Thursday, May 9, 2019

RC MTAKA AONGOZA WANANCHI MAZISHI YA RC MSTAAFU WA SHINYANGA BRIGEDIA JENERALI. DKT.BALELE


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka leo Mei 09, 2019 amewaongoza mamia ya waombolezaji kutoka Mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Mwanza , Dar es Salaam na maeneo mengine nchini, katika mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambayo yamefanyika katika eneo la Malinoni, Mtaa wa Kidinda Mjini Bariadi.

Akizungumza na waombolezaji hao kabla ya kuaga mwili wa Marehemu Dkt.Balele, Mtaka amesema mkoa wa Simiyu unatambua mchango wa Marehemu katika jitihada za kuanzisha mkoa wa Simiyu na mapinduzi makubwa aliyoyafanya katika Elimu na kuahidi kuweka alama yake katika mkoa kumuenzi.

"Uongozi wa Mkoa kwa kutambua mchango wa Marehemu Dkt.Balele katika kuanzisha mkoa huu na katika mapinduzi ya Elimu aliyoyafanya wilayani Bariadi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, tunaweka alama ya maisha yake kama kumbukumbu katika Shule ya Sekondari Majahida ambayo itabadilishwa Jina kuwa Dkt.Balele Sekondari na Barabara moja katikati ya Mji wa Bariadi itaitwa Barabara ya Dkt.Balele"  alisema Mtaka.

Akisoma Wasifu wa Marehemu, Dkt.Balele  Kapteni Zaharani Masimba wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) amesema amelitumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa zaidi ya miaka 32 na kutunikiwa medali mbalimbali, ikiwemo ya Vita, Kagera, miaka 20 ya JWTZ, Miaka 40 ya JWTZ, Utumishi wa muda mrefu na Utumishi uliotukuka.

Naye mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, Brigedia Jenerali, Robson Mboli Mwanjela amesema, licha ya Marehemu kustaafu Jeshi, alitumia vizuri taaluma yake ya Udaktari kuwasaidia watu mbalimbali na kuwataka wananchi wa Simiyu kuiga mema mengi aliyoyafanya.

"Marehemu atakumbukwa daima kwa mchango wake mkubwa alioutoa wakati wa utumishi wake  jeshini na kwa Taifa kwa ujumla, katika vyeo na madaraka mbalimbali aliyopewa wakati wa utumishi wake na hata baada ya kustaafu" alisema Brig. Jen. Mwanjela.

Nao baadhi ya viongozi waliofanya kazi na Marehemu Dkt. Balele wamemuelezea kuwa alikuwa mwaminifu, mchapakazi, hodari na mwenye Upendo huku wakitoa wito kwa wananchi Mkoani Simiyu na hapa nchini kwa ujumla kuyaenzi mema yake.

"Dkt.Balele alikuwa kiongozi halisi maana alitumia uwezo na ushawishi wake kuwafanya watu wake wawe kama anavyotamani wawe, alipenda sana Elimu alitaka watu wasome na pengine hata zaidi yake, ndiye aliyehamasisha Wafanyabiashara kujenga Biashara Sekondari hapa BARIADI, naomba wana Simiyu tumuenzi kwa kuwekeza katika elimu" alisema Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Change

"Marehemu Dkt.Balele alikuwa mdau mkubwa wa Elimu katika kipindi chake alifanikiwa kuanzisha shule za Sekondari 44 Wilaya ya Bariadi na Itilima ambayo pia kipindi hicho ilikuwa sehemu ya Bariadi, lakini pia wakati wa mpango wa kuugawa mkoa wa Shinyanga alikuwa na mchango mkubwa wa kuanzisha mkoa wa Simiyu na makao makuu kuwa Bariadi, naomba tuendelee kuenzi mema yake" Baraka Konisaga, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mstaafu.

Marehemu Dkt.Balele ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga mwaka 2006 hadi  mwaka 2011 alizaliwa Desemba 28, 1948 katika Kijiji Cha Kasoli wilayani Bariadi na alipatwa na mauti Mei 02, 2019 katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
MWISHO

Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) wakiwa  wamebeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,  Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele,  ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Kutoka kulia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge wakiteta jambo kabla ya zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga , Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) wakiweka  Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele,  ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Kulia ni Mjane wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele akiweka shada la maua kwenye kaburi la mume wake ,  ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Naibu wa ziri waMadini, Mhe. Stanslaus Nyongo akiweka shada la Maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato, Mch.Elias Swita(wa pili kulia) akibariki kaburi ambalo umezikwa mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Komredi Kheri James (mwenye kofia) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na wengine ni baadhia ya viongozi wakiondoka eneo alilozikwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Kutoka kushoto Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael  Isamuhyo, Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Njelu Kasaka, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga wakiteta jambo mara baada ya zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele kumalizika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  akiweka shada la Maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Kutoka kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa Komredi Enock Yakobo, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Simiyu, Lumen Mathias , Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Komredi Kheri James na Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Njelu Kasaka,wakiteta jambo mara baada ya zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele kumalizika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waliofanya kazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele baada ya zoezi la kuaga mwili  wa marehemu  kumalizika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Njelu Kasaka , Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka , Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Komredi Kheri James, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga  na Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew  Chenge wakiteta jambo mara baada ya zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele kumalizika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Baadhi ya Waombolezaji wakifuatilia zoezi  la kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele lililofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Baadhi ya Waombolezaji wakifuatilia zoezi  la kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele lililofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Baadhi ya Waombolezaji wakifuatilia zoezi  la kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele lililofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Baadhi ya Waombolezaji wakifuatilia zoezi  la kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele lililofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Baadhi ya Waombolezaji wakifuatilia zoezi  la kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele lililofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (wa tatu kulia) akiwaongoza wakuu wa wilaya wenzake kuweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Baadhi ya viongozi katika ibada kabla ya zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele kumalizika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge akitoa salamu za rambirambi kwa ndugu, jama na marafiki wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, kabla ya kuaza zoezi la kuaga mwili wa marehemu, lililofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Komredi Kheri James akitoa salamu za rambirambi kwa ndugu, jama na marafiki wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, kabla ya kuaza zoezi la kuaga mwili wa marehemu, lililofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Daktari wa magonjwa ya wanawake katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Herbert Kairuki akitoa salamu za rambirambi  rambirambi kwa ndugu, jama na marafiki wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, kabla ya kuaza zoezi la kuaga mwili wa marehemu, lililofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Baraka Konisaga akitoa salamu  rambirambi kwa ndugu, jama na marafiki wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, kabla ya kuaza zoezi la kuaga mwili wa marehemu, lililofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge na mkewe wakiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Bw. Masanja Kadogosa akitoa salamu za rambirambi kwa ndugu, jama na marafiki wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, kabla ya kuaza zoezi la kuaga mwili wa marehemu, lililofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,  Jenerali Venance Mabeyo, Brigedia Jenerali  Robsob Mboli Mwanjela akiwasilisha salamu za rambirambi za Jenerali  Mabeyo kwa ndugu, jama na marafiki wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, kabla ya kuaza zoezi la kuaga mwili wa marehemu, lililofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Baadhi ya Waombolezaji wakifuatilia zoezi  la kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele lililofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Naibu wa ziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo akiweka udongo  kwenye kaburi la aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akisalimiana na kumpa pole mjane wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.


0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!