Tuesday, October 23, 2018

WAZIRI MKUU MAJALIWA AITAKA SIDO KUPANUA WIGO KUWAFIKIA WAJASILIAMALI KUANZIA NGAZI YA CHINI


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika la viwanda vidogo nchini SIDO  kuweka mikakati ya kupanua wigo wa shughuli zake kwa kuanzisha vituo katika ngazi ya halmashauri za wilaya ili kuwafikia wajasiliamali wengi zaidi, kuwajengea uwezo, kuwapa miongozo bora ya namna ya kuendesha shughuli zao kwa tija na kuwaunganisha na taasisi za fedha  waweze kupata mikopo.

Waziri mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo katika ufunguzi wa maonesho ya SIDO Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu ambapo amesema umefika wakati kwa SIDO kutilia mkazo sekta ya viwanda na hivyo kuifanya jukwaa la kuwakutanisha wabunifu pia kuwapa fursa ya kuonyesha uwezo wao katika matumizi ya teknolojia rafiki na rahisi zitakazoharakisha maendeleo ya viwanda nchini.

Pia Waziri Mkuu Majaliwa amesema SIDO inapaswa kujielekeza katika kubuni mashine , mitambo na teknolojia rahisi zitakazotumika kuongeza thamani ya bidhaa na kusisitiza kuwa  kutokana na umuhimu wa sekta ya viwanda nchini katika kukuza ajira na kuongeza pato la taifa serikali itaendelea kuweka miundombinu wezeshi itakayoharakisha kasi ya ukuaji wa viwanda.

“ Bila shaka nyote mnafahamu tumedhamiria kufikia uchumi wa kati kufikia mwaka 2025, ninaamini tunao uwezo wa kulifikia lengo hili, sasa tunachotakiwa kufanya kuhakikisha halmashauri zetu zote zinatenga maeneo maalumu kwa ajili shughuli za viwanda kama mlivyofanya hapa Simiyu, lakini pia lazima mhakikishe mnawajengea uwezo wajasiliamali ili waweze kuingia katika soko la ushindani, alisisitiza Waziri Mkuu Majaliwa”
.
Waziri Mkuu Majaliwa  amewasisitiza SIDO waendelee kubuni mikakati itakayoleta mabadiliko katika sekta ya viwanda huku akiwataka wananchi kuthamini bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini ambazo tayari zimeonyesha kukidhi mahitaji ya soko.

Halikadhalika waziri Mkuu Majaliwa ameziagiza halmashauri za wilaya nchini kuendelea kutekeleza agizo la kutenga 10%  ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya mikopo ya wanaweke, vijana na walemavu huku  akiwasisitiza madiwani katika halmashauri zote nchini kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa agizo hilo.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa ameupongeza uongozi wa mkoa wa Simiyu kwa kujenga mahusiano mema na wananchi, viongozi  wa kisiasa pamoja na taasisi mbalimbali jambo ambalo amesema ni chachu ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii mkoani Simiyu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo(SIDO), Prof. Sylvester Mpanduji amesema Shirika hilo litaendelea kutoa mafunzo kwa wajasriamali ili kuwajengea uwezo zaidi, ambapo amebainisha kuwa katika mwaka wa fedha 2017/2018 SIDO imetoa mafunzo kwa wajasiriamali 16,900.

Aidha, Prof. Mpanduji ameishukuru Serikali kwa kutenga shilingi bilioni 29 katika mwaka wa fedha 2018/2019 ambazo zitasaidia kutatua changamoto mbalimbali za wajasiriamali ikiwemo upatikanaji wa mashine mpya zitakazotumika katika vituo vya SIDO vya kuendeleza viwanda, kukopesha wajasiriamali mitaji na kujenga miuondombinu mingi ya viwanda katika sehemu hapa nchini.

Naye Mkuu wa Mkoa  wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemhakikishia Waziri mkuu  kuwa  Mkoa huo utahakikisha unaendelea kutekeleza maagizo ya serikali ikiwemo agenda ya kitaifa ya Uchumi wa Viwanda kupitia Falsafa ya Wilaya Moja Bidhaa Moja.

“Simiyu ni Mkoa wenye ajenda na kazi yetu ni kutekeleza maelekezo na miongozo yote ya Serikali, tunatekeleza Sera ya Viwanda chini ya Falsafa ya Wilaya Moja Bidhaa Moja na sasa tunaenda kwenye utekelezaji wa Kijiji Kimoja Bidhaa Moja na sisi tunaamini Mapinduzi ya Viwanda yanaanza na SIDO” alisema Mtaka.

Maonesho hayo ya SIDO ambayo yanafanyika kwa mara ya kwanza mkoani Simiyu yamehudhuriwa na wajasiliamali zaidi ya 500  kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini ambayo yanatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.
MWISHO
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa  akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa  akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Simiyu, katika Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa  akifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (katikati) akiangalia moja ya mashine zitumikazo kutengeneza bidhaa mbalimbali zilizoletwa katika Maonesho ya Viwanda Vidogo(SIDO) Kitaifa, yatakayofanyika kuanzia Oktoba 23-28, 2018 katika Viwanja vya  Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiangalia sabuni zinazotengenezwa katika Kiwanda kidogo cha Itilima mkoani Simiyu, wakati wa Ufunguzi wa wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiangalia teknolojia rahisi ya utengenezaji wa chaki  kabla ya Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa (SIDO), uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(wa tatu kulia) akiangalia baadhi ya mashine zilizoletwa katika Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa(SIDO) yanayofanyika Mkoani Simiyu, Oktoba 23-28, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Mjasiriamali kutoka mkoa wa Kagera(kushoto) akiwasilisha changamoto zake kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akipata maelezo ya mbegu bora za alizeti kutoka kwa Mjasiriamali kutoka Mkoa wa Singida,  wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.

Kikundi cha Ngoma cha BASEKI kutoka Mjini Bariadi kikitoa burudani wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (katikati) akiangalia moja ya mashine zitumikazo kutengeneza bidhaa mbalimbali zilizoletwa katika Maonesho ya Viwanda Vidogo(SIDO) Kitaifa, yatakayofanyika kuanzia Oktoba 23-28, 2018 katika Viwanja vya  Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwasalimia wananchi kabla ya kuwasilisha salamu za Mkoa, wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akipanda mti  mara baada ya kufungua Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kwa kufungua Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiagana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini mara baada ya kufungua Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (mwenye shati la kitenge)akiwaongoza wakuu wa mikoa jirani Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela(mwenye kofia) na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi. Robert Gabriel katika kupanda mti , mara baada ya Ufunguzi  wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ( wa pili kulia) na Viongozi wa wengine wa SIDO na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji  wakimuongoza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kueleka kwenye mabanda ya maonesho wakati Ufunguzi  wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.



0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!