Friday, September 27, 2019

MAMIA YA WAOMBOLEZAJI WAJITOKEZA KUMZIKA MTOTO WA MKUU WA MAJESHI ALIYEFARIKI KWA AJALI YA NDEGE


Mamia ya wananchi kutoka mikoa ya Simiyu, Mara, Shinyanga, Mwanza na Dar es Salaam wameshiriki katika mazishi ya mtoto wa Mkuu wa Majeshi  marehemu Nelson Mabeyo aliyekuwa rubani wa ndege ya Shirika la Auric Air, ambaye alifariki Septemba 23, 2019 kwa ajali ya ndege iliyotokea katika Uwanja mdogo wa Seronera  uliopo katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara.

Mazishi hayo yamefanyika Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha Masanzakona wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, ambapo yalitanguliwa na ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yuda Tadei lililipo kijijini hapo ambapo ni nyumbani kwao na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo.

Akihubiri wakati wa ibada ya mazishi, Askofu Michael Msonganzila, Jimbo Katoliki Musoma amewasihi waombolezaji wote kuendelea kuifariji na kuiombea familia ya Mkuu wa Majeshi ili wapokee msiba huo kwa jicho la imani, masikio ya imani na kama mpango wa Mungu.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akitoa salamu za serikali  amesema “marehemu Nelson Mabeyo alikuwa  kijana mcheshi na mchapakazi leo hatuko naye tena nitoe pole kwa familia ya Jenerali Mabeyo, sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea niwaombe tuendelee kuwaombea katika kipindi hiki kigumu Mwenyezi Mungu awape ustahimilivu.”

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza  kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Simiyu na wakuu wa mikoa ametoa pole kwa familia ya Mkuu wa Majeshi na kumshukuru kwa namna Mkuu  alivyowaunganisha watu wa Masanza, Busega na Simiyu katika masuala mbalimbali ya  ikiwemo Ujenzi wa Kanisa ambalo ibada ya mazishi ya marehemu Nelson imefanyika.

Kwa upande wake  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenrali Venance Mabeyo amewashukuru watu wote walioshirikiana na familia yake tangu msiba wa mwanaye Nelson ulipotokea , ambapo amesema kama familia hawauchukulii msiba huo kama adhabu bali makusudi ya Mungu mwenyewe kwa mtoto wao .

Mazishi ya marehemu  Nelson Mabeyo yalihudhuriwa na  watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, viongozi na Maafisa wa JWTZ walioko kazini na wastaafu, mawaziri na manaibu waziri, makatibu wakuu, wakuu wa Taasisi, viongozi wa Vyombo vya Usalama, wabunge, Wakuu wa mikoa ya Simiyu, Mara, Shinyanga, Kagera, Kigoma, Mwanza na Dar es salaam , kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Simiyu na wakuu wa wilaya.
MWISHO




Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo na mkewe Tina Mabeyo  wakiweka shada la maua katika kaburi la mtoto wao Rubani Nelson Mabeyo  ambaye alifariki katika ajali ya ndege Septemba 23, 2019 Seronera katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mkoani Mara ; ambaye amezikwa Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha Masanza wilayani Busega Mkoani Simiyu.


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akiweka shada la maua katika Kaburi la Rubani Nelson Mabeyo  mtoto wa Mkuu wa Majeshi  ambaye alifariki katika ajali ya ndege Septemba 23, 2019 Seronera katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mkoani Mara ambaye amezikwa Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha Masanza wilayani Busega Mkoani Simiyu.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto) na wakuu wa mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga, Kagera, Kigoma na Dar es Salaam wakiweka shada la maua katika Kaburi la Rubani Nelson Mabeyo  mtoto wa Mkuu wa Majeshi  ambaye alifariki katika ajali ya ndege iliyotokea Septemba 23, 2019 Seronera katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mkoani Mara, ambaye amezikwa Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha Masanza wilayani Busega Mkoani Simiyu.


Baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiweka Jeneza lenye mwili wa mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, marehemu rubani Nelson Mabeyo aliyefariki kwa ajali ya ndege Septemba 23, 2019 Seronera Mkoani Mara ; ambaye amezikwa Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha Masanza wilayani Busega Mkoani Simiyu.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo na mkewe Tina Mabeyo  wakishuhudia jeneza lenye mwili wa  mtoto wao Nelson Mabeyo  ambaye alifariki katika ajali ya ndege Septemba 23, 2019 Seronera katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mkoani Mara likishushwa kaburini wakati wa mazishi yake yaliyofanyika Septemba 26, 2019 Kijiji cha Masanza wilayani Busega Mkoani Simiyu.
 Viongozi mbalimbali wa Serikali wakitoa heshima za mwisho kwa mwili mtoto wa Mkuu wa majeshi Jenerali Venance Mabeyo, marehemu rubani Nelson Mabeyo  aliyefariki katika ajali ya ndege Septemba 23, 2019 Seronera katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mkoani Mara, ambaye amezikwa Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha Masanza wilayani Busega Mkoani Simiyu.


 Maaskofu wa Katoliki kutoka Majimbo ya Mara na Geita wakiweka shada la maua katika kaburi la mtoto wa Mkuu wa majeshi Jenerali katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti Venance Mabeyo, marehemu rubani Nelson Mabeyo  aliyefariki katika ajali ya ndege Septemba 23, 2019 Seronera Mkoani Mara, ambaye amezikwa Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha Masanza wilayani Busega Mkoani Simiyu.
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita akiongoza ibada ya mazishi ya mtoto wa Mkuu wa majeshi Jenerali Venance Mabeyo, marehemu rubani Nelson Mabeyo  aliyefariki katika ajali ya ndege Septemba 23, 2019 Seronera katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mkoani Mara, ambaye amezikwa Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha Masanza wilayani Busega Mkoani Simiyu.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi(mwenye miwani katikati) akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali mara baada ya ibada ya mazishi ya mtoto wa Mkuu wa majeshi Jenerali Venance Mabeyo, marehemu rubani Nelson Mabeyo  aliyefariki katika ajali ya ndege Septemba 23, 2019 Seronera katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mkoani Mara, ambaye amezikwa Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha Masanza wilayani Busega Mkoani Simiyu.








Wednesday, September 25, 2019

UONGOZI WA MKOA SIMIYU WABAINI UBADHILIFU WA SHILINGI MILIONI 55 BUSEGA

Uongozi wa Mkoa wa Simiyu umebaini Ubadhilifu wa kiasi cha shilingi  55,580,000/= ambazo ni sehemu ya mkopo uliotolewa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Urasimishaji wa makazi Viwanja 3700 katika kata nne za Halmashauri ya Wilaya ya Busega uliofanywa na Watumishi wanne wa Halmashauri hiyo.

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini wakati akiwasilisha taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya  fedha za mradi huo katika kikao cha  Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 Busega Septemba 06,2019 Nyashimo Busega.

Sagini amewataja watumishi waliohusika katika ubadhilifu huo kuwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri, Anderson Njiginya, Mkuu wa Idara ya Ardhi, Magesa Magesa, msimamizi wa mradi Raymond Mahendeka na mhasibu wa mradi,Augustina Kitau na kuwataka kurejesha fedha hizo mara moja na kushauri mamlaka zao za nidhamu kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria

Sagini ameongeza kuwa timu ya uchunguzi imebaini mapungufu mbalimbali katika matumizi ya fedha hizo ikiwa ni pamoja na ukikwaji wa sheria, kanuni na taratibu za fedha, ukiukwaji wa masharti ya mkataba, ukiukwaji wa sheria kanuni na taratibu za manunuzi ya Umma, udanganyifu na uzembe na usimamizi dhaifu wa Mradi.

“Kutokana na mapungufu yaliyobainishwa katika uchunguzi huu Uongozi wa mkoa unaelekeza watumishi waliohusika warejeshe fedha hizo haraka ili mradi utekelezwe kama ilivyokusudiwa na tunashauri mamlaka za nidhamu zichukue hatua stahiki kwa watumishi hao kwa mujibu wa sheria na taratibu za Utumishi wa Umma,” alisema Sagini.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mhe. Vumi Magoti amewashukuru viongozi wa Mkoa kutuma wataalam wa Mkoa kufanya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mradi na kumuagiza Mkurugenzi kuanzisha utaratibu wa kuwachukulia hatua watumishi waliohusika walio chini  ya mamlaka yake kama  viongozi wa mkoa walivyoelekeza.

Diwani wa Kata ya Mkula, Mhe, Goodluck Nkalango amesema madiwani wa Halmashauri ya Busega wakiwemo wajumbe wa kamati inayoshughulikia masuala ya ardhi hawakushirikishwa katika utekelelezaji wa mradi wa urasimishaji, makazi jambo ambalo lilipelekea wananchi kutokuwa na taarifa sahihi za mradi ikiwemo utaratibu wa kuchangia gharama za upimaji.

Kwa upande wake Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu, Bw. Alex Mpemba amesema TAKUKURU imepokea taarifa ya Kamati ya Uchunguzi na itaanza kuifanyia kazi mara moja kwa lengo la kuthibitisha makosa ya jinai kwa waliohusika.

“Tumeipokea taarifa ya uchunguzi kupitia kikao cha baraza la dharura na kwa sababu wenzetu wa ukaguzi wamemaliza kazi yao na sisi tutaanzia pale walipoishia kwa lengo la kuthibitisha makosa ya jinai,” alisema Mpemba.

Halmashauri ya Wilaya ya Busega ilipokea mkopo wa shilingi 100,000,000/=kutoka Wizara ya Ardhi kutekeleza Mradi wa urasimishaji wa makazi viwanja 3700 katika kata za Mwamanyili, Mkula, Kiloleli na Lamadi; kwa mujibu wa taarifa ya Uchunguzi hadi kufikia Septemba  06, 2019 utekelezaji wa mradi ulikuwa umefikia asilimi 8.5 na fedha zilizokuwa zimetumika ni  asilimia 98.

MWISHO


Katibu Tawala wa Mkoa wa Simyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega katika kikao cha Baraza Maalum la madiwani, Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mhe. Vumi Magoti akifungua kikao cha Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Njiginya akizungumza kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Vumi Magoti kufungua kikao cha Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega wakifuatilia kikao cha Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega wakifuatilia kikao cha Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mhe. Vumi Magoti akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simyu, Bw. Jumanne Sagini katika kikao cha Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Baadhi ya viongozi wakifuatilia kikao cha Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Diwani wa Kata ya Mkula, Mhe.akichangia hoja katika kikao cha Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Diwani wa Kata ya Mkula, Mhe.akichangia hoja katika kikao cha Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mmoja wa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega akichangia hoja katika kikao cha Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Friday, September 13, 2019

WASIMAMIZI WA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA SIMIYU WAAPISHWA, WAASWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA MIONGOZO KUEPUSHA MALALAMIKO


Wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kutoka katika Halmashauri sita za Mkoa wa Simiyu wameapishwa Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi, ambapo Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amewataka wazingatie sheria, kanuni, taratibu na miongozo katika uchaguzi huo ili kuepusha malalamiko yasiyo ya lazima.

Sagini amesema wasimamizi hao  wanapaswa kutambua kuwa wamepewa jukumu zito ambalo linahitaji umakini wa hali ya juu na utulivu wa akili, hivyo ni vema wakasoma na kuzipitia tena sheria, kanuni na miongozo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa walizopewa ili wazielewe na waweze kufanya kazi bila kubabaika.

“Kumbukeni kuwa Uchaguzi huu unaweka msingi na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 hivyo ni imani yangu kuwa kila mmoja wenu atakahakikisha anazingatia sheria, kanuni,miongozo na taratibu zilizotolewa ili kuepusha malalamiko yasiyo ya lazima; matarajio yangu ni kwamba mtaishi viapo mlivyoapa leo” alisema Sagini.

Aidha, Sagini amewataka wasimamizi hao kujiepusha na ushabiki wa kisiasa kwa kuwa wao kama wasimamizi ni waamuzi, hivyo hawapaswi kwa namna yoyote kujihusisha na masuala ya ushabiki wa vyama vya kisiasa, ili waaminiwe kuwa wanaweza kutoa haki; watakaobainika kujihusisha na itikadi za kisiasa watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Akizungumza mara baada ya kuwaapisha wasimamizi hao, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio amewataka wasimamizi hao kuishi viapo vyao na kuhakikisha wanafanya majukumu yao kwa uadilifu na kwa mujibu wa sheria kwa sababu watakapokiuka sheria , kanuni na taratibu wataiingiza serikali kwenye gharama.

Kwa upande wao wasimamizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa mkoani Simiyu mwaka 2019 wamesema watahakikisha wanatekeleza wajibu na majukumu waliyopewa kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu na miongozo kama walivyoelekezwa.

“Tunashukuru kwa kuaminiwa katika jukumu hili nyeti la Kitaifa, tunaamini kama tulivyoelekezwa kama wasimamizi tutasimamia yale tunayopaswa tutafanye kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu na tutaviishi viapo vyetu tulivyoapa siku ya leo na kutimiza wajibu wetu kama watumishi wa Umma” alisema Wilbert Siogopi msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.

“Tunaahidi kwamba tutakitekeleza kiapo tulichoapa leo, tunafahamu kuwa kazi hii ngumu lakini kama mlivyotuasa tukiamua kwa dhati kabisa tukapitia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya uchaguzi tutafanya kazi inayotarajiwa” alisema Bi . Amina Mbwambo msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Wilaya ya Itilima.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019 nchini kote ambapo katika Mkoa wa Simiyu utahusisha  Vijiji 470, Mitaa 92 na Vitongoji 2652.
MWISHO

Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Eng. Wilbert Siogopi Makala akila kiapo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto), zoezi ambalo limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bibi. Pelagia  Daudi Sogoti akila kiapo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto), zoezi ambalo limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini,(kushoto walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Wasimamizi wa chaguzi wa Serikali za Mitaa baada ya wasimimizi hao kuapishwa ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto), zoezi ambalo limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
Bi.Amina Mbwambo msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Wilaya ya Itilima akizungumza kwa niaba ya wenzake  mara baada ya kuapishwa ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto), zoezi ambalo limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto) akizungumza na wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mara baada ya kuwaapisha Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanna Sagini akizungumza na wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mara baada ya kuwaapisha Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Joyce Thomas Ndunguru akila kiapo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto), zoezi ambalo limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe akitoa neno kwa wasimamizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao waliapiswa Septemba 12, 2019  Mjini Bariadi na   Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bibi. Mwanaishamu Nassoro Shemagembe  akila kiapo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto), zoezi ambalo limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
Baadhi ya wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019 na viongozi wakifuatlia halfa tya kuapisha wasimamizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao waliapiswa Septemba 12, 2019  Mjini Bariadi na   Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini
Baadhi ya wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019 na viongozi wakifuatlia halfa tya kuapisha wasimamizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao waliapiswa Septemba 12, 2019  Mjini Bariadi na   Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini
Baadhi ya wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019 na viongozi wakifuatlia halfa tya kuapisha wasimamizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao waliapiswa Septemba 12, 2019  Mjini Bariadi na   Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Gidion John Burton akila kiapo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto), zoezi ambalo limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bibi. Bi . Amina Mbwambo akila kiapo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto), zoezi ambalo limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.



MAAFISA WATAKAIWA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA CHAKULA KUKABILIANA NA UTAPIAMLO


Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifungua Mkutano wa wadau wa lishe wa lengo la makabidhiano ya mradi mapambano dhidi ya utapiamlo kutoka Shirika lisilo la kiserikali la DOCTORS WITH AFRICA (CUAMM) ambalo limemaliza muda wake wa utekelezaji  mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi akichangia hoja katika Mkutano wa wadau wa lishe, uliofanyika Mjini Bariadi Septemba 10, 2019 kwa lengo la makabidhiano ya mradi mapambano dhidi ya utapiamlo kutoka Shirika lisilo la kiserikali la DOCTORS WITH AFRICA-CUAMM ambalo limemaliza muda wake wa utekelezaji  mkoani Simiyu.
Meneja wa mradi wa DOCTORS WITH AFRICA Mkoani Simiyu, Bi.  Fortihappiness Mumba akiwasilisha taarifa ya mradi huo katika Mkutano wa wadau wa lishe, uliofanyika Mjini Bariadi Septemba 10, 2019 kwa lengo la makabidhiano ya mradi mapambano dhidi ya utapiamlo kutoka Shirika lisilo la kiserikali la DOCTORS WITH AFRICA-CUAMM ambalo limemaliza muda wake wa utekelezaji  mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif  Shekalaghe akichangia hoja katika Mkutano wa wadau wa lishe, uliofanyika Mjini Bariadi Septemba 10, 2019 kwa lengo la makabidhiano ya mradi mapambano dhidi ya utapiamlo kutoka Shirika lisilo la kiserikali la DOCTORS WITH AFRICA-CUAMM ambalo limemaliza muda wake wa utekelezaji  mkoani Simiyu.
Afisa Lishe wa mkoa wa Simiyu Dkt. Chacha Magige, akiwasilisha taarofa ya hali ya lishe ya mkoa, katika Mkutano wa wadau wa lishe, uliofanyika Mjini Bariadi Septemba 10, 2019 kwa lengo la makabidhiano ya mradi mapambano dhidi ya utapiamlo kutoka Shirika lisilo la kiserikali la DOCTORS WITH AFRICA-CUAMM ambalo limemaliza muda wake wa utekelezaji  mkoani Simiyu.
Baadhi ya wadau wa lishe wakifuatilia Mkutano wa wadau wa lishe, uliofanyika Mjini Bariadi Septemba 10, 2019 kwa lengo la makabidhiano ya mradi mapambano dhidi ya utapiamlo kutoka Shirika lisilo la kiserikali la DOCTORS WITH AFRICA-CUAMM ambalo limemaliza muda wake wa utekelezaji  mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (katikati) akiwa katika picha pamoja na wadau wa lishe mkoa wa Simiyu mara baada ya kufungua Mkutano wa wadau wa lishe, uliofanyika Mjini Bariadi Septemba 10, 2019 kwa lengo la makabidhiano ya mradi mapambano dhidi ya utapiamlo kutoka Shirika lisilo la kiserikali la DOCTORS WITH AFRICA-CUAMM ambalo limemaliza muda wake wa utekelezaji  mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (katikati) akiwa katika picha pamoja na wadau wa lishe mkoa wa Simiyu mara baada ya kufungua Mkutano wa wadau wa lishe, uliofanyika Mjini Bariadi Septemba 10, 2019 kwa lengo la makabidhiano ya mradi mapambano dhidi ya utapiamlo kutoka Shirika lisilo la kiserikali la DOCTORS WITH AFRICA-CUAMM ambalo limemaliza muda wake wa utekelezaji  mkoani Simiyu.
Baadhi ya wadau wa lishe wakifuatilia Mkutano wa wadau wa lishe, uliofanyika Mjini Bariadi Septemba 10, 2019 kwa lengo la makabidhiano ya mradi mapambano dhidi ya utapiamlo kutoka Shirika lisilo la kiserikali la DOCTORS WITH AFRICA-CUAMM ambalo limemaliza muda wake wa utekelezaji  mkoani Simiyu.
Baadhi ya wadau wa lishe wakifuatilia Mkutano wa wadau wa lishe, uliofanyika Mjini Bariadi Septemba 10, 2019 kwa lengo la makabidhiano ya mradi mapambano dhidi ya utapiamlo kutoka Shirika lisilo la kiserikali la DOCTORS WITH AFRICA-CUAMM ambalo limemaliza muda wake wa utekelezaji  mkoani Simiyu.
Baadhi ya wadau wa lishe wakifuatilia Mkutano wa wadau wa lishe, uliofanyika Mjini Bariadi Septemba 10, 2019 kwa lengo la makabidhiano ya mradi mapambano dhidi ya utapiamlo kutoka Shirika lisilo la kiserikali la DOCTORS WITH AFRICA-CUAMM ambalo limemaliza muda wake wa utekelezaji  mkoani Simiyu.
Mkazi wa Bariadi, Bw. Richard Singi akishuhudia namna tiba lishe ilivyomsaidia mwanae Penina Richard ambaye alipata utapiamlo mkali kurudi kwenye hali yake ya kawaida, katika Mkutano wa wadau wa lishe, uliofanyika Mjini Bariadi Septemba 10, 2019 kwa lengo la makabidhiano ya mradi mapambano dhidi ya utapiamlo kutoka Shirika lisilo la kiserikali la DOCTORS WITH AFRICA-CUAMM ambalo limemaliza muda wake wa utekelezaji  mkoani Simiyu.


Wednesday, September 11, 2019

WANAFUNZI WA DARASA LA SABA SIMIYU WAAHIDI KUFANYA VIZURI MTIHANI WA TAIFA


Wanafunzi wa darasa la saba katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani  Simiyu wamemuahidi Mkuu wa mkoa Anthony Mtaka hawatamuangusha katika mtihani wa Taifa  Septemba 11-12, kwa kuwa wamejiandaa vizuri na wanaimani watafanya vizuri.

Wanafunzi hao wa shule ya msingi Somanda A na B wametoa ahadi hiyo kwa niaba ya wanafunzi wote  wa darasa la saba wa mkoa wa Simiyu, mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthoy Mtaka wakati akizungumza nao na kuwatakia heri katika Mtihani huo.

Wamesema wana imani ya kufanya vizuri kwa sababu hata Mtihani wa Mkoa Utilimilifu(Mock) walifanya vizuri, wameandaliwa vizuri kwa kupewa mazoezi na mitihani ya mara kwa mara na wamepata mbinu na maarifa mapya ya kujibu maswali ya mitihani kupitia  kambi za kitaaluma zilizofanyika katika kila shule.

“Sisi tumejiandaa vizuri sana na nina uhakika tutafanya vizuri katika Mtihani wa Taifa kama tulivyofanya vizuri kwenye Mock, walimu wametuandaa vizuri tulikuwa na kambi ya kitaaluma ambayo imetusaidia kukutana na walimu tofauti waliotufundisha vizuri zaidi, tunamuahidi Mkuu wa Mkoa kuwa hatutamuangusha” alisema Luhinda Nalisha kutoka S/M Somanda A.

“Tumejiandaa vizuri na tumejipanga kufanya vizuri, pia tunamshukuru Mkuu wa Mkoa kuja kututembelea na kutupa mawaidha tutayafanyia kazi, shule ipo vizuri kitaaluma na nidhamu  hivyo tuna uhakika wa kufaulu mtihani wa Taifa” alisema Bugumba Nindwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Somanda B

Akizungumza na wanafunzi hao, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewatakia mtihani mwema na kuwataka watumie mbinu walizopewa na walimu kufanya vizuri, huku akiwaonya  kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu wa aina yoyote.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa wahitimu wa vyuo vikuu  kufundisha masomo ya maandalizi ya Kidato cha kwanza(Pre-form one) kwa wanafunzi watakaohitimu darasa la saba  kwa ajili ya kuwaandaa wanafunzi na masomo ya elimu ya sekondari.

Naye Afisa elimu Msingi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mwl. Christopher Ligonda akishukuru kwa niaba ya walimu amesema wanafunzi wameandaliwa vizuri na wamefundishwa vizuri na wako tayari kwa ajili ya mtihani na matarajio yao ni kupata ufaulu mzuri kama  walivyoahidi wenyewe.

Mkoa wa Simiyu una jumla ya wanafunzi 29, 248 wa darasa la saba wanaotarajia kufanya mtihani wa Taifa mwaka huu, ambao kati yao wavulana ni 13, 594 na wasichana 15, 654.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa darasa la Saba katika Shule ya Msingi Somanda A na B Mjini Bariadi wakiwa katika maandalizi ya Mtihani wa Taifa utakaofanyika Septamba 11-12, 2019, wakati akiwatakia heri katika mtihani huo kwa niaba ya wenzao wote wa mkoa wa Simiyu Septemba 10, 2019.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifurahia jambo na  wanafunzi wa darasa la Saba katika Shule ya Msingi Somanda A na B Mjini Bariadi wakiwa katika maandalizi ya Mtihani wa Taifa utakaofanyika Septamba 11-12, 2019, wakati akiwatakia heri katika mtihani huo kwa niaba ya wenzao wote wa mkoa wa Simiyu Septemba 10, 2019.


Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Somanda A na B Mjini Bariadi wakimshika mkono Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kama ishara ya kupokea mkono wake wa heri kwao katika Mtihani wa Taifa utakaofanyika Septemba 11-12, 2019


Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Somanda A na B Mjini Bariadi wakimshika mkono Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kama ishara ya kupokea mkono wake wa heri kwao katika Mtihani wa Taifa utakaofanyika Septemba 11-12, 2019
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Somanda A na B Mjini Bariadi wakishangilia mara baada ya kupokea salamu za heri ya Mtihani wa Taifa utakaoanza Septemba 11-12, 2019 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati alipowatembelea Septemba 10, 2019 shuleni hapo kwa lengo la kuwatakia heri katika mtihani huo.
Afisa Elimu Msingi Halamashauri ya Mji wa Bariadi,  Mwl. Christopher Legonda akitoa neno la shukrani mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kuzungumza na wanafunzi wa darasa la Saba katika Shule ya Msingi Somanda A na B Mjini Bariadi wakiwa katika maandalizi ya Mtihani wa Taifa utakaofanyika Septemba 11-12, 2019, kwa lengo la kuwatakia heri katika mtihani huo kwa niaba ya wenzao wote wa mkoa wa Simiyu Septemba 10, 2019.
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Somanda A na B Mjini Bariadi wakiimba wimbo wa Tanzania Tanzania na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu =, Mhe. Anthony Mtaka wakati alipowatembelea Septemba 10, 2019 shuleni hapo kwa lengo la kuwatakia heri katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Septemba 11-12, 2019.


Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!