Wednesday, August 21, 2019

MILA ZINAZOCHANGIA JAMII KUTOTUMIA VYOO ZIPIGWE VITA: RC MTAKA


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ametoa wito kwa jamii kupiga viya mila na desturi zinazochangia watu kutotumia vyoo na kusisitiza kila kaya ione umuhimu wa kuwa na choo bora, ikiwa ni njia ya kuboresha afya na usafi wa mazingira na kuondokana  na hatari ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

Mtaka ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo ambao umefanyika Agosti 20, 2019 Mjini Bariadi ambapo amesema ni  vema mila hizo zikapigwa vita ili jamii iweze kurudi kwenye msingi.

“Kwenye culture(tamaduni) zetu zipo sababu kwa nini baadhi ya watu walikuwa hawatumii vyoo ambazo ni sababu za kitamaduni, kwamba baba mkwe  hawezi kuchangia choo na mke wa kijana wake, kwa hiyo ilikuwa hata ukijenga choo kwa baadhi ya kaya huko nyuma bado kulikuwa na upinzani wa watumiaji”

“Unakuta kuna choo kwenye kaya Fulani lakini bado wanajamii wa hiyo kaya wanaenda kujisiri porini, huu ni utamaduni ambao ni lazima tuufanyie kampeni kama tulivyofanya kampeni za kukataa mambo mengine kama ukeketaji ili jamii zetu zirudi kwenye msingi, katika mkoa wetu kufikia mwezi Novemba, 2019 kila kaya itakuwa na choo bora na kinachotumika” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka amesema anaiunga mkono kwa asilimia 100 Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo kwa kuwa ni kampeni inayolisaidia Taifa katika usafi wa mazingira na kubainisha kuwa itakapofika mwezi Novemba 2019 kila kaya katika Mkoa wa Simiyu itakuwa na choo bora kinachotumika.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema Mkoa wa Simiyu umetajwa  kuwa na  kaya 215,316  ambapo kati ya hizo zenye vyoo ni 208,856  sawa na asilimia 97  na zenye vyoo bora zikiwa ni  97,536  sawa na asilimia 46.7.

Naye Mratibu  wa Kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Afya Anyitike Mwakitalima  amesema kampeni hii inafanyika kwa lengo la kusaidia uboreshaji wa afya nchini kwa sababu magonjwa mengi yanatokana na uchafu na njia moja wapo ya kukabili uchafu ni matumizi wa vyoo bora na unawaji wa mikono kwa maji safi, salama na sabuni.

 Amesema Serikali imeendelea kutoa elimu katika jamii kuhusiana na matumizi na ujenzi wa vyoo bora katika ngazi ya kaya na taasisi na tayari mikoa tisa imefikiwa, mkoa wa Simiyu ukiwa mkoa wa kumi ambapo amesema lengo ni kuifikia mikoa yote 26 kabla ya Juni 2020

Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo itafanyika kwa takribani siku 20 katika Halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu
MWISHO

Balozi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto(kushoto) akimkabidhi fulana yenye Ujumbe wa kampeni hiyo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka Ofisini kwake Mjini Bariadi kuashiria Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Balozi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto(kushoto) akimkabidhi fulana yenye maandishi ya kampeni hiyo Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini Ofisini katika Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na timu ya hamasa ya Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Ofisini kwake Mjini Bariadi wakati wa Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Balozi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpotoakizungumza katika Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akipandisha bendera ya Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo  wakati wa Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Balozi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto na Timu ya hamasa ya kampeni hiyo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) akizungumza katika Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akitoa taarifa ya hali ya vyoo Mkoani Simiyu wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo uliofanyika Agosti 20, 2019 Mjini Bariadi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na timu ya hamasa ya Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Ofisini Mjini Bariadi mara baada ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akionesha fulana yenye maneno ya Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Ofisini kwake Mjini Bariadi mara baada ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na timu ya hamasa ya Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Ofisini Mjini Bariadi mara baada ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akifurahia jambo na Balozi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto Mjini Bariadi mara baada ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Kutoka kulia ni Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Msanii na Balozi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Mrisho Mpoto na Mratibu wa Kampeni ya Taifa ya Usafi wa mazingira kutoka Wizara ya Afya, Bw. Anyitike Mwakitalima wakiteta jambo mara baada ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Balozi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto(kushoto) akimkabidhi fulana yenye Ujumbe wa kampeni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza  kwa naba ya Wakurugenzi wa Mkoa wa Simiyu kuashiria Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mjini Bariadi. Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019 .
Balozi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto(kushoto) akimkabidhi fulana yenye Ujumbe wa kampeni hiyo Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani kwa naba ya Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Simiyu wakati wa Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mjini Bariadi. Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019 .
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akiteta jambo na Balozi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto Mjini Bariadi mara baada ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
.



0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!