Saturday, June 15, 2019

SIMIYU ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WALEMAVU KUHAKIKISHA WANAPATA HUDUMA KWA WAKATI: DC KISWAGA

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga amesema Serikali mkoani Simiyu itaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na watu wenye ulemavu wa makundi yote  bila kubagua na kuhakikisha wanapata huduma kwa wakati katika taasisi za Serikali wanapoenda kupata huduma.


Kiswaga ameyasema hayo Juni 13, 2019 wakati wa alipofungua kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi Mkoa wa Simiyu, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, kilichofanyika Mjini Bariadi.

Amesema watu wenye ulemavu wana haki sawa na watu wengine hivyo akatoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na maeneo mengine ya kutoa huduma za jamii mkoani Simiyu kufanya utaratibu wa kuweka wataalam maalum wenye uelewa wa lugha ya alama ili kuondoa changamoto ya mawasiliano kwa watu wenye ulemavu hususani viziwi.

“Vyombo vya ulinzi na usalama vihakikishe vina mtu au watu kwa ajili ya kuwasaidia viziwi kuondoa changamoto ya mawasiliano pamoja na watu wenye ulemavu kwa ujumla wanaohitaji huduma, si lazima kuajiri kwa sasa kwa kuwa suala la ajira linaweza kuchukua muda; lakini wahakikishe wana mtu wa kutoa msaada viziwi wapate huduma” alisema Kiswaga.

Aidha, Kiswaga amesisitiza umuhimu wa kutoa elimu kwa viziwi kuhusu maeneo yaliyozuiwa kama vile katika vyombo vya ulinzi (majeshi) na kushauri kuwa ikiwa wanapaswa kwenda katika maeneo hayo waombe msaada kwa watu wenye uwezo wa kuzungumza ili kuepuka watu hao kuonekana kuwa wamevunja sheria kwa kukusudia kwenda maeneo hayo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania(CHAVITA) Mkoa wa Simiyu, Mhandi Zephania amesema viziwi wanakabiliwa na changamoto ya mawasiliano wanapoenda kupata huduma mbalimbali hivyo chama hicho kinaendelea kutoa elimu ya lugha ya alama kwa watumishi wa maeneo mbalimbali ya kutolea huduma ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Naye Mkalimani wa lugha ya alama Bw. Jonathan Livingstone amesema Wizara ya Elimu imekubali kupokea jukumu la kusanifisha lugha ya alama iingizwe katika mitaala ifundishwe katika shule za msingi, sekondari na vyuo.

Katika hatua nyingine Kamanda wa Wilaya ya Maswa, Jonas Nyaoga amesema Jeshi la polisi limejipanga kuwahudumia viziwi kwa namna ambayo wakiwa wanahitaji huduma wanasaidiwa kwa kuhakikisha kuwa kila wanapowahoji viziwi wanatafuta watu wanaofahamu lugha ya alama ili waweze kuwatafsiria.

Kikao cha kujadili uboreshaji wa huduma za jamii kwa viziwi mkoani Simiyu kilijumuisha viongozi wa Chama cha Viziwi(CHAVITA) Mkoa wa Simiyu, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya zote tano za Mkoa wa Simiyu.
MWISHO
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifungua kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anthony Mtaka, kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania(CHAVITA) Mkoa wa Simiyu, Bw. Mhandi Zephania akitoa taarifa ya Chama hicho katika kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.
Mkalimani wa lugha ya alama Jonathan Livingstone akifafanua jambo katika katika kikao cha cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi
Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Maswa, akichangia hoja katika kikao cha cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.
:- Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (wa tano kushoto mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi mara baada ya kufunga kikao hicho.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bariadi, Bibi. Veronica Kinyemi, akichangia hoja katika kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi wakifuatilia hoja mbalimbali katika kikao hicho.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali Mkoani Simiyu na baadhi ya viziwi Mkoani Simiyu wakimsikiliza Bw. Jonathan Livingstone (mkalimani wa lugha ya alama) wakati akiwasilisha taarifa katika kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.


Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani akichangia hoja katika kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya Viongozi wa Serikali Mkoani Simiyu na baadhi ya viziwi Mkoani Simiyu wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyowasilishwa katika kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akiagana na Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania(CHAVITA) Mkoa wa Simiyu, Bw. Mhandi Zephania mara baada ya kufunga kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.

Thursday, June 13, 2019

NIDHAMU YATAJWA KUWA MSINGI WA MAFANIKIO KATIKA MICHEZO NA ELIMU SIMIYU


Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu amewataka wanafunzi walimu na maafisa elimu walio katika kambi ya Michezo ya UMITASHUMTA Ngazi ya mkoa kudumisha nidhamu wakati wote watakapokuwa katika kambi hiyo ili Mkoa uweze kufanya vizuri katika michezo na elimu kwa ujumla.

Mujungu ameyasema hayo Juni 12, 2019 wakati akifungua Mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, ambayo kwa mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu “MICHEZO NA SANAA KWA ELIMU BORA PIA NI AJIRA”.

“Ili tuweze kufanya vizuri katika michezo na Elimu kwa ujumla napenda kusisitiza nidhamu ya usimamizi wakati wa mashindano, kambi na ngazi ya Taifa; ni lazima kuwe na nidhamu binafsi kwenu ninyi wachezaji na wasimamizi wanaowasimamia, kama hakuna nidhamu tusitarajie matokeo mazuri” alisema Mujungu.

Aidha, Mujungu ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani hapa kuwawezesha Walimu wa michezo kupata mafunzo ili waweze kujua vema sheria za michezo mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi kufahamu michezo hiyo na kuamua michezo hiyo kwa haki.

Katika hatua nyingine ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya michezo ikiwa ni pamoja na upungufu wa miundombinu ya viwanja, walimu wa michezo na ratiba ya michezo kutofuatwa.

Awali akitoa taarifa ya mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa mwaka 2019, Kaimu Afisa Elimu wa mkoa, Mwl. Onesmo Simime amesema mashindano hayo yatashirikisha michezo ya aina sita ambayo ni riadha, mpira wa miguu, mpira wa wavu, mpira wa mikono, mpira wa pete(wavulana na wasichana kwa michezo yote mitano) na fani za ndani.

Kwa upande wake Kaimu Afisa michezo wa Mkoa, Bw. Charles Maganga amesema kupitia mashindano haya ya UMITASHUMTA mwaka 2019 Walimu kwa kushirikiana na Maafisa Michezo waliopo kambini watahakikisha wanachagua wachezaji wazuri watakaounda timu ya Mkoa yenye ushindani na matarajio yao ni kufanya vizuri katika mashindano ya Kitaifa.

Naye mwanamichezo (mwanafunzi) Jeremia Boniface Jeremia kutoka Halamshauri ya Wilaya ya Bariadi akizungumza kwa niaba ya wenzake amesema matarajio yao ni Mkoa wa Simiyu kufanya vizuri kwa kuwa wameandaliwa vizuri na kaahidi kuwa watakuwa na nidhamu wakati wote wa mashindano hayo.
MWISHO
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu akizungumza na wanafunzi wa shule za Msingi walio katika Kambi ya Mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa  ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Kaimu Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo Simime akitoa taarifa ya mashindano ya UMITASHUMTA mwaka 2019 ambayo yanayoendelea  katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Baadhi ya wachezaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Maswa wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa  ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji wa Mpira wa Miguu kutoka Halmashauri ya Mji wa  Bariadi na Halmashauri ya Wilaya ya Meatu wakiwa katika mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa ambayo yanaendelea katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.

Baadhi ya wachezaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi  wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa  ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi  wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa  ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa  ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Busega wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa  ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Meatu wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa  ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji kutoka Halmashauri ya Mji wa Bariadi wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa  ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Itilima wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa  ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya Maafisa Elimu na Michezo mkoani Simiyu, wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Mashindano ya UMITASHUMTA mwaka 2019 ambayo yanayoendelea  katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu(hayupo pichani).


WAZIRI MKUU APONGEZA SIMIYU KUJENGA SHULE YA MICHEZO

Waziri Mkuu Jamhuri ya Muungan, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb), ameupongeza Mkoa wa Simiyu kwa kuwa mmoja kati ya Mikoa ya mfano katika kutekeleza agizo lake la mwaka jana alilolitoa kupitia michezo hiyo la kuanzishwa kwa shule maalumu za michezo.


Waziri Mkuu ameyasema hayo Juni 10, 2019 wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya UMISSETA Kitaifa katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mjini Mtwara.

Mkoa wa Simiyu umejenga Shule ya Sekondari itakayokuwa kituo cha kukuza vipaji vya wanafunzi katika michezo. “Naagiza mwakani wanafunzi wote walioonesha vipaji katika michezo watakaofaulu Mtihani wa Elimu ya Msingi wapangwe katika shule hiyo ili wakakuze vipaji vyao.”

                             Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. , Kassim Majaliwa 
Wanamichezo kutoka Mkoa wa Simiyu wakiingia kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona kushiriki katika Ufunguzi wa Michezo ya UMISETA uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Juni 10, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ( wa tatu kulia) akiwa nabaadhi ya wataalam wakiangalia baadhi ya mawe yaliyotolewa katika eneo unapojengwa uwanja wa mpira wa miguu katika Shule ya Sekondari Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  na baadhi ya wananchi wa Kata ya Malambo  wakishuhudia zoezi la kutoa mawe katika eneo unapojengwa uwanja wa mpira wa miguu katika Shule ya Sekondari Simiyu.


Tuesday, June 4, 2019

SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA KUMBUSHENI VIONGOZI, WATUMISHI KUTIMIZA WAJIBU WAO: RC MTAKA


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema ni vema Sekreatarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma iendelee kuwakumbusha viongozi na watumishi wa umma nchini kutimiza wajibu wao ili kuweza kufikia malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  na Serikali.

Mtaka ameyasema hayo Juni 03, 2019 Mjini Bariadi, wakati akifungua mafunzo kwa Viongozi wa Umma mkoani Simiyu, ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora.

Amesema ikiwa kila mmoja katika Utumishi wa Umma atatimiza wajibu wake na kwa kuzingatia mgawanyo wa uongozi ulivyo ndani ya nchi; jamii na nchi kwa ujumla wake itaweza kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali katika nyanja mbalimbali kwa wakati.

“Ni vizuri Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ikiendelea kuwakumbusha watu wote wanaofanya kazi zinazoihusu jamii kutimiza wajibu wao, kila mmoja akitimiza wajibu wake yapo mambo mengi sana sisi kama jamii, mkoa na kwa namna ambavyo uongozi na mgawanyiko wa .nchi yetu ulivyo tutafikia malengo yetu kwa wakati” alisema Mtaka.

Aidha, ametoa wito kwa viongozi wa Umma ambao ni watoa maamuzi katika maeneo yao ya kazi kuwa makini katika kutoa maamuzi na wahakikishe wanafanya maamuzi kwa wakati.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Msaidizi Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Gerald Mwaitebele amesema viongozi wa Umma wanapaswa kutoa maamuzi kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyowekwa ili kutoiletea hasara Serikali.

Ameongeza kuwa Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma itaendelea kutoa elimu kwa viongozi wa umma juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi ya uadilifu katika uongozi na endapo ikitokea kiongozi yeyote atakengengeuka na kutofuata maadili sheria itachukua mkondo wake.

Kwa upande wake Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio ameshukuru Sekretarieti ya Maadili kwa kutoa mafunzo ya maadili  kwa viongozi wa Umma na akatoa wito kwa viongozi hao kuwa waadilifu, kutekeleza majukumu yao na kutojilimbikizia mali kinyume na taratibu na maadili ya viongozi wa Umma.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Bahame Kaliwa ametoa wito kwa Sekretarieti ya Maadili kwa viongozi wa Umma kutoa elimu ya maadili kila viongozi wapya wanapoteuliwa au kuchaguliwa, hususani madiwani wanapochaguliwa na kuunda Mabaraza mapya ya madiwani ili wajue misingiya uadilifu inayopaswa kuwaongoza katika kazi zao
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi wa Umma mkoani humo, wakati akifungua mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Umma mkoani Simiyu wakifuatilia  mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili yao na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani humo, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi
Kaimu Katibu Msaidizi Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Gerald Mwaitebele, akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Afisa Maadili kutoka Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Onesmo Msalangi akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Umma mkoani Simiyu wakifuatilia  mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili yao na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.

Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio akichangia hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekitia wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo akichangia hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Menejimenti ya Serikali za Mitaa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Maganga Simon akichangia hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Makamu Mwenyekiti wa Halamashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Bahame Kaliwa akichangia hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Somanda, Mhe. Said Majaja akichangia hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Kaimu Katibu Msaidizi Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Gerald Mwaitebele, akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa umma mkoani humo, mara baada ya kufungua mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi hao , ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa umma mkoani humo, mara baada ya kufungua mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi hao , ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa umma mkoani humo, mara baada ya kufungua mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi hao , ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari mkoani humo( waliosimama, kulia ni Afisa Habari Mkoa) , mara baada ya kufungua mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma , ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi

Friday, May 31, 2019

RC MTAKA AWAHAKIKISHIA USHIRIKIANO WA SERIKALI WAUMINI, VIONGOZI WA MADHEHEBU YA DINI

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewahakikishia waumini na viongozi wa madhehebu ya dini mkoani hapa kuwa viongozi wa serikali wako pamoja nao na wataendelea kushirikiana na kila watakapo wahitaji .

Mtaka ameyasema hayo jana Mei 30, 2019 katika futari aliyoiandaa kwa waumini na viongozi wa madhehebu ya Kiislam katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi.

“Ndugu zangu waislam mliopo hapa naomba muamini kabisa kwamba viongozi wa mkoa na viongozi wote wa Serikali kwenye maeneo yetu  ndani ya mkoa wa Simiyu wako pamoja na ninyi; kwa jambo lolote, eneo lolote ambalo mngehitaji ushirikiano kwenye mkoa wetu sisi tuko tayari kuunga mkono” alisema Mtaka.

Aidha, ameshauri viongozi wa BAKWATA Mkoa wa Simiyu kuomba kuandaa tukio moja kubwa la Kitaifa kufanyika Mkoani Simiyu kama ambavyo yamekuwa yakifanyika katika mikoa mingine na akaahidi kushirikiana na viongozi hao endapo watakuwa tayari kuandaa tukio lolote.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito pia kwa viongozi wa Madhehebu ya Kiislam kutengeneza mazingira mazuri kwa vijana na kuwafundisha ikiwa ni njia moja wapo ya kuwaandaa kushiriki katika mashindano ya kuhifadhi Quran ili Mkoa wa Simiyu na nchi kwa ujumla iweze kuwakilishwa vema katika mashindano hayo.

Sambamba na hilo amewashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuiombea nchi, viongozi wake, kuombea amani, umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania ambapo amebainisha kuwa Serikali inatambua mchango wa Taasisi za dini katika nchi na kwa namna viongozi wa dini wanavyoshirikiana na Serikali katika masuala na mtukio mbalimbali.

Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mahamoud Kalokola amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa namna anavyoenzi waislam na akatoa wito kwa watu wengine kuiga mfano wake kwa kuwa kila anyefanya hivyo anapata thawabu yake kwa Mwenyezi Mungu.

Ameongeza kuwa tendo hilo la kufuturisha linawakusanya watu pamoja walio waislam na wasio waislam jambo ambalo linadumisha umoja, upendo, ushirikiano na mshikamano kwa wote bila kujali tofauti ya dini zao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amempongeza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambao nao watajipanga kufanya jambo hili ili nao waweze kupata baraka za Mwenyezi Mungu.

Huu umekuwa ni utaratibu kwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu, kuandaa furati kwa waumini viongozi wa madhehebu ya dini ya Kiisla, ambayo pia huwahusisha viongozi wengine wa chama na Serikali wakati wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akiteta jambo na Sheikh wa Mkoa wa Simiyu, Mahamoud Kalokola  mara baada ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi wengine jana Mei 30, 2019.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi mbalimbali walioshiriki katika futari aliyoindaa Mei 30, 2019.
Baadhi ya waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi mbalimbali walioshiriki katika futari aliyoandaliwa  na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili yao, Mei 30, 2019.
Baadhi ya waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi mbalimbali walioshiriki katika futari aliyoandaliwa  na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili yao, Mei 30, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi mbalimbali walioshiriki katika futari aliyoindaa kwa ajili yao, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili ya waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi wengine jana Mei 30, 2019.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga baada ya futari aliyoandaliwa  na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili ya waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi wengine jana Mei 30, 2019.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi mbalimbali walioshiriki katika futari aliyoindaa kwa ajili yao, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili ya waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi wengine jana Mei 30, 2019.
Baadhi ya waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi wa Chama na Serikali wakishiriki futari iliyoandaliwa kwa ajili ya na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka jana Mei 30, 2019.
Baadhi ya waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi wa Chama na Serikali wakishiriki futari iliyoandaliwa kwa ajili ya na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka jana Mei 30, 2019.
Mwakilishi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu akizungumza na waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi mbalimbali walioshiriki katika futari aliyoindaa kwa ajili yao, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili ya waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi wengine jana Mei 30, 2019.

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!