Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo ametoa
muda wa siku moja kwa Mkandarasi SUMA
JKT anayejenga Jengo la Kituo cha Umahiri Simiyu kuamilisha sehemu ya Jengo
hilo iliyopangwa kutumika kama Soko la Madini la Mkoa.
Nyongo ameyasema hayo Mei 02, 2019 wakati alipofanya ziara ya kukagua
maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo ambalo sehemu litatumika kama kituo cha
umahiri na sehemu kama Soko la Madini la Mkoa.
“ Kwa mkoa wa
Simiyu tumeona hapa tunaweza kupatumia kwa kuanzia kwenye soko la madini,
nimeshatoa maagizo kuwa jengo hili walimalizie mara moja, ili waweze kutoa
sehemu ambayo itatumika kwa ajili ya soko la madini na kufikia kesho jioni
tunataka jengo hili lianze kutumika kama soko la Madini “ amesema Nyongo.
Aidha, Nyongo amesema anatumia fursa hiyo kuwajulisha wachimbaji wadogo wadogo wa madini kuwa Simiyu kutakuwa
na jengo ambalo litatumika kununua na kuuza madini.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka amesema kama mkoa wamejipanga vizuri katika soko la madini, huku
akiwakaribisha wafanyabiashara wa madini kutoka mkoa wa Simiyu na mikoa jirani kufika katika kituo hicho
ambacho amesema kitakuwa kituo bora chenye uhakika wa kufanya biashara hapa
nchini.
Mtaka ameongeza kuwa kituo hicho ambacho
kitafunguliwa rasmi wiki ijayo kitatoa fursa kwa Watanzania kuanza kuangalia
ufanyaji wa biashara katika eneo la madini kwa njia ambazo ni halali, akatoa
wito kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Simiyu pamoja na kuwekeza biashara katika
kilimo, mifugo na viwanda wawekeze pia katika biashara ya madini.
Naye Sajenti Emmanuel Igogo kutoka SUMA JKT amesema
agizo la Naibu Waziri la kukamilisha sehemu ya Jengo la Kituo ca Umahiri ambayo
itatumika kama soko la madini (Kituo cha kuuzia madini) litatekelezwa kama
lilivyoagizwa.
“ Tutatekeleza agizo la Mhe. Naibu Waziri tutaanza
leo kulifanyika kazi na kwa kuwa kazi hii haikuwepo kwenye mkataba wetu wa
awali nitawasiliana na viongozi wangu na tutakamilisha” alisema Sajenti Igogo.
MWISHO
Naibu Waziri wa Madini,
Mhe. Stanslaus Nyongo( wa pili kushoto)
akizungumza na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipotembelea
Kituo cha Umahiri kilichopo Nyaumata Bariadi kukagua maendeleo ya ujenzi wa
Kituo hicho, ambacho kimeamriwa kuwa sehemu ya jengo hilo ikamilike haraka na
ianze kutumika kama Soko la Madini.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (
watatu kushoto) akichangia jambo kwenye mazungumzo wakati wa ziara ya Naibu
Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo( wa pili kushoto) alipotembelea Kituo cha Umahiri kilichopo
Nyaumata Bariadi kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo hicho, ambacho kimeamriwa
kuwa sehemu ya jengo hilo ikamilike haraka na ianze kutumika kama Soko la
Madini.
Naibu Waziri wa Madini,
Mhe. Stanslaus Nyongo( wa pili kulia)
akizungumza na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipotembelea
Kituo cha Umahiri kilichopo Nyaumata Bariadi kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo
hicho, ambacho kimeamriwa kuwa sehemu ya jengo hilo ikamilike haraka na ianze
kutumika kama Soko la Madini.
Jengo la Kituo cha
Umahiri Simiyu kilichopo Nyaumata Bariadi, ambacho kimeamriwa kuwa sehemu ya
jengo hilo ikamilike haraka na ianze kutumika kama Soko la Madini.
Meneja wa TANROADS Mkoa
wa Simiyu, Mhandisi. Albert Kent (kushoto) akizugumza na baadhi ya viongozi
wakati wa Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo( wa pili kushoto) alipotembelea Kituo cha Umahiri Simiyu kilichopo
Nyaumata Bariadi kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo hicho, ambacho kimeamriwa
kuwa sehemu ya jengo hilo ikamilike haraka na ianze kutumika kama Soko la
Madini.
Fundi akiendelea kupaka
rangi katika hatua za ukamilishaji
kwenye Jengo la Kituo cha Umahiri Simiyu Simiyu kilichopo Nyaumata Bariadi,
ambacho kimeamriwa kuwa sehemu ya jengo hilo ikamilike haraka na ianze kutumika
kama Soko la Madini.
0 comments:
Post a Comment