Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela na Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wameongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi
ya aliyekuwa Katibu tawala wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, Bw. Boniphace
Maiga Juma aliyefariki dunia kwa ajali ya gari Julai 11, 2020, yaliyofanyika
Julai 13, 2020 kijiji cha Lyamisanga wilayani Butiama Mara.
Akitoa salamu za pole Mhe. Shigela amesema amepokea
taarifa ya kifo cha Bw. Boniphace Maiga kwa mshtuko na majonzi makubwa kwa kuwa
ameondoka wakati ambao taifa linamhitaji na kumtegemea.
“Boniphace alikuwa kiungo kati ya serikali na wananchi,
serikali kuu na halmashauri, serikali na taasisi; tangu nianze kufanya kazi na
Boniphace sijawahi kumuona amekasirika alikuwa mcheshi na alifanya kazi zake
kwa bidii na unyenyekevu mkubwa, niwahakikishie familia kuwa tutakuwa bega kwa
bega na ninyi popote mtakapohitaji msaada wetu, ” alisema Shigela.
“Mhe.
Rais alivyopata taarifa ya msiba huu alimsikitisha sana, alinipigia simu
alfajiri akiwa na taarifa zote na picha
zote za tukio, tunaye Rais anayependa watu wake, kwa hiyo wafiwa muamini
Boniphace ametangulia lakini amepanda mbegu ya upendo kwa Watanzania akiwepo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli” aliongeza
Shigela.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemzungumzia marehemu Boniphace kama rafiki yake na sehemu
ya familia yake, huku akiahidi kuendelea kushirikiana na familia ya marehemu(
mama mzazi na mke wa marehemu).
“Boniphace
alikuwa rafiki yangu na sehemu ya familia hivyo mimi na familia yangu
tutaendelea kuwa sehemu ya familia ya Boniphace, watu wa serikali wamezungumza
namna watakavyosaidia kama serikali lakini sisi kama familia kwa lile ambalo mtaona
mngehitaji msaada kutoka kwangu sisi bado tuko pamoja,” alisema Mtaka.
Akimzungumzia
marehemu Boniphace Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Godwin Gondwe ambeye alifanya
naye kazi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni amesema Boniphace alikuwa kijana
mchapakazi anayesikiliza na kutekeleza maagizo ya viongozi wake.
“Siku
aliyofariki Boniphace ndiyo siku nilikuwa naenda kumkabidhi ofisi Mkuu mpya wa
Wilaya ya Handeni, Mhe. Toba; siku hiyo tulifanya vikao vitatu mfululizo
kuanzia asubuhi mpaka jioni na siku hiyo marehemu Boniphace alikuwa na utani
mwingi sana, kweli kifo ni fumbo na hakuna anayeweza kuzoea kifo,” alisema
Gondwe.
Akitoa
salamu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima Mkuu wa Wilaya ya Rorya,
Mhe. Simon Chacha ametoa pole kwa familia ya marehemu na viongozi wote
waliofanya kazi na marehemu kwa kuondokewa na mtu ambaye kwa mkoa wa Mara
walimuona kama balozi wao kwa utendaji kazi wake uliotukuka.
Marehemu Boniphace Maiga Juma alizaliwa Aprili 17,
1984 ambapo enzi za uhai wake amewahi kuwa mwalimu na mtumishi wa tume ya
utumishi wa walimu na baadaye aliteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya
Handeni mwezi Mei 2018, ameacha mke na watoto watatu.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Mhe. Martine Shigela na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakitoa
heshima za mwisho kwa mwili wa Bw. Boniphace Maiga Juma aliyekuwa Katibu Tawala
wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga ambaye alifariki kwa ajali ya gari Julai
11,2020, kabla ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Lyamisanga wilayani
Butiama mkoani Mara Julai 13, 2020.Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Bw. Boniphace Maiga Juma , aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga ambaye alifariki kwa ajali ya gari Julai 11,2020, kabla ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Lyamisanga wilayani Butiama mkoani Mara Julai 13, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Bw. Boniphace Maiga Juma aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga ambaye alifariki kwa ajali ya gari Julai 11,2020, kabla ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Lyamisanga wilayani Butiama mkoani Mara Julai 13, 2020.
Kutoka kushoto aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Temeke, Mhe. Godwin Gondwe ambaye pia alikuwa mkuu wa wilaya ya Handeni, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Toba Nguvila, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Mhe. Simon Chacha wakifuatilia ibada ya mazishi ya Bw. Boniphace Maiga Juma aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga ambaye alifariki kwa ajali ya gari Julai 11,2020, kabla ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Lyamisanga wilayani Butiama mkoani Mara Julai 13, 2020.
Baadhi ya makatibu tawala wa wilaya nchini wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Bw. Boniphace Maiga Juma ambaye alifariki kwa ajali ya gari Julai 11,2020, katika mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Lyamisanga wilayani Butiama mkoani Mara Julai 13, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela (kushoto) na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakiteta jambo katika mazishi ya aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Bw. Boniphace Maiga Juma ambaye alifariki kwa ajali ya gari Julai 11,2020, kabla ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Lyamisanga wilayani Butiama mkoani Mara Julai 13, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya makatibu tawala wa wilaya nchini walioshiriki mazishi ya ya aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Bw. Boniphace Maiga Juma ambaye alifariki kwa ajali ya gari Julai 11,2020, baada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Lyamisanga wilayani Butiama mkoani Mara Julai 13, 2020.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Handeni mkoani Tanga wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Bw. Boniphace Maiga Juma ambaye alifariki kwa ajali ya gari Julai 11,2020, baada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Lyamisanga wilayani Butiama mkoani Mara Julai 13, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Bw. Boniphace Maiga Juma ambaye alifariki kwa ajali ya gari Julai 11,2020, baada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Lyamisanga wilayani Butiama mkoani Mara Julai 13, 2020.
Mkuu wa Wilaya ya
Temeke, Mhe. Godwin Gondwe ambaye pia aliwahi kuwa mkuu wa wilaya ya Handeni, akiteta
jambo na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Toba Nguvila wakati wa mazishi ya aliyekuwa
Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Bw. Boniphace Maiga Juma ambaye
alifariki kwa ajali ya gari Julai 11,2020, baada ya mazishi yake yaliyofanyika
kijiji cha Lyamisanga wilayani Butiama mkoani Mara Julai 13, 2020.
TAZAMA PICHA MBALIMBALI KATIKA MAZISHI YA ALIYEKUWA KATIBU TAWALA WA WILAYA YA HANDENI MKOANI TANGA
TAZAMA PICHA MBALIMBALI KATIKA MAZISHI YA ALIYEKUWA KATIBU TAWALA WA WILAYA YA HANDENI MKOANI TANGA
0 comments:
Post a Comment