Msajili
wa Watoa Huduma ya Msaada wa Kisheria Tanzania, Bi. Felistas Joseph kutoka
Wizara ya Katiba na Sheria ametoa wito kwa jamii kuwatambua na kuwatumia
wasaidizi wa kisheria pindi wanapohitaji msaada katika masuala ya kawaida ya
kisheria, ikiwemo migogoro ya ardhi, migogoro ya ndoa, utelekezaji wa familia
na masuala mengine wanayokutana nayo siku kwa siku, ambao amesema wanatoa
huduma hizo bila malipo yoyote.
Bi Felistas ameyasema
hayo jana katika kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu wa Huduma za Msaada wa
kisheria Mkoani Simiyu kilichofanyika
Mjini Bariadi.
Amesema kada hii
inatambuliwa kwa mujibu wa sheria ya msaada wa kisheria na wamefundishwa
mafunzo ya awali ya sheria katika masuala ambayo wananchi wanakutana nayo siku
kwa siku hivyo ni vema jamii na wadau wengine wakawatambua na kuwapokea kwa
kuwa ni watu waliojitoa kuisaidia jamii bila malipo yoyote.
“Nia yetu ni kwamba
jamii iweze kuwafahamu na kuwapokea wasaidizi wa kisheria, hawa ni watu
wanaojitolea kwa dhati kufanya hii kazi bila kudai malipo, wanachohitaji ni
ushirikiano na wadau wengine wa Serikali pamoja na wananchi; kada hii
inatambuliwa rasmi chini ya sheria ya msaada wa kisheria na wameshapewa vigezo
na mipaka ya kufanyia kazi” alisema.
Ameongeza
kuwa Serikali imeandaa mtaala wa
kufundisha wasaidizi wa huduma za kisheria na hadi sasa takribani wasaidizi wa
kisheria 4500 wamefundishwa katika kipindi cha miaka mitatu nyuma ambao
wamejiunga katika vikundi na kujisajili kama mashirika ambapo hadi sasa kuna
jumla ya mashirika 200.
Awali akifungua kikao
cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya
Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani Simiyu, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka amesema endapo wasaidizi
wa kisheria watutumiwa vizuri kero nyingi za wananchi zitatatuliwa na kufikia
mwisho, huku kutoa wito kwa Wakuu wa wilaya, wabunge, madiwani na viongozi
wengine kuwashirikisha wasaidizi wa kisheria katika mikutano ya hadhara ambapo
wananchi huwasilisha kero zao.
Aidha, Mtaka amesema
ili kuongeza uewelewa wa masuala ya msaada wa kisheria mkoani Simiyu ni vema
Wizara ya Katiba na Sheria ikaona haja ya kuendela kutoa elimu kwa jamii,
ambapo amewaalika kutoa elimu hiyo katika kambi za kitaaluma mkoani hapa ambazo
zinatarajia kuanza mwezi Septemba, 2019 kwa kidato cha nne.
Kwa upande wake Katibu
Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini amesema viongozi wa Mkoa watahakikisha
kamati za uratibu wa huduma za kisheria ngazi ya wilaya zinaundwa na wasaidizi
wa kisheria wanatumiwa ipasavyo.
Naye Sheikh wa Mkoa wa
Simiyu, Mahamoud Kalokola amesema viongozi wa madhehebu ya dini wataendelea
kutoa elimu kupitia makusanyiko ya ibada kwa waumini wao ili wananchi hususani wale
ambao hawana na uwezo wa kifedha wa kuwalipa mawakili wajue kuwa wasaidizi wa
kisheria wapo katika jamii na wanaweza kuwasaida kutatua changamoto zao.
Kamati ya Uratibu wa
Shughuli za Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Simiyu imeundwa na kuzinduliwa chini ya Katibu Tawala wa Mkoa
ambaye ni Mwenyekiti, Msajili msaidizi(Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa), mtaalamu
wa ardhi, jeshi la polisi (dawati la jinsia) Magereza, TAKUKURU, Mahakama, Mwanasheria,
Afisa wa dawati la malalamiko, viongozi wa dini na Afisa ustawi wa jamii na Afisa
habari ngazi.
Wajumbe wengine ni mwakilishi
wa vyombo vya habari, wawakilishi wa wadau wa maendeleo, wawakilishi wa taasisi
za watoa huduma za msaada wa kisheria,Mwenyekiti wa baraza la ardhi na
mwakilishi kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), ambapo kwa muundo huu
huu kamati za wilaya zitaundwa ziweze kutekeleza jukumu la uratibu wa shughuli
za huduma za kisheria wilayani
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (katikati) akizungumza na wadau wa Huduma za Msaada wa
Kisheria Mkoani Simiyu, wakati wa kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu wa
Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani humo kilichofanyika Agosti 13, 2019 Mjini
Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) akizungumza
na wadau wa Huduma za Msaada wa Kisheria Mkoani Simiyu, wakati wa kikao cha
Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani humo kilichofanyika
Agosti 13, 2019 Mjini
Bariadi.
Msajili wa Watoa Huduma
ya Msaada wa Kisheria Tanzania, Bi. Felistas Joseph(kulia) kutoka Wizara ya
Katiba na Sheria akiwasilisha mada katika kikao cha Uundaji wa
Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani Simiyu kilichofanyika Agosti
13, 2019 Mjini Bariadi, kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini na Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
Mwakilishi wa Taasisi
za watoa huduma za msaada wa kisheria mkoani Simiyu akichangia hoja katika
kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani
humo kilichofanyika Agosti 13, 2019 Mjini
Bariadi.
Wakili wa Serikali
Lilian Kilembe kutoka Wizara ya katiba na Sheria akiwasilisha mada katika
katika kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria
Mkoani Simiyu kilichofanyika Agosti 13,
2019 Mjini Bariadi
Baadhi ya wajumbe wa
kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani
Simiyu kilichofanyika Agosti 13, 2019 Mjini
Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo
pichani) wakati akifungua kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa
kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani
Simiyu kilichofanyika Agosti 13, 2019
Mjini Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo
pichani) wakati akifungua kikao hicho.
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu na Mwenyekiti wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa
kisheria Mkoa, Bw. Jumanne Sagini
(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kikao
cha Uundaji wa Kamati hiyo kilichofanyika Agosti 13, 2019 Mjini
Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu na Mwenyekiti wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa
kisheria Mkoa, Bw. Jumanne Sagini
(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kikao
cha Uundaji wa Kamati hiyo kilichofanyika
Agosti 13, 2019 Mjini Bariadi.
\
Baadhi ya wajumbe wa
kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani
Simiyu kilichofanyika Agosti 13, 2019
Mjini Bariadi wakimsikiliza Mratibu Msaidizi wa Huduma za Kisheria Ngazi ya
Mkoa ambaye pia ni Afisa Maendeleo wa Mkoa, Bw. Fadhili Wilhem wakati
akiwasilisha mada katika kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa
kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani
Simiyu kilichofanyika Agosti 13, 2019
Mjini Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo
pichani) wakati akifungua kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa
kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani
Simiyu kilichofanyika Agosti 13, 2019
Mjini Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo
pichani) wakati akifungua kikao hicho.
0 comments:
Post a Comment