Wednesday, May 1, 2019

RAS SIMIYU ASAINI MKATABA NA SUMA JKT UJENZI WA JENGO LA OFISI YA MKUU WA MKOA


Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesaini Mkataba wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Msimamizi Mkuu wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa, Kapteni Fabian Buberwa.
Mkataba huo umesainiwa Aprili 30, 2019 mbele ya Wataalam wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na SUMA JKT katika Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini ambaye aliwataka SUMA JKT kujenga jengo hilo kwa viwango na kuhakikisha linakamilika kwa wakati.
“SUMA JKT mmepewa heshima kubwa na Serikai yetu na viongozi wetu pia tunaomba muendelee kufanya vizuri ili kulinda heshima yenu; tunaomba mfanye kazi usiku na mchana jengo hili likamilike mapema na ka viwango” alisema Sagini.

Kwa upande wake Msimamizi Mkuu wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa, Kapteni Fabian Buberwa amemhakikishia Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini kuwa wakipata fedha watahakikisha wanakamilisha jengo hilo kwa wakati na kwa viwango vya juu, ili kuendellea kulinda heshima waliyopewa na Serikali

Naye Mhandisi wa Ujenzi wa Mkoa wa Simiyu, mashaka Luhamaba amesema Jengo hilo litakalojengwa eneo la Nyaumata Mjini Bariadi, litagharimu zaidi ya shilingi bilioni 5, 718, 387,926.20

Jengo hili linatarajiwa kuanza kujengwa mwezi Mei, 2019 na kukamilika baada ya miezi 18.
MWISHO.




Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto)  na Msimamizi wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa Kapteni. Fabian Buberwa  wakisaini Mkataba wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,inayotajarajiwa  kujengwa katika eneo la Nyaumata Mjini Bariadi kuanzia mwezi Mei, 2019.

Mkuu wa Kitengo cha Ugavi na Ununuzi, Bi. Vivian Watugulu akiwaonesha jambo Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto)  na Msimamizi wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa Kapteni. Fabian Buberwa katika Mkataba wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,inayotajarajiwa  kujengwa katika eneo la Nyaumata Mjini Bariadi kuanzia mwezi Mei, 2019.
Msimamizi wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa Kapteni. Fabian Buberwa  akizungumza na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) kabla ya viongozi hao kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,inayotajarajiwa  kujengwa katika eneo la Nyaumata Mjini Bariadi kuanzia mwezi Mei, 2019(kulia) Mhandisi wa Ujenzi wa Mkoa wa Simiyu, Mashaka Luhamba.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na Wataalam kutoka SUMA JKT na wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kabla ya kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Msimamizi wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa Kapteni. Fabian Buberwa  ,inayotajarajiwa  kujengwa katika eneo la Nyaumata Mjini Bariadi kuanzia mwezi Mei, 2019.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini na Msimamizi wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa Kapteni. Fabian Buberwa  ) kabla ya viongozi hao kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,inayotajarajiwa  kujengwa katika eneo la Nyaumata Mjini Bariadi kuanzia mwezi Mei, 2019.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na Wataalam kutoka SUMA JKT na wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kabla ya kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Msimamizi wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa Kapteni. Fabian Buberwa  ,inayotajarajiwa  kujengwa katika eneo la Nyaumata Mjini Bariadi kuanzia mwezi Mei, 2019.
Msimamizi wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa Kapteni. Fabian Buberwa(katikati) akioneshwa ramani ya Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Wakala wa Ujenzi (TBA) Simiyu, wakati aliopofika 

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!