Thursday, August 29, 2019

SIMIYU YAANDAA MKAKATI MAALUM WA MIAKA MITANO 2019-2024 WA MAPINDUZI YA KILIMO CHA PAMBA


Katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa  soko la pamba mkoa wa Simiyu umeandaa mkakati maalum wa miaka mitano (2019-2024) wa mapinduzi ya kilimo cha zao hilo ili kujibu changamoto zinazowakabili wakulima wa pamba.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Mkutano wa Wadau wa Pamba uliofanyika uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014,
Akifungua Mkutano huo Mtaka amesema upo umuhimu mkubwa kwa Mkoa wa Simiyu kuwa na kiwanda/viwanda vya kuongeza thamani ya zao la pamba ikiwemo viwanda vya nguo kama suluhisho la soko la pamba kwa wakulima.
“Kama hatutakuwa na viwanda vinavyoongeza thamani kwenye pamba,hata kama tukiongeza uzalishaji, itafika mahali tutatukanana tu, maana pamba itakuwa nyingi na hakuna mtu wa kukununua na wanaonunua wanajua hatuna kwa kuipeleka, kwa hiyo ni lazima tukubaliane na ndiyo maana tukasema tuje na mkakati huu unaoanza na mkulima kuanzia kwenye kulima” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka amesema ili kuwasaidia wakulima katika upatikanaji wa mikopo ni vema benki zikaweka utaratibu rafiki wa kutoa mikopo kwa wakulima huku akitoa wito kwa Benki Kuu kupitia Kurugenzi ya Sera kuandika maandiko ya miradi ya mazao ya mikakati likiwemo pamba ambayo yatasaidia katika kuyaongezea thamani mazao hayo.

Akiwasilisha mkakati huo kwa wadau wa pamba mkoani Simiyu, Katibu Tawala Msaidizi wa Mipango na Uratibu Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah amesema uongezaji thamani kwenye pamba mkoani Simiyu bado liko chini; ambapo kwa sasa kinachofanyika ni kutengenisha pamba nyuzi, mbegu na kuchuja mafuta, huku akibainisha kuwa matarajio ya mkoa ni kwenda kwenye hatua nyingine zaidi ya kuchambua pamba.

Pamoja na kuongeza thamani ya zao la pamba wadau wa pamba wametoa maoni mbalimbali katika kuboresha kilimo cha Pamba ili kiwe chenye tija na kubainisha kuwa “Ili tuweze kuboresha kilimo cha pamba ni lazima teknolojia zitakazokabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, wadudu na magonjwa” alisema Epifania Temu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo(TARI) Ukiriguru

“Mbegu ndiyo msingi wa tija ya pamba inayopaswa kuzalishwa kwenye soko, hivyo kwenye eneo lililokubaliwa kuzalisha mbegu kama Meatu na Igunga ginners (wenye viwanda vya kuchambua pamba) watakaokununua pamba ya eneo wapewe jukumu la kuzalisha mbegu ili kuwa na mwendelezo wa mbegu bora” alisema Mkondo Cornelius Afisa Kilimo Mkuu, Wizara ya Kilimo.

Mkurugenzi wa Miradi kutoka Gatsby Africa, Samweli Kilua ametoa wito kwa wadau wote kuhakikisha kila mdau anatimiza wajibu wake katika kuhakikisha mkakati huo unatekelezwa kwa ufanisi katika kuboresha kilimo cha pamba.


Akifunga kikao Katibu Tawalawa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema mkakati wa mapinduzi ya kilimo cha pamba Mkoani Simiyu utatekelezwa kwa vitendo  na akazitaka  Taasisi za fedha, viongozi na wataalam wanaosimamia wakulima, vyama vya ushirika  na wadau wengine waanze mazungumzo ili mkakati huo utakapoanza kutekelezwa kuwe na uelewa wa pamoja kwa wadau wote.

Mkutano wa kuboresha mkakati maalum wa miaka mitano (2019-2024) wa mapinduzi ya kilimo cha pamba ulijumuisha wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba ambao ni pamoja na viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Simiyu, Watalaam wa kilimo kutoka Taasisi za Utafiti wa Kilimo, Wizara ya Kilimo, Halmashauri na Mkoa, Watendaji wa Taasisi za Fedha, viongozi  wa vyama vya msingi vya ushirika.
MWISHO


 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba katika ufunguzi wa Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.


 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na Wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba katika Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.



Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Komredi Kheri James akitoa salamu zake kwa Wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba katika Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.



Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Komredi Enock Yakobo akizungumza na  Wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba katika Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.



Baadhi ya wadau wa kilimo cha pamba wakimsikiliza  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.



Baadhi ya wadau wa kilimo cha pamba Mkoani Simiyu wakifuatilia uwasilishaji wa Mkakati Maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014,  katika Mkutano wa kuboresha Mkakati huo uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa Miradi wa Gatsby Africa, Samweli Kilua akitoa taarifa ya namna shirika hilo lilivyoshiriki katika uaandaaji wa Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, kwenye mkutano wa kuboresha  mkakati huo uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa Miradi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wwa Mataifa(UNDP), Amon Manyama akichangia hoja Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Mipango na Uratibu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah akiwasilisha mkakati wa maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014,  katika Mkutano wa kuboresha Mkakati huo uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mmoja wa Wawakilishi wa Wakurugenzi na wamiliki wa Viwanda vya Kuchambua pamba kutoka kiwanda cha Alliance Ginneries Ltd, akichangia hoja katika Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza, akichangia hoja Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Simiyu, Mariam Manyangu, akichangia hoja katika Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe akichangia hoja katika Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wadau wa kilimo cha pamba Mkoani Simiyu wakifuatilia uwasilishaji wa Mkakati Maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014,  katika Mkutano wa kuboresha Mkakati huo uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya wadau wa kilimo cha pamba Mkoani Simiyu wakifuatilia uwasilishaji wa Mkakati Maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014,  katika Mkutano wa kuboresha Mkakati huo uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.


Baadhi ya wadau wa kilimo cha pamba Mkoani Simiyu wakifuatilia uwasilishaji wa Mkakati Maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014,  katika Mkutano wa kuboresha Mkakati huo uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.


Thursday, August 22, 2019

WANAFUNZI WALIOPATA SIFURI MTIHANI WA ‘MOCK’ KIDATO CHA NNE SIMIYU KUWEKWA KAMBI MAALUM YA KITAALUMA

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka amesema wanafunzi kidato cha nne waliopata daraja sifuri katika mtihani wa Mkoa wa Kujipima ‘Mock’ watawekwa  katika kambi maalum ya kitaaluma na kufundishwa na walimu mahiri  kwa lengo la kuwasaidia kuongeza ufaulu na kufikia  daraja la nne na kuendelea,  katika mtihani wa Taifa mwaka huu 2019.


Mtaka ameyasema hayo Agosti 22, 2019  katika kikao cha tathmini ya matokeo ya mtihani wa Mock kwa wanafunzi wa kidato cha nne na matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha sita mwaka 2019, ambapo mkoa wa Simiyu umekuwa miongoni mwa mikoa kumi bora Kitaifa.

Mtaka amesema lengo la Mkoa ni kuona wanafunzi wote waanafanya vizuri na hakuna mwanafunzi wa kidato cha nne anapata daraja sifuri hivyo wanafunzi wote wenye daraja sifuri na wale walipata daraja la nne alama za mwisho watawekwa pamoja na kutafutiwa walimu mahiri ili wawasaidie kupanda kitaaluma na kupata ufaulu mzuri.
\
“ Tutaweka kambi ya wanafunzi wote waliopata sifuri kwenye mtihani wa ‘Mock’ lakini pia hata wale waliopata daraja daraja la nne alama zinazoashiria kuelekea kwenye sifuri, Siku sitini kabla ya mtihani wafundishwe masomo manne tu, Civics(Uraia), Kiswahili, Kiingereza na Historia ngalau wapate alama D ili wapate cheti; nia yetu kama mkoa ni kuona kila mwanafunzi anafanya vizuri" alisema.

Katika hatua nyingine Mtaka amewahimiza wakuu wa shule kusimamia kwa karibu ufundishaji na kuhakikisha katika kipindi hiki kuelekea katika mitihani wa Taifa wa Kidato cha nne, kuongeza ufaulu kutoka nafasi ya tisa ya mwaka 2018 kwenda kwenye nafasi nzuri zaidi.

Afisa elimu wa mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju  amewataka wakuu wa shule na maafisa elimu kata na wilaya  kuendelea kusimamia ufundishaji ili wanafunzi waweze kufanya vizuri na wale ambao shule zao hazikufanya vizuri waimarishe usimamizi ili kuongeza ufaulu.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Itilima amezungumzia kambi maalum za kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata sifuri kwenye mtihani wa Mock ambao wapo takribani  2000 kati ya wanafunzi zaidi ya 9000, kwamba zitakuwa msaada kwao na wanatarajia kuzifanya kwa ufanisi ili mkoa uwe kati ya mikoa tisa bora Kitaifa mwaka 2019(Single digit).

Mkuu wa mkoa ameahidi kutoa shilingi elfu 30 kwa mwalimu katika kila alama A itakayopatikana kwenye somo lake, shilingi milioni tano kwa shule itakayoingia kumi bora kitaifa, Milioni tano kwa Halmashauri itakayoingia kumi bora kitaifa, na milioni mbili kwa mwanafunzi atakayepata ufaulu  daraja la kwanza pointi saba na kuwa katika kumi bora kitaifa na ikiwa hatakuwa miongoni mwa wanafunzi bora kitaifa atapewa shilingi milioni moja.

Mkutano wa tathimini ya matokeo ya kidato cha sita mkoani Simiyu unawakutanisha wakuu wa shule za sekondari,maafisa elimu wilaya ,wakurugenzi watendaji, wenyeviti wa halmashauri za wilaya na wenyeviti wa Kamati za Elimu za Halmashauri lengo likiwa ni kuangalia walipo na wanapoelekea katika maendeleo ya elimu mkoani Simiyu
MWISHO.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na viongozi na wadau wa elimu katika mkoawa Simiyu katika Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.

Maafisa Elimu wa Wilaya, kata, wakuu wa shule na wadau wengine wa elimu mkoani Simiyu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika kikao cha tathmini ya ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.



Maafisa Elimu wa Wilaya, kata, wakuu wa shule na wadau wengine wa elimu mkoani Simiyu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika kikao cha tathmini ya ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani), ya kufunga Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi zawadi mmoja wa walimu walifanikisha wanafunzi kupata  alama A  katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita mwaka 2019 katika Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi
\
Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Mkoa wa Simiyu akichangia hoja katika Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.




Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na viongozi na wadau wa elimu katika mkoawa Simiyu katika Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.

RC MTAKA AMPONGEZA JPM KUWA MWENYEKITI SADC, ATOA WITO KWA WAWEKEZAJI VIWANDA VYA DAWA, VIFAA TIBA










Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MHE. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini  mwa Afrika (SADC), ambapo pia ametoa wito kwa wawekezaji kuwekeza kwenye viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa nchini, ili kuiwezesha Bohari ya Dawa (MSD) ambayo ni mzabuni wa dawa na vifaa tiba wa nchi za SADC kupunguza uagizaji wa dawa na vifaa tiba nje ya nchi.

Mtaka ametoa pongezi hizo Agosti 21, 2019 wakati akifunga mkutano wa siku tatu wa Menejimenti ya Bohari ya Dawa (MSD) na mameneja wa Kanda za Bohari ya Dawa (MSD) uliofanyika kwa lengo la kufanya tathmini ya utendaji.

Mtaka amesema Bohari ya Dawa kama mzabuni wa dawa na vifaa tiba katika nchi za SADC wanapaswa kutumia fursa ya Rais Magufuli kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa kuhimiza wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda vya dawa na vifaa tiba.

“Nampongeza Rais Magufuli kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC na Pongezi nzuri kwa Mhe. Rais ni pale ambapo nchi yetu ambao pia tuna faida ya kuwa mzabuni wa dawa na vifaa tiba kwenye SADC; tutapata Watanzania wengi watakaochangamkia fursa ya kuwekeza na kutumia nafasi ya Tanzania kuwa Mwenyekiti wa SADC tukiwa na Idadi ya watu wengi kwenye soko la dawa na vifaa tiba” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka ameongeza kuwa Kiwanda cha Vifaa tiba kinachotarajiwa kujengwa mkoani Simiyu   


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifunga mkutano wa Menejimenti ya Bohari ya Dawa MSD Agosti 21, 2019  iliyofanyika kwa lengo la kufanya tathmini ya utendaji ambao umefanyika kwa muda wa siku tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Laurian Bwanakunu akizungumza na wajumbe wa menejimenti ya MSD katika Mkutano wao maalum wa tathmini ya utendaji ambao umefanyika kwa muda wa siku tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Bohari ya Dawa(MSD), Victoria Mwanri Elangwa  akitoa taarifa ya yaliyofanyika katika Mkutano wao maalum wa tathmini ya utendaji ambao umefanyika kwa muda wa siku tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu mkutano amabo umehitimishwa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka Agosti 21, 2019.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi na Mameneja wa Kanda wa Bohari ya Dawa (MSD) baada ya kufunga Mkutano wao maalum wa tathmini ya utendaji ambao umefanyika kwa muda wa siku tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Bohari ya Dawa(MSD), Victoria Mwanri Elangwa akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa  Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka Agosti 21, 2019 baada ya kufungwa kwa Mkutano maalum wa tathmini ya utendaji wa Menejimenti ya MSD ambao umefanyika kwa muda wa siku tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Bohari ya Dawa(MSD), Victoria Mwanri Elangwa akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa  Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka Agosti 21, 2019 baada ya kufungwa kwa Mkutano maalum wa tathmini ya utendaji wa Menejimenti ya MSD ambao umefanyika kwa muda wa siku tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

Mmoja wa Wakurugenzi katika Bohari ya Dawa(MSD) akitoa taarifa wakati wa kufunga Mkutano maalum wa tathmini ya utendaji wa Menejimenti ya MSD ambao umefanyika kwa muda wa siku tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Laurian Bwanakunu(wa pili kulia) na Wajumbe wengine wa Menejimenti ya MSD baada ya kufungwa kwa Mkutano maalum wa tathmini ya utendaji wa Menejimenti ya MSD ambao umefanyika kwa muda wa siku tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Bohari ya Dawa(MSD), Victoria Mwanri Elangwa akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa  Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka Agosti 21, 2019 baada ya kufungwa kwa Mkutano maalum wa tathmini ya utendaji wa Menejimenti ya MSD ambao umefanyika kwa muda wa siku tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.


Wednesday, August 21, 2019

MILA ZINAZOCHANGIA JAMII KUTOTUMIA VYOO ZIPIGWE VITA: RC MTAKA


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ametoa wito kwa jamii kupiga viya mila na desturi zinazochangia watu kutotumia vyoo na kusisitiza kila kaya ione umuhimu wa kuwa na choo bora, ikiwa ni njia ya kuboresha afya na usafi wa mazingira na kuondokana  na hatari ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

Mtaka ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo ambao umefanyika Agosti 20, 2019 Mjini Bariadi ambapo amesema ni  vema mila hizo zikapigwa vita ili jamii iweze kurudi kwenye msingi.

“Kwenye culture(tamaduni) zetu zipo sababu kwa nini baadhi ya watu walikuwa hawatumii vyoo ambazo ni sababu za kitamaduni, kwamba baba mkwe  hawezi kuchangia choo na mke wa kijana wake, kwa hiyo ilikuwa hata ukijenga choo kwa baadhi ya kaya huko nyuma bado kulikuwa na upinzani wa watumiaji”

“Unakuta kuna choo kwenye kaya Fulani lakini bado wanajamii wa hiyo kaya wanaenda kujisiri porini, huu ni utamaduni ambao ni lazima tuufanyie kampeni kama tulivyofanya kampeni za kukataa mambo mengine kama ukeketaji ili jamii zetu zirudi kwenye msingi, katika mkoa wetu kufikia mwezi Novemba, 2019 kila kaya itakuwa na choo bora na kinachotumika” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka amesema anaiunga mkono kwa asilimia 100 Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo kwa kuwa ni kampeni inayolisaidia Taifa katika usafi wa mazingira na kubainisha kuwa itakapofika mwezi Novemba 2019 kila kaya katika Mkoa wa Simiyu itakuwa na choo bora kinachotumika.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema Mkoa wa Simiyu umetajwa  kuwa na  kaya 215,316  ambapo kati ya hizo zenye vyoo ni 208,856  sawa na asilimia 97  na zenye vyoo bora zikiwa ni  97,536  sawa na asilimia 46.7.

Naye Mratibu  wa Kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Afya Anyitike Mwakitalima  amesema kampeni hii inafanyika kwa lengo la kusaidia uboreshaji wa afya nchini kwa sababu magonjwa mengi yanatokana na uchafu na njia moja wapo ya kukabili uchafu ni matumizi wa vyoo bora na unawaji wa mikono kwa maji safi, salama na sabuni.

 Amesema Serikali imeendelea kutoa elimu katika jamii kuhusiana na matumizi na ujenzi wa vyoo bora katika ngazi ya kaya na taasisi na tayari mikoa tisa imefikiwa, mkoa wa Simiyu ukiwa mkoa wa kumi ambapo amesema lengo ni kuifikia mikoa yote 26 kabla ya Juni 2020

Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo itafanyika kwa takribani siku 20 katika Halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu
MWISHO

Balozi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto(kushoto) akimkabidhi fulana yenye Ujumbe wa kampeni hiyo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka Ofisini kwake Mjini Bariadi kuashiria Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Balozi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto(kushoto) akimkabidhi fulana yenye maandishi ya kampeni hiyo Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini Ofisini katika Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na timu ya hamasa ya Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Ofisini kwake Mjini Bariadi wakati wa Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Balozi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpotoakizungumza katika Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akipandisha bendera ya Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo  wakati wa Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Balozi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto na Timu ya hamasa ya kampeni hiyo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) akizungumza katika Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akitoa taarifa ya hali ya vyoo Mkoani Simiyu wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo uliofanyika Agosti 20, 2019 Mjini Bariadi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na timu ya hamasa ya Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Ofisini Mjini Bariadi mara baada ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akionesha fulana yenye maneno ya Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Ofisini kwake Mjini Bariadi mara baada ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na timu ya hamasa ya Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Ofisini Mjini Bariadi mara baada ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akifurahia jambo na Balozi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto Mjini Bariadi mara baada ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Kutoka kulia ni Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Msanii na Balozi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Mrisho Mpoto na Mratibu wa Kampeni ya Taifa ya Usafi wa mazingira kutoka Wizara ya Afya, Bw. Anyitike Mwakitalima wakiteta jambo mara baada ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Balozi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto(kushoto) akimkabidhi fulana yenye Ujumbe wa kampeni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza  kwa naba ya Wakurugenzi wa Mkoa wa Simiyu kuashiria Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mjini Bariadi. Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019 .
Balozi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto(kushoto) akimkabidhi fulana yenye Ujumbe wa kampeni hiyo Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani kwa naba ya Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Simiyu wakati wa Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mjini Bariadi. Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019 .
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akiteta jambo na Balozi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto Mjini Bariadi mara baada ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
.



Tuesday, August 20, 2019

MSD KUJENGA KITUO CHA MAUZO NA USAMBAZAJI DAWA SIMIYU


Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya dawa (MSD)  Laurean Bwanakunu amesema Bohari ya dawa inatarajia kuanza ujenzi wa kituo cha mauzo na  usambazaji  dawa mkoani Simiyu ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa mkoa wa Simiyu na mikoa jirani.

Bwanakunu ameyasema hayo Agosti 19,2019 katika ufunguzi wa  mkutano wa tathmini ya utendaji  kazi wa menejimenti na mameneja wa kanda wa bohari ya dawa nchini.
lengo likiwa   ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu.

Bwanakunu amesema wameamua kufanyia mkutano wa tathimini mkoani Simiyu ili kuweza kujionea eneo la ujenzi wa kituo cha mauzo ya dawa ikiwa ni moja ya kuongeza wigo mpana wa utoaji huduma.

“Tutakuwa na mkutano wa siku tatu hapa Simiyu kwa ajili kufanya tathmini ya utendaji kazi ulivyokuwa kwa mwaka mzima, tutawafanyia tathmini wakurugenzi wote na wenyewe watamfanyia Mkurugenzi Mkuu; lakini pia tutatumia fursa hii kutembelea mahali tulipoamua kujenga bohari kwa kuwa tunatarajia kujenga bohari hapa Simiyu”alisema Bwanakunu.

Akifungua mkutano huu, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema  maboresho ya usambazaji wa dawa yaliyofanywa na Bohari ya Dawa (MSD) yameongeza upatikanaji wa dawa mkoani Simiyu ambapo kwa sasa upatikananji wa dawa ni zaidi ya asilimi 88.

Aidha, Sagini ametoa wito kwa Taasisi zote za Umma zinazohitaji maeneo kwa ajili ya kujenga Ofisi zao kufika mkoani Simiyu, ambapo amewahakikishia upatikanaji wa maeneo lengo likiwa ni kuendelea kusogeza huduma mbalimbali karibu na wananchi.

Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa  Bohari ya Dawa(MSD), Bibi. Victoria Elangwa amesema uwepo wa kituo cha kusambaza dawa Simiyu kutapunguza umbali kwa Mkoa wa Simiyu na mikoa ya Mara na Shinyanga  kupata huduma za Bohari ambazo kwa sasa zinapatikana Mwanza.

Ameongeza kuwa ujenzi wa Kituo hicho unatarajia kuanza mara moja kwa kuwa tayari wataalam wameshaanza kushughulikia masuala ya ukamilifu wa mazingira na baada kukamilisha kazi hiyo atatafutwa mkandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi.
MWISHO
Mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD)  Laurean Bwanakunu akitoa neno la utangulizi katika mkutano wa tathimini ya utendaji kazi wa  Bohari ya Dawa(MSD) unaofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu kwa siku tatu  na lengo likiwa  ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu, Agosti 19, 2019.

Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu akifungua mkutano wa tathimini ya utendaji kazi wa  Bohari ya Dawa(MSD) unaofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu kwa siku tatu  na lengo likiwa  ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu, Agosti 19, 2019.
Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu akifungua mkutano wa tathimini ya utendaji kazi wa  Bohari ya Dawa(MSD) unaofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu kwa siku tatu  na lengo likiwa  ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu, Agosti 19, 2019.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Bohari ya Dawa(MSD), Victoria Mwanri Elangwa akitoa taarifa katika mkutano wa tathimini ya utendaji kazi wa  Bohari ya Dawa(MSD) unaofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu kwa siku tatu  na lengo likiwa  ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu, Agosti 19, 2019.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, bw. Jumanne Sagini (wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa idara mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa nchini(MSD) mara baada ya kufungua mkutano wao wa siku tatu, Agosti 19, 2019 ambao unafanyika kwa siku tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu

Baadhi ya wakurugenzi wa idara mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa nchini(MSD) wakiwa katika mkutano wao wa siku tatu,uliofunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, bw. Jumanne Sagini  Agosti 19, 2019 ambao unafanyika kwa siku tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wakurugenzi wa idara mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa nchini(MSD) wakiwa katika mkutano wao wa siku tatu,uliofunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, bw. Jumanne Sagini  Agosti 19, 2019 ambao unafanyika kwa siku tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wakurugenzi wa idara mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa nchini(MSD) wakiwa katika mkutano wao wa siku tatu,uliofunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, bw. Jumanne Sagini  Agosti 19, 2019 ambao unafanyika kwa siku tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu..
Baadhi ya wakurugenzi wa idara mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa nchini(MSD) wakiwa katika mkutano wao wa siku tatu,uliofunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, bw. Jumanne Sagini  Agosti 19, 2019 ambao unafanyika kwa siku tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu..


Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!