Thursday, June 4, 2020

CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA SIMIYU KIMETENGA MILIONI 36.7 KUSAIDIA JAMII

Chama kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu(SIMCU) kimetenga jumla ya shilingi milioni 36.7 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo elimu na afya katika Mkoa wa Simiyu.

Hayo yamesemwa na makamu mwenyekiti wa SIMCU, Bw. Emmanuel Mwerere Juni 04, 2020 Mjini Bariadi  wakati akikabidhi fedha na baiskeli kwa mtoto Ritha Elias (08)  mwenye ulemavu wa miguu.

“Chama kikuu cha ushirika mkoa wa Simiyu kimetenga jumla ya shilingi 36,700,000/= kati ya hizo shilingi 24,000,000/= itasaidia elimu kwa watoto wenye ulemavu shilingi 12,000,000/= tutanunua mashuka kwa ajili ya Hospitali zote za mkoa wa Simiyu na shilingi 700,000/= kwa ajili ya kumsaidia mtoto Ritha Elias ambaye ni mlemavu wa miguu,”alisema Mwerere.

“SIMCU leo tunamkabidhi mtoto Ritha Elias kiasi cha shilingi 300,000/=  ikiwa ni ada ya shule na nauli ya kwenda na kurudi na baiskeli yenye thamani ya shilingi 400,000/= ambayo itamsaidia akiwa nyumbani na shuleni, "aliongeza Mwerere.

Aidha, Mwerere ameongeza kuwa mpango huo ni mwendelezo wa shughuli za chama hicho katika kusaidia jamii huku akiongeza kuwa awali walitoa zaidi ya shilingi milioni 3 kwa ajili ya chakula cha wanafunzi waliokuwa kwenye kambi za kitaaluma.

Katika hatua nyingine Mwerere ameomba makampuni ya pamba yaliyonunua pamba msimu wa wa mwaka 2018/2019 kulipa fedha za ushuru kiasi cha shilingi  milioni 729,520,255.

Awali akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ameipongeza SIMCU  kwa kutenga fedha hizo na kurudisha shukrani kwa jamii ikiwemo kumsaidia mtoto mwenye ulemavu wa miguu.

‘’Baadhi ya vyama vya ushirika vinafanya vizuri lakini fedha zao zinaishia kwenye posho na vikao, niwapongeze kwa kutenga kiasi cha milioni 36.7 kwa ajili ya huduma za kijamii ,leo mmekabidhi baiskeli kwa mtoto huyu mwenye ulemavu na mmemwingiza katika mpango wa kumsomesha mpaka mwisho wa masomo yake niwapongeze sana na kingine huyu binti ana kipaji cha kuchora ni mchoraji mzuri sana ’’  alisema Kiswaga.

Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Simiyu, Ibrahimu Kadudu amesema kurudisha kwa jamii sehemu ya faida ambayo vyama vya ushirika vinapata  huo ndio umuhimu wa ushirika, ambapo amebainisha kuwa pamoja na kutenga fedha kwa ajili ya elimu na afya,  awali SIMCU ilichangia fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya janga la CORONA.

Kwa upande wake bibi wa mtoto wa Ritha Elias, Perpetua Mtaima amesema mtoto huyo alizaliwa akiwa hana miguu yote  miwili  huku akiongeza kuwa pamoja na ulemavu huo mtoto huyo ana uelewa wa  vitu vingi japokuwa ni mdogo na kwa hivi sasa anasoma darasa la tatu  katika shule ya watoto wenye ulemavu ya Jeshi la Wokovu iliyopo jijini Dar es salaam na amekuwa akifanya vizuri darasani.

“Nilikuwa naomba msaada kwa watu mbalimbali akiwemo Mkuu wa wilaya ili mtoto huyu apate elimu na hana miguu nikushukuru sana baba (mkuu wa wilaya ) na mjukuu wangu huyu amekuwa  akiniambia siku moja atanibeba kwenye gari lake pia atanipeleka ofisini kwake na akimaliza masomo atapata kazi…nawashukuru wote mlionisaidia kunipatia nauli ya kumpeleka Dar es Salaam’’ alisema Perpetua.
MWISHO 
Mkuu wa wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga (kushoto) akipokea baiskeli iliyotolewa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu (SIMCU) kwa mtoto Ritha Elias mwenye ulemavu wa miguu(hayupo pichani) kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa SIMCU, Bw. Emmanuel Mwerere makabidhiano hayo yamefanyika sambamba na makabidhiano ya fedha taslimu shilingi 300,000/= Juni 04, 2020 Mjini Bariadi
 Mkuu wa wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga (kulia) akimkabidhi mtoto Ritha Elias mwenye ulemavu wa miguu fedha taslimu shilingi 300,000/= iliyotolewa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu(SIMCU) kwa ajili ya kumsaidia mtoto huyo katika elimu makabidhiano ambayo yamefanyika sammbamba na makabidhiano ya baiskeli kwa ajili yamtoto huyo  Juni 04, 2020 Mjini Bariadi.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu(SIMCU) Bw. Emmanuel Mwerere akizungumza kabla ya kukabidhi baiskeli na fedha taslimu shilingi 300,000/= kwa ya kumsaidia mtoto huyo katika elimu,  makabidhiano ambayo yamefanyika kati ya Uongozi wa SIMCU na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga Juni 04, 2020 Mjini Bariadi. 
 Wajumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu(SIMCU) wakiwa katika picha ya pamoja na mtoto Ritha Elias(mbele), viongozi wa Mkoa wa Simiyu, mlezi wa mtoto huyo (kulia) Perpetua Mtaima(kulia) mara baada ya uongozi wa SIMCU kumkabidhi mtoto huyo baiskeli na fedha taslimu shilingi 300,000/= Juni 04, 2020 kwa ajili ya kumsaidia katika elimu.


 Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Simiyu, Bw. Ibrahimu Kadudu kabla ya Uongozi wa Chama Kikuu cha ushirika Simiyu(SIMCU) kukabidhi baiskeli na fedha taslimu shilingi 300,000/= kwa ya kumsaidia mtoto huyo katika elimu,  makabidhiano ambayo yamefanyika kati ya Uongozi wa SIMCU na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga Juni 04, 2020 Mjini Bariadi.Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu(SIMCU), Bw. Emmanuel Mwerere akifurahia jambo na mtoto Ritha Elias ambaye ni mlemavu wa miguu baada ya kumkabidhi baiskeli na fedha taslimu kwa ya kumsaidia katika elimu,  makabidhiano yamefanyika kati ya Uongozi wa SIMCU na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga Juni 04, 2020 Mjini Bariadi.
  
 Wajumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu (SIMCU) wakiwa katika picha ya pamoja na mtoto Ritha Elias(mbele) na mlezi wa mtoto huyo(kulia) Perpetua Mtaima(kulia) mara baada ya uongozi wa SIMCU kumkabidhi mtoto huyo baiskeli na fedha taslimu shilingi 300,000/= Juni 04, 2020 kwa ajili ya kumsaidia katika elimu.Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) na Afisa Elimu watu wazima mkoa wa Simiyu, Mwl. Jusline Gilbert wakiwa katika picha ya pamoja na mtoto Ritha Elias mara baada ya uongozi wa SIMCU kumkabidhi mtoto huyo baiskeli na fedha taslimu shilingi 300,000/= Juni 04, 2020 kwa ajili ya kumsaidia katika elimu.
  

Mtoto Ritha Elias akiwa katika kiti chake alichopewa msaada na Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu (SIMCU) 

NANENANE KITAIFA MWAKA 2020 ITAKUWEPO NA ITAFANYIKA SIMIYU: RC MTAKA


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameujulisha Umma wa Watanzania kuwa Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane Kitaifa kwa mwaka 2020 yatakuwepo na yatafanyika katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi na viongozi wakuu wa Kitaifa wanatarajiwa kufungua na kufunga maonesho hayo ambayo yanafanyika kwa mara ya tatu mfululizo.

Mtaka ameyasema hayo leo Juni 03, 2020 katika kikao cha pamoja kati ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega ambaye yuko mkoani Simiyu kwa ziara ya siku mbili.

"Kumekuwa na maswali kwa baadhi ya watu kuhusu Nanenane kuwa itakuwepo au haitakuwepo, nitumie nafasi hii kuwaambia Watanzania kuwa tumepokea taarifa rasmi kutoka Wizara ya Kilimo kuwa sherehe za Nanenane Kitaifa mwaka 2020 zipo na zitafanyika mkoani Simiyu na viongozi wakuu wa Kitaifa watashiriki katika ufunguzi na ufungaji; mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga inayoandaa sherehe hizi imeanza maandalizi, taasisi za Umma na binafsi pia zimethibitisha kushiriki na nyingine zimeanza maandalizi,” alisema Mtaka.Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiteta jambo na  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega wakati alipowasili Mjini Bariadi kwa ajili ya kuanza ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu, Juni 03, 2020.Monday, June 1, 2020

WALIOSABABISHA HOJA ZA UKAGUZI WACHUKULIWE HATUA: SAGINI

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amewataka viogozi wa Halmashauri mkoani hapa kuwachukulia hatua watumishi wote waliosabaisha hoja za ukaguzi.
Sagini ameyasema hayo katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya Itilima, ambacho kimefanyika kwa lengo kujdili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali(CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Wednesday, May 27, 2020

HALMASHAURI ZA MKOA WA SIMIYU ZAAGIZWA KULIPA STAHILI ZA MADIWANI

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani hapa kuhakikisha wanawalipa Madiwani stahili zao zote wanazodai kabla ya kuvunjwa kwa mabaraza ya Halmashauri ambayo yanatarajiwa kuvunjwa kabla ya tarehe 10 Juni 2020.

Mtaka ametoa agizo hilo Mei 26, 2020 katika kikao cha baraza maalum la Madiwani wilayani Busega ambacho kimefanyika kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

"Waheshimiwa madiwani wamefanya kazi nzuri kwa miaka mitano haitakuwa busara wamalize muda wao wakiwa wanadai; nisingependa kuona baada ya mabaraza kuvunjwa madiwani waanze kwenda kwenye ofisi za wakurugenzi kufuatilia madai yao, malipo yao yawe ndiyo kipaumbele cha Wakurugenzi wetu" alisema Mtaka.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Njiginya ameahidi kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa na kuhakikisha madiwani wote wanalipwa madai yao kwa wakati.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Imalamate, Mhe. Richard Magoti amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuliweka suala la malipo ya stahili za madiwani katika mkoa wa Simiyu kuwa kipaumbele, jambo ambalo limeonesha namna Serikali inavyothamini na kutambua mchango wa viongozi hao.
Naye Mbunge wa Busega Dkt. Raphael Chegeni amesema pamoaj na maendeleo yanayoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya tano katika wilaya ya Busega wilaya hiyo inakabiliana na changamoto ya upungufu wa miundombinu ya elimu kutokana na ongezeko la wanafunzi, hivyo akatoa wito kwa Serikali kushirikiana na jamii kuona namna ya kukabiliana na changamoto hiyo.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Busega lililofanyika Mei 26, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, mhe. Vumi Magoti akifungua kikao maalum cha Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo  lililofanyika Mei 26, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).

 Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega wakifuatilia kikao maalum cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Busega lililofanyika Mei 26, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).
 Mbunge wa Jimbo la Busega, Dkt. Raphael Chegeni akichangia hoja katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Busega lililofanyika Mei 26, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).
 Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera  akizungumza katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Busega lililofanyika Mei 26, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamti ya Ulinzi na usalama ya Wilaya ya Busega wakifuatilia kikao maalum cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Busega lililofanyika Mei 26, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).
 Diwani wa Kata ya Nyashimo, Mhe. Mickness Mahela akichangia hoja katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Busega lililofanyika Mei 26, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).
 Wakuu wa Idara za Halmashauri ya Wilaya ya Busega wakifuatilia kikao maalum cha Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo  lililofanyika Mei 26, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).
 Diwani wa kata ya Imalamate, Mhe. Richard Magoti akichangia hoja katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Busega lililofanyika Mei 26, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).
 Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega wakifuatilia kikao maalum cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Busega lililofanyika Mei 26, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Busega lililofanyika Mei 26, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).


Tuesday, May 26, 2020

WASHIRIKI NANENANE KITAIFA MWAKA 2020 SIMIYU WAHIMIZWA KUANZA MAANDALIZI

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini ametoa wito kwa Taasisi, mashirika ya Umma na binafsi na wadau wote wa kilimo, mifugo na uvuvi wanaotarajia kushiriki maonesho ya Kitaifa ya Nanenane mwaka huu kuanza maandalizi ya maonesho hayo.

Sagini ameyasema hayo jana mara baada ya kukagua na kuona  hali ya maandalizi ya maonesho hayo katika Viwanja vya Nyakabindi katika maeneo ya wadau mbalimbali wa maonesho hayo.ambayo yatafanyika kwa mara ya tatu mfululizo  katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.

“Halmashauri za mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga  ambayo ndiyo inaunda Kanda ya Ziwa Mashariki zimeanza vizuri, taasisi zilizo  chini ya Wizara ya kilimo nazo zimefanya vizuri lakini baadhi ya wadau wa sekta ya kilimo hawajajitokeza; nitoe wito kwa wadau wote watakaoshiriki katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka huu mkoani Simiyu waweze kuja kuanza maandalizi,” alisema Sagini.

Amesema maandalizi ya vipando vya mazao, mashamba darasa, mabanda ya mifugo na mabwawa ya samaki yanahitaji muda hivyo ni vema wakaanza mapema ili kupata vitu vizuri vitakavyotumika kuelimisha wakulima, wafugaji na wavuvi kuhusu teknolojia rahisi zinazotumika katika uzalishaji wenye tija.

Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao kutoka  wizara ya kilimo, Bw. Nyasebwa Chimagu  amesema ameridhishwa na maandalizi ya maonesho ya nane nane huku akiwataka wadau kuyatumia kama kichecheo kikubwa cha ueneaji wa technolojia za kisasa katika sekta ya kilimo, mifugo na uvivu ili mazao yao yaweze kuwa na tija.

Pamoja na kukiri kuwa hamasa ya maandalizi ya maonesho ya Nanenane mwaka 2020 ilishuka baada ya kuibuka kwa  homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona, Chimagu amesema kuwa kwa sasa maandalizi yanaendelea katika viwanja vyote nane vya kanda za maonesho hayo nchi nzima.

Aidha Chimagu amewatoa hofu wananchi wote  juu ya sintofahamu ya maonesho ya nane nane na kusema kuwa yatakuwepo na kuwasisitiza wadau ambao hawajajitokeza kujitokeza kwenye viwanja vya maonesho kwa ajili ya kuanza shughuli za maandalizi kwani tayari wengine wameanza na maendeleo ni mazuri.

"Niwatoe hofu wananchi wote  nchini kuwa maonesho ya nanenane yatakuwepo kwenye viwanja vyote vya kanda,  kitaifa yatafanyika mkoani Simiyu kwa mara ya tatu mfululizo, hivyo wadau binafsi, taasisi za umma na binafsi pamoja na halmashauri ambazo bado hazijaanza maandalizi kuanza shughuli za maandalizi  ya maonesho, "alisema Chimagu.

Kwa upande wake Bwana shamba kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Ishengoma Julius amesema  maandalizi  ya vipando kwa ajili ya maonesho ya nane nane yamefikia 75% na  vipando vya muda mfupi vimebaki kwa 25% na kusema kuwa mpaka kufikia maonesho hayo vitakuwa tayari.

Naye mkuu wa kambi ya jeshi la magereza kwenye maonesho ya nane nane Nyakabindi, Bw. Patrick Matiku amesema  wanafanya ukaguzi kila siku kwenye vipando vyao ili waweza kubaini kama kuna tatizo na kulitatua mapema.

Maonesho ya Nanenane mwaka 2020 yanaongozwa na Kauli Mbiu inayosema “KWA MAENDELEO YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020”.

MWISHO
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (mbele) akiwa na baadhi ya viongozi na watendaji wa Wizara ya kilimo na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa waSimiyu wakikagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane ambayo mwaka 2020 yatafanyika kwa mara ya tatu mfululizo katika kanda ya ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao kutoka  wizara ya kilimo, Bw. Nyasebwa Chimagu  na baadhi ya viongozi na watendaji wa Wizara ya kilimo na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa waSimiyu wakikagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane ambayo mwaka 2020 yatafanyika kwa mara ya tatu mfululizo katika kanda ya ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu. 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) na Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao kutoka  wizara ya kilimo, Bw. Nyasebwa Chimagu  wakikagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane ambayo mwaka 2020 yatafanyika kwa mara ya tatu mfululizo katika kanda ya ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (mbele) akiwa na baadhi ya viongozi na watendaji wa Wizara ya kilimo na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa waSimiyu wakikagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane ambayo mwaka 2020 yatafanyika kwa mara ya tatu mfululizo katika kanda ya ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (mbele) akiwa na baadhi ya viongozi na watendaji wa Wizara ya kilimo na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa waSimiyu wakikagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane ambayo mwaka 2020 yatafanyika kwa mara ya tatu mfululizo katika kanda ya ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kulia) akiwa na baadhi ya viongozi na watendaji wa Wizara ya kilimo na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa waSimiyu wakiangalia mche wa mkorosho ulipandwa viwanja vya nanenane Simiyu wakati wa ziara ya kukagua  maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane ambayo mwaka 2020 yatafanyika kwa mara ya tatu mfululizo katika kanda ya ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao kutoka  wizara ya kilimo, Bw. Nyasebwa Chimagu  wakikagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa ambayo mwaka 2020 yatafanyika kwa mara ya tatu mfululizo katika kanda ya ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
 
:-Mapapai yaliyopandwa katika  vibando vya mazao ya kilimo katika viwanja vya nanenane Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
 
Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao kutoka  wizara ya kilimo, Bw. Nyasebwa Chimagu akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) mara baada ya kukagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) mara baada ya kukagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao kutoka  wizara ya kilimo, Bw. Nyasebwa Chimagu akiangalia mazao yaliyopandwa katika vipando kwenye uwanja wa maoenesho ya nanenane  wakati wa kukagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.

 

Mkuu wa kambi ya jeshi la magereza kwenye maonesho ya nane nane Nyakabindi, Bw. Patrick Matiku(kulia) akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini zawadi ya papai ambayo yamepandwa katika vipando vya jeshi hilo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.


Saturday, May 23, 2020

SIMIYU TUMEJIPANGA KIKAMILIFU KUWAPOKEA KIDATO CHA SITA KUANZA MASOMO JUNI MOSI: SAGINI


Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema mkoa huo umejipanga kikamilifu kuwapokea wanafunzi wa kidato cha sita kwa ajili ya kuanza masomo Juni Mosi, 2020 kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe  Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari leo 23 Mei,2020 Sagini amesema Simiyu iliandaa mkakati maalum kwa kushirikiana na wadau kuwawezesha wanafunzi kujisomea hivyo, mkoa utahakikisha muda uliotolewa na Wizara ya elimu kufanya maandalizi ya mtihani wa Taifa wa kidato cha sita (Juni Mosi-Juni 28) unatumika vizuri na walimu na wanafunzi kwa ajili ya rejea na kukamilisha mada.

“Sisi kama mkoa elimu ni kipaumbele cha kwanza  hivyo tumejipanga kikamilifu kuwapokea vijana wetu wa kidato cha sita, ikumbukwe pia kuwa kama mkoa tuliandaa mkakati wa kuwasaidia wanafunzi kujisomea hususani madarasa ya mitihani wakati walipokuwa likizo ya tahadhari ya Corona; tutahakikisha muda uliotolewa na wizara ya elimu kujiandaa na mtihani wa Taifa unatumika vizuri kufanya marejeo na kukamilisha mada zilizobaki,”alisema Sagini.

Aidha, Sagini amesema viongozi katika maeneo yote watahakikisha tahadhari zote zinazotolewa na Wizara yenye dhamana na Afya katika  kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona zinazingatiwa katika shule zote za kidato cha sita Mkoani Simiyu.

Vile vile Sagini ametoa wito kwa wazazi na walezi mkoani Simiyu kuendelea kuwahimiza na kuwasimamia watoto wao walioko majumbani kujisomea wakati huu ambao wengine bado wako likizo mpaka shule zitakapofunguliwa, huku akisisitiza kuwa mkakati wa mkoa wa kuwawezesha wanafunzi kujisomea wakati wakiwa likizo utaendelea kutekelezwa.

Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema pamoja na utekelezaji wa mkakati maalum wakati likizo, kabla ya serikali kutangaza kufunga shule wanafunzi wa kidato cha sita walikuwa katika kambi ya kitaaluma, ambapo takribani mada zote zilikuwa zimeshakamilika na wanafunzi walikuwa wakipewa majaribio na kurudia mada ambazo hazikueleweka vizuri.

Naye  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza amesema  idara ya elimu katika Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na waratibu elimu kata  wamejipanga kuhakikisha kuwa wanakamilisha mahitaji yote ya kujisomea kwa wanafunzi wa kidato cha sita yanaandaliwa na kukamilika kwa wakati ili kuwawezesha kujiandaa na mtihani wa Taifa.


Kwa upande wake mmoja wa wazazi wenye wanafunzi wa kidato cha Sita mjini Bariadi, Bw. Chambwite Sadala amesema anaunga mkono uamuzi wa Mhe. Rais wa wanafunzi wa kidato cha sita kurudi shuleni, hivyo akatoa wito kwa wanafunzi hao kwenda kufanya bidii katika kujisomea katika muda waliopewa ili waweze kufanya vizuri na hatimaye kufikia malengo yao.

Mkoa wa Simiyu una jumla ya shule 13 za sekondari za Kidato cha tano na Sita, ambapo kwa mwaka 2020 jumla ya wanafunzi 953 wa kidato cha Sita wanatarajiwa kufanya mtihani wa Taifa kuanzia tarehe 29 Juni 2020 kama ilivyotangazwa na Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako.
MWISHO
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Mei 23, 2020 kuhusu utayari wa mkoa katika kuwapokea wanafunzi wa kidato cha sita kwa ajili ya kuanza masomo Juni Mosi, 2020 kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akitoa ufafanuzi wa jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)  Mei 23, 2020 kuhusu utayari wa mkoa katika kuwapokea wanafunzi wa kidato cha sita kuanza masomo Juni Mosi, 2020 kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Thursday, May 14, 2020

SEKTA BINAFSI ILELEWE NA IPENDWE-RC MTAKA

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa viongozi wa Serikali mkoani hapa kuilea na kuipenda sekta binafsi na kuona namna sahihi ya kutatua changamoto zinazoikabili badala ya kufikiria namna ya kukusanya mapato tu kutoka katika sekta hiyo.

Mtaka ameyasema hayo katika kikao maalum cha kujadili Hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/2019 katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambapo Halmashauri ya Mji Bariadi na nyingine za Mkoa wa Simiyu pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa. Simiyu zimepata hati safi.

“Viongozi wa Serikali tujifunze kuilea sekta binafsi, sekta binafsi ni lazima ilelewe na ipendwe pia, tuone namna ya kutatua changamoto zinazoikabili na kuwafanya watu wapende kufanya biashara badala ya kufikiria kukusanya mapato tu,” alisema Mtaka.

Mtaka ametoa wito huo kutokana na mapendekezo yaliyotolewa katika ripoti ya CAG kuwa pamoja na Halmashauri ya Mji Bariadi kupata hati safi, iko haja kwa Halmashauri hiyo kuimarisha mifumo ya  ukusanyaji na  Usimamizi wa Mapato yatokanayo na vyanzo vya ndani, huku akisistiza kuweka utaratibu mzuri wa utoaji wa mikopo ya wanawake, vijana na wenye ulemavu kutoka katika asilimia 10 ya mapato hayo ya ndani.

Aidha, Mtaka amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani Simiyu kuhakikisha wanawalipa madiwani stahili zao kabla ya muda wao kuisha (kabla ya mabaraza ya amadiwani kuvunjwa, “tusingehitaji tuvunje mabaraza madiwani wetu wakiwa wanadai stahili zao, Wakurugenzi wote hili liwe kipaumbele chenu.”

 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Madiwani na wataalam katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichofanyika Mei 12, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu  za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo akifungua  Kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichofanyika Mei 12, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu  za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bw. Melckizedeck  Humbe akitoa taarifa katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichofanyika Mei 12, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu  za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
 Baadhi ya Madiwani na wataalam wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi wakiwa katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichofanyika Mei 12, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu  za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Baadhi ya Madiwani na wataalam wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi wakiwa katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichofanyika Mei 12, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu  za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Diwani wa Kata ya Nyangokolwa Mhe. Lukonge Nyakali akichangia katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichofanyika Mei 12, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu  za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akitoa salamu za Wilaya katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichofanyika Mei 12, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu  za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa Wa Simiyu, ACP. Henry Mwaibambe akizungumza katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichofanyika Mei 12, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu  za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akitoa salamu za Wilaya katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichofanyika Mei 12, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu  za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Madiwani na wataalam katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichofanyika Mei 12, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu  za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Baadhi ya viongozi wakiwa katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichofanyika Mei 12, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu  za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
  Wajumbe wa Kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu wakifuatilia Kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichofanyika Mei 12, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu  za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Wednesday, May 13, 2020

TARURA SIMIYU KUFUNGUA BARABARA ZILIZOATHIRIWA NA MVUA KUZIFANYA ZIPITIKE WAKATI WOTE

Mratibu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Simiyu, Dkt. Eng. Philemon Msomba amesema Serikali imedhamiria kufungua barabara zote zilizoharibiwa na mvua mkoani hapa na kuhakikisha zinapitika kwa mwaka mzima ili kuwarahisisha wananchi  mawasiliano na usafirishaji wa bidhaa na mazao mbalimbali.

Dkt. Msomba ameyasema hayo Mei 13, 2020 wakati wa ziara yake ya kukagau maendeleo ya ujenzi wa madaraja katika wilaya ya Bariadi eneo la Mto  Ndoba linalounganisha Mtaa wa Bunamhala na Majahida litakalogharimu shilingi milioni 33 na daraja la Mto Nyambuli linalounganisha kijiji cha Mwamondi na Lulai (Dutwa) litakalogharimu kiasi cha shilingi milioni 25 yanayojengwa kwa mpango wa dharura.

“Azma ya Serikali ni kuhakikisha barabara zote zinapitika kwa mwaka mzima, tunaishukuru Serikali imetoa fedha kwa ajili ya matengenezo ya barabara mkoani Simiyu, mwaka wa fedha 2019/2020 tulitenga bajeti ya shilingi bilioni tano, kufikia Mei 13, 2020 tumepokea shilingi bilioni 4.23 sawa na asilimia 84; kwa hiyo barabara zote zilizoathiriwa na mvua tuna uhakika wa kuzifungua,” alisema Mratibu wa TARURA Simiyu, Dkt. Eng. Philemon Msomba.

Aidha, Dkt. Msomba amesema TARURA itafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kuwa miradi yote  ikiwemo ya dhararua inatekelezwa kwa kiwango na kwa wakati ili barabara hizo ziweze kuwanufaisha wananchi kiuchumi ambapo amebainisha kuwa TARURA Simiyu imeomba kiasi cha shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali kwa mpango wa dharura.

Dkt. Msomba amesema pamoja na ujenzi wa madaraja katika mwaka wa fedha 2019/2020  TARURA imejipanga kutengeneza mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometa 690 huku akiwataka Mameneja wa TARURA wa wilaya kusimamia ubora wa kazi katika ujenzi huo na kuhakikisha kazi zote zinakamilika kwa wakati.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewashukuru viongozi wa TARURA kwa namna walivyochukua hatua madhubuti kuhakikisha madaraja yanatengenezwa na barabara za vijijini zinapitika hususani kwenye kipindi cha mvua nyingi, huku akitoa rai kwa viongozi hao kuwasimamia wakandarasi ili wafanye kazi kwa kuzingatia viwango vya kitaalam na thamani ya fedha.

Naye Diwani wa Kata ya Dutwa, Mhe.Mapolu Mkingwa amesema matengenezo ya daraja la Mto Nyambuli linalounganisha kijiji cha Mwamondi na Lulai utaondoa adha iliyokuwa ikiwapata wananchi kufika makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Dutwa na kurahisisha usafirishaji wa mazao kwa kuwa Mwamondi ndiyo ghala la chakula kwa kata hiyo.

Wakizungumzia ujenzi wa madaraja yaliyokuwa yamesombwa na maji kutokana na mvua wananchi wa Mtaa wa Bunamhala na Majahida katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Kulwa Nyanza, Lazaro Samwel na Magreth Magile wamesema baada ya daraja kukatika iliwalazimu kutumia usafiri wa pikipiki na baiskeli  kutokana na eneo la mto Ndoba kutopitika kwa magari.

“Tulikuwa tunapata shida kuvuka mto huu na mvua zinaponyesha tulikuwa tunalazimika kutengeneza daraja la miti ili litusaidie kuvuka, tunaishukuru serikali kuchukua hatua za kuanza kujenga daraja tunaomba likamilike mapema maana huku kuna wananchi wengi na vile vile kuna chuo cha maendeleo ya jamii,” alisema Lazaro Samwel.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Simiyu unahudumia mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometa 4038.16 ambapo kati ya hizo asilimia 55 zinapitika na ziko katika hali nzuri na wastani, huku asilimia 45 ya mtandao zinahitaji matengenezo na jitihada zinafanyika ili zifanyiwe matengenezo kuhakikisha zinapitika kwa mwaka mzima.

MWISHO

 Mratibu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Simiyu, Dkt. Eng. Philemon Msomba akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja linalojengwa kwa mpango wa dharura katika eneo la Mto  Ndoba linalounganisha Mtaa wa Bunamhala na Majahida katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mei 13, 2020.
 Ujenzi wa daraja katika eneo la Mto  Ndoba linalounganisha Mtaa wa Bunamhala na Majahida katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi ukiendelea ambao unatarajia kukamilika Mei 15, 2020 kupitia fedha za mpango wa dharura. Ujenzi wa daraja katika eneo la Mto  Ndoba linalounganisha Mtaa wa Bunamhala na Majahida katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi ukiendelea ambao unatarajia kukamilika Mei 15, 2020 kupitia fedha za mpango wa dharura.

Ujenzi wa daraja la Mto Nyambuli linalounganisha kijiji cha Mwamondi na Lulai katika kata ya Dutwa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ukiendelea ambao ambao unatarajia kukamilika Mei 15, 2020 kupitia fedha za mpango wa dharura.

 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) Mei 13, 2020 mjini Bariadi  juu ya kazi mbalimbali zilizofanywa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Simiyu.


 Diwani wa Kata ya Dutwa, Mhe.Mapolu Mkingwa akizungumza akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) Mei 13, 2020  wakati wa zaira ya Matibu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Simiyu, Dkt. Eng. Philemon Msomba. Lazaro Samwel mkazi wa Mtaa wa Bunamhala katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi akizungumzia ujenzi wa daraja katika eneo la Mto  Ndoba linalounganisha Mtaa wa Bunamhala na Majahida ukiendelea ambao unatarajia kukamilika Mei 15, 2020.


 Magreth Magile mkazi wa Mtaa wa Bunamhala katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi akizungumzia ujenzi wa daraja katika eneo la Mto  Ndoba linalounganisha Mtaa wa Bunamhala na Majahida ukiendelea ambao unatarajia kukamilika Mei 15, 2020.


Mratibu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Simiyu, Dkt. Eng. Philemon Msomba akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja katika eneo la Mto  Ndoba linalounganisha Mtaa wa Bunamhala na Majahida katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mei 13, 2020 ambalo linajengwa kupitia fedha za mpango wa dharura.Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) Mei 13, 2020 mjini Bariadi  juu ya kazi mbalimbali zilizofanywa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Simiyu.


Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!