Sunday, March 14, 2021

VIONGOZI SIMIYU WAASWA KUTUMIA BUSARA BADALA YA NGUVU

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ametoa rai kwa Viongozi wa Serikali mkoani hapa kutumia busara na akili badala ya kutumia nguvu katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi katika maeneo waliyopo na kuhakikisha ufumbuzi unaotolewa unaleta tija kwa wananchi.

 

Mtaka ametoa rai hiyo wakati akifungua  kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) , kilichofanyika Machi 13, 2021 Mjini Bariadi kwa lengo la kupitia Rasimu ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Simiyu ya mwaka 2021/2022.

“Wito wangu kwa viongozi wenzangu tupunguze kutumia nguvu, tuongeze matumizi ya akili tuone matokeo kwa wananchi wetu, leo tunapitisha mapendekezo ya bajeti ya mkoa mwaka 2021/2022 lakini ningetamani kuona miradi mipya ya Halmashauri inayogusa watu, halmashauri zetu zijielekeze kwenye kuanzisha miradi ambayo itakuwa vyanzo vipya vya mapato,” alisema.

Aidha, Mtaka ametoa rai kwa Viongozi wa Mkoa na Halmashauri kupima tija ya vikao vyao na kuhakikisha vikao wanavyokaa vinaleta tija ikiwa ni pamoja na namna vikao hivyo vinavyosaidia kubuni na kuongeza vyanzo vya mapato.

Akiwasilisha mapendekezo ya rasimu ya mpango na bajeti ya Mkoa wa Simiyu, Katibu Tawala Msaidizi-Sehemu ya Mipango na Uratibu, Bw. Donatus Weginah amesema katika mwaka wa fedha 2021/2022 Simiyu inatarajiwa kutengewa shilingi bilioni 200.5 kwa ajili ya miradi ya maendeleo, mishahara na matumizi mengineyo. 

Akizungumza kwa niaba ya wabunge  Mwenyekiti wa Wabunge wa mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa ameunga mkono mapendekezo ya mpango na bajeti ya mkoa na kuahidi ushirikiaono wa wabunge hao katika kupitisha bajeti hiyo bungeni.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ametoa wito kwa kwa viongozi wote mkoani Simiyu kushirikiana na vyombo vinavyohusika na usimamizi wa fedha kudhibiti na kusimamia matumizi ya fedha zote za Serikali ili ziweze kuleta tija.

Akitoa salamu kwa naiba ya Chama cha Mapinduzi, Katibu wa CCM mkoa wa Simiyu, Bi. Haula Kachwamba amewashauri wataalam kila mmoja kutimiza wajibu wake katika kubuni vyanzo na mbinu za kuongeza mapato kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mkoa wa Simiyu .

MWISHO

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) , kilichofanyika Machi 13, 2021 Mjini Bariadi kwa lengo la kupitia Rasimu ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Simiyu ya mwaka 2021/2022.

 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) , kilichofanyika Machi 13, 2021 Mjini Bariadi kwa lengo la kupitia Rasimu ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Simiyu ya mwaka 2021/2022.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akifafanua jambo  katika kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) , kilichofanyika Machi 13, 2021 Mjini Bariadi kwa lengo la kupitia Rasimu ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Simiyu ya mwaka 2021/2022.

Katibu Tawala Msaidizi-Sehemu ya Mipango na Uratibu, Bw. Donatus Weginah akiwasilisha Rasimu ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Simiyu ya mwaka 2021/2022, katika Kikao maalum  cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) , kilichofanyika Machi 13, 2021 Mjini Bariadi kwa lengo la kupitia rasimu hiyo. 

Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Simiyu na Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina akichangia hoja katika  kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) , kilichofanyika Machi 13, 2021 Mjini Bariadi kwa lengo la kupitia Rasimu ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Simiyu ya mwaka 2021/2022. 
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika Machi 13, 2021 Mjini Bariadi kwa lengo la kupitia Rasimu ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Simiyu ya mwaka 2021/2022.
Katibu wa CCM wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Haula Kachwamba akichangia hoja katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika Machi 13, 2021 Mjini Bariadi kwa lengo la kupitia Rasimu ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Simiyu ya mwaka 2021/2022.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kupitia Mkoa wa Simiyu, Bw. Gungu Silanga akichangia hoja katika kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika Machi 13, 2021 Mjini Bariadi kwa lengo la kupitia Rasimu ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Simiyu ya mwaka 2021/2022.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifunga kikao  maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, kilichofanyika Machi 13, 2021 Mjini Bariadi kwa lengo la kupitia Rasimu ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Simiyu ya mwaka 2021/2022.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifunga kikao  maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, kilichofanyika Machi 13, 2021 Mjini Bariadi kwa lengo la kupitia Rasimu ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Simiyu ya mwaka 2021/2022.

Baadhi ya wajumbe na waalikwa wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika Machi 13, 2021 Mjini Bariadi kwa lengo la kupitia Rasimu ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Simiyu ya mwaka 2021/2022.

Baadhi ya wajumbe na waalikwa wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika Machi 13, 2021 Mjini Bariadi kwa lengo la kupitia Rasimu ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Simiyu ya mwaka 2021/2022.

Baadhi ya viongozi wakifuatilia kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika Machi 13, 2021 Mjini Bariadi kwa lengo la kupitia Rasimu ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Simiyu ya mwaka 2021/2022.




Tuesday, March 9, 2021

SERIKALI YAANZA MAANDALIZI UJENZI WA RELI YA KISASA MWANZA-ISAKA, BANDARI KAVU KUJENGWA SIMIYU

 

Serikali imeanza maandalizi ya ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka yenye urefu wa kilomita 341 ambayo itajengwa kwa gharama ya shilingi trilioni 3.0267 fedha za ndani, ambapo katika mradi huu Bandari kavu na stesheni  vinatarajiwa kujengwa katika eneo la Malampaka wilayani Maswa mkoani Simiyu..

 

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa Machi 08, 2021 katika kikao cha pamoja cha wadau ambacho kilifanyika katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja juu ya utekelezaji wa mradi huu ili  kufanya maandalizi muhimu.

 

“Hapa Malampaka tutakuwa na kambi ya watu zaidi ya 3000 kwa hiyo ni vizuri wananchi wakaandaliwa ili waweze kushiriki fursa mbalimbali, tunatarajia pia kujenga bandari kavu kama ilivyo Isaka mizigo kutoka mikoa mbalimbali itaishia hapa; Malampaka pia tutajenga stesheni jengo kubwa lenye mita za mraba 8000 ambayo ndani itakuwa na benki, maduka na huduma nyingine,” alisema Kadogosa.

 

“Mradi huu ni lazima uwe na maana kwa maisha ya watu wa kawaida, mahitaji mbalimbali yatahitajika na watenda kazi kwenye mradi huu kama vile malazi, chakula mfano kuku tu zitahitaji zaidi ya kuku 40,000 kwa mwezi, kwa hiyo hii ni fursa nzuri itakayobadilisha maisha ya wengi, wananchi wajipange kutumia fursa hii,” alisisitiza.

 

Aidha, Kadogosa ametoa wito kwa wananchi na wadau wengine kutoka taasisi mbalimbali kushirikiana na TRC ili utekelezaji wa mradi huu usiathiri shughuli mbalimbali za wananchi na taasisi hizo zinazotoa huduma kwa jamii, huku akiahidi kuwa TRC itaendelea kusimamia upatikanaji wa fursa zipatikane kwa usawa kama ilivyoelekezwa na Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa wa Simiyu umepokea mradi huo kwa asilimia 100 na kuahidi kutoa ushirikiano, huku akiwahakikishia usalama wakandarasi na watu wote watakaohusika na utekelezaji wa mradi huu.

Kiswaga ameagiza idara ya ardhi Maswa kupima maeneo ili wananchi waweze kupata maeneo ya kujenga na kuwekeza kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali, ambapo pia ametoa wito kwa wananchi kununua maeneo hayo yatakapotangazwa, ili waweze kujenga nyumba za kuishi na kuwekeza katika fursa mbalimbali kuinua uchumi wao, mkoa na Taifa kwa ujumla.

Katibu wa CCM mkoa wa Simiyu, Bi. Haula Kachwamba ametoa wito kwa Wananchi wa Malampaka kila mmoja kuwa mlinzi wa mali za mkandarasi na serikali, “ Hatutegemei mali ya serikali na mkandarasi ikaibiwa, tunategemea itafanya kazi iliyokusudiwa hivyo kila mmoja akawe mlinzi, lakini pia mjiandae kutumia fursa hii, wakulima, wafugaji, mama ntilie kila mmoja kwa namna yake.”

Mwenyekiti Kijiji cha Ikungu Bw. Chuma Gashi amesema wananchi wa Kijiji hicho wameupokea mradi huo kwa mikono miwili na wako tayari kupisha maeneo yatakayohitajika kwa kufuata taratibu huku akibainisha kuwa yeye binafsi kama mwananchi amejipanga kufanya biashara ya kuku katika kambi itakayojengwa Malampaka na baadaye reli ikikamilika atasafirisha kwenda Dar es salaam.

Naye Julia Musa amesema “mradi wa reli tumeupokea kwa furaha maana tunajua mji wetu wa Malampaka utapata maendeleo, vijana watapata ajira, tunamuombea Mhe. Rais azidi kutuletea miradi mingine ili sisi wana Malampaka tuzidi kupata maendeleo, tuko tayari kupisha mradi na kwenda kwenye maeneo tutakayopangiwa na serikali tukilipwa fidia ili kupisha ujenzi wa reli hii.”

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Aswege Kaminyoge amesema eneo la Malampaka linakadiriwa kuwa na wakazi wapatao 14,300.

Kikao cha uongozi wa TRC kilihusisha pia viongozi wa chama na Serikali ngazi ya mkoa nawwilaya ya Maswa, viongozi wa dini, wazee maarufu, baadhi ya wananchi na wakandarasi pamoja na watekeelzaji wengine wa mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR). 

MWISHO 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa (wa tatu kushoto) akiwaonesha jambo baadhi ya viongozi na wadau wa reli ya kisasa (SGR) baada ya kutembelea eneo ambalo litajengwa stesheni ya Malampaka wilayani Maswa wakati wa utekelezaji wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka, mara baada ya kikao chake na wadau hao kilichofanyika Machi 08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka Maswa .
Mtaalam kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) akitoa maelezo ya eneo linalotarajiwa kujengwa stesheni ya Malampaka wilayani Maswa wakati wa utekelezaji wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka, mara baada ya kikao cha uongozi wa TRC na viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi 08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na wadau wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, kikao ambacho kilihusisha uongozi wa TRC na viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi 08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa akizungumza na wadau wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, kikao ambacho kilihusisha uongozi wa TRC na viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi 08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa.
Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Bi. Haula Kachwamba akitoa salamu za Chama katika kikao cha wadau wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka, ambacho kilihusisha uongozi wa TRC na viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi 08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa.
Baadhi ya wadau wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka, wakifuatilia kikao cha uongozi wa TRC na viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi 08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa.

Baadhi ya wadau wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka, wakifuatilia kikao cha uongozi wa TRC na viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi 08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa.

Baadhi ya wadau wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka, wakifuatilia kikao cha uongozi wa TRC na viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi 08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Aswege Kaminyoge akizungumza katika kikao wadau wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka, kilichohusisha uongozi wa TRC na viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi 08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Maswa, Eng. Paul Jidayi akitoa salamu za Chama wilaya katika kikao cha wadau wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka, ambacho kilihusisha uongozi wa TRC na viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi 08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa.
Baadhi ya wadau wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka, wakifuatilia kikao cha uongozi wa TRC na viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi 08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa.

Baadhi ya wadau wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka, wakifuatilia kikao cha uongozi wa TRC na viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi 08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa ( kushoto) akiwaonesha jambo baadhi ya viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu  baada ya kutembelea eneo ambalo litajengwa stesheni ya Malampaka wilayani Maswa wakati wa utekelezaji wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka, mara baada ya kikao chake na wadau hao kilichofanyika Machi 08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka Maswa .




ZAIDI YA MILIONI 138 ZATOLEWA MIKOPO KWA WANAWAKE SIMIYU

                

Katika mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri sita za Mkoa wa Simiyu zimetoa shilingi 138,030,500/= kwa vikundi 122 vya wanawake kama mikopo kutoka katika asilimia nne ya mapato ya ndani ya halmashauri, kwa ajili ya kuwapatia mitaji ya kuanzisha na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi. 

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga kupitia hotuba yake iliyosomwa kwa naiba yake na Mwanasheria wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bi, Manahamisi Kawega wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Machi 08, 2021 ambayo kimkoa yamefanyika Wilayani Maswa.

“Halmashauri ya Mji wa Bariadi, imetoa shilingi 10,000,000/= kwa vikundi 25, Halmashauri wilaya ya Bariadi shilingi 48,000,000/= vikundi 37, Busega shilingi 16,000,000/=kwa vikundi 16, Itilima shilingi 12,000,000/= vikundi 12, Maswa shilingi 39,200,000/= vikundi 18 na Meatu shilingi 12,830,500 kwa vikundi 14,” alisema.

Aidha, Mmbaga amewaagiza Wakurugenzi wa Mamalaka za Serikali za Mitaa kuendelea kutenga na kupeleka fedha asilimia nne kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake kwani haina riba kuliko mikopo kutoka taasisi nyingine za kifedha.

Vile vile Mmbaga amesema kauli mbiu ya siku ya wanawake mwaka 2021 “ Wanawake katika Uongozi:Chachu ya kufikia Dunia yenye Usawa” itumike kuwawezesha wanawake kwenye nafasi za uongozi katika mkoa wa Simiyu kwa kuwa jamii bado haijatambua umuhimu wa kumuwezesha mwanamke nafasi za uongozi tunapoelekea kwenye Dunia ya usawa.

Naye Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Bi. Haula Kachwamba ametoa wito kwa viongozi wanawake kufanya kazi kulingana na matarajio ya wanawake huku akisisitiza wahakikishe wanatafuta ufumbuzi wa changamoto za wanawake.

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera amewataka wanawake kujiamini na  kujitokeza katika fursa mbalimbali za uongozi katika jamii kwa kuwa viongozi wanawake ni wachache, hivyo kila fursa inapopatikana wasisite kujitokeza ili kuwe na viongozi wengi wanawake katika kuelekea dunia yenye usawa.

Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Kimkoa yaliambatana na maonesho ya shughuli za wanawake wajasiriamali, uchangiaji damu, kutoa misaada kwa wagonjwa ambapo chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali (TUGHE) walitoa msaada wa mashuka 30 kwenye wodi ya wazazi katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa.

MWISHO

Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bi. Mwanahamisi Kawega(wa pili kushoto) ambaye alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga kama Mgeni rasmi , akimsikiliza mjasiriamali mwanamke katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kimkoa Uwanja wa Nguzo nane Wilayani Maswa alipotembelea mabanda ya maonesho Machi 08, 2021.

Baadhi ya watumishi wanawake kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakiwa wamebeba bango kwenye maandamano ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzo nane Machi 08, 2021.



Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera  akitoa salamu kwa wanawake wa mkoa wa Simiyu wakati maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa Machi 08, 2021.
 Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Simiyu,Mama Mariam Manyangu Mwera  akitoa salamu kwa wanawake wa mkoa wa Simiyu wakati maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa Machi 08, 2021.
Baadhi ya watumishi wanawake kutoka Ofisi mbalimbali za Mkoa wa Simiyu wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe maalum kwenye maandamano ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzo nane Machi 08, 2021.


Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakiimba wimbo wenye ujumbe maalum katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Machi 08, 2021 ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nugzonane wilayani Maswa.

Baadhi ya wanawake wakikimbia mbio za magunia ikiwa ni sehemu ya burudani katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Machi 08, 2021 ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nugzonane wilayani Maswa.


Baadhi ya viongozi na wanawake wa mkoa wa Simiyu wakicheza wimbo maalum  ulioimbwa na baadhi ya walimu wa kike katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Machi 08, 2021 ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.

Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bi. Mwanahamisi Kawega(wa pili kulia) ambaye alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga kama Mgeni rasmi , akimsikiliza mdau katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa Uwanja wa Nguzo nane Wilayani Maswa alipotembelea mabanda ya maonesho Machi 08, 2021.

Vijana wa sarakasi wakitoa burudani wakati maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa Machi 08, 2021.

Kutoka kulia, Katibu Tawala wa Wilaya ya Maswa  Bi. Agnes Alex, Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bi. Mwanahamisi Kawega wakiteta jambo wakati maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa Machi 08, 2021,(wa tatu kushoto) ni  Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu Bi. Haula Kachwamba.
Baadhi ya wanawake wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa Machi 08, 2021.
Baadhi ya wanawake wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa Machi 08, 2021.

Baadhi ya wanawake wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa Machi 08, 2021.

Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bi. Mwanahamisi Kawega(wa pili kushoto) ambaye alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga kama Mgeni rasmi , akimsikiliza mjasiriamali mwanamke katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kimkoa Uwanja wa Nguzo nane Wilayani Maswa alipotembelea mabanda ya maonesho Machi 08, 2021.
Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bi. Mwanahamisi Kawega(katikati) ambaye alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga kama Mgeni rasmi , akiangalia baadhi ya bidhaa za wajasiriamali mwanamke katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kimkoa Uwanja wa Nguzo nane Wilayani Maswa alipotembelea mabanda ya m

Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bi. Mwanahamisi Kawega(wa pili kushoto) ambaye alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga kama Mgeni rasmi , akimsikiliza mjasiriamali mwanamke katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kimkoa Uwanja wa Nguzo nane Wilayani Maswa alipotembelea mabanda ya maonesho Machi 08, 2021.

Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bi. Mwanahamisi Kawega ambaye alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga kama Mgeni rasmi , akizungumza na mwanamke katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kimkoa Uwanja wa Nguzo nane Wilayani Maswa alipotembelea mabanda ya maonesho Machi 08, 2021.

Baadhi ya watumishi wanawake kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakiwa kwenye maandamano ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzo nane Machi 08, 2021.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Maswa,Bi. Agnes Alex akitoa salamu kwa wanawake wa mkoa wa Simiyu wakati maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa Machi 08, 2021.




Baadhi ya watumishi wanawake kutoka Ofisi mbalimbali za Mkoa wa Simiyu wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe maalum kwenye maandamano ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzo nane Machi 08, 2021.
Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa akitoa taarifa ya chimbuko la Siku ya wanawake wakati maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa Machi 08, 2021.
Baadhi ya watumishi wanawake kutoka Ofisi mbalimbali za Mkoa wa Simiyu wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe maalum kwenye maandamano ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzo nane Machi 08, 2021.


Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!