Saturday, May 25, 2019

WAKULIMA WAKIWEZESHWA ZANA BORA ZA KILIMO WATALIMA KWA TIJA ZAIDI: KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali ametoa wito kwa viongozi wilayani Meatu kuwasaidia wakulima wa pamba  kupata zana bora za kilimo ili kuongeza tija  katika uzalishaji  na wilaya hiyo iendelee kuwa kinara katika uzalishaji wa zao la pamba nchini.


Ndg. Ali ameyasema hayo wakati Mwenge wa Uhuru ulipopita na kukagua  Shamba la Mbegu bora ya pamba lenye ukubwa wa ekari 13 katika Kijiji cha Mwabusalu ambapo alimpongeza mkulima Jidayi Charles na kumtunuku cheti cha kumtambua kama mkulima bora.

“Ninampongeza sana Bwana Jidayi maana ni wazee wachache sana wanaojihusisha na kilimo ni vizuri mkachukua jitihada za makusudi kumsaidia apate zana za kisasa, kama analima ekari 13 akiwa hana trekta nina uhakika akiwezeshwa atafanya vizuri zaidi, kama mmeshaanza utaratibu wa kumpatia mkopo uharakishwe ili kiwango cha uzalishaji kiweze kuongeza zaidi” alisema Mzee  Mkongea Ali.

Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani amesema wilaya ya Meatu ndiyo wilaya kinara katika uzalishaji wa pamba nchini ambapo amebainisha kuwa katika msimu wa mwaka 2018/2019 ilizalisha takribani kilo milioni 31 za pamba na akaeleza kuwa mkakati wa wilaya ni kuendelea kuwasaidia wakulima kwa utaalam na mikopo za kununua zana bora ili waweze kuzalisha kwa tija  zaidi.

Akitoa taarifa ya mradi wa shamba hilo, Afisa Kilimo wa Wilaya ya Meatu, Bw.Thomas Shilabu amesema uzalishaji wa zao la pamba unakabiliwa na changamoto ya baadhi ya wakulima kulima wa kilimo cha mazoea kwa kusia mbegu na kupalilia maotea.

Kwa upande wake Bw. Jidayi Charles amesema kwa sasa anatumia trekta ya kukodi kulima shamba lake lenye ukubwa wa ekari 13 ambalo linachangia kuchelewesha uandaaji wa shamba kwa kuwa linatumiwa na wakulima wengi, lakini endapo atakapata trekta lake litamrahisishia kuandaa shamba mapema na kwa urahisi zaidi.

Pamoja na kutembelea mradi wa shamba za kuzalisha mbegu bora za pamba, Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Meatu umezindua vyumba viwili vya maabara shule ya Sekondari Mwandoya, kutembelea mradi wa maji wa SangaItiinje na kupanda miti katika Chanzo cha maji, kukagua klabu ya wanafunzi ya wapinga RUSHWA na Klabu ya wanafunzi ya kupambana na mimba za utotoni shule ya msingi Isengwa.

Wakati mwenge wa uhuru ulipopita kuona shughuli za klabu ya mapambano dhidi ya mimba za utotoni, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ameupongeza uongozi wa wilaya ya Meatu kuanzisha klabu hizo shuleni na akatoa wito kwa wataalam wa Ustawi wa Jamii na Dawati la jinsia na vyombo vya dola kutowahurumia wote wanaobanika kusababisha mimba za utotoni.

Aidha, ulifungua Nyumba ya kulala wageni TS Lodge, kukagua shughuli za kikundi cha vijana wajasiriamali, kukagua shughuli za mapambano dhidi ya rushwa, mapambano dhidi ya mimba za utotoni na mapambano dhidi ya malaria.
MWISHO


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  akikagua shamba la mbegu bora za pamba katika Kijiji cha Mwabusalu wilayani Meatu, Mei 23, 2019.
Sehemu ya shamba la mbegu bora za pamba ekari 13 linalomilikiwa na Mkulima Jidayi Charleas wilayani Meatu, lililotembelewa na kukaguliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru Mei 23, 2019 wilayani humo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  akifungua Vyumba viwili vya maabara katika shule ya sekondari Mwandoya wilayani Meatu, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  akipanda mti katika chanzo cha maji cha Mradi wa maji wa SangaItinje wilayani Meatu, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali   akiwa na wakimbiza mwenge wa Uhuru wengine wakikagua pampu ya maji katika Mradi wa maji wa Sanga Itinje wilayani Meatu, Mei 23, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani (kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe katika Kijiji cha Sangaitinje wilayani Meatu, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  (mwenye galoni la maziwa ya Meatu(Meatu Milk) akiangalia bidhaa za maziwa zinazozalishwa katika kiwanda cha Meatu Milk kinachomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Klabu ya Wapinga Rushwa katika shule ya Msingi Isengwa, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  (kulia) akiangalia burudani kutoka kwa Wanachama wa Klabu ya Kupinga Mimba za Utotoni katika shule ya Msingi Isengwa, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 22, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  ( wa tatu kulia) akizungumza na kikundi vijana wanaotengeneza Batiki Mjini Mwanhuzi wilayani Meatu, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  akizungumza na Wanachama wa klabu ya Kupinga mimba za Utotoni katika Shule ya Msingi Isengwa wilayani Meatu, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  akiangalia mazoezi kwa vitendo ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mwandoya wilayani Meatu, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  akiangalia mazoezi kwa vitendo ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mwandoya wilayani Meatu, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Sehemu ya mbele ya Vyumba vya maabara vilivyozinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru Mei 23, 2019 katika shule ya sekondari Mwandoya wilayani Meatu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akizungumza na wanachama wa Klabu ya Wapinga Rushwa katika shule ya Msingi Isengwa, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akisaini cheti cha Klabu ya Wapinga Rushwa katika shule ya Msingi Isengwa, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Baadh ya vikundi vya vijana vya wilaya ya Meatu vilivyokaguliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akitoa ujumbe wa mbio za Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuzindua vyumba viwili vya maabara katika Shule ya Sekondari Mwandoya wilayani Meatu, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali, wakimbiza Mwenge wa Uhuru wengine na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Meatu wakiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa klabu ya Kupinga mimba za Utotoni katika Shule ya Msingi Isengwa wilayani Meatu, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Nyumba ya pampu na jenereta katika Mradi wa Maji wa SangaItinje wilayani Meatu ambao ulitembelewa na Mbio za Mwenge wa Uhuru Mei 23, 2019 wilayani humo.
Sehemu ya Vyumba vya maabara vilivyozinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru Mei 23, 2019 katika shule ya sekondari Mwandoya wilayani Meatu.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!