Friday, July 31, 2020

CRDB YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 60 UDHAMINI WA NANENANE KITAIFA 2020 SIMIYU

Benki ya CRDB imekabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 60 kama mchango wa udhamini wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yanayofanyika katika  Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu, Kanda ya Ziwa Mshariki inayoundwa na mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga kuanzia 01 Agosti, 2020 mpaka 08 Agosti, 2020 

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Julai 30, 2020 Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Bw. Lusingi Sitta amesema benki hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia wakulima ambapo amesema benki hiyo imejipanga katika kuhakikisha kuwa wakulima wote wa pamba wanapata malipo yao kupitia akaunti za benki ya CRDB.

“Tumehakikisha kuwa AMCOS zote tumefungua nao akaunti kama CRDB tutahakikisha kwamba kila mkulima anayeuza pamba yake atalipwa kupitia akaunti yake ya CRDB na tumejipanga kwamba kila alipo mkulima wa pamba nasi tupo hapo ,” alisema Lusingi.

Aidha, Lusingi amesema CRDB imefungua tawi lingine katika Wilaya ya Meatu ambapo amebainisha kuwa benki hiyo imepeleka gari ambalo lina mahitaji yote muhimu katika utoaji wa huduma na wateja(wananchi ) hivyo wanaweza kupata huduma zote katika gari hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ameishukuru benki ya CRDB kwa kukubali kuwa mdhamini Mkuu wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 na kwa namna ambavyo imekuwa ikiwajali wateja hususani wakulima ambapo imetoa zaidi ya asilimia 60 ya mikopo kwa wanunuzi wa pamba msimu wa mwaka 2019/2020 ili pamba ya wakulima inunuliwe.

“Kuna maana kubwa sana kwa CRDB kudhamini maonesho ya nanenane kwa sababu, lengo la maonesho haya ni kuwasaidia wakulima wa kawaida kwenda kwenye ukulima wa kisasa, hivyo inapotokea CRDB inajitokeza kusaidia maonesho kufana, inaenda sambamba na lengo la nchi la kuinua wakulima wadogo wadogo kwenda kwenye ukulima wenye tija,” alisema Kiswaga.

Wakati huo huo Kiswaga amewahakikishia viongozi wa benki ya CRDB kuwa serikali itaendelea kufanya kazi na benki hiyo katika matawi yote huku akitoa wito kwa viongozi hao kutosita kuwaeleza viongozi wa serikali kila wanapohitaji msaada katika maeneo mbalimbali.

Katika hatua nyingine Kiswaga ametoa wito kwa wananchi kutoka mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga inayounda Kanda ya Ziwa Mashariki ya Maonesho ya Nanenane pamoja na maeneo mengine ndani na nje ya nchi; kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maonesho ya Nanenane Kitaifa huku akiwahakikishia kuwa maonesho hayo yatakuwa ya tofauti kuwataka watarajia kuona teknolojia mbalimbali zinazoleta mapinduzi katika kilimo.

Kauli Mbiu ya Maonesho ya Nanenane mwaka 2020 ni “KWA MAENDELEO YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020.”

MWISHO

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Bw. Lusingi Sitta (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (kulia) mfano wa hundi ya shilingi milioni 60, Julai 30, 2020  ikiwa ni udhamini wa Benki hiyo katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yatakayofanyika  Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu; Kiswaga amepokea kwa niaba ya Wakuu wa mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga inayounda Kanda ya Ziwa Mashariki ya Maonesho hayo.

:- Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Bw. Lusingi Sitta akizungumza na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu kabla ya kukabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 60, leo  Julai 30, 2020  ikiwa ni udhamini wa Benki hiyo katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yatakayofanyika  Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.

Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Benki ya CRDB baada ya makabidhiano ya  mfano wa hundi ya shilingi milioni 60, leo  Julai 30, 2020  ikiwa ni udhamini wa Benki hiyo katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yatakayofanyika  Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga akizungumza mara baada ya kupokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 60, leo  Julai 30, 2020 kitoka kwa Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa Bw. Lusingi Sitta ikiwa ni udhamini wa Benki hiyo katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yatakayofanyika  Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu; Kiswaga amepokea kwa niaba ya Wakuu wa mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga inayounda Kanda ya Ziwa Mashariki ya Maonesho hayo.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Bw. Lusingi Sitta (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga baada ya makabidhiano ya  mfano wa hundi ya shilingi milioni 60, leo  Julai 30, 2020  ikiwa ni udhamini wa Benki hiyo katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yatakayofanyika  Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Bw. Lusingi Sitta (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga baada ya makabidhiano ya  mfano wa hundi ya shilingi milioni 60, leo  Julai 30, 2020  ikiwa ni udhamini wa Benki hiyo katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yatakayofanyika  Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.

Thursday, July 30, 2020

NMB YATOA MILIONI 42.5 KUCHANGIA MAONESHO YA NANENANE SIMIYU

Benki ya NMB imetoa shilingi milioni 42.5 kwa ajili ya kudhamini Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yatakayofanyika katika kanda ya Ziwa Mashariki  Viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Agosti 01 hadi Agosti 08, 2020.

Akikabidhi mfano wa hundi ya fedha hizo Julai 27, 20202  kwa Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi, Bw. Sospeter Magese amesema pamoja na mchango huo, NMB imetoa fulana 300 ambazo zitatumika katika maonesho hayo.

Bw. Magese amesema NMB imekuwa ikidhamini maonesho haya tangu mwaka wa 2018 yalipoadhimishwa kwa mara kwanza mkoani Simiyu ambapo mpaka sasa benki hiyo  imeshatoa shilingi 100.

“Pamoja na kudhamini maonesho ya nanenane Benki ya NMB imekuwa ifanya kazi na katika maeneo mengi katika sekta ya elimu pamoja na kilimo; katika kilimo ndani ya miaka miwili tumeweza kufungua akaunti 500,000 lakini kati ya hizo akaunti 86,000 ni za wakulima wa pamba wa mkoa wa Simiyu,” alisema Magese.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa mkoa wilaya ya Bariadi, Mku wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ameishukuru Benki ya NMB kwa namna inavyojitoa kusaidia mambo mbalimbali katika mkoa wa Simiyu ikiwemo katika sekta ya elimu pamoja na kilimo huku akiwahakikishia kuwa serikali iko tayari kushirikiana na benki hiyo kila itakapohitaji.

Katika hatua nyingine Kiswaga ametoa wito kwa wananchi wa mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na maeneo yote nchini kujitokeza kwa wingi kujionea maonesho ya kilimo nanenaneyanayofanyika Kitaifa katika kanda ya ziwa Mashariki ili kuona fursa mbalimbali pamoja na teknolojia rahisi zinazotumika katika sekta ya kilimo.
MWISHO

 Meneja wa NMB kanda ya magharibi, Bw. Sospeter Magese (kushoto) akikabimkabidhi Mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga mfano wa hundi ya shilingi milioni 42.5 kama ikiwa ni mchango wa wa benki hiyo kwa ajili ya maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Viwanja vya vya Nyakabindi mkoani hapa. Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na Meneja wa NMB Tawi la Bariadi, Bw. Gabriel Paul.

 Meneja wa NMB kanda ya magharibi, Bw. Sospeter Magese (kushoto) akimkabikabidhi Mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga moja ya fulana kama ikiwa ni mchango wa wa benki hiyo kwa ajili ya maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Viwanja vya vya Nyakabindi mkoani hapa. Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na Meneja wa NMB Tawi la Bariadi, Bw. Gabriel Paul.
 Meneja wa NMB Tawi la Bariadi, Bw. Gabriel Paul akitoa taarifa ya utangulizi kabla ya makabidhiano ya fulana 300 na mfano wa hundi ya shilingi milioni 42.5  kati ya Meneja wa NMB kanda ya magharibi, Bw. Sospeter Magese ( wa pili kushoto)  na Mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga(wa tatu kushoto) ikiwa ni mchango wa benki hiyo kwa ajili ya maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Viwanja vya vya Nyakabindi mkoani hapa.

Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na viongozi wa NMB baada ya makabidhiano ya fulana 300 na mfano wa hundi ya shilingi milioni 42.5  kati ya Meneja wa NMB kanda ya magharibi, Bw. Sospeter Magese ( wa nne kushoto)  na Mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga(wa tano kushoto) ikiwa ni mchango wa benki hiyo kwa ajili ya maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Viwanja vya vya Nyakabindi mkoani hapa.

Wednesday, July 29, 2020

RC MALIMA: TUNAWAKARIBISHA WANANCHI KUJIONEA NANENANE KITAIFA 2020 YA KIWANGO

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Kighoma Malima ametoa wito wananchi wa mikoa ya Simiyu, Mara, Shinyanga na maeneo mengine nchini kafika katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yatakayofanyika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu katika Kanda ya Ziwa Mashariki inayoundwa na mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga  ili wajionee maonesho yenye kiwango.

Mhe. Malima ameyasema hayo Juni  27, 2020 katika kikao cha maandalizi ya Maonesho hayo ambayo yatafanyika kitaifa katika kanda hiyo kwa mara ya tatu mfululizo kilichofanyika katika Uwanja wa Maonesho wa nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

“Ingawa maandalizi yetu yaliathiriwa na changamoto ya Corona bado tuna uhakikia wa kufanya vizuri kwani tumepita kuangalia maendeleo ya vipando, vipando viko katika hali nzuri na tunaamini kuwa maonesho haya yatakwenda vizuri kama ilivyo kawaida yetu, hivyo tunawakaribisha wananchi wote kushiriki maonesho haya ambayo yatakuwa ya viwango,” alisema Malima.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack amesema Kanda ya Ziwa Mashariki itafanya vizuri katika maonesho ya kitaifa mwaka 2020 kuliko miaka miwili  ya mwanzo, kwa kuwa pamoja na changamoto zilizojitokeza katika maandalizi kumekuwa na mwamko mkubwa wa ushiriki wa wadau katika maonesho haya.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amesema wadau mbalimbali zikiwemo taasisi binafsi na za Umma, wananchi wakiwemo wajasiriamali na wafanyabiashara wameonesha mwitikio mkubwa na wanaendelea na maandalizi ambapo alibainisha kuwa katika maonesho ya nanenane mwaka huu washiriki takribani 500 wanatarajiwa kushiriki.

Aidha Bi. Mmbaga ametoa wito kwa wananchi wote nchini hususani wa mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga kuitumia vizuri fursa ya kuwa maonesho haya ya Kitaifa kufanyika katika kanda ya ziwa Mashariki na wajitokeze kwa wingi katika maonesho haya ili waweze kupata kuona mambo mbalimbali yatakayosaidia kuongeza tija kwenye maeneo yao ya uzalishaji

Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yanaongozwa na Kauli Mbiu inayosema “KWA MAENDELEO YA KILIMO MIFUGO NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020.”
MWISHO
 Baadhi ya viongozi na wataalam wakitembelea vipando mbalimbali  vya mazao vilivyoandaliwa kwaa jili ya maonesho ya nanenane kabla ya kikao cha maandalizi ya maonesho ya nanenane Kitaifa ambayo yanafanyika katika kanda ya ziwa mashariki inayojumuisha mikoa hiyo mitatu ambayo yatafanyika kwa mara ya tatu mfululizo sasa  katika Uwanja wa NaneNane Nyakabindi jana uwanjani hapo.

 Mkuu wa mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima akizungumza na viongozi na wataalam kutoka mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga katika kikao cha maandalizi ya maonesho ya nanenane Kitaifa ambayo yanafanyika katika kanda ya ziwa mashariki inayojumuisha mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ambayo yatafanyika katika Uwanja wa NaneNane Nyakabindi jana uwanjani hapo.

 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na viongozi na wataalam kutoka mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga katika kikao cha maandalizi ya maonesho ya nanenane Kitaifa ambayo yanafanyika katika kanda ya ziwa mashariki inayojumuisha mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ambayo yatafanyika katika Uwanja wa NaneNane Nyakabindi jana uwanjani hapo.

AANGALIA BAADHI YA PICHA ZA VIONGOZI KATIKA KIKAO CHA MAANDALIZI YA NANENANE, PICHA ZAO WAKITEMBELEA VIPANDO, PICHA ZA VIPANDO, MAJENGO NA UJENZI WA MAHEMA

Tuesday, July 28, 2020

RC MALIMA: TUNAWAKARIBISHA WANANCHI KUJIONEA NANENANE KITAIFA 2020 YA KIWANGO

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Kighoma Malima ametoa wito wananchi wa mikoa ya Simiyu, Mara, Shinyanga na maeneo mengine nchini kafika katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yatakayofanyika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu katika Kanda ya Ziwa Mashariki inayoundwa na mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga  ili wajionee maonesho yenye kiwango.

Mhe. Malima ameyasema hayo Juni  27, 2020 katika kikao cha maandalizi ya Maonesho hayo ambayo yatafanyika kitaifa katika kanda hiyo kwa mara ya tatu mfululizo kilichofanyika katika Uwanja wa Maonesho wa nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

“Ingawa maandalizi yetu yaliathiriwa na changamoto ya Corona bado tuna uhakikia wa kufanya vizuri kwani tumepita kuangalia maendeleo ya vipando, vipando viko katika hali nzuri na tunaamini kuwa maonesho haya yatakwenda vizuri kama ilivyo kawaida yetu, hivyo tunawakaribisha wananchi wote kushiriki maonesho haya ambayo yatakuwa ya viwango,” alisema Malima.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack amesema Kanda ya Ziwa Mashariki itafanya vizuri katika maonesho ya kitaifa mwaka 2020 kuliko miaka miwili  ya mwanzo, kwa kuwa pamoja na changamoto zilizojitokeza katika maandalizi kumekuwa na mwamko mkubwa wa ushiriki wa wadau katika maonesho haya.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amesema wadau mbalimbali zikiwemo taasisi binafsi na za Umma, wananchi wakiwemo wajasiriamali na wafanyabiashara wameonesha mwitikio mkubwa na wanaendelea na maandalizi ambapo alibainisha kuwa katika maonesho ya nanenane mwaka huu washiriki takribani 500 wanatarajiwa kushiriki.

Aidha Bi. Mmbaga ametoa wito kwa wananchi wote nchini hususani wa mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga kuitumia vizuri fursa ya kuwa maonesho haya ya Kitaifa kufanyika katika kanda ya ziwa Mashariki na wajitokeze kwa wingi katika maonesho haya ili waweze kupata kuona mambo mbalimbali yatakayosaidia kuongeza tija kwenye maeneo yao ya uzalishaji.

Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yanaongozwa na Kauli Mbiu inayosema “KWA MAENDELEO YA KILIMO MIFUGO NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020.”

Baadhi ya viongozi na wataalam wakitembelea vipando mbalimbali  vya mazao vilivyoandaliwa kwaa jili ya maonesho ya nanenane kabla ya kikao cha maandalizi ya maonesho ya nanenane Kitaifa ambayo yanafanyika katika kanda ya ziwa mashariki inayojumuisha mikoa hiyo mitatu ambayo yatafanyika kwa mara ya tatu mfululizo sasa  katika Uwanja wa NaneNane Nyakabindi jana uwanjani hapo.

Wednesday, July 22, 2020

TACAIDS YAKABIDHI MASANDUKU 10 YA KUCHANGIA FEDHA ZA KUBORESHA HUDUMA ZA VVU NA UKIMWI SIMIYU

Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI imekabidhi masanduku 10 kutoka Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi kwa Mkoa wa Simiyu ili yatumike kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za VVU na UKIMWI.

Akikabidhi masanduku hayo Mkurugenzi wa TACAIDS Dkt. Leonard Maboko amesema karibuni Wafadhili wamepunguza kwa kiasi kikubwa ufadhili katika masuala ya Ukimwi ni  vema zikatumika  fedha zetu wenyewe (wadau wa ndani)  badala ya kutegemea Wafadhili

“ Ili Kuchangia fedha hizo Mfuko  umebuni Masanduku ambayo Wanainchi wanaweza kutoa michango kwa Fedha taslim, tumeleta masanduku haya 10 ikiwa ni maagizo ya Waziri wa nchi ofisi ya Waziri  Mkuu Kazi, Vijana,Ajira na Wenye  Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama ambaye alikuwa mgeni rasmi akimwakilisha  Mhe. Kassim Majaliwa  Waziri Mkuu,wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Mwanza 2019”

“ Katika maadhimisho hayo kila mkoa uliagizwa kuwa na   masanduku hayo na kuhamasisha wananchi kuchangia jitihada hizi, Siku ya Ukimwi Duniani 2020 kila mkoa utatakiwa kutoa taarifa kuwa umechangia Serikali kiasi gani kupitia Mfuko wa Udhamini wa  kudhibiti Ukimwi, alisema Dkt. Maboko.

Aidha, Dkt. Maboko amesema michango hiyo inaweza  kuwakilishwa kwa kuchangia Moja kwa moja au kupitia AIrtel Money +255 684 909090 au kwa Viongozi kuchukua masanduku na kuhamasisha wananchi kuchangia katika ziara na matukio mbalimbali ambayo wao wanayaongoza huku akibainisha kuwa mpaka sasa fuko umeshaipatia Serikali kiasi cha shilingi 660.

Katika hatua nyingine Dkt. Maboko amefafanua kuwa katika fedha zote zinazokusanywa  katika mfuko huu, asilimia 60 hutumika kwenye ununuzi wa dawa/vitendanishi,  asilimia 25 hutumika   kwenye kinga na asilimia 15 kwenye shughuli za bodi na Utawala.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Wa Simiyu, Mhandisi.Mashaka Luhamba ameshukuru TACAIDS kwa kutimiza ahadi ya kuleta masanduku hayo kama walivyoahidi kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa huku akiwahakikishia TACAIDS kuwa mkoa utatumia kila fursa kuhakikisha kuwa unawahamasisha Wananchi wa  Simiyu kuchangia katika Mfuko huu.

Akieleza hali ya maambukizi ya VVU/UKIMWI katika Mkoa wa Simiyu, Mratibu wa Kudhibiti UKIMWI Simiyu, Dkt.Khamis  Kulemba amesema kutokana na utafiti wa Mwaka  2016-2017 ushamiri wa maambuziki ya VVU Mkoani Simiyu umefikia kiwango cha  3.9%  ambayo ni chini ya  4.7% ikiwa ni  kiwango cha  kitaifa

“ Tunaendelea na kazi ya kuzuia maambukizi mapya kwa kuwezesha asilimia 90 watu wanatambua hali za afya zao,  asilimia 90% ya  wagonjwa  wanatumia dawa na asilimia 90 nyingine kushusha kiwango cha virusi vya UKIMWI katika damu ya Mgonjwa ( Viral suppression)

Dkt. Kulemba ameongeza kuwa Mkoani Simiyu asilimia 91 ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI wanatumia dawa za kufubaza makali ya VVU na kiwango cha maambukizi katika damu zao kimeshuka, huku akitoa wito kwa wananchi kuchangia mfuko wa kudhibiti UKIMWI kwani vita dhidi ya VVU/UKIMWI ni ya kila mmoja katika jamii.

Mfuko wa Udhamini wa kudhibiti ukimwi  ulianzishwa Mwaka  2015, Kusudi la Mfuko huu ni  kuchangia fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za VVU na UKIMWI.
MWISHO

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS),  Dkt. Leonard Maboko(kushoto) akimkabidhi moja ya sanduku Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,  Mhandisi.Mashaka Luhamba yaliyotolewa na TACAIDS kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za VVU na UKIMWI.
 Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,  Mhandisi.Mashaka Luhamba (kushoto) akimkabidhi Mratibu wa Kudhibiti UKIMWI Simiyu, Dkt.Khamis  Kulemba moja ya masanduku yaliyotolewa na TACAIDS kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za VVU na UKIMWI.
 Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,  Mhandisi.Mashaka Luhamba (katikati) akimshukuru Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS),  Dkt. Leonard Maboko baada ya makabidhiano ya masanduku 10 yaliyotolewa na TACAIDS kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za VVU na UKIMWI mkoani Simiyu.

 Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS),  Dkt. Leonard Maboko (kushoto) akizungumza kabla ya kukabidhi kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,  Mhandisi. Mashaka Luhamba (wa tano kulia) masanduku 10 yaliyotolewa na TACAIDS kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za VVU na UKIMWI mkoani Simiyu.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,  Mhandisi.Mashaka Luhamba  akizungumza kabla ya kupokea masanduku yaliyotolewa na TACAIDS kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za VVU na UKIMWI kutoka TACAIDS.

Sunday, July 19, 2020

SIMIYU YAJIPANGA KUONGEZA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA UGANI KUONGEZA TIJA KWENYE UZALISHAJI WA PAMBA

Katika kutekeleza mpango Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano (2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu, mkoa unakusudia kuongeza hali ya upatikanaji wa huduma za ugani kwa lengo la kuongeza tija katika uzalishaji kutoka kilo 175 kufikia kilo 600 kwa ekari ifikapo mwaka 2024.

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala msaidizi sehemu ya mipango na uratibu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah wakati akitoa mada katika mafunzo ya maafisa ugani, maafisa ushirika na viongozi waandamizi wa wilaya na Halmashauri juu utekelezaji wa mpango mkakati huo yaliyofanyika Julai 18, 2020 Mjini Bariadi.

Weginah amesema kutokana na upungufu wa maafisa ugani wapatao 200 katika mkoa wa Simiyu, mkoa unatarajia kutoa mafunzo ya muda mfupi ya kilimo bora cha pamba kwa baadhi ya vijana ili waweze kuwasaidia wakulima kulima kilimo chenye tija hususani katika maeneo ambayo hakuna maafisa ugani.

“Tunataka kuongeza uzalishaji kutoka wastani wa kilo 175 zinazozalishwa sasa hivi mpaka kufikia kilo 600 kwa ekari ifikapo mwaka 2024, ili tuweze kufikia hapo ni lazima tuhakikishe huduma za ugani ambazo ni changamoto zinapatikana, tutatumia vijana ambao watapa mafunzo ya muda mfupi ili waweze kuwapatia elimu wakulima wetu huko vijijini,” alisema Weginah.

Aidha, Weginah amebainisha kuwa mafunzo yataanza kwa vijana wataohudumia Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) 26 vilivyochaguliwa kuwa maeneo ya mfano ya kuanzia (pilot areas) kwa mwaka huu na baadaye kuanzia mwaka 2021 vijana hao watapelekwa katika mkoa mzima hususani katika maeneo yenye upungufu mkubwa wa maafisa ugani.

Afisa ugani wa kata ya Chinamili wilayani Itilima, Bw. Gaudence Mlay amesema vijana hao watakaopewa mafunzo pamoja na wakulima wawezeshaji watawasaidia maafisa ugani katika utoaji wa elimu kwa wakulima na watawafikia wakulima wengi zaidi kuliko ilivyo sasa ambapo katika baadhi ya maeneo afisa ugani mmoja anahudumia vijiji vitatu mpaka vinne.

Kwa upande wake Afisa Ushirika wa Halmashauri ya mji wa Bariadi, Bw. Billwater Mbilinyi amesema mkakati wa mapinduzi ya kilimo cha pamba umeanza kutekelezwa kwa kuwatambua wakulima, ukubwa wa maeneo wanayolima na mahitaji ya pembejeo jambo ambalo litasaidia wakulima kupata kiasi cha pembejeo kinachotakiwa  kwa wakati.

Wakati huo huo Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Simiyu, Bw. Ibrahimu Kadudu amesema katika utekelezaji wa mkakati huo mkoa wa Simiyu utahakikisha unasimamia matumizi ya mizani za kidijitali ambazo zitatatua changamoto ya mizani kuchezewa hivyo mkulima atapata kile anachostahili kupata wakati anapouza pamba yake.

Awali akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema mpango mkakati huo umekuja katika kipindi muafaka huku akitoa wito kwa wananchi, viongozi wa serikali, iongozi wa dini na wadau wengine wa pamba kuunga mkono utekelezaji wa mkakati huu kwa manufaa ya mkoa na Taifa kwa ujumla.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Mhandisi, Mashaka Luhamba akifunga mafunzo hayo amewataka washiriki wote wa mafunzo hayo kila mmoja akatimize wajibu wake katika kutekeleza mkakati huo kwa lengo la kufikia matokeo yaliyotarajiwa ikiwa ni pamoja na kuongeza tija ya kilimo cha pamba  kwa wakulima.

Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano (2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu ulizinduliwa rasmi tarehe 05  Machi 2020 na Naibu Waziri wa kilimo, Mhe. Hussein Bashe, ambapo utekelezaji wake umeanza na Vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS)  26 na baadaye utatekelezwa katika mkoa wote wa Simiyu.
MWISHO

Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Mipango na Uratibu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah akitoa mada katika mafunzo ya viongozi na wataalam juu ya utekelezaji wa mpango Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano (2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu yaliyofanyika Julai 17, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi na watalaam wa kilimo na ushirika wakifuatilia mada iliyowasilishwa katika mafunzo ya viongozi na wataalam juu ya utekelezaji wa mpango Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano (2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu yaliyofanyika Julai 17, 2020 Mjini Bariadi.
 Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka) akifungua mafunzo ya viongozi na wataalam juu ya utekelezaji wa mpango Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano (2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu yaliyofanyika Julai 17, 2020 Mjini Bariadi.

Kaimu katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Mhandisi. Mashaka Luhamba akifunga mafunzo ya viongozi na wataalam juu ya utekelezaji wa mpango Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano (2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu, yaliyofanyika Julai 17, 2020 Mjini Bariadi.

Mrajisi msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Simiyu, Bw. Ibrahimu Kadudu akiwasilisha mada  katika mafunzo ya viongozi na wataalam juu ya utekelezaji wa mpango Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano (2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu, yaliyofanyika Julai 17, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi na watalaam wa kilimo na ushirika wakifuatilia mada iliyowasilishwa katika mafunzo ya viongozi na wataalam juu ya utekelezaji wa mpango Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano (2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu, yaliyofanyika Julai 17, 2020 Mjini Bariadi.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bi. Suzy Sabuni akichangia hoja katika mafunzo ya viongozi na wataalam juu ya utekelezaji wa mpango Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano (2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu, yaliyofanyika Julai 17, 2020 Mjini Bariadi.
 Afisa Tarafa kutoka  wilayani Maswa akichangia hoja katika mafunzo ya viongozi na wataalam juu ya utekelezaji wa mpango Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano (2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu, yaliyofanyika Julai 17, 2020 Mjini Bariadi.

 Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu, akichangia hoja katika mafunzo ya viongozi na wataalam juu ya utekelezaji wa mpango Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano (2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu, yaliyofanyika Julai 17, 2020 Mjini Bariadi.

Afisa Kilimo wa Wilaya ya Meatu, akichangia hoja katika mafunzo ya viongozi na wataalam juu ya utekelezaji wa mpango Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano (2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu yaliyofanyika Julai 17, 2020 Mjini Bariadi.
 Baadhi ya viongozi na watalaam wa kilimo na ushirika wakifuatilia mada iliyowasilishwa katika mafunzo ya viongozi na wataalam juu ya utekelezaji wa mpango Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano (2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu yaliyofanyika Julai 17, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi na watalaam wa kilimo na ushirika wakifuatilia mada iliyowasilishwa katika mafunzo ya viongozi na wataalam juu ya utekelezaji wa mpango Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano (2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu yaliyofanyika Julai 17, 2020 Mjini Bariadi.
 Baadhi ya viongozi na watalaam wa kilimo na ushirika wakifuatilia mada iliyowasilishwa katika mafunzo ya viongozi na wataalam juu ya utekelezaji wa mpango Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano (2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu yaliyofanyika Julai 17, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi na watalaam wa kilimo na ushirika wakifuatilia mada iliyowasilishwa katika mafunzo ya viongozi na wataalam juu ya utekelezaji wa mpango Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano (2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu yaliyofanyika Julai 17, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi na watalaam wa kilimo na ushirika wakifuatilia mada iliyowasilishwa katika mafunzo ya viongozi na wataalam juu ya utekelezaji wa mpango Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano (2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu yaliyofanyika Julai 17, 2020 Mjini Bariadi. 

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!