Friday, May 10, 2019

MWAUWASA, BENNET CONTRACTORS WASAINI MKATABA UJENZI WA MRADI WA MAJI WA BILIONI 1.8 BUSEGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi. Anthony Sanga  na Mkurugenzi wa Kampuni ya  Bennet Contractors Sabato Boaz kutoka Mwanza, wamesaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa Maji wa Nyashimo wilayani Busega utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.8.

Mkataba wa Mradi huo utakaonufaisha vijiji vya Bukabile, Mwagulanja na Bulima na kuhudumia wananchi 20,030 , umesainiwa Nyashimo wilayani Busega na kushuhudiwa na wananchi, viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya ya Busega na Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

Akizungumza na wananchi na viongozi waliofika kushuhudia zoezi hilo Mtaka amemtaka Mkandarasi Kampuni ya  Bennet Contractors kuzingatia muda na viwango katika utekelezaji wa mradi huo, huku akisisitiza kuhakikisha mradi huo unawanufaisha wananchi wanaozunguka eneo la mradi kwa kutoa ajira za muda na ununuzi wa vifaa vya ujenzi.

“Mkataba unaonesha mradi huu ni wa miezi 15, nikuombe mkandarasi miezi 15ni mingi tungehitaji tunapoanza maandalizi ya kutengeneza ilani ya CCM mwaka 2020 tuzungumzie utekelezaji wa ilani siyo mpango; tunahitaji jamii yetu inufaike kupitia mradi huu, vijana wapate ajira, mama ntilie wapike chakula na baadhi ya vifaa vya ujenzi vinunuliwe kwenye maduka ya hapa” alisema Mtaka.

Ameongeza kuwa Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 16.4  kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maji wilayani Busega, ikiwa ni pamoja na Mradi wa Lamadi, Kiloleli, Mwamanyili na ukarabati wa visima maeneo mbalimbali, ambayo itakapokamilika  itaongeza hali ya upatikanaji wa maji safi na salama Busega kutoka asilimia 39 ya sasa na kufikia asilimia 74.

Naye Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni amesema pamoja na mradi wa Nyashimo Serikali inatekeleza miradi mingine ya maji wilayani Busega ukiwepo wa Kiloleri Mradi wa Lamadi, hivyo akasisitiza wananchi kulinda na kutunza miradi hiyo ili iwanufaishe.

Nao wananchi wamesema“Tunashukuru kuletewa huu mradi tulikuwa tunapata adha ya maji tulikuwa tunanunua kwenye madumu na kufua ziwani, lakini endapo mradi huu uliosainiwa mkataba leo ukikamilika itakuwa ni neema kwetu hasa sisi wakina mama ambao ndiyo tunapata tabu zaidi na familia zetu” Sara Nanyori mkazi wa kijiji cha Bulima.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi. Anthony Sanga  amesema mradi wa Nyashimo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa kwa wananchi na unafadhiliwa kwa asilimia 100 na fedha za Serikali ya Tanzania.
Mkurugenzi wa Kampuni ya  Bennet Contractors(Mkandarasi) Sabato Boaz kutoka Mwanza, amesema pamoja na kwamba mkataba unaonesha utekelezaji ni miezi 15, kampuni yake inatarajia kutekeleza kwa ubora na kwa muda mfupi kadri itakavyowezekana ili kuleta  huduma ya maji safi na salama haraka kwa wananchi wa Nyashimo.
MWISHO


Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza(MWAUWASA), Mhandisi. Anthony Sanga  (kushoto) na  Mkurugenzi wa Kampuni ya Bennet Contractors, Sabato Boaz  kutoka Jijini Mwanza  wakibadilishana  nakala za mkataba waliosaini Mei 10, 2019 wilayani Busega ,  kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Maji wa Nyashimo na kushuhudiwa na viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya ya Busega na Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anthony Mtaka (mwenye suti ya rangi ya kijivu)  ambao utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.8

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi. Anthony Sanga  (kushoto) na  Mkurugenzi wa  Kampuni ya Bennet Contractors Sabato Boaz  kutoka Jijini Mwanza  wakitia saini  mkataba wa ujenzi wa mradi wa Maji wa Nyashimo Mei 10, 2019 wilayani Busega na kushuhudiwa na viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya ya Busega na Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye suti ya rangi ya kijivu)  ambao utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.8.
Kutoka kushoto Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza(MWAUWASA), Mhandisi. Anthony Sanga,   Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael  Chegeni wakielekea eneo maalum la utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Nyashimo wakifuatilia zoezi la  utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera akitoa neno la shukrani wakati wa  kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael  Chegeni akizungumza na wananchi wa Kata ya Nyashimo wakati wa kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Mwananchi kutoka kata ya Nyashimo akifurahia jambo na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Mickness Mahela wakati wa  zoezi la  kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wajumbe wa Bodi ya MWAUWASA wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kabla ya zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wajumbe wa Bodi ya MWAUWASA wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kabla ya zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Nyashimo wakiwa wamejipanga kwa lengo la kutoa kero zao kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kulia) kabla ya kuanza kwa zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kulia) akitoa ufafanuzi wa moja ya kero iliyowasilishwa na mkazi wa Kata ya Nyashimo, kabla ya kushuhudia  zoezi la  kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu akitambulisha viongozi wa mkoa walifika kushuhudia zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Busega, Komredi. kueleza juu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo, kabla ya kushuhudia  zoezi la  kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Nyashimo wakifuatilia zoezi la  kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kata ya Nyashimo, kabla ya kushuhudia  zoezi la  kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kulia) akiwahamasisha viongozi kumchangia mama mwenye uhitaji na pichani ni baadhi ya viongozi waliojitokeza kumsaidia mama huyo, kabla ya kushuhudia  zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.


0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!