Monday, October 29, 2018

WAZIRI MWIJAGE: SERIKALI INAENDELEA KUJENGA UCHUMI IMARA NA SHINDANI


Waziri wa viwanda,biashara na uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema serikali  inaendelea kujenga uchumi wa Kitaifa(jumuishi) ulio imara na wenye ushindani  kuelekea uchumi wa kati ifikapo 2025  kwa kuanzia uzalishaji mashambani hadi sokoni.

Hayo ameyasema wakati akihitimisha Maonesho ya (SIDO) Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, yakiwa na Kauli Mbiu: “PAMOJA TUJENGE VIWANDA KUFIKIA UCHUMI WA KATI”

Mhe. Mwijage amezitaja baadhi ya sifa za uchumi wa Kitaifa (Jumuishi) kuwa ni pamoja na Kipato cha wastani kwa Mtanzania kufikia dola 3000 kwa mwaka ifikapo 2025, Watanzania kuwa na maisha mazuri, watu kuwa na elimu na wepewi kwa kujifunza, pamoja na kuwa na uchumi imara ulio shindani.

“Tunataka mwaka 2025 tuwe na uchumi imara na shindani lakini tuendelee kudumisha amani na msihikamano; njia rahisi ya kufikia mahali mbapo kipato cha wastani cha Mtanzania kuwa dola 3000 kwa mwaka ni kupitia uchumi wa viwanda na uchumi wa viwanda ni zaidi ya viwanda, uchumi wa viwanda unaanzia shambani hadi sokoni” alisema.

Katika hatua nyingine alitoa wito kwa Watanzania kulinda viwanda vya ndani hapa nchini kwa kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Mhe. Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema  Mapinduzi ya viwanda yanatokana na Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO), hivyo ni vema  wizara ya viwanda ,biashara na uwekezaji ikaliwezesha shirika la kuhudumia  viwanda vidogo ili kutekeleza azma ya Tanzania ya viwanda.

Akizungumzia maonesho ya Viwanda vidogo Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Prof. Silvester Mpanduji, amesema jumla ya wajasiriamali 515 kutoka mikoa 23 nchini na nchi jirani za Uganda na Burundi, wameshiriki manesho haya na kupata fursa ya kuonesha bidhaa wanazozalisha na kubadilisha uzoefu katika masuala mbalimbali.

Aidha, amesema kupitia maonesho hayo mashine za kuongeza thamani katika mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na misitu zenye thamani ya zaidi ya shilingi 800 zimenunuliwa na nyingine kuwekewa ahadi ya kununuliwa.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa UNDP anayeshughulikia miradi Amoni Manyama ameahidi kuwa Shirika hilo liko tayari kushirikiana na Serikali hapa nchini katika Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda kwa kutoa msaada wa kifedha na utaalam wa kuchambua miradi ya viwanda katika Mkoa wa Simiyu na mikoa mingine pia.

Maonesho ya Viwanda Vidogo SIDO Kitaifa yaliyofanyika kwa muda wa siku sita katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu yalifunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Oktoba 23, 2018, pamoja na wajasirimali 515 kushiriki takribani taasisi za Umma na Binafsi 24 zimeshiriki maonesho haya.
MWISHO 

 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akiangalia bidhaa za baadhi ya wajasiriamali mara baada ya kutembelea mabanda yao katika Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi,kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.


PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI: https://simiyuregion.blogspot.com/2018/10/mwijage-viwanda-vidogo-biashara-ndogo.html

MWIJAGE: VIWANDA VIDOGO, BIASHARA NDOGO VINA MCHANGO MKUBWA KATIKA UCHUMI, MAENDELEO, USTAWI WA NCHI


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema viwanda vidogo na vya kati vina mchango mkubwa katika uchumi, maendeleo na  ustawi wa nchi yoyote, kwa kuwa vinatoa ajira kwa watu wengi ikilinganishwa na viwanda vikubwa hivyo havipashwi kubezwa kwa namna yoyote.

Mhe. Mwijage ameyasema hayo Oktoba 28, 2018 wakati akihitimisha Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa yaliyofanyika Kitaifa kwa mara ya kwanza katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 23.

“ Najua kuna watu wanapenda kubeza lakini napenda niwaeleze nafasi ya viwanda na biashara ndogo katika uchumi, maendeleo na ustawi ya nchi yoyote, Sisi Tanzania tangu uhuru mpaka leo tuna viwanda 54,000 lakini asilimia 99 ni viwanda vidogo, vidogo sana na vya kati; sisi siyo kilema kwenye viwanda nchi zote zipo hivyo, viwanda vyenye tija  na vinavyoajiri watu wengi ni viwanda vidogo, vidogo sana na vya kati” alisema Mwijage.

Amesema pamoja na viwanda vidogo na vidogo sana kuwa na tija katika uchumi wa nchi viwanda hivyo pia ni shule na vinaweza kumilikiwa kirahisi huku akisisitiza kuwa lengo la Serikali ni kujenga uchumi jumuishi ambao nji rahisi ya kuufikia ni kupitia uchumi wa viwanda.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO), Prof.Sylvester Mpanduji ametoa wito kwa Watanzania kuwa, ili waweze kushiriki katika Ujenzi wa Uchumi waViwanda hawana budi kuanza na viwanda vidogo ambavyo SIDO itakahakikisha vinakuwa endelevu.

Akizungumzia Maonesho ya Viwanda Vidogo Prof. Mpanduji amesema yamesaidia kuwaleta wajasiriamali pamoja kuonesha bidhaa zao na kubadilisha uzoefu katika teknolojia, usindikaji na masuala mengine yanayohusu bidhaa wanazozalisha kupitia viwanda vidogo na vya kati.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa huo umebeba ajenda ya Tanzania ya viwanda huku akibainisha kuwa  mwaka 2019 Simiyu imedhamiria Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli atakapotembelea mkoa huo afanye uzinduzi wa Falsafa ya Wilaya Moja Bidhaa Moja  kwa kufungua kiwanda katika kila wilaya.

Aidha, Mtaka amemhakikishia Waziri Mwijage kuwa Simiyu itaongeza uzalishaji wa malighafi ya viwanda hapa nchini mara mbili na kuomba wizara ya viwanda isaidie upatikanaji wa teknolojia za viwanda kuja nchini.

Akizungumzia dhamira ya kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika Ujenzi wa Uchumi wa viwanda Mkurugenzi Msaidizi wa UNDP anayeshughulikia miradi Amoni Manyama, amesema Shirika hilo liko tayari kushirikiana na Mkoa wa Simiyu na mikoa mingine nchini, katika nyanja ya kifedha na kitaalam kwa kufanya uchambuzi wa viwanda vinavyowezekana katika mikoa mbalimbali.

Maonesho ya Viwanda Vidogo ambayo yamefanyika Kitaifa kwa mara ya kwanza, chini ya kauli mbiu “PAMOJA TUJENGE VIWANDA KUFIKIA UCHUMI WA KATI” yameshirikisha wajasiriamali 515 kutoka mikoa 23 hapa nchini na nchi jirani za Burundi na Uganda, ambapo pia Mabalozi kutoka nchi za Nigeria na Angola walishiriki.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji  wa Mkoa huo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage wakati wa Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa  katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani humo,kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018(kulia) Balozi wa Nigeria nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Shahabi Issa Gada. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony  Mtaka akimkabidhi nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji  wa Mkoa huo Balozi wa Nigeria nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Shahabi Issa Gada wakati wa Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa  katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani humo,kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018(kulia) Balozi wa Nigeria nchini (kushoto) ni  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akizungumza na wajasiriamali mara baada ya kutembelea mabanda yao katika Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi,kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (mwenye tai) akiangalia baadhi ya mashine zilizoletwa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) katika Maonesho ya Viwanda Vidogo, wakati wa kilele cha maonesho hayo yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi, kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.
Viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (mwenye tai) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) wakiimba pamoja na Kwaya ya Walimu Bariadi, katika Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi, kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.
Kikundi cha Ngoma cha BASEKI kikitoa burudani katika Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi, kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera akiwasalimia wananchi wakati wa Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi, kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akiangalia bidhaa za baadhi ya wajasiriamali mara baada ya kutembelea mabanda yao katika Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi,kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.
Mkurugenzi wa Msaidizi wa UNDP anayeshughulikia miradi Amoni Manyama akizungumza namna Shirika hilo linavyofanya kazi na mkoa wa Simiyu, katika Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani humo katika Viwanja vya Nyakabindi,kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.
Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO)Prof. Elifas Tozo Bisanda wakiangalia jambo kwa makini, katika Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani humo katika Viwanja vya Nyakabindi,kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.
Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO)Prof. Elifas Tozo Bisanda wakiangalia jambo kwa makini, katika Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani humo katika Viwanja vya Nyakabindi,kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akiangalia bidhaa za baadhi ya wajasiriamali mara baada ya kutembelea mabanda yao katika Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi,kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia), katibu Tawala wa Mkoa(kushoto) wakimuongoza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage(katikati) kuelekea katika ukaguzi wa mabada ya maonesho kabla ya kuhitimisha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi,kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.
Balozi wa Nigeria nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Shahabi Issa Gada akipanda mti wa kumbukumbu mara baada ya kushiriki Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi,kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.
Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhe. Andrew Chenge (kulia) akisalimiana na Balozi wa Nigeria nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Shahabi Issa Gada, wakati wa Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi,kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akipanda mti wa kumbukumbu mara baada ya kuhitimisha  Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi,kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.


Saturday, October 27, 2018

NAIBU WAZIRI MABULA ASHAURI WIZARA YA VIWANDA KUANZISHA KLINIKI NGAZI YA KANDA KUWASAIDIA WAFANYABIASHARA


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula ameshauri Wizara ya Viwand, Biashara na Uwekezaji kuona namna ya kuwa na Kliniki za Biashara ngazi ya kanda ili kuwasaidia wafanyabiashara hususani wale wanaoanza, wajasiriamali wadogo na wasiojua taratibu za uendeshaji wa biashara zao kujua na kuwa wafanyabiashara wazuri.

Mhe.Mabula ameyasema hayo mara baada ya kutembelea banda la Maonesho la Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara(TanTrade) katika Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yanayoendelea katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.

Amesema amepongeza Wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji kubuni Kliniki ya biashara ambayo inachangia kuwandaa wafanyabiashara kufahamu wafanye nini kabla na baada ya kuanzisha biashara na kufanya biashara zao kwa kuzingata sheria, kanuni na taratibu za nchi hii

“Ili mtu awe huru kufanya biashara yake ni lazima zingatie sheria kanuni na taratibu za nchi hii, mtu anapokuja kwenye kliniki hii anaambiwa kabla ya kuanza anatakiwa apitie hatua zipi na aweke mazingira yapi, ili atambulike na TRA anapaswa afanye nini  na mambo mengine mengi na wakizingatia wanachoambiwa hapa hawahitaji kukimbizana na mgambo wa polisi”

“Ninashauri Wizara ya Viwanda ione namna ya kuwa na kliniki za biashara kikanda ili wafanyabiashara wanaoanza, wajasiriamali wadogo na wale wasiojua taratibu waweze kujua taratibu na wawe wafanyabiashara wazuri” alisema Mhe. Mabula.

Afisa Biashara Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara hapa nchini (TanTrade) Bi. Magdalena Shirima amesema hadi kufikia Oktoba 26, 2018 wajasiriamali zaidi ya 60 walioshiriki katika Maonesho ya SIDO Kitaifa wamehudhuria Kliniki hiyo kupata huduma.

Baadhi ya Wajasiriamali waliopata nafasi ya kushiriki na kupata huduma za ushauri wa kibiashara kupitia Kliniki hiyo wamesema imewasaidia kubadili mitazamo dhidi ya biashara zao na kufahamu mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uanzishaji wa biashara, namna ya kutangaza biashara zao na umuhimu wa kusajili biashara zao ili ziweze kutambulika kisheria.

Maonesho haya ya Viwanda Vidogo (SIDO) ni ya kwanza Kitaifa yakiwa na Kauli Mbiu “Pamoja Tujenge Viwanda Kufikia Uchumi wa Kati” ambayo yalianza Oktoba 23, 2018 yatahitimishwa Oktoba 28, 2018.
MWISHO
Naibu Waziri waNyumba na Maendeleo ya makazi, Mhe. Angelina Mabula akizungumza na Watumishi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) alipotembelea banda la Mamlaka hiyo katika Maonesho ya SIDO Kitaifa Oktoba 26, 2018  yanayoendelea katika  Viwanja vya Nyakabindi Simiyu, ambapo huduma za Kliniki ya Biashara zinatolewa. 

Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya makazi, Mhe. Angelina Mabula(wa pili kushoto) akiongozwa na viongozi wa Shirika la Kuhudumia viwanda Vidogo (SIDO) kuelekea katika kutembelea mabanda ya maonesho ya Maonesho ya SIDO Kitaifa Oktoba 26, 2018  yanayoendelea katika  Viwanja vya Nyakabindi Simiyu.

Naibu Waziri waNyumba na Maendeleo ya makazi, Mhe. Angelina Mabula akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la maonesho la Kiwanda cha Chaki Maswa Oktoba 26, 2016 wakati alipotembelea mabanda mbalimbali ya maonesho katika ya Maonesho ya SIDO Kitaifa Oktoba 26, 2018  yanayoendelea katika  Viwanja vya Nyakabindi Simiyu.
 Afisa kutoka Shirika la Viwango nchini (TBS) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri waNyumba na Maendeleo ya makazi, Mhe. Angelina Mabula mara baada ya kutembelea banda la maonesho la shirika hilo, wakati alipotembelea mabanda mbalimbali ya maonesho katika ya Maonesho ya SIDO Kitaifa Oktoba 26, 2018  yanayoendelea  katika  Viwanja vya Nyakabindi Simiyu.
Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula akipewa maelezo kuhusu mashine mbali za kuongeza thamani mazao mbalimbali wakati alipotembelea mabanda mbalimbali ya maonesho katika ya Maonesho ya SIDO Kitaifa Oktoba 26, 2018  yanayoendelea  katika  Viwanja vya Nyakabindi Simiyu.
Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula akiangalia baadhi ya bidhaa za ngozi zilizotengenezwa a wajasiriamali wadogo , wakati alipotembelea mabanda mbalimbali ya maonesho katika ya Maonesho ya SIDO Kitaifa Oktoba 26, 2018  yanayoendelea  katika  Viwanja vya Nyakabindi Simiyu.

NAIBU WAZIRI MABULA ATOA WITO WANANCHI SIMIYU KUCHANGAMKIA FURSA YA NYUMBA ZA SHIRIKA LA NYUMBA

Naibu waziri wa ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi Mhe.Angelina Mabula ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa SIMIYU kutumia fursa za nyumba za makazi zinazotarajiwa kujengwa katika eneo la Isanga Mjini Bariadi na Shirika la Nyumba la Taifa


Wito huo ameutoa mkoani Simiyu alipokutana na wadau mbalimbali katika kongamano la ujenzi wa nyumba za makazi mkoani Simiyu lililohudhuriwa na viongozi wa serikali mkoani humo wakiongozwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa mkoa wa Simiyu,wakuu wa wilaya wakurugenzi, makatibu tawala wilaya, wakuu wa idara na watumishi wa kada mbalimbali kutoka halmashauri zote, wafanyabiashara na viongozi wa vyama vya wafanyakazi lengo likiwa ni kuangalia aina ya nyumba zitakazojengwa na Wateja watarajiwa.

Mabula amesema azma ya wizara ya ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi ni kumwezesha kila mtanzania kunufaika na nyumba zinazojengwa na shirika hilo, huku akisisitiza Taasisi nyingine zinazohusika na uwekaji wa miundombinu muhimu kuanza utaratibu wa kuweka miundombinu hiyo ili kuwapunguzia gharama wanunuzi.

“ Tunatarajia taasisi zinazohusika ziwe zimeshaanza kupeleka huduma huko, wakati NHC wanaanza kujenga nyumba zao pale gharama itakuwa iko chini kwa sababu hivi vitu vingine vitakuwa vimewekwa na taasisi nyingine na kazi yao itakuwa ni kurudiisha fedha zao kupitia bili za umeme, maji”

“Awali nyumba za NHC zilikuwa zikilalamikiwa kuwa ni za gharama kubwa kutokana na wao kufanya kazi zote wao wenyewe, ujenzi wa nyumba na uwekaji wa miundombinu ya maji , umeme, barabara, viwanja vya michezo na huduma nyingine, lakini tunamshukuru Mhe. Rais alishatoa maelekezo kwa wizara na mamlaka husika kuhakikisha wanaweka miundombinu ya huduma zote muhimu mahali ambapo NHC wanajenga nyumba zao” alisema.

Wakitoa maoni yao baadhi ya wadau wametoa ushauri kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuona namna ya kujenga nyumba zenye gharama nafuu zaidi ili wananchi wengi hususani wale wenye kipato cha chini waweze kunufaika na mradi huu.

“Ninaiomba Serikali kuangalia upya gharama za nyumba za makazi zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) ili kuwawezesha watumishi na wananchi wengi kumudu gharama za kununua nyumba hizo kwa kuwa wengi ni wenye vipato vya chini, pia benki zinazowakopesha wananchi wanaonunua nyumba hizo zitoe mikopo kwa masharti ambayo hayatawaumiza wakopaji” alisema Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga.

“Ninashauri Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuona haja ya kuwa na mpango mkakati wa kuboresha makazi ya wakulima ambao wamejiunga na Vyama vya Ushirika vya Msingi(AMCOS) ili vyama hivyo, benki pamoja na NHC waje namna   kujenga nyumba zenye bei nafuu zaidi na kundi kubwa zaidi liweze kunufaika” alisema Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa kwa kuwa chachu ya Maendeleo ya makazi bora nchini, huku akibainisha kuwa Shirika hilo linaweza kuona namna ya kufanya kazi na Halmashauri mkoani humo katika kukabiliana na changamoto ya makazi kwa watumishi.

Wakizungumza katika Kongamano hilo Wawakilishi wa taasisi za fedha zikiwemo Benki za NMB, CRDB na Azania Bank  wamesema wamejipanga katika utoaji wa mikopo ya nyumba kwa wale walio tayari na wenye vigezo vinavyotakiwa.
MWISHO

Naibu waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Mhe. Angelina Mabula akizungumza na wadau mbalimbali katika Kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wadau mbalimbali katika Kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi.



Naibu waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Mhe. Angelina Mabula(kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka katika Kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.
Kutoka kushoto Kaimu Mkurugenzi Mauzo na Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)  Itandula Gambalagi, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka na Naibu waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Mhe. Angelina Mabula wakiteta jambo katika Kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Sagamiko akichangia hoja katika Kongamano lililohusu  ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa Bariadi, lililofanyika  Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.
Mshauri wa Jeshi la Akiba Mkoani Simiyu, akichangia hoja katika kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani akichangia hoja katika semina kuhusu ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa Bariadi, ambayo imefanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.
Baadhi ya viongozi na wadau mbalimmbali mkoani Simiyu wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, lililofanyika Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga  akichangia hoja katika Kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.
Mmoja wa Wafanyakazi wa Benki ya NMB akichangia hoja katika kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.
Meneja  wa  Benki ya NMB Bariadi  akichangia hoja katika kongamano lilohusu ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau  mbalimbali.
Mmoja wa Watumishi wa Benki ya CRDB akiwasilisha mada katika Kongamano lililohusu  ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.
Naibu waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Mhe. Angelina Mabula(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Mkoa wa Simiyu baada ya kufungua kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika hilo katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera  akichangia hoja katika kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.
Naibu waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Mhe. Angelina Mabula(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Wakuu wa Idara Mkoa wa Simiyu baada ya kufungua kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika hilo katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.
Naibu waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Mhe. Angelina Mabula(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Wakurugenzi, Makatibu Tawala wa Wilaya na Makatibu Tawala Wasaidizi Mkoa wa Simiyu, baada ya kufungua Kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika hilo katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.








Tuesday, October 23, 2018

WAZIRI MKUU MAJALIWA AITAKA SIDO KUPANUA WIGO KUWAFIKIA WAJASILIAMALI KUANZIA NGAZI YA CHINI


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika la viwanda vidogo nchini SIDO  kuweka mikakati ya kupanua wigo wa shughuli zake kwa kuanzisha vituo katika ngazi ya halmashauri za wilaya ili kuwafikia wajasiliamali wengi zaidi, kuwajengea uwezo, kuwapa miongozo bora ya namna ya kuendesha shughuli zao kwa tija na kuwaunganisha na taasisi za fedha  waweze kupata mikopo.

Waziri mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo katika ufunguzi wa maonesho ya SIDO Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu ambapo amesema umefika wakati kwa SIDO kutilia mkazo sekta ya viwanda na hivyo kuifanya jukwaa la kuwakutanisha wabunifu pia kuwapa fursa ya kuonyesha uwezo wao katika matumizi ya teknolojia rafiki na rahisi zitakazoharakisha maendeleo ya viwanda nchini.

Pia Waziri Mkuu Majaliwa amesema SIDO inapaswa kujielekeza katika kubuni mashine , mitambo na teknolojia rahisi zitakazotumika kuongeza thamani ya bidhaa na kusisitiza kuwa  kutokana na umuhimu wa sekta ya viwanda nchini katika kukuza ajira na kuongeza pato la taifa serikali itaendelea kuweka miundombinu wezeshi itakayoharakisha kasi ya ukuaji wa viwanda.

“ Bila shaka nyote mnafahamu tumedhamiria kufikia uchumi wa kati kufikia mwaka 2025, ninaamini tunao uwezo wa kulifikia lengo hili, sasa tunachotakiwa kufanya kuhakikisha halmashauri zetu zote zinatenga maeneo maalumu kwa ajili shughuli za viwanda kama mlivyofanya hapa Simiyu, lakini pia lazima mhakikishe mnawajengea uwezo wajasiliamali ili waweze kuingia katika soko la ushindani, alisisitiza Waziri Mkuu Majaliwa”
.
Waziri Mkuu Majaliwa  amewasisitiza SIDO waendelee kubuni mikakati itakayoleta mabadiliko katika sekta ya viwanda huku akiwataka wananchi kuthamini bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini ambazo tayari zimeonyesha kukidhi mahitaji ya soko.

Halikadhalika waziri Mkuu Majaliwa ameziagiza halmashauri za wilaya nchini kuendelea kutekeleza agizo la kutenga 10%  ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya mikopo ya wanaweke, vijana na walemavu huku  akiwasisitiza madiwani katika halmashauri zote nchini kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa agizo hilo.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa ameupongeza uongozi wa mkoa wa Simiyu kwa kujenga mahusiano mema na wananchi, viongozi  wa kisiasa pamoja na taasisi mbalimbali jambo ambalo amesema ni chachu ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii mkoani Simiyu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo(SIDO), Prof. Sylvester Mpanduji amesema Shirika hilo litaendelea kutoa mafunzo kwa wajasriamali ili kuwajengea uwezo zaidi, ambapo amebainisha kuwa katika mwaka wa fedha 2017/2018 SIDO imetoa mafunzo kwa wajasiriamali 16,900.

Aidha, Prof. Mpanduji ameishukuru Serikali kwa kutenga shilingi bilioni 29 katika mwaka wa fedha 2018/2019 ambazo zitasaidia kutatua changamoto mbalimbali za wajasiriamali ikiwemo upatikanaji wa mashine mpya zitakazotumika katika vituo vya SIDO vya kuendeleza viwanda, kukopesha wajasiriamali mitaji na kujenga miuondombinu mingi ya viwanda katika sehemu hapa nchini.

Naye Mkuu wa Mkoa  wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemhakikishia Waziri mkuu  kuwa  Mkoa huo utahakikisha unaendelea kutekeleza maagizo ya serikali ikiwemo agenda ya kitaifa ya Uchumi wa Viwanda kupitia Falsafa ya Wilaya Moja Bidhaa Moja.

“Simiyu ni Mkoa wenye ajenda na kazi yetu ni kutekeleza maelekezo na miongozo yote ya Serikali, tunatekeleza Sera ya Viwanda chini ya Falsafa ya Wilaya Moja Bidhaa Moja na sasa tunaenda kwenye utekelezaji wa Kijiji Kimoja Bidhaa Moja na sisi tunaamini Mapinduzi ya Viwanda yanaanza na SIDO” alisema Mtaka.

Maonesho hayo ya SIDO ambayo yanafanyika kwa mara ya kwanza mkoani Simiyu yamehudhuriwa na wajasiliamali zaidi ya 500  kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini ambayo yanatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.
MWISHO
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa  akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa  akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Simiyu, katika Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa  akifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (katikati) akiangalia moja ya mashine zitumikazo kutengeneza bidhaa mbalimbali zilizoletwa katika Maonesho ya Viwanda Vidogo(SIDO) Kitaifa, yatakayofanyika kuanzia Oktoba 23-28, 2018 katika Viwanja vya  Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiangalia sabuni zinazotengenezwa katika Kiwanda kidogo cha Itilima mkoani Simiyu, wakati wa Ufunguzi wa wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiangalia teknolojia rahisi ya utengenezaji wa chaki  kabla ya Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa (SIDO), uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(wa tatu kulia) akiangalia baadhi ya mashine zilizoletwa katika Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa(SIDO) yanayofanyika Mkoani Simiyu, Oktoba 23-28, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Mjasiriamali kutoka mkoa wa Kagera(kushoto) akiwasilisha changamoto zake kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akipata maelezo ya mbegu bora za alizeti kutoka kwa Mjasiriamali kutoka Mkoa wa Singida,  wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.

Kikundi cha Ngoma cha BASEKI kutoka Mjini Bariadi kikitoa burudani wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (katikati) akiangalia moja ya mashine zitumikazo kutengeneza bidhaa mbalimbali zilizoletwa katika Maonesho ya Viwanda Vidogo(SIDO) Kitaifa, yatakayofanyika kuanzia Oktoba 23-28, 2018 katika Viwanja vya  Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwasalimia wananchi kabla ya kuwasilisha salamu za Mkoa, wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akipanda mti  mara baada ya kufungua Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kwa kufungua Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiagana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini mara baada ya kufungua Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (mwenye shati la kitenge)akiwaongoza wakuu wa mikoa jirani Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela(mwenye kofia) na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi. Robert Gabriel katika kupanda mti , mara baada ya Ufunguzi  wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ( wa pili kulia) na Viongozi wa wengine wa SIDO na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji  wakimuongoza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kueleka kwenye mabanda ya maonesho wakati Ufunguzi  wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.



Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!