Friday, May 31, 2019

RC MTAKA AWAHAKIKISHIA USHIRIKIANO WA SERIKALI WAUMINI, VIONGOZI WA MADHEHEBU YA DINI

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewahakikishia waumini na viongozi wa madhehebu ya dini mkoani hapa kuwa viongozi wa serikali wako pamoja nao na wataendelea kushirikiana na kila watakapo wahitaji .

Mtaka ameyasema hayo jana Mei 30, 2019 katika futari aliyoiandaa kwa waumini na viongozi wa madhehebu ya Kiislam katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi.

“Ndugu zangu waislam mliopo hapa naomba muamini kabisa kwamba viongozi wa mkoa na viongozi wote wa Serikali kwenye maeneo yetu  ndani ya mkoa wa Simiyu wako pamoja na ninyi; kwa jambo lolote, eneo lolote ambalo mngehitaji ushirikiano kwenye mkoa wetu sisi tuko tayari kuunga mkono” alisema Mtaka.

Aidha, ameshauri viongozi wa BAKWATA Mkoa wa Simiyu kuomba kuandaa tukio moja kubwa la Kitaifa kufanyika Mkoani Simiyu kama ambavyo yamekuwa yakifanyika katika mikoa mingine na akaahidi kushirikiana na viongozi hao endapo watakuwa tayari kuandaa tukio lolote.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito pia kwa viongozi wa Madhehebu ya Kiislam kutengeneza mazingira mazuri kwa vijana na kuwafundisha ikiwa ni njia moja wapo ya kuwaandaa kushiriki katika mashindano ya kuhifadhi Quran ili Mkoa wa Simiyu na nchi kwa ujumla iweze kuwakilishwa vema katika mashindano hayo.

Sambamba na hilo amewashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuiombea nchi, viongozi wake, kuombea amani, umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania ambapo amebainisha kuwa Serikali inatambua mchango wa Taasisi za dini katika nchi na kwa namna viongozi wa dini wanavyoshirikiana na Serikali katika masuala na mtukio mbalimbali.

Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mahamoud Kalokola amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa namna anavyoenzi waislam na akatoa wito kwa watu wengine kuiga mfano wake kwa kuwa kila anyefanya hivyo anapata thawabu yake kwa Mwenyezi Mungu.

Ameongeza kuwa tendo hilo la kufuturisha linawakusanya watu pamoja walio waislam na wasio waislam jambo ambalo linadumisha umoja, upendo, ushirikiano na mshikamano kwa wote bila kujali tofauti ya dini zao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amempongeza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambao nao watajipanga kufanya jambo hili ili nao waweze kupata baraka za Mwenyezi Mungu.

Huu umekuwa ni utaratibu kwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu, kuandaa furati kwa waumini viongozi wa madhehebu ya dini ya Kiisla, ambayo pia huwahusisha viongozi wengine wa chama na Serikali wakati wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
MWISHO




Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akiteta jambo na Sheikh wa Mkoa wa Simiyu, Mahamoud Kalokola  mara baada ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi wengine jana Mei 30, 2019.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi mbalimbali walioshiriki katika futari aliyoindaa Mei 30, 2019.
Baadhi ya waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi mbalimbali walioshiriki katika futari aliyoandaliwa  na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili yao, Mei 30, 2019.
Baadhi ya waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi mbalimbali walioshiriki katika futari aliyoandaliwa  na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili yao, Mei 30, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi mbalimbali walioshiriki katika futari aliyoindaa kwa ajili yao, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili ya waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi wengine jana Mei 30, 2019.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga baada ya futari aliyoandaliwa  na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili ya waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi wengine jana Mei 30, 2019.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi mbalimbali walioshiriki katika futari aliyoindaa kwa ajili yao, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili ya waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi wengine jana Mei 30, 2019.
Baadhi ya waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi wa Chama na Serikali wakishiriki futari iliyoandaliwa kwa ajili ya na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka jana Mei 30, 2019.
Baadhi ya waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi wa Chama na Serikali wakishiriki futari iliyoandaliwa kwa ajili ya na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka jana Mei 30, 2019.
Mwakilishi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu akizungumza na waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi mbalimbali walioshiriki katika futari aliyoindaa kwa ajili yao, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili ya waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi wengine jana Mei 30, 2019.

Wednesday, May 29, 2019

MWENGE WA UHURU WAHITIMISHA MBIO ZAKE MKOANI SIMIYU ASILIMIA 97 YA MIRADI YAKUBALIWA

Mwenge wa Uhuru umemaliza mbio zake leo Mkoani Simiyu na kukabidhiwa katika Mkoa wa Mara, ambapo miradi 33 kati 34 sawa na asilimia 97 ya miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri zote sita imekubaliwa na kuzinduliwa, kukaguliwa, kuonwa na kuwekewa mawe ya msingi.
Akitoa taarifa kabla ya kukabidhi Mwenge wa Uhuru mkoani Mara, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema ni mradi mmoja tu wa maji ambao umeonekana kuwa na kasoro ambapo amebainisha kuwa kasoro hizo zitafanyiwa kazi na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2019 atapata taarifa mapema iwezekanavyo ya namna zilivyofanyiwa kazi.

Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali amewapongeza viongozi na wananchi Mkoani Simiyu, huku akibainisha kuwa  tangu mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 zizinduliwe rasmi Mkoani Songwe, Simiyu ni mkoa wa Tisa lakini umeonekana kuwa mkoa nambari moja kwa namna ulivyolitekeleza jukumu hili.


Aidha, amesema yeye pamoja na wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa wengine katika kipindi cha siku sita walizokaa Simiyu wamebaini kuwepo kwa umoja, ushirikiano na kuheshimiana miongoni mwa wananchi, watumishi na viongozi mambo ambayo ni ya msingi katika maendeleo.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima, Mei 28, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akiongea na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu kabla ya kukabidhiwa rasmi mkoani Mara, Mei 28, 2019
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akiagana na Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini kabla ya kukabidhiwa rasmi mkoani Mara, Mei 28, 2019 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye karatasi mkononi) akiwasilisha taarifa yam bio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu, kabla ya kukabidhi Mwenge wa Uhuru Mkoani Mara, Mei 27, 2019.


WANANCHI 17,084 KUNUFAIKA NA HUDUMA ZA VIPIMO IGALUKILO BUSEGA

Jumla ya Wananchi 17,084 wa kata ya Igalukilo na Vijiji jirani wilayani Busega wanatarajia kunufaika na huduma za vipimo mbalimbali vya afya na kupunguza umbali wa kupata huduma hiyo mara baada ya kukamilika kwa Jengo la Maabara linalojengwa katika Kituo cha Afya cha Igalukilo


Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Busega, Dkt. Godfrey Mbangali wakati akiwasilisha taarifa ya Ujenzi wa jengo hilo kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo hilo.

Pamoja na Jengo hilo Mwenge wa Uhuru umepitia miradi mbalimbali wilayani Busega ikiwa ni pamoja na Vyumba vitatu vya madarasa na matundu sita ya vyoo Shule ya Sekondari Ngasamo, ujenzi wa Jengo la Benki ya NMB na Ujenzi wa Kisima Kirefu cha Maji Kijiji cha Bukabile. 

Aidha, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 amekagua kazi zinazofanywa na vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu pamoja na kuzindua klabu ya Wapinga rushwa katika Shule ya Sekondari Kabita.

Baadhi ya wananchi wakishuhudia Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee  Mkongea Ali, akiweka jiwe la msingi Jengo la Maabara katika kituo cha Afya Igalukilo, wakati wa mbio za Mweng  wa uhuru wilayani Busega Mei 27, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga(kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera, kwa ajili ya kuanza mbio zake wilayani Busega Mei, 27, 2019.
 Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee  Mkongea Ali, akiweka jiwe la msingi Jengo la Benki ya NMB lililopo NYASHIMO, wakati wa mbio za Mweng  wa uhuru wilayani Busega Mei 27, 2019.


Jengo la Benki ya NMB lililopo NYASHIMO, lilowekewa jiwe la msingi wakati wa mbio za Mweng  wa uhuru wilayani Busega Mei 27, 2019.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee  Mkongea Ali (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi ambao ni wanachama wa klabu ya kupinga rushwa shule ya sekondari Kabita, walimu wao walezi,  Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni (mwenye shati la kijani) na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera(mwenye skafu na nguo ya kitenge), mara baada ya kuzindua klabu hiyo Mei 27, 2019.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee  Mkongea Ali, wakimbiza mwenge wa uhuru wengine  na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Busega wakieleka eneo la kutoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru, mara baada ya kukagua matundu sita ya vyoo, katika shule ya sekondari Ngasamo, wakati wa mbio za Mweng  wa uhuru wilayani Busega Mei 27, 2019.
Mbunge wa Busega Dkt. Raphael Chegeni (mwenye shati la kijani) akizungumza jambo na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee  Mkongea Ali, kabla ya kufungua mradi wa  Kirefu cha Maji Kijiji cha Bukabile, wakati wa mbio za Mweng  wa uhuru wilayani Busega Mei 27, 2019.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee  Mkongea Ali akipokea maelezo kutoka kwa kiongozi wa kikundi cha vijana wanaotengeneza bidhaa za ngozi wialayni Busega, wakati wa mbio za Mweng  wa uhuru wilayani Busega Mei 27, 2019.

WANANCHI WAISHUKURU SERIKALI KUWAJENGEA DARAJA BARIADI


Wananchi wa Vijiji vya Ikinabushu na Isuyu wilayani Bariadi wameishukuru Serikali kwa kuwajengea daraja ambalo limerahisisha mawasiliano na usafirishaji wa abiria, mazao na mizigo kutoka Ikinabushu-Isuyu-Dutwa-Bariadi na Lamadi.

Shukrani hizo zimetolewa mara baada ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali kufungua daraja la Isuyu Mei 26, 2019

Wananchi hao wamesema kabla ya kujengwa kwa daraja hilo walikuwa wakitumia daraja la kamba na miti na kutozwa fedha.

“ Tunaishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kutuwezesha kupata daraja sasa hivi watoto wetu wanaenda shuleni kwa raha hata mvua ikinyesha, kabla ya kujenga daraja hili watu walikuwa wanahatarisha maisha” alisema John Maduhu.

“mvua ikinyesha ilikuwa shida kuvuka kwenda Dutwa maana tulikuwa tunatakiwa kuvushwa kwa kamba” alisema Ester Saguda.

Awali akikagua kiwanda cha kuchakata alizeti kilichopo kijiji cha Igaganulwa Kata ta Dutwa, Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali ametoa wito kwa Halmashauri na wawekezaji wengine kutoa kipaumbele kwa wataalam wazawa katika fursa za ajira ili waweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa kati na kulitumikia Taifa.

Akiwasilisha taarifa kwa kiongozi  huyo, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema kuanzishwa kwa kiwanda hicho ni kuunga mkono utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Viwanda kufikia uchumi wa kati na ni mradi wa kujipatia mapato ya ndani.

Ukiwa wilayani Bariadi Mwenge wa Uhuru umepitia miradi minane yenye thamani ya shilingi milioni 700.


Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali (wa tatu kushoto) akifungua daraja la Isuyu wilayani Bariadi, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mei 25, 2019.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe(kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Bw. James John katika Kijiji cha Igaganulwa, Mei 25, 2019.
Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  akikagua daraja la Isuyu wilayani Bariadi kabla ya kulifungua, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mei 25, 2019.
Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali (wa pili  kushoto) akikagua kiwanda cha kuchakata alizeti kilichopo kijiji cha Igaganulwa Kata ta Dutwa, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mei 25, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa Igaganulwa Dutwa kabla ya kumkaribisha :- Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali (wa tatu kulia) baada ya kukagua kiwanda cha kuchakata alizeti kilichopo kijiji cha Igaganulwa Kata ta Dutwa, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mei 25, 2019.
Sehemu ya Jengo la Kiwanda cha kuchakata alizeti kilichopo kijiji cha Igaganulwa Kata ta Dutwa
Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akimtwisha maji mwananchi wa Kijiji cha Msanga B mara baada ya kuzindua mradi wa maji, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mei 25, 2019.

Hifadhi ya Msitu katika Kijiji cha Sengerema wilayani Bariadi ilikaguliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Mei 25, 2019.
Sehemu ya Bweni lililowekewa jiwe la msingi katika shule ya sekondari Dutwa na Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mei 25, 2019.
Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akikabidhi cheti Klabu ya Kupambana na dawa za kulevya katika Shule ya Sekondari Mwantimba, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mei 25, 2019.

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MWAKA 2019 AWEKA JIWE LA MSINGI SHULE YA DKT. BALELE MAJAHIDA



Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019,  Ndg. Mzee Mkongea Ali akiweka jiwe la msingi katika Madarasa sita ya Shule ya Sekondari tarajiwa ya Dkt. Yohana Balele iliyopo Majahida Mjini Bariadi,wakati wa mbio za mwenge wa uhuru mjini Bariadi Mei 25, 2019.



Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019,  Ndg. Mzee Mkongea Ali ameweka Jiwe la Msingi katika Madarasa sita ya Shule ya Sekondari tarajiwa ya Dkt. Yohana Balele iliyopo Majahida Mjini Bariadi, ambayo kikamilika kwake kutawapunguzia wanafunzi wa Kata ya Isanga kutembea Mwendo mrefu ambapo sasa wanasoma katika Shule za Sekondari Biashara Kata ya Sima na Kidinda Kata ya Bariadi.


Awali akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, Ndg. Mzee Mkongea Ali, Mwenyekiti wa Mtaa wa Majahida, Ndimi Silanga amesema vyumba hivyo vimejengwa kwa gahrama ya shilingi milioni 97 ikiwa ni michango ya wananchi, wadau mbalimbali wa elimu pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhe. Andrew Chenge.  

Kwa upannde wake Elizabeth Jailo ambaye ni mkazi wa Majahida na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Biashara amesema kujengwa kwa shule hiyo kutasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa madarasa katika shule anayosoma maana wanafunzi wa shule hiyo wanaotoka karibu na Shule mpya watasoma hapo na kupunguziwa adha ya kutembea takribani kilometa 15 kwa siku.

Pamoja na kuweka Jiwe la Msingi Madarasa hayo, Mwenge wa Uhuru umepitia miradi mbalimbali ikiwepo kufungua Nyumba ya Kulala wageni Nghunde Classic Lodge, kuona mradi wa Uhifadhi wa Mazingira wa Msitu wa Kanisa Katoliki Old Maswa Sesele.

Aidha,umefungua jengo la Wodi ya Wazazi Zahanati ya Mwakibuga na kuona shughuli za wanawake Wajasiriamali pamoja na kuzindua klabu ya kupinga rushwa na klabu ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya shule ya Sekondari Kusekwa.
MWISHO


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019,  Ndg. Mzee Mkongea Ali akiweka jiwe la msingi katika Madarasa sita ya Shule ya Sekondari tarajiwa ya Dkt. Yohana Balele iliyopo Majahida Mjini Bariadi,wakati wa mbio za mwenge wa uhuru mjini Bariadi Mei 25, 2019.


Baadhi ya wananchi wa Kata ya Isanga wakishuhidia uwekaji wa jiwe la msingi katika Madarasa sita ya Shule ya Sekondari tarajiwa ya Dkt. Yohana Balele iliyopo Majahida Mjini Bariadi,wakati wa mbio za mwenge wa uhuru mjini Bariadi Mei 25, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019,  Ndg. Mzee Mkongea Ali akikagua moja ya vyumba sita vya madarasa Shule ya Sekondari tarajiwa ya Dkt. Yohana Balele iliyopo Majahida Mjini Bariadi,wakati wa mbio za mwenge wa uhuru mjini Bariadi Mei 25, 2019.
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru na askari wa FFU wakiondoka baada ya kufungua Nyumba ya Kulala wageni Nghunde Classic Lodge wakati wa mbio za mwenge wa uhuru mjini Bariadi Mei 25, 2019.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019,  Ndg. Mzee Mkongea Ali akizindua Jengo la Wodi ya wazazi katika Zahanati ya Mwakibuga, wakati wa mbio za mwenge wa uhuru mjini Bariadi Mei 25, 2019.

Jengo la Wodi ya wazazi katika Zahanati ya Mwakibuga lililozinduliwa wakati wa mbio za mwenge wa uhuru mjini Bariadi Mei 25, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019,  Ndg. Mzee Mkongea Ali akipewa maelezo kuhusu namna hifadhiya msitu wa Sesele inavyotunzwa, wakati wa mbio za mwenge wa uhuru mjini Bariadi Mei 25, 2019.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019,  Ndg. Mzee Mkongea Ali akipewa maelezo na mwenyekiti wa Klabu ya wapinga rushwa katika Shule ya Sekondari Kusekwa, wakati wa mbio za mwenge wa uhuru mjini Bariadi Mei 25, 2019.


WANANCHI ZAIDI YA 300,000 KUNUFAIKA NA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA

Jumla ya wakazi 346,365 wa Wilaya ya Itilima na maeneo ya jirani wanatarajia kunufaika na ujenzi wa mradi wa hospitali ya Wilaya ya Itilima inayotarajiwa kukamilika Juni 30 mwaka 2019.


Mradi huo wenye lengo la kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya na kusogeza karibu huduma hiyo kwa wananchi ,hadi kukamilika kwake unatarajia kutumia kiasi cha sh bil 1 .5.


Akisoma taarifa ya mradi wa Ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Itilima kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2019,Mzee Mkongea Ali ,mganga mkuu wa Wilaya hiyo Dk Anorld Charles amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutarahisisha huduma za  wananchi wa Wilaya humo.

Dk Charles ameeleza kuwa wananchi wengi wa Wilaya hiyo wamekuwa wakitembea umbali mrefu wa wastani wa kilometa 45 hadi 50 kufuata huduma za afya katika hospitali ya Bariadi.

Amesema kutokana na hali hiyo ya kutembea umbali mrefu,wengi wao hupoteza maisha kwa kukosa huduma stahiki za haraka hususani akinamama wajawazito ambao wengi wao hupoteza damu nyingi njiani.

Ameongeza kuwa endapo hospitali hiyo itakamilika kwa muda muafaka,itasaidia sana kupunguza vifo vya akinamama wajawazito wanaopoteza damu nyingi pindi wawapo njiani kuelekeza katika hospitali ya wilaya ya Bariadi.

Amesema kwa mwaka 2018 (Jan hadi Dec) pekee jumla ya akinamama 5 walipoteza maisha kwa kuvuja damu nyingi kwa kucheleweshwa kufika mapema katika zahanati na hospitali zilizo karibu nao.

Naye kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2019 Ndg. Mzee Mkongea Ali alisema kuwa jitihada za Ukamilishaji wa hospitali hiyo zinatakiwa ziwe za haraka iwezekanapo kabla ya kuisha mwaka wa fedha, kwani endapo wakishindwa kukamilisha kwa muda husika hawataweza kupata fedha za ukamilishaji huo.

" napenda kuwashauri kuwa ukamilishaji wa hospitali hiyo unatakiwa uwe Juni 30 mwaka huu kama ilivyoelekezwa hivyo ni lazima ujenzi uende kwa haraka usiku na mchana...la sivyo mwaka ya fedha 2018/2019 utakapomalizika itakuwa vigumu kupata fedha hizo zilizokuwa zimetengwa katika bajeti ya 2018/2019.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi amesemaViongozi wilayani humo watahakikisha Hospitali hiyo inakamilika kabla ya juni 30, 2019 kama ilivyoelekezwa na Waziri wa nchi, Ofisi ya Rai TAMISEMI.

Marangwa Maduhu mkazi wa kijiji cha Nguno Wilayani humo,amesema uwepo wa hospitali hiyo itawasaidia sana kupunguza gharama za usafiri walizokuwa wakizitumia kufuata matibabu Wilayani Bariadi.

Mpaka sasa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Itilima tayari imeshatumia kiasi cha sh bil 1.2 sawa na asilimia 81 ya utekelezaji wake

Katika hatua nyingine kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2019 Ndg. Mzee Mkongea Ali ametoa wito kwa wananchi kutunza vyanzo vya maji kwa kupanda miti rafiki katika vyanzo vya maji na kusisitiza wale wote ambao watakiuka sheria wachukuliwe hatua.
MWISHO




Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akipata maelezo kuhusu ramani ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Itilima, wakati wa mbio za mwenge wa uhuru Mei 24, 2019 wilayani humo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akimtwisha mama ndoo mara baada ya kuzindua mradi wa maji wa Mwamapalala wilayani Itilima, wakati wa mbio za mwenge wa Uhuru wilayani humo,  Mei 24, 2019. 

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akikabidhi cheti wanachama wa Klabu ya wapinga rushwa katika shule ya Sekondari Mwamapalala, mara baada ya kuzindua klabu hiyo wakati wa mbio za mwenge wa uhuru Mei 24, 2019 wilayani humo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akikagua moja ya vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya Msingi Lagangabilili, wakati wa mbio za mwenge wa uhuru Mei 24, 2019 wilayani humo.
wanachama wa Klabu ya wapinga rushwa katika shule ya Sekondari Mwamapalala, wakifurahia uzinduzi wa klabu hiyo wakati wa mbio za mwenge wa uhuru Mei 24, 2019 wilayani humo
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali (mwenye skafu) akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa misitu wilayani Itilima, mara baada ya kutembelea mradi huo wakati wa mbio za mwenge wa uhuru Mei 24, 2019 wilayani humo.
                                     Moja ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Itilima
Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Benson Kilangi akimkaribisha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali kabla ya kukabidhiana Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza :- Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali (hayupo pichani) wakati wa mbio za mwenge wa uhuru Mei 24, 2019 wilayani humo.

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!