Sunday, August 4, 2019

MANYANYA ATOA WITO KWA WANANCHI KUSHIRIKI MAONESHO YA NANENANE KUJIFUNZA, WAONGEZE TIJA KWENYE UZALISHAJI


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi. Stella Manyanya ametoa wito kwa wananchi kushiriki katika Maonesho ya Nanenane kwa lengo la kujifunza ili waongeze tija katika uzalishaji, huku akibainisha kuwa maonesho haya yameboreshwa, kwa wadau na Taasisi zinazotoa huduma kuongezeka na maonesho hayo kuwa sura ya kuwasaidia wananchi kubadilika.

Mhandisi Manyanya ameyasema hayo Agosti 02, 2019 kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu.

“ Maonesho ya mwaka huu yamefana sana na kufana kwake hakupo katika namna mahema yalivyo, bali ushiriki wa waoneshaji, wakulima wenyewe na nimefurahi kuona baadhi ya mambo yanafanyika kwa vitendo kama uhimilishaji wa ng’ombe, ufugaji wa samaki, uwepo wa taasisi kama TBS, Wakala wa vipimo na vyama vya ushirika”

“ Mimi naona tumeboresha zaidi namna ya kufanya haya maonesho kwenda zaidi katika sura ya kuwagusa wananchi ili waweze kubadilika na kutumia huduma zinazohitajika, nipende kuwashawishi wananchi wengi zaidi wasikose kuja kujifunza kupitia maonesho haya, wanapojifunza wanaongeza tija katika maeneo yao” alisisitiza Mhandisi. Manyanya.

Aidha, amezihamasisha Halmashauri zote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda na uwekezaji mwingine ili wawekezaji wanapopatikana kusiwe na mlolongo mrefu  katika kupata ardhi na kupata vibali mbalimbali, huku akibainisha kuwa Serikali imeshaweka miundombinu wezeshi  kwa uwekezaji kama upatikanaji wa umeme.

Amesema sekta binafsi ndiyo injini ya ukuaji wa uchumi katika Taifa hasa kwenye eneo la biashara na viwanda huku akiongeza kuwa ni vyema maonesho hayo yakawa na kiu ya kufanya mambo yatakayoweza kurahihisha shughuli za kibiashara.

Awali Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema wananchi wengi wa Mkoa wa Simiyu wanajishughulisha  na shughuli za kilimo hivyo ipo haja ya kuwepo kituo endelevu  cha mafunzo ya kilimo ili wakulima waweze kupata mahala pa kujifunzia .

“Kutokana na kwamba wananchi wengi wa Mkoa wa Simiyu wanategemea sana hasa shughuli za kilimo ipo haja ya kuwepo kituo endelevu kwa ajili ya mafunzo kitachowasaidia wakulima kupata elimu kila siku kutokana na uhitaji wao”.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi na wajasiriamali wa mkoa wa Simiyu kutembelea Viwanja vya Nanenane kwa lengo la kujifunza kutoka kwa wenzao kutoka maeneo mbalimbali ya nchi yetu namna wanavyofanya shughuli zao na namna walivyofanikiwa.
MWISHO

Naibu Waziri  wa viwanda na Baishara , Mhandisi. Stella Manyanya akikagua vipando vya mazao ya kilimo vya Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Agosti 02, 2019 wakati wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi bariadi mkoani Simiyu.
Naibu Waziri  wa viwanda na Baishara , Mhandisi. Stella Manyanya akikagua mabanda ya maonesho ya mifugo, Agosti 02, 2019 wakati wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi bariadi mkoani Simiyu.
Mmoja wa ng.ombe walio katika mabanda ya maonesho ya mifugo, kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu.
Naibu Waziri  wa viwanda na Baishara , Mhandisi. Stella Manyanya akiangaliabaadhi ya bidhaa zikiwemo viatu zinazotengenezwa  na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la kujenga Taifa (SUMA JKT) , Agosti 02, 2019 wakati wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu.
Naibu Waziri  wa viwanda na Baishara , Mhandisi. Stella Manyanya akimsikiliza mwananchi ambaye aliyekuwa akipatiwa huduma katika kliniki  ya biashara, Agosti 02, 2019 wakati wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari  Biashara Mjini Bariadi wakipatiwa elimu katika mabanda ya maonesho ya mifugo kutoka wizara ya mifugo, Agosti 02, 2019 wakati wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa kilimo, Mhe. Hussein Bashe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mahojiano maalum Agosti 02, 2019 wakati akiwa kwenye  Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu.


Baadhi ya Viongozi na  Wataalam wakipatiwa elimu katika mabanda ya Taasisi ya Utafiti wa kilimo, Agosti 02, 2019 wakati wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu.
Baadhi ya wananchi wakielekea kwenye mabanda mbalimbali kwa lengo la kujione huduma na bidhaa mbalimbali zinazopatikana, kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!