Sunday, August 4, 2019

WAZIRI WA KILIMO AZINDUA BIMA YA MAZAO

Serikali kupitia waziri wa kilimo  Japhet Hasunga imezindua Bima  ya Kilimo inayokinga mazao ya mkulima yanapokuwa shambani dhidi ya ukame, magonjwa ,wadudu waharibifu , mvua zilizozidi, moto, uharibifu unaoweza kusababishwa na wanyapori, pamoja na mvua ya mawe.

Akizundua bima hiyo Hasunga amesema kuwa wameamua kuanza na kipaumbele katika zao la pamba ambalo huzalishwa kwa wingi Mkoani hapa lengo likiwa ni kuwainua wakulima wenye vipato vya chini sambamba na kuwasaidia kupata msaada pindi wanapopatwa na majanga  ambapo bima hiyo inatarajiwa kuzinduliwa kwenye mazao mengine ya kimkakati.

Aidha waziri Hasunga amewataka wakulima walio katika vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) kuhakikisha wanajiunga na bima ya mazao itakayowasaidia kukuza uchumi wao na kuongeza kuwa idadi ya vyama vya ushirika katika mazao yote imeongezeka na kufikia  11,331 ambapo kiwango cha ukaguzi wa vyama hivyo ni 70% na kuisisitiza  Tume ya Maendeleo ya Ushirika kuongeza kasi ya ukaguzi ili ifikie 100%.

“Bima hiyo ya mazao itamsadia mkulima kuepukana na majanga mbalimbali na kwamba tumeamua kulipa kipaumbele zao la pamba na baada ya hapa tutaenda Kagera kuzindua bima kwenye zao la kahawa na  serikali imelenga kuongeza kuwainua wakulima ili waweze kuchangia katika kukuza pato la Taifa”alisema waziri Hasunga

Ameongeza kuwa wakati umefika wa kuwachukulia hatua za kisheria waliohujumu vyama vya ushirika awali huku akiwataka waliopewa majukumu kwenye AMCOS kuwa wachapakazi, waadilifu na waaminifu katika utendaji kazi wao.

“nitoe tamko kuwa viongozi wote wa vyama vya ushirika ambao wanawafanya ubadhilifu na kuihujumu serikali ni lazima wachukuliwe hatua za kisheria na pia ni vyema sasa sheria na miongozo iliyopo ibadilishwe ili iweze kuendana na kasi ya ushirika uliopo” alisema

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima ya Taifa (NIC) dokta Elirehema Doriye amesema kuwa shirika hilo linatarajia kutoa bima ya mazao kwa wakulima wote nchini huku akiwashauri wakulima kukata bima ili kuepukana na changamoto.

Aidha ameongeza kuwa bima hiyo itamsaidia mkulima kuweza kukopesheka kwenye mabenki kwani tayari mkulima atakuwa na kinga hivyo  kutoa mazao yatakayochangia pato lake na Taifa kwa ujumla huku akiongeza kuwa shirika hilo linalomilikiwa na serikali kwa asilimia mia moja 100% likiwafikia wakulima wote na kwa kuanzia wataanza na wakulima wadogo.

Pamoja na hayo ameongeza kuwa bima hiyo ina manufaa makubwa kwa mkulima na  itamkomboa kutoka katika kilimo kidogo na kwenda kikubwa kitakachomuwezesha  kuwekeza katika kilimo cha kisasa bila kuwa na hofu ya kupoteza mtaji aliowekeza shambani ikiwa sekta kilimo imeajiri zaidi ya 75% ya Watanzania.

Kwa upande wake Kamishina wa Bima hapa nchini Dkt. Mussa Juma ameeleza kuwa lengo la bima hiyo ni kusaidia kuinua kipato cha watu wenye kipato cha chini ili waweze kuchangia katika ukuzaji wa uchumi wa nchi .

Mbali na hayo amesema kuwa uchumi wa nchi unategemea sekta mbalimbali ambazo ni kama kilimo, uvuvi, mifugo, madini na ili kuwa na viwanda ambavyo vinaweza kusaidia kukuza uchumi wa nchi lazma kuwe na namna ya kudhibiti majanga.

Hata hivyo ameongeza kuwa bima ambazo zinahusu watu wengi hasa wenye kipato cha chini mamlaka imeona iweze kuwafikia kwa namna moja nyingine.

Awali akimkaribisha waziri Hasunga mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amesema kuwa mkoa umejiandaa kikamilifu kusaidiana na NIC katika kuhakikisha zaidi ya wakulima 100,000 wa pamba waliosajiliwa wanapata bima ya mazao.
MWISHO



Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga akionesha nakala ya Mpango wa Bima ya Mazao  kwa viongozi na wananchi mara baada ya kuzindua bima hiyo Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga akimkabidhi Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Bima ya Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye  nakala ya Mpango wa Bima ya Mazao  mara baada ya kuzindua bima hiyo Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.



Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  nakala ya Mpango wa Bima ya Mazao  mara baada ya kuzindua bima hiyo Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga akipandisha bendera ya Bima ya Mazao katika Banda la Shirika la Bima ya Mazao kama  ishara ya kuzindua rasmi bima hiyo  Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

Baadhi ya wananchi wakishuhudia zoezi la uzinduzi wa Bima ya Mazao lililofanywa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wwa Simiyu, Mhe. Anthony  Mtaka akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga kuzungumza na wananchi na kuzindua rasmi bima ya mazao, Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akitoa  neon la shukrani mara baaada ya uzinduzi wa Bima ya mazao Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga akimkabidhi Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika , Dkt. Titus Kamani  nakala ya Mpango wa Bima ya Mazao  mara baada ya kuzindua bima hiyo Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima ya Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye  nakala ya Mpango wa Bima ya Mazao  mara baada ya kuzindua bima hiyo Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika , Dkt. Titus Kamani  akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga(kulia) wakati alipotembelea banda la Maendeleo ya Ushirika Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Kutoka kushoto Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima ya Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye  na Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika , Dkt. Titus Kamani  wakiteta jambo, mara baada ya kuzindua bima ya mazao Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga(wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Simiyu na wawakilishi wa taasisi zilipokea vyeti vya kutambua mchango wake katika kilimo, mifugo na uvuvi, Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga(wan ne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Simiyu na watumishi wa Shirika la Bima la Taifa  Agosti 03, 2019 mara baada ya kuzindua bima ya mazao,  katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima ya Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye(kulia) akimkabidhi Mfuko Mbadala Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, mara baada ya kuzindua bima ya mazao,  katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika , Dkt. Titus Kamani  akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga wakati wa zoezi la uzinduzi wa bima ya mazao  Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019,  yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo, Mhandisi. Mathew Mtigumwe akizungumza kwenye zoezi maalum la uzinduzi wa bima ya mazao, Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019,  yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Mazao kutoka Wizara ya kilimo, akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga  wakati alipotembelea mabanda ya wizara hiyo, Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019,  yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Banda la ASDP kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019,  yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya viongozi na wananchi wakipita kwenye mabanda ya maonesho kwa ajili ya  kujionea huduma na bidhaa mbalimbali, kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019,  yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Banda la Chama cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu (SIMCU)

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!