Tuesday, December 31, 2019

TANROADS, TARURA SIMIYU WATAKIWA KUTENGA FEDHA KUBORESHA BARABARA ZINAZOUNGANISHA SIMIYU NA MIKOA MINGINE


Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amezipongeza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoa wa Simiyu kwa kazi nzuri zinazofanya na kuzisisitiza kutenga bajeti ya kuboresha ujenzi wa Barabara zote zinazounganisha Mkoa wa Simiyu na mikoa mingine ili zipitike wakati wote.

Kiswaga ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Simiyu, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Desemba 30, 2019 mjini Bariadi ambapo amebainisha kuwa barabara zikiboreshwa zitarahisisha usafiri kwa wananchi na usafirishaji wa malighafi mbalimbali za viwanda na bidhaa zitakazozalishwa na viwanda, vinavyotarajiwa kujengwa Mwaka 2020.

“Kazi inayofanywa na TANROADS na TARURA ni kazi ambayo inatia moyo  na itakuwa na mchango mkubwa kwa viwanda vya nguo, glasi na vifaa tiba vitakavyoanzishwa mwakani; kwa maana ya material(malighafi) itakayoingia na bidhaa zitakazotengenezwa zitasafirishwa kwa urahisi,” alisema Kiswaga.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. John Mkumbo  amesema katika robo ya pili ya mwaka wa fedha 2019/20 kazi  za matengenezo ya barabara  ambazo zipo kwenye utekelezaji ni kilometa 108.12 na madaraja 14.3 sawa na 54.3% huku iliyokamilika kwa barabara kuu ni kilometa 246.52 na madaraja 19.71 sawa na 40.8%.

Kwa upande wake Mratibu wa TARURA mkoa wa Simiyu  Mhandisi Dkt. Philemon Msomba amesema kuwa wametekeleza jumla ya miradi 30 ambayo tayari imekamilika  yenye thamani ya shilingi 3,694,627,194 bila VAT .

Katika hatua nyingine  Mkuu wa wilaya ya Meatu, Dkt Joseph Chilongani amesema ni vyema wakala wa barabara nchini (TANROADS) na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini  (TARURA) kuboresha madaraja yaliyopo wilaya ya Meatu kwa kujenga madaraja ya juu badala ya yale yaliyopo sasa ambayo ni ya chini  ili  barabara hizo zipitike wakati wote.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu Enock Yakobo aliwataka wakala hao kuweka taa kwenye maeneo ya katika ya miji ili wananchi waweze kufanya biashara zao nyakati zote ( saa 24).

Mbunge wa Busega, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni ameshauri kuwa ni vema Serikali ikafanya marekebisho  katika mgao wa fedha za bajeti ya barabara kati ya wakala Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kutoka kwenye uwiano wa sasa,  ambapo TANROADS inapata asilimia 70 na TARURA  asilimia 30, iwe asilimia 40 kwa TARURA na asilimia 60 kwa TANROADS ili kuongeza ufanisi kwa TARURA.
MWISHO

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifungua kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka, kikao kilichofanyika Desemba 30, 2019 mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu, wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyowasilishwa katika kikao hicho, Desemba 30, 2019.


Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. John Mkumbo akiwasilisha taarifa katika  kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Desemba 30, 2019 mjini Bariadi.


Mratibu wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini Tanzania (TARURA) Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Dkt.Philemon Msomba  akiwasilisha taarifa katika  kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Desemba 30, 2019 mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini , akifafanua jambo katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Desemba 30, 2019 mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akichangia hoja katika  kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Desemba 30, 2019 mjini Bariadi.
Mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe. Njalu Silanga akichangia hoja katika  kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Desemba 30, 2019 mjini Bariadi.
 
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu, wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyowasilishwa katika kikao hicho, kilichofanyika Desemba 30, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu, wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyowasilishwa katika kikao hicho, kilichofanyika Desemba 30, 2019 Mjini Bariadi.



Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo akichangia hoja katika  kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Desemba 30, 2019 mjini Bariadi.


Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu, wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyowasilishwa katika kikao hicho, kilichofanyika Desemba 30, 2019 Mjini Bariadi.


Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu, wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyowasilishwa katika kikao hicho, kilichofanyika Desemba 30, 2019 Mjini Bariadi.


Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu, wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyowasilishwa katika kikao hicho, kilichofanyika Desemba 30, 2019 Mjini Bariadi.


Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu, wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyowasilishwa katika kikao hicho, kilichofanyika Desemba 30, 2019 Mjini Bariadi.


Mbunge wa Jimbo la Busega  Mhe. Dkt. Raphael Chegeni  akichangia hoja katika  kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Desemba 30, 2019 mjini Bariadi.



Monday, December 23, 2019

JAMII YATAKIWA KUACHA IMANI POTOFU MATUMIZI YA VIRUTUBISHI KWA WATOTO WA KIKE




Wito umetolewa kwa jamii kuondokana na mila potofu ya kuwazuia watoto wa kike wenye umri wa kuanzia miaka 10 mpaka 19 kutumia virutubishi vya madini chuma  na foliki asidi vinavyotolewa kwa rika hilo  kwa ajili ya kuwakinga na upungufu wa damu kwa madai kuwa virutubisho hivyo vibaharibu uzazi jambo ambalo halina ukweli.


Wito huo umetolewa na Afisa Lishe wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Chacha Magige katika kikao cha Kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa na Shirika lisilo la Kiserikali la AMREF Health Africa kwa kushirikiana na Serikali kilichofanyika jana Mjini Bariadi.

"Baadhi ya wazazi wamekuwa wakizuia watoto wao kupata virutubisho vinavyotolewa shuleni kutokana na imani potofu kwa madai kuwa vinaharibu uzazi; tunaendelea kutoka elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa virutubisho hivi na tunapendekeza masuala ya lishe yajumuishwe katika mitaala ya elimu na itakapobidi kufanyike mabadiliko ya mitaala ili kuongeza uelewa wa masuala haya kwa jamii," alisema Chacha.

Awali akitoa taarifa ya hali ya lishe ya Mkoa, Dkt. Magige amesema utoaji wa huduma kwa watoto wenye utapiamlo umeongezeka kutoka asilimia 14 mwaka  2017 hadi kufikia asilimia 88.4 Septemba 2019; huku uwekezaji katika utoaji wa elimu ya unasihi wa masuala ya lishe ngazi ya jamii pia ukiongezeka kutoka asilimia 50 mwaka 2017 hadi asilimia 72.2 Septemba 2019.

Kwa upande wake Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Ngulyati wilayani Bariadi, Nyabuho Paschal ambaye pia ni muelimishaji rika, amesisitiza watoto wa kike kuona umuhimu wa kutumia Virutubishi vya Madini Chuma na foliki asidi kwa kuwa vina mchango mkubwa katika rika balehe kwa wasichana na kutosikiliza maneno ya upotoshaji yanayotolewa na baadhi ya wazazi na walezi kuhusu virutubishi hivyo.

Naye Mratibu wa lishe ya Mama, watoto na vijana balehe kutoka Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia,  wazee na watoto, Bibi. Tufingene Malambugi amesema katika ziara iliyofanywa na Kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start katika vituo vya kutolea huduma za afya wilayani Bariadi, ilibainika kuwa shughuli mbalimbali za afya na lishe zinatolewa  ikiwemo matibabu ya utapiamlo na utoaji wa elimu ya lishe.

Meneja Mradi wa Right Start Initiatives  mikoa ya Simiyu na Mwanza, Dkt. Rita Mutayoba amesema pamoja na shughuli za afya na lishe mradi huu pia unatoa elimu ya lishe ngazi ya jamii kupitia vipeperushi na mabango, kufanya uhamasishaji kupitia wahudumu wa afya ngazi ya jamii, mikutano ya uhamasishaji ya mara kwa mara ambao unafanywa kwa kutumia ngoma za asili ili kufikisha ujumbe katika maeneo husika.

Sanjali na hilo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la AMREF Health Africa, Dkt. Florence Temu amewashukuru wadau wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika utekelezaji wa mradi wa Right Start unaotarajiwa kufikia ukomo  wake mwezi Machi 2020, huku akibainisha kuwa mradi huo umesaidia kuboresha masuala mbalimbali ya afya na lishe.

Wakati huo huo Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah Bw. Donatus Weginah amesema Mkoa wa Simiyu utaendelea kuweka mipango madhubuti ya kuendeleza shughuli mbalimbali za masuala ya afya na lishe zinazofanywa na Mradi wa Right Start na kuhakikisha malengo yaliyowekwa ya wananchi kuwa na lishe bora yanafikiwa.
MWISHO


 Afisa Lishe wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Chacha Magige  akiwasilisha taarifa yahali ya lishe katika Mkoa wa Simiyu, kwenye kikao cha kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, kilichofanyika Desemba 20, 2019 Mjini Bariadi.


 Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Mipango na Uratibu, katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah akifungua kikao cha kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, kilichofanyika Desemba 20, 2019 Mjini Bariadi.


 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, Dkt. Florence Temu akizungumza na wajumbe wa kikao cha kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, kilichofanyika Desemba 20, 2019 Mjini Bariadi.


 Meneja Mradi wa Right Start, Dkt. Rita Mutayoba akiwasilisha taarifa ya mradi huo kwa wajumbe wa kikao cha kamati tendaji ya Kitaifa ya mradi huo unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, kilichofanyika Desemba 20, 2019 Mjini Bariadi.


 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo Dugange akizungumza na wajumbe wa kikao cha kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, kilichofanyika Desemba 20, 2019 Mjini Bariadi.


 Baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, wakiwa katika kikao kilichofanyika Desemba 20, 2019 Mjini Bariadi.

 Afisa Lishe wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Chacha Magige (kulia) akiwaongoza baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, wakati walipotembelea kituao cha Afya cha Ngulyati wilayani Bariadi Desemba 19, 2019 kujionea hali ya utekelezaji wa masuala ya lishe .
 Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Ngulyati wilayani Bariadi, Nyabuho Paschal  akitoa elimu kwa wanfunzi wenzake kuhusu masuala ya matumizi na umuhimu wa virutubishi kwa wasichana balehe wakati wa ziara ya wajumbe wa kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, iliyofanyika shuleni hapo Desemba 19, 2019.
 Baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ngulyati iliyopo wilayani Bariadi, baada ya ziara yao yenye lengo la kujionea hali ya utekelezaji wa masuala ya lishe shuleni hapo Desemba 19, 2019.
 Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah akizungumza na Baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, walipomtembelea ofisini kwake  Desemba 19, 2019 Mjini Bariadi.
 Baadhi ya wakina mama na wakina baba wakipata elimu ya masuala ya lishe katika kituo cha afya cha Ngulyati .
 Baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, wakiwa katika kikao kilichofanyika Desemba 20, 2019 Mjini Bariadi.
 Baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, wakiwa katika shule ya msingi Ngulyati iliyopo wilayani Bariadi, kwenye  ziara yao yenye lengo la kujionea hali ya utekelezaji wa masuala ya lishe shuleni hapo Desemba 19, 2019.
 Baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, wakiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ngulyati iliyopo wilayani Bariadi, baada ya ziara yao yenye lengo la kujionea hali ya utekelezaji wa masuala ya lishe shuleni hapo Desemba 19, 2019.
 Mratibu wa Lishe ya baba na mtoto na vijana balehe kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Bibi. Tufingene Malambugi akitoa maelekezo kwa Muuguzi wa Wodi ya Wazazi katika Kituo cha Afya cha Ngulyati, Bi. Kabula Tambilija wakati wa ziara ya wajumbe wa kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, katika kituo hicho Desemba 19, 2019.
 Mwenyekiti wa kikao cha kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, Bw. Donatus Weginah (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo na watumishi wa AMREF, mara baada ya kikao hicho kumalizika Desemba 20, 2019 Mjini Bariadi.
 Mwenyekiti wa kikao cha kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, Bw. Donatus Weginah (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo kutoka wizara mbalimbali mara baada ya kikao hicho kumalizika Desemba 20, 2019 Mjini Bariadi.
 Mwenyekiti wa kikao cha kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, Bw. Donatus Weginah (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo kutoka wizara mbalimbali mara baada ya kikao hicho kumalizika Desemba 20, 2019 Mjini Bariadi.
 Afisa Lishe wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Chacha Magige  akiwasilisha taarifa yahali ya lishe katika Mkoa wa Simiyu, kwenye kikao cha kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, kilichofanyika Desemba 20, 2019 Mjini Bariadi.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah akizungumza na Baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, walipomtembelea ofisini kwake  Desemba 19, 2019 Mjini Bariadi.

Wednesday, December 11, 2019

RC MTAKA AIPONGEZA AGPAHI KWA KUTEKELEZA MIRADI YENYE TIJA KWENYE SEKTA YA AFYA

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka Shirika lisilo la Kiserikali linaloshughulikia masuala ya UKIMWI la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) kwa kutekeleza miradi yenye tija  katika sekta ya Afya ambayo inayoonekana na inayowagusa wananchi moja kwa moja.

Mhe. Mtaka ametoa pongezi hizo Desemba 6, 2019 kwenye kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa Afya  mkoani Simiyu kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu mjini Bariadi

Mtaka alisema AGPAHI miongoni mwa wadau wa afya mkoani Simiyu shirika ambalo  limefanya kazi nzuri  ambayo inaonekana kutokana na kwamba imekuwa ikifanya vitu vinavyoonekana katik sekta ya afya mkoani humo kwa kusaidia wananchi.

“Nawapongeza sana AGPAHI kazi yenu inaonekana kazi yenu haihitaji tochi ili kuona mnachofanya, huwezi kuzungumzia mafanikio ya mkoa wa Simiyu kwenye sekta ya afya bila kuwataja AGPAHI”, alisema Mhe. Mtaka.

“Tunazo taasisi takribani 14 zinazojishughulisha na masuala ya afya mkoani Simiyu; hawa wadau 13 wangefanya walau robo tu ya kilichofanywa na AGPAHI,tungekuwa na maendeleo makubwa sana katika mkoa wetu na nchi kwa ujumla”,aliongeza Mtaka.

Aidha, Mtaka aliipongeza Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI inayoongozwa na Watanzania kwa kutekeleza miradi inayogusa maisha ya wananchi huku akitoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano wa AGPAHI na kuahidi kushirikiana na wote wa maendeleo mkoani humo ili katika kuwaletea maendeleo wananchi.

 .

“Wajumbe wa bodi ya AGPAHI mna ujasiri wa kutembelea miradi yenu kwenye mikoa kwa sababu miradi ipo.Nyinyi mna vitu,magari yenu pia yamekuwa yakitusaidia sana.Kuna baadhi ya taasisi hazina ujasiri wa kutembelea miradi kwa sababu hawana miradi,wengine kazi yao ni kugonga semina tu mwaka mzima.Hebu tufanye kazi zinazogusa wananchi tubadilishe mkoa huu”,alieleza Mtaka.


Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Dkt. Edith Ngirwamungu alisema AGPAHI inatekeleza miradi yake ya UKIMWI kwa kushirikiana na serikali lengo likiwa ni kuhakikisha fedha zinazotolewa na wafadhili zinawanufaisha watanzania.

“Tunaushukuru mkoa wa Simiyu kwa ushirikiano mnaotupatia,tunajitahidi kufanya kazi kuwafikia wananchi,AGPAHI tunataka mtoto asizaliwe na maambukizi ya VVU,hivyo tutaendelea kushirikiana na serikali katika kutoa huduma za VVU na UKIMWI kwa wananchi”,alisema Dkt. Ngirwamungu.

Alisema AGPAHI inaendelea kuongeza ubora na upatikanaji wa huduma za matunzo na tiba za VVU kwa watoto wachanga,vijana na watu wazima katika mikoa ya Simiyu,Mwanza,Mara na Shinyanga.

Meneja Miradi AGPAHI mkoa wa Simiyu Dkt. Julius Sipemba alisema AGPAHI inatoa huduma za VVU na UKIMWI kwa mkoa mzima wa Simiyu ambapo alibainisha kuwa Simiyu una vituo 233 vya kutolea huduma za afya na 73 kati ya hivyo hupata usimamizi wa moja kwa moja kutoka AGPAHI. Alisema wagonjwa wanaopata huduma kwenye vituo 73 ni sawa na 95% ya wagonjwa wote walioko kwenye vituo 233.

"AGPAHI inaboresha miundombinu kwa kujenga na kukarabati majengo, huduma za maabara kwa kununua madawa na vifaa 'iliwezesha maabara za wilaya kutoka nyota moja mpaka tatu', imetoa magari mapya kwa halmashauri 4 kati ya 6, imetoa pikipiki, msaada wa kuchunguza kifua kikuu, Saratani ya mlango wa kizazi",alieleza Dkt. Sipemba.

Aliongeza kuwa AGPAHI pia inaajiri watoa huduma wa afya kwenye maeneo yenye uhitaji na inatoa mafunzo kwa watoa huduma kulingana na miongozo ya wizara ya afya.


Wakiwa mkoani Simiyu,Wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI wametembelea Kituo cha Tiba na Matunzo cha Hospitali ya Mji wa Bariadi,kukutana na Mganga Mkuu wa mkoa wa Simiyu na Mkuu wa mkoa wa Simiyu pamoja na wadau wa VVU na UKIMWI mkoani Simiyu.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu Desemba 6,2019. Kushoto ni Mkurugenzi wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa,kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Dkt. Edith Ngirwamungu.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Dkt. Edith Ngirwamungu akizungumza  katika kikao cha wadau wa afya na kueleza kuwa AGPAHI itaendelea kushirikiana na serikali katika kutoa huduma za VVU na UKIMWI.
 Mganga Mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt. Festo Dugange akichangia hoja wakati wa kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi.  




Katibu Tawala mkoa wa Simiyu Bw. Jumanne Sagini akichangia hoja wakati wa kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi. 


Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu Desemba 6, 2019 kilichofanyika Mjini Bariadi.


Kijana James Leonard akielezea jinsi alivyonufaika na Klabu za watoto na vijana zinazohudumiwa na AGPAHI wakati wa kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi. 


Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI wakiwa kwenye kikao cha Bodi hiyo na  wadau wa afya mkoani, kilichofanyika Desemba 6, 2019 kilichofanyika Mjini Bariadi.


Picha ya pamoja uongozi wa mkoa wa Simiyu,AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu mara baada ya kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI  na wadau wa Afya mkoani Simiyu kilichofanyika Desemba 6, 2019 kilichofanyika Mjini Bariadi.


Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji, Dkt. Gamitwe Mahaza akichangia hoja wakati wa kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi. 
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia hoja wakati wa kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi. 
 Meneja Miradi AGPAHI mkoa wa Simiyu Dkt. Julius Sipemba akiwasilisha mada kuhusu shughuli zinazofanywa na Shirika lisilo la Kiserikali la AGPAHI mkoani Simiyu katika kikao kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi.  




Baadhi ya viongozi na wadau wa afya mkoani Simiyu wakiwa katika kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi. 


Picha ya pamoja uongozi wa mkoa wa Simiyu,AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu mara baada ya kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI  na wadau wa Afya mkoani Simiyu kilichofanyika Desemba 6, 2019 kilichofanyika Mjini Bariadi.



Picha ya pamoja uongozi wa mkoa wa Simiyu,AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu mara baada ya kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI  na wadau wa Afya mkoani Simiyu kilichofanyika Desemba 6, 2019 kilichofanyika Mjini Bariadi.


Baadhi ya viongozi na wadau wa afya mkoani Simiyu wakiwa katika kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi. 


Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini akiagana na baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI mara baada ya kikao cha Bodi hiyo na  wadau wa afya mkoani, kilichofanyika Desemba 6, 2019 kilichofanyika Mjini Bariadi.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  akiagana na baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI mara baada ya kikao cha Bodi hiyo na  wadau wa afya mkoani, kilichofanyika Desemba 6, 2019 kilichofanyika Mjini Bariadi.



Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!