Mkuu wa
mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka amesema wanafunzi kidato cha nne waliopata
daraja sifuri katika mtihani wa Mkoa wa Kujipima ‘Mock’ watawekwa katika
kambi maalum ya kitaaluma na kufundishwa na walimu mahiri kwa lengo la kuwasaidia kuongeza ufaulu na
kufikia daraja la nne na kuendelea, katika mtihani wa Taifa mwaka huu 2019.
Mtaka
ameyasema hayo Agosti 22, 2019 katika
kikao cha tathmini ya matokeo ya mtihani wa Mock kwa wanafunzi wa kidato cha nne
na matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha sita mwaka 2019, ambapo mkoa wa
Simiyu umekuwa miongoni mwa mikoa kumi bora Kitaifa.
Mtaka
amesema lengo la Mkoa ni kuona wanafunzi wote waanafanya vizuri na hakuna
mwanafunzi wa kidato cha nne anapata daraja sifuri hivyo wanafunzi wote wenye
daraja sifuri na wale walipata daraja la nne alama za mwisho watawekwa pamoja
na kutafutiwa walimu mahiri ili wawasaidie kupanda kitaaluma na kupata ufaulu
mzuri.
\
“ Tutaweka
kambi ya wanafunzi wote waliopata sifuri kwenye mtihani wa ‘Mock’ lakini pia hata
wale waliopata daraja daraja la nne alama zinazoashiria kuelekea kwenye sifuri,
Siku sitini kabla ya mtihani wafundishwe masomo manne tu, Civics(Uraia),
Kiswahili, Kiingereza na Historia ngalau wapate alama D ili wapate cheti; nia
yetu kama mkoa ni kuona kila mwanafunzi anafanya vizuri" alisema.
Katika
hatua nyingine Mtaka amewahimiza wakuu wa shule kusimamia kwa karibu
ufundishaji na kuhakikisha katika kipindi hiki kuelekea katika mitihani wa
Taifa wa Kidato cha nne, kuongeza ufaulu kutoka nafasi ya tisa ya mwaka 2018 kwenda
kwenye nafasi nzuri zaidi.
Afisa
elimu wa mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amewataka wakuu wa shule na
maafisa elimu kata na wilaya kuendelea
kusimamia ufundishaji ili wanafunzi waweze kufanya vizuri na wale ambao shule
zao hazikufanya vizuri waimarishe usimamizi ili kuongeza ufaulu.
Kwa
upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Itilima amezungumzia kambi maalum za
kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata sifuri kwenye mtihani wa
Mock ambao wapo takribani 2000 kati ya
wanafunzi zaidi ya 9000, kwamba zitakuwa msaada kwao na wanatarajia kuzifanya
kwa ufanisi ili mkoa uwe kati ya mikoa tisa bora Kitaifa mwaka 2019(Single
digit).
Mkuu
wa mkoa ameahidi kutoa shilingi elfu 30 kwa mwalimu katika kila alama A itakayopatikana
kwenye somo lake, shilingi milioni tano kwa shule itakayoingia kumi bora kitaifa,
Milioni tano kwa Halmashauri itakayoingia kumi bora kitaifa, na milioni mbili
kwa mwanafunzi atakayepata ufaulu daraja la kwanza pointi saba na kuwa
katika kumi bora kitaifa na ikiwa hatakuwa miongoni mwa wanafunzi bora kitaifa
atapewa shilingi milioni moja.
Mkutano wa
tathimini ya matokeo ya kidato cha sita mkoani Simiyu unawakutanisha wakuu wa
shule za sekondari,maafisa elimu wilaya ,wakurugenzi watendaji, wenyeviti wa
halmashauri za wilaya na wenyeviti wa Kamati za Elimu za Halmashauri lengo
likiwa ni kuangalia walipo na wanapoelekea katika maendeleo ya elimu mkoani
Simiyu
MWISHO.
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na viongozi na wadau wa elimu
katika mkoawa Simiyu katika Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa
wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika
Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
Maafisa
Elimu wa Wilaya, kata, wakuu wa shule na wadau wengine wa elimu mkoani Simiyu, wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika kikao cha
tathmini ya ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na
Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
Maafisa
Elimu wa Wilaya, kata, wakuu wa shule na wadau wengine wa elimu mkoani Simiyu, wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika kikao cha
tathmini ya ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na
Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi
ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakifuatilia hotuba ya Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani), ya kufunga Kikao cha Tathmini
ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya
Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi zawadi mmoja wa walimu
walifanikisha wanafunzi kupata alama A katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita
mwaka 2019 katika Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha
Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019
Mjini Bariadi
\
Mwenyekiti
wa Chama Cha Walimu Mkoa wa Simiyu akichangia hoja katika Kikao cha Tathmini ya
Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani
wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na viongozi na wadau wa elimu
katika mkoawa Simiyu katika Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa
wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika
Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment