Tuesday, March 26, 2019

IFM KUJENGA TAWI JIPYA SIMIYU


Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinatarajia kujenga Tawi jipya katika Kata ya Sapiwi Tarafa ya Dutwa wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.

Viongozi wa chuo hicho wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Tadeo Andrew Satta wametembelea eneo hilo leo Machi 26, 2019 na baadaye kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa Mkoa wa Simiyu ambapo wamekubaliana kushirikiana  katika hatua zote kuanzia upimaji wa eneo mpaka ujenzi wa majengo ya chuo.

Akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Andrew Satta amewashukuru viongozi hao kwa kutoa eneo la ekari ishirini bure akaahidi kushirikiana na Serikali mkoani hapa kuhakikisha tawi hilo linajengwa mkoani Simiyu ili kusogeza karibu huduma kwa wananchi wa Simiyu.

Awali akizungumza na viongozi hao Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo iko tayari kushirikiana na viongozi wa Chuo hicho kwa kutoa wataalam watakaosaidia katika Usimamizi wa upimaji na akashauri ujenzi wa majengo ya chuo hicho ufanyike kwa kutumia mfumo wa ‘Force Account’  ili kupunguza gharama.

Amesema mfumo huu utapunguza gharama kwa kuwa hautumii wakandarasi badala yake ujenzi utafanywa na mafundi wa kawaida wakisimamiwa  na wahandisi wa ujenzi Mkoa na Halmashauri mkoani Simiyu huku vifaa vyote vya ujenzi vikinunuliwa  kwa pamoja na chuo hicho.

Aidha, amemhakikishia upatikanaji wa wanafunzi kwa kuwa hadi sasa Mkoa wa Simiyu bado una Vyuo vichache vya elimu ya juu, huku akibainisha kuwa tayari Serikali mkoani hapa imeshatoa ardhi bure kwa ajili ujenzi wa Matawi ya Vyuo mbalimbali vya elimu ya juu ikiwemo  Chuo cha Mipango, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Chuo cha Mahakama.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema wanaendelea kushawishi Taasisi nyingi za Elimu ya Juu kujenga matawi yake Mkoani hapa, ili kutoa nafasi kwa Wanasimiyu kupata elimu ya juu  itakayochangia kuleta mapinduzi makubwa  ya kiuchumi na kijamii.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akizungumza Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta alipomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.




 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akizungumza  na baadhi ya viongozi wa  Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), walipomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne A. Sagini (wa pili kushoto) akifurahia jambo na Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta( wa tatu kushoto) na watumishi wengine wa chuo hicho walimpomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati), baadhi ya watumishi wa Mkoa wa Simiyu (watatu wa mwanzo kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta( wa tano kulia) na watumishi wengine wa chuo hicho walimpomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta(kulia) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka walimpomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi , kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto), akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta( wa tatu kushoto) na watumishi wengine wa chuo hicho walimpomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea  na kuona eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Mwenyekiti wa RAAWU Taifa, Dkt. Micahel Mawondo  akizungumza jambo wakati Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta( wa tatu kushoto) na watumishi wengine wa chuo hicho walimpomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea  na kuona eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi , kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne A. Sagini (katikati),  baadhi ya watumishi wa Mkoa wa Simiyu (watatu wa mwanzo kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta( wa tatu kulia mbele) na watumishi wengine wa chuo hicho walimpomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea na kuona eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta akisaini Kitabu cha wageni katika Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) walimpomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea na kuona eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akizungumza  na baadhi ya viongozi wa  Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), walipomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu, katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne  Sagini (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi na watumishi  wa  Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), walipomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.



SIMIYU YAKISIWA KUTUMIA SHILINGI 175,260,331 KATIKA BAJETI YA MWAKA 2019/2020

Sekretarieti ya Mkoa  na Mamlaka za Serikali za Mitaa Mkoani Simiyu zimekisia kutumia jumla ya shilingi 175,260,331/=  kwa ajili ya miradi ya maendeleo, mishahara na matumizi mengineyo.


Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  Machi 15, 2019  wakati akiwasilisha rasimu ya Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti ya mwaka 2019/2020 katika kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC) kilichofanyika Mjini Bariadi.

Amesema katika kiasi tajwa, shilingi 41,960,264,000/= zitatumika katika miradi ya maendeleo,  shilingi 18,522,914,000/= kwa ajili ya matumizi mengineyo na shilingi 114,777,153,000/= kwa ajili ya mishahara.

Aidha, Sagini amesema Mamlaka za Serikali za Mitaa zimekadiria kukusanya jumla ya shilingi 13, 004,878,000/= kutokana na vyanzo vyake vya ndani, ambapo kati ya hizo shilingi 4,745,216,000/= sawa na asilimia 36.5 zitatumika katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo  na shilingi 8,259,662,000/= zitatumika kwa ajili ya uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Ameongeza kuwa mpango wa bajeti umezingatia masuala muhimu kwa mkoa ambayo ni kusimamia  na kudumisha masuala ya amani na utulivu, kuimarisha utawala bora na uwajibikaji kwa kuhakikisha uchaguzi wa Serikali za Mitaa unafanyika kwa amani na utulivu, kujenga mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje, kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya, elimu na maji hususani kwa wananchi waishio vijijini.

Masuala mengine ni Kuzisimamia Halmashauri ili kubuni,  kuandaa maandiko na kufuatilia utekelezajiwa miradi ya maendeleo ya kuongeza kipato cha halmashauri, kuimarisha mipango ya matumizi bora ya ardhi,kuendeleza ujenzi wa ofisi, nyumba za viongozi na hospitali za wilaya Itilima, Bariadi na Busega.

Pamoja na hayo mpango huu umezingatia kuimarisha upatikanaji wa huduma za kijamii na kiuchumi, kuimarisha  usimamizi wa mapato ya ndani na kuibua vyanzo vipya, kuhuisha mipango mkakati ya mkoa na halmashauri na kuanza kutekeleza dhana ya kuimarisha utendaji wa kuongeza tija katika utekelezaji wa kazi na miradi ya kiuchumi.

Awali akifungua kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemshukuru  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Magufuli kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na Hospitali tatu za Wilaya mkoani hapa.

“Tunamshukuru Mhe. Rais kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa na pia tumepata shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya ya Bariadi, Busega na Itilima” alisema  Mtaka .

Katika hatua nyingine Mtaka  amewapongeza Wabunge wa Mkoa huu kwa namna wanavyoshiriki katika kuhimiza shughuli za maendeleo huku akiwataka viongozi wote kuwaunga mkono ikiwa ni pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo kujipambanua katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo itawasaidia kuongeza kipato, huku ikiipongeza wilaya ya Maswa kwa kuanza utekelezaji wa ujenzi wa kiwanda cha vifungashio na upanuzi wa kiwanda cha chaki miradi ambayo itakuwa chanzo cha uhakika cha mapato kwa Halmashauri.

Wajumbe mbalimbali waliohudhuria katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa waliunga mkono mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2019/2020 huku wakisisitiza Halmashauri kuwa na miradi ya kimkakati ili ziweze kupata vyanzo vipya vya mapato na wananchi kujiunga na bima ya afya ili kujihakikishia huduma za matibabu.

“Ninashauri Halmashauri ziwe na mradi ya kimkakati itakayoziongezea mapato yao ya ndani kama ilivyofanya Maswa ambayo inaenda kuwa na viwanda vikubwa viwili cha chaki na kiwanda cha vifungashio,  tena hasa nashauri kasi iongezeke hapa Bariadi ambapo ndiyo sura ya Mkoa”alisema Gungu Silanga Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa,kupitia Simiyu.

“Mhe. Mkuu wa Mkoa naunga mkono suala la kuhamasisha wananchi wetu kujiunga na Bima ya Afya tena natoa wito kwa viongozi wenzangu tuwe mabalozi kwa wananchi wetu tuwaelimishe na kuwahamasisha kujiunga na Bima ya Afya ili wawe na uhakika wa kupata matibabu”alisema Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Mhe. Pius Machungwa.
MWISHO
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(kushoto)akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC) kilichofanyika Machi 15, 2019 Mjini Bariadi.

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akiwasilisha  rasimu ya Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti ya mwaka 2019/2020 katika kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC) kilichofanyika Machi 15, 2019 Mjini Bariadi.



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC) kilichofanyika Machi 15, 2019 Mjini Bariadi.


Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe akichangia jambo katika kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC) wa Simiyu kilichofanyika Machi 15, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi wa Simiyu wakifuatilia kwa makini kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC) kilichofanyika Machi 15, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa Halmashari ya Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe akichangia jambo katika kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC) wa Simiyu kilichofanyika Machi 15, 2019 Mjini Bariadi.
Meneja wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Bariadi(BARUWASA) akichangia jambo katika kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC) wa Simiyu kilichofanyika Machi 15, 2019 Mjini Bariadi.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa kupitia Simiyu, Mhe. Gungu Silanga akichangia jambo katika kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC) wa Simiyu kilichofanyika Machi 15, 2019 Mjini Bariadi.




Baadhi ya viongozi wa Simiyu wakifuatilia kwa makini kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC) kilichofanyika Machi 15, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi wa Simiyu wakifuatilia kwa makini kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC) kilichofanyika Machi 15, 2019 Mjini Bariadi.


Saturday, March 16, 2019

DARAJA LA SIBITI KUKAMILIKA MACHI 24 MWAKA HUU


Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. Albert Kent amesema Ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti linalounganisha Mikoa ya Simiyu na Singida unatarajiwa kukamilika kwa awamu ya kwanza na magari kuanza kupita ifikapo Machi 24, mwaka huu.

Kent ameyasema hayo jana Machi 14, 2019 katika kikao cha bodi ya Barabara kilichofanyika Mjini Bariadi, kinachowashirikisha viongozi na wadau mbalimbali wakiwemo watendaji wa Wakala wa Barabara(TANROADS) na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA)Mkoani humo.

Kent amesema agizo la Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la kuhakikisha wanakamilisha daraja hilo kufikia mwezi Machi, 2019 ambalo alilitoa wakati aipoweka jiwe la Msingi la ujenzi wa daraja hilo Septemba, 2018.

“Ujenzi wa Daraja la Sibiti awamu ya kwanza kama ilivyoagizwana Mhe. Rais utakamilika tarehe 24 mwezi huu,mkandarasi anaendelea na umaliziaji watutala barabara kwenye mwingilio wa daraja kubwa; taratibu za kuongeza kazi ili kukamilisha kuweka tabaka la lami kilomita 25 zinaendelea” alisema Mhandisi. Kent.

Katika hatua nyingine Kent ameeleza mapenddkezo ya bajeti kuwa TANROADS Mkoa wa Simiyu imependekeza na kuomba jumla ya shilingi 11, 461,470 kwa ajili ya matengenezo ya barabara zenye urefu wa kilometa 1008.76, madaraja makubwa 62 na madaraja madogo 50.

Naye Mratibu wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), Mkoa wa Simiyu, Mhandisi.Salvatory Yambi amasema bajeti ya matengenezo ya barabara chini ya wakala huo Mkoani Simiyu ni shilingi 5,469,051,603.32 (Bajeti inayozingatia ukomo).

Nao baadhi ya wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara wametoa maoni yao juu ya kazi ya matengenezo ya barabara inayofanywa na TANROADS pamoja na TARURA kama ifuatavyo:-

“Tunaomba Serikali ione namna ya kuiongezea bajeti TARURA ili iweze kutekeleza majukumu yake vizuri maana na mtandao mkubwa wa barabara mjini na vijijini, itoke kwenye asilimia 30 na kufikia asilimia 40 na TANROADS wabaki na asilimia 60 kutoka kwenye asilimia 70 ya sasa” Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Bariadi, Mhe. Robert Lweyo

“ Sisi tumeanza ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Bariadi pale , tunaomba TARURA waweke kwenye bajeti yao fedha za ujenzi wa daraja la Mto Bariadi unaounganisha kata saba za Halmashauri yetu” alisema Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Bahame Kaliwa.

“ Naishukuru sana TANROADS kwa kuweka taa katika Mji wa Lamadi, mmepafanya Lamadi papendeze na watu waweze kufanya biashara vizuri, ombi langu muone uwezekano wa kuweka taa katika Mji wa Nyashimo ambao ndiyo makao makuu ya Wilaya ya Busega”Mhe. Tano Mwera, Mkuu wa Wilaya ya Busega.

Naye Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemtaka Mratibu wa TARURA Mkoa kuhakikisha agizo la Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Pombe Magufuli la kujenga barabara ya kilometa tatu katika Mji Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mwanhuzi.
 MWISHO

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. Albert Kent akitoa taarifa ya matengenezo ya barabara na madaraja kwa wajumbe wa Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa, kilichofanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi..


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa kilichofanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.


Mratibu wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa  wa Simiyu, Mhandisi.Salvatory Yambi, akiwasilisha taarifa ya matengenezo ya barabara zilizo chini ya wakala huo, katika Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa kilichofanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Ephraim Lema akichangia hoja katika kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa kilichofanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Bariadi, Mhe. Robert Lweyo akichangia hoja katika kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa kilichofanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi(kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera wakiteta jambo, katika Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe na wadau wa Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Simiyu wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyowasilishwa katika kikao hicho ambacho kilifanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe na wadau wa Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Simiyu wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyowasilishwa katika kikao hicho ambacho kilifanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akichangia hoja katika kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa kilichofanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe na wadau wa Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Simiyu wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyowasilishwa katika kikao hicho ambacho kilifanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.





RAS SIMIYU AWATAKA WATUMISHI SIMIYU KUWA MABALOZI WEMA WA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA


Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amewataka watumishi wa Umma mkoani humo kuwa mabalozi wema wa maadili ya utumishi wa umma katika maeneo ya kazi ikiwa ni pamoja na kutopokea zawadi kwa wananchi wanaowahudumia kwa kuwa wanalipwa mshahara na Serikali kwa kazi hizo.

Sagini ameyasema hayo Machi 14, 2019 Mjini Bariadi wakati akifungua mafunzo ya Kamati za Kudhibiti Uadilifu za Mkoa wa Simiyu, yanayoendeshwa na Mratibu wa Utawala Bora kutoka Ofisi ya Rais kwa kushirikiana na  Maafisa kutoka TAKUKURU na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Amesema watumishi wa umma wanalipwa mishahara ili waweze kuwahudumia wananchi hivyo hawapaswi kudai chochote kutoka kwa wananchi.

"'Acheni kupokea vizawadi vidogo vidogo kwa huduma tunazotoa kwa wananchi ambazo tunalipwa mshahara kutokana na huduma hizo; muwe mabalozi wa kueneza maadili mema kwa watumishi wenzenu na nje ya maeneo yenu ya kazi ili ofisi zetu za Umma mkoani Simiyu ziwe mfano wa kuigwa" alisema Sagini.

Aidha, Sagini amezitaka kamati zote za kudhibiti uadilifu mkoani Simiyu  mara baada ya mafunzo ziandae mpango kazi wa namna ya kushughulikia kero mbalimbali za watumishi zinazohusiana na ukiukwaji wa maadili katika utumishi wa Umma, ili kuwa na watumishi wanaozingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ya Utumishi wa Umma.

Akitoa taarifa ya mwenendo wa makosa ya rushwa kwa watumishi wa umma, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu, Bw. Adili Elinipenda ametoa wito kwa Wakurugenzi kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU kuona namna watakavyosaidia pale wanapoletewa barua za kuwafikisha watumishi mahakamani  kwa makosa ya rushwa ili kutokuharibu ushahidi.

“Kesi tulizonazo mahakamani nyingi ni za watumishi wa umma na baadhi ya mashahidi tunaowahitaji wanatoka ofisi hizo hizo sasa wakurugenzi wamekuwa hawawasimamishi kazi,  kwa hiyo imekuwa ngumu kwa mtumishi kumtolea ushahidi mtumishi mwenzake aliye naye ofisi moja na wakati mwingine ni bosi wake, sasa hapa nafikiri mtaona ni busara gani itumike tunapowatumia barua za kuwafikisha watu mahakamani” alisema Mkuu huyo wa TAKUKURU.

Naye Mratibu wa Utawala Bora kutoka Ofisi ya Rais Ikulu, Bw. Apolinari Tamayamali amesema ni vema Mamlaka za Serikali za Mitaa zikazingatia utaratibu wa sheria unaopaswa kufuatwa wakati mtumishi anapohukumiwa kifungo au faini ili kupata ufumbuzi wa suala hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bi. Pendo Haule kuhusu kusimamishwa kazi kwa mtumishi ambaye ameshtakiwa mahakamani amesema kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, sheria imempa nafasi  mwajiri ya kumsimamisha kazi au kutomsimamisha kazi mtumishi  ambaye ana kesi mahakamani, lakini ikiwa kuwepo kwa mtumishi huyo kazini kunaweza kuharibu ushahidi ni vema sheria ikafuatwa akasimamishwa kazi.

Awali akizungumzia  lengo la kuandaa mafunzo kwa kamati za kudhibiti wa Uadilifu,  Mratibu wa Utawala Bora kutoka Ofisi ya Rais Ikulu, Bw. Apolinari Tamayamali, amesema ni kuwezesha kamati hizo kupata uelewa wa pamoja juu ya mkakati wa mapambano dhidi ya rushwa awamu ya tatu, namna ya kuandaa mpango kazi na utoaji wa taarifa katika masuala ya mapambano dhidi ya rushwa hapa nchini.

Ameongeza kuwa jithada hizi za kutoa elimu kwa kamati za udhibiti wa uadilifu zimaeanza mwaka 2017, ambapo hadi kufikia mwaka 2018 mikoa takribani 16 imefikiwa na kwa sasa timu ya wataalam iko katika mikoa yote 10 iliyo salia ili kukamilisha mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.
MWISHO

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(katikati) akizungumza na wajumbe wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu za Mkoa wa Simiyu(hawapo pichani) wakati akifungua mafunzo ya kamati hizo, Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.
Mratibu wa Utawala Bora kutoka Ofisi ya Rais Ikulu, Bw. Apolinari Tamayamali akizungumza na wajumbe wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu za Mkoa wa Simiyu(hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kamati hizo, Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu, Bw. Adili Elinipenda akitoa taarifa ya mwenendo wa makosa ya rushwa kwa watumishi wa umma, wakati wa mafunzo ya Kamati za Kudhibiti Uadilifu za Mkoa wa Simiyu, yaliyofanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi. 

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(katikati) akiwa katika Picha ya pamoja na Maafisa kutoka Ofisi ya Rais Ikulu na wajumbe wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu za Mkoa wa Simiyu, baada ya kufungua mafuzo ya kamati hizo Mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu za Mkoa wa Simiyu wakifuatilia mafunzo ya kamati hizo yaliyotolewa Machi 14, 2019 Mjini Bariadi na wataalam kutoka Ofisi ya Rais Ikulu.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu za Mkoa wa Simiyu wakifuatilia mafunzo ya kamati hizo yaliyotolewa Machi 14, 2019 Mjini Bariadi na wataalam kutoka Ofisi ya Rais Ikulu.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu za Mkoa wa Simiyu wakifuatilia mafunzo ya kamati hizo yaliyotolewa Machi 14, 2019 Mjini Bariadi na wataalam kutoka Ofisi ya Rais Ikulu.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na wajumbe wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu za Mkoa wa Simiyu(hawapo pichani) wakati akifungua mafunzo ya kamati hizo, Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na wajumbe wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu za Mkoa wa Simiyu (hawapo pichani) wakati akifungua mafunzo ya kamati hizo, Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.

Friday, March 15, 2019

ASILIMIA 80 YA WANANCHI SIMIYU KUTUMIA BIMA YA AFYA


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa huo umejiwekea malengo ya kuhakikisha zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wake kuwa na kadi za bima ya afya ili kujihakikishia upatikanaji wa  huduma za matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya hapa nchini.
.
Mtaka ameyasema hayo wakati ufunguzi wa Jukwaa la Ushirika Afya wa Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.

Amesema yeye kama Mkuu wa Mkoa atafanya vikao na wanachama wa AMCOS  na makundi mbalimbali ya wananchi katika wilaya zote mkoani hapa na kuzungumza nao kuwaelimisha juu ya umuhimu wa kila mwananchi kuwa na Bima ya Afya kwa ajili ya matibabu.

Aidha, amesema atawaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuwa katika Vyama vya Ushirika Vya Msingi ambavyo vinawapa nafasi ya kupata matibabu makubwa katika vituo vya kutolea huduma za afya vya binafsi na vya umma kwa gharama nafuu ya shilingi 76,800/= kwa mtu mmoja(mwanachama wa ushirika).

“Nitafanya vikao na wanachama wa AMCOS zote, wakulima, wafugaji, wajasiriamali, makundi yote ya wananchi kwenye mkoa wetu wa Simiyu, tuweze kuwaelimisha faida ya mwananchi wa mkoa wa Simiyu kuwa na bima ya afya, kubwa zaidi umuhimu wa kuwa kwenye ushirika ambao utamwezesha kupata matibabu makubwa kwa bei nafuu” alisema

Katika hatua Nyingine Mtaka amesema katika kipindi cha msimu wa pamba katika kila kituo cha kununulia pamba NHIF itaweka Afisa wake kwa ajili ya kusajili wakulima na wanachama wa vyama vya ushirika walio tayari, hivyo akatoa wito kwa viongozi walioshiriki jukwaa la ushirika afya kutoa taarifa na elimu kwa wenzao juu ya umuhimu wa suala hilo.

Mtaka pia ametoa wito kwa wakulima wote wa pamba kulipa kipaumbele suala la afya kwa kuchukua hatua ya kuwa na bima za afya ili waweze kuona manufaa ya Serikali kuboresha huduma za afya ikiwa ni pamoja na kujenga Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Hospitali za wilaya kwa kila wilaya na Vituo vingine vya kutolea huduma za afya.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko  wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernad Konga  amesema NHIF ni wadau wakubwa mkoani Simiyu, hivyo wako tayari kutoa huduma bora na wanawafikia wananchi wa makundi yote mkoani hapa na watahakikisha wanatoa kadi za bima ya afya kwa wakati kwa wanachama wote watakaojiunga.

Katika jukwaa hili  washiriki wamepata nafasi ya kuchangia michango mbalimbali huku wanachama wa AMCOS wakiunga mkono mpango huo wa kupata bima ya afya kwa gharama ya shilingi 76,800/= ili waweze kumudu gharama za matibabu.

“Mpango huu nimeupokea vizuri ila ninashauri elimu iendelee kutolewa zaidi na zaidi ili wanachama wote wajue umuhimu wa kuwa na kadi za bima ya afya na namna zitakavyowasaidia” Lucas Ephraim mshiriki kutoka AMCOS ya Dutwa Bariadi.

“ Binafsi niko tayari kujiunga na mfuko wa bima ya afya ili nipate hiyo kadi itakayonifanya niweze kutibiwa popote hapa Tanzania, lakini naomba tutakapolipia hiyo 76,800/= kadi zetu tuzipate mapema” Mmoja wa Wanachama wa Vyama vya Ushirika vya msingi, Bw. Magwashi Gandila

Mkoa wa Simiyu una vyama vya Ushirika Vya Msingi(AMCOS) zaidi ya 300 na Jukwaa hili limeazimia wanachama wa AMCOS  wakawe mabalozi wazuri  kuwahamasisha wananchi kujiunga na Bima ya Afya.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)mkoani humo katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.


Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), Benard Konga akizungumza na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)mkoani humo,  katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) aizungumza na Meneja wa Wanachama kutoka NHIF(kushoto) na Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), Benard Konga, mara baada ya kumalizika kwa Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi wa Serikali na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)mkoani Simiyu, wakifuatilia masuala mbalimbali yakiwasilishwa katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi wa dini, viongozi na watumishi wa Serikali na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)mkoani Simiyu, wakifuatilia masuala mbalimbali yakiwasilishwa katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Mwanachama wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Dutwa wilayani Bariadi, Bw. Lucas Ephraim akichangia hoja katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akitoa taarifa ya utangulizi katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kupitia mkoa wa Simiyu, Mhe.  Gungu Silanga ,akichangia hoja katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Mkoa wa Simiyu(SIMCU), Bw........ akichangia hoja katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Mmoja wa Wanachama wa Vyama vya Ushirika vya msingi akichangia hoja katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.

Shekhe Mkuu wa BAKWATA Mkoa wa Simiyu, Shekhe Mahamoud Kalokola akitoa dua kwa ajili ya ufunguzi wa Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.


Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!