|
Jumatatu
|
||
5.
|
MASWA
|
Lalago
|
Jumatatu
|
Malampaka
|
Jumatano
|
||
Jija
|
Alhamisi
|
||
Senani
|
Jumamosi
|
||
Nyalikungu
|
Jumapili
|
||
6.
|
MEATU
|
Bukundi
|
Jumatano
|
Mwanhunzi
|
Jumapili
|
||
Sanga
Itinje
|
Jumanne
|
||
Tindabulige
|
Alhamisi
|
||
Mwankali(Usiulize)
|
Jumatatu
|
Chanzo:
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa (2016)
HUDUMA ZA FEDHA NA MAWASILIANO
Huduma za Fedha na
Mawasiliano katika Mkoa zinaongezeka kwa kasi na uhitaji wa huduma hizo ni
mkubwa kutoka na ukuaji wa shughuli za kiuchumi na idadi ya wahitaji kuongezeka
hivyo Mkoa una watoa huduma za fedha na
mawsiliano kama wafuatao;
Huduma za Fedha na Mawasiliano
Na.
|
BENKI
|
HUDUMA
ZA MIKOPO
|
MAWASILIANO
|
1.
|
CRDB
|
PLATNUM CREDITS
|
AIRTEL
|
2.
|
NMB
|
BAYPORT CREDITS
|
MPESA
|
3.
|
POSTA
|
SACCOS
|
TIGO
|
4.
|
HALOTEL
|
Chanzo:
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa (2016)
UWEKEZAJI
Mkoa wa Simiyu
umejaliwa maliasili nyingi ambazo zinatoa fursa mbalimbali za uwekezaji, fursa
hizi zinapatikana katika maeneo ya maliasili na utalii, kilimo, mifugo, madini
na uvuvi. Pia kuna miundombinu na maeneo yaliyotengwa kwaajili ya shughuli za sekta
ya uwekezaji kama ifuatavyo:-
a)
Barabara: Mkoa unazo barabara za lami,
changarawe na udongo zinazopitika mwaka mzima, Barabara za lami ni jumla ya
kilomita 72 ambazo zinaunganisha Mkoa na barabara ya Mwanza-Musoma na kilometa
849.3 za changarawe.
b)
Reli: Mkoa una huduma za reli
Malampaka wilyani Maswa, Usafirishaji wa abiria na mizigo unafanyika katika
kituo cha Malampaka.
c)
Maeneo
ya Viwanda:- Mkoa una maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda katika kila
wilaya, pia eneo la ukubwa wa hekta 2000 zimebainishwa kwa ajili ya uwekezaji
katika Ukanda wa Usafirishaji Bidhaa Nje
(EPZ) katika wilaya ya Bariadi.
Pakua(download) nyaraka, Fomu na taarifa mbalimbali
- Fomu ya Maombi ya Leseni ya Biashara
- Sheria ya Leseni za Biashara na. 25 ya 1972
- Sheria ya Fedha Na. 2 ya 2014
- Sheria ya Makampuni ya 2002
- Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 1997
- Muongozo wa Kodi(Tax Guide)
- Fursa za uwekezaji Tanzania
- Mwongozo wa Uwekezaji Tanzania
- Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Simiyu
Tovuti Muhimu za Sekta ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
Tovuti ina maelezo yenye kujitosheleza kuhusu uwekezaji ndani ya mkoa wa Simiyu. Kama TRA hawajafungua ofisi ya mkoa basi juhudi zifanyike ofisi hiyo iweze kufunguliwa ili kurahisisha huduma kwa wafanya biashara na wananchi kwa ujumla.
ReplyDelete