Thursday, October 31, 2019

NAIBU WAZIRI IKUPA APONGEZA UBUNIFU WA KAMBI ZA KITAALUMA SIMIYU


Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, amefunga rasmi kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne Mkoani Simiyu, ambapo amewapongeza viongozi wa mkoa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka kwa ubunifu huo ambao utawasaidia wanafunzi hao kufanya vizuri katika mitihani yao.

Naibu Waziri Ikupa ameyasema hayo Oktoba 30, 2019 wakati wa kuhitimisha kambi ya kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha nne ambayo imefanyika kwa muda wa siku 60 katika Shule ya sekondari Simiyu na Chuo cha Ualimu Bariadi Mjini Bariadi, kwa lengo la kuwaandaa na mtihani wa Taifa unaotarajia kufanyika kuanzia Novemba 04, 2014.

“Nampongeza Mkuu wa Mkoa kwa ubunifu mkubwa wa kuandaa kambi hizi kwani, naamini wanafunzi mmejifunza mambo mengi  na mtafanya vizuri katika mtihani wenu, ningeshauri watu  wengine waige jambo hili, niwakumbushe wanafunzi mtakaoanza mtihani wenu Novemba 4, 2019, kumuomba Mungu ili awaongoze kipindi chote cha mitihani,” alisema Ikupa.

 Aidha, Ikupa amesema Serikali imeendelea kuboresha sekta ya elimu nchi kwa kuongeza bajeti katika shule, kujenga madarasa, na anaamini kuwa itaendelea kutatua changamoto ya walimu  katika mkoa wa Simiyu, na nchini kwa ujumla.       

Mkuu wa Mkoa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema uongozi wa Mkoa, walimu, wazazi na wadau wote wa elimu mkoani humo wamefanya uwekezaji mkubwa kwa wanafunzi wote waliokuwa katika kambi za kitaaluma na kupitia kazi nzuri iliyofanywa na walimu anaamini kwamba watafanya vizuri katika mtihani wa Taifa utakaoanza  Novemba 4, 2019. 

 Ameongeza Serikali mkoani Simiyu itaendelea kuwapa motisha walimu, wanafunzi na shule  zote zitakazofanya vizuri katika mitihani ya Kitaifa, huku akiahidi kuwalinda walimu wote, ambapo ameahidi  kuwa kuanzia Desemba Mosi, 2019 viongozi wa mkoa watawatembelea walimu katika Halmashauri zote na kuzungumza nao.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amewaomba wadau kuendelea kuunga mkono kambi hizi ili waweze kutimiza ndoto zao huku akibainisha kuwa kupitia kambi hizo watapatikana viongozi mahiri wa baadaye.

Katibu Mkuu, Chama cha Walimu Tanzania, Deus Seif amesema walimu wana imani na Serikali na wameamua kufanya kazi yao kwa bidii na wanaiomba Serikali kuendelea kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kupandishwa madaraja na mishahara kwa wakati na malipo ya fedha za likizo na malimbikizo ya mishahara.

Naye Afisa Elimu wa Mkoa, Mwl. Ernest Hinju amesema tangu kambi hizi zianze mwaka 2016 zimesaidia kuongeza kiwango cha  ufaulu katika matokeo ya darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita, ambapo kwa kidato cha nne  mwaka 2017 ufaulu ulikuwa 70.68% na mwaka 2019, ufaulu umekuwa 86.46%.                

Naye Diana Boniphace mwanafunzi kutoka Shule ya sekondari Kidinda amesema, “kupitia kambi hii wanafunzi tumejifunza mambo mengi kupitia kwa walimu mahiri na kiwango cha ufaulu kimeongezeka tofauti na tulivyoingia hivyo tunaahidi kuwa tutafanya vizuri katika mtihani wa Taifa tutakaoanza Novemba 04, 2019.”

Kambi ya Kitaaluma iliyohitimishwa Oktoba 30, 2019 ilihusisha wanafunzi 1512 ambao walikuwa na ufaulu hafifu(daraja sifuri), wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa Mkoa(Mock) na wanafunzi kutoka shule  zenye wanafunzi chini ya 30 na wamekaa kambini siku 60.
MWISHO

Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne Mkoani Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, mara baada ya kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi hao kuhitimishwa Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
\
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, akizungumza na walimu pamoja na wanafunzi wa kidato cha nne mkoani Simiyu, wakati wa kufunga  kambi ya kitaaluma ya siku 60 Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha nne kutoka shule mbalimbali mkoani Simiyu, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, wakati wa kufunga  kambi yao ya kitaaluma ya siku 60 Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Kutoka kulia Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Katibu Tawala Mkoa, Bw. Jumanne Sagini, Afisa Elimu Mkoa, Ernest Hinju na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga wakifurahia jambo, wakati wa kufunga  kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wa kidato cha nne Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne Mkoani Simiyu wakishangilia jambo wakati wa hafla ya kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wananfunzi wao ambayo imehitimishwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya wanafunzi Kidato cha nne kutoka shule mbalimbali mkoani Simiyu wakicheza na kufurahi na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka mara baada ya kufunga  kambi ya kitaaluma ya siku 60 Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi wakifuatilia kitu wakati wa kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wa kidato cha nne Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi , kutoka kulia walioketi mbele, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas, Katibu wa CWT Taifa, Mwl. Deus Seif na Mbunge la Afrika Mashariki, Mhe. Happyness Lugiko.

Baadhi ya walimu mahiri  waliofundisha kambi ya kitaaluma ya kidato cha nne wakishangilia jambo wakati wa hafla ya kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wao ambayo imehitimishwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akitoa salamu za Chama,  wakati wa hafla ya kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wao ambayo imehitimishwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Sheikh wa Mkoa wa Simiyu, Mahamoud Kalokola akitoa dua wakati wa hafla ya kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wao ambayo imehitimishwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mmoja wa wanafunzi wa kidato cha nne walio kuwa katika kambi ya kitaaluma mkoani Simiyu, ambayo imehitimishwa  Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi akitoa  ushuhuda wa namna kambi zilivyomsaidia kuongeza ufaulu wake mbele ya wanafunzi wenzake, walimu na viongozi mbalimbali.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas(kulia) na Katibu wa CWT Taifa, Mwl. Deus Seif wakiteta jambo wakati wa hafla ya kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wao ambayo imehitimishwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne mkoani Simiyu wakimvika skafu Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika ufungaji wa kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi wakicheza pamoja na waimbaji wa kwaya ya walimu Bariadi, wakati wa hafla ya kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wao ambayo imehitimishwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne Mkoani Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, mara baada ya kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi hao kuhitimishwa Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa pili kushoto) akizungumza na walimu pamoja na wanafunzi wa kidato cha nne mkoani Simiyu, wakati wa kufunga  kambi ya kitaaluma ya siku 60 Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mbunge la Afrika Mashariki, Mhe. Happyness Lugiko , akipokea cheti cha shukrani ya kuchangi kambi ya kitaaluma mkoani Simiyu, wakati wa hafla ya kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wao ambayo imehitimishwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akiteta jambo na na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, wakati wa kufunga  kambi ya kitaaluma ya siku 60 Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na walimu pamoja na wanafunzi wa kidato cha nne mkoani Simiyu, wakati wa kufunga  kambi ya kitaaluma ya siku 60 Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na walimu pamoja na wanafunzi wa kidato cha nne mkoani Simiyu, wakati wa kufunga  kambi ya kitaaluma ya siku 60 Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.

Kutoka Kushoto Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa mara baada ya kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, kabla ya hafla ya kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wa kidato cha nne ambayo imehitimishwa na Naibu Waziri huyo,  Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Katibu wa CWT Taifa, Mwl. Deus Seif akizungumza na viongozi wa Mkoa na Simiyu na viongozi wengine, mara baada ya kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, kabla ya hafla ya kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wa kidato cha nne ambayo imehitimishwa na Naibu Waziri huyo,  Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi walioshiriki katika halfa ya kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wa kidato cha nne mkoani Simiyu wakifuatilia masuala mbalimbali katika hafla hiyo iliyofanyika Oktoba 30, 2019.



Friday, October 25, 2019

WANANCHI ZAIDI YA 1000 WAPATIWA MSAADA WA KISHERIA MKOANI SIMIYU

Msajili wa Taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Felistas Mushi amesema  takribani wananchi 1018  wamepata huduma ya msaada wa kisheria katika maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria tangu Oktoba 21, 2019 mpaka Oktoba 25, 2019, yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Mushi ametoa taarifa hiyo katika Kilele cha Maadhimisho hayo, Oktoba 25, 2019 ambapo amebainisha kuwa asilimia kubwa ya matatizo ya kisheria yalihusu migogoro ya ardhi na yameshafikishwa mahakamani  na yako katika hatua mbalimbali.

Amesema huduma walizopata wananchi katika wiki ya msaada wa kisheria ni pamoja na huduma za usuluhishi, ushauri wa kisheria, kuandaa nyaraka na maelekezo ya sehemu  sahihi ya kwenda pindi wanapopata migogoro.

“Mbali na huduma kwa wananchi mafunzo yametolewa kwa makundi mbalimbali ya watumishi wa umma wapatao 1300 wakiwemo, wajumbe wa menejimenti ya sekretarieti ya mkoa, wajumbe wa kamati ya parole, wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya kata na vijiji, wajumbe wa kamati ya maadili ya mahakimu, askari polisi na magereza, wajumbe wa kamati za shule na watendaji wa vijiji na kata, “ alisema Mushi.

Kwa upande wake Hakimu Mary Nyangusi akimwakilisha Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio, ametoa wito kwa wananchi kuandika wosia ili kupunguza migogoro ya ardhi ambayo mingi inatokea mara nyingi wanaume(baba) wanapofariki na wake(mke) na watoto kudhulumiwa haki zao.

Adam Kisinza ni Mmoja wa wananchi waliofika kupata msaada wa kisheria katika maadhimisho hayo amesema, “nashukuru nimeelewesha ninachotakiwa kufanya maana kule kwetu baba mwenye mji anapokuwa amefariki wakabaki watoto na mama, wanakuwa hawana mamlaka juu ya mali iliyoachwa maana kila mtu anataka achukue chake wakati mzee hakuacha hata  wosia”.

Akifunga Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema ni vema wizara ya katiba na sheria ikaona umuhimu wa kupeleka maadhimisho ya wiki ya msaada wa huduma za kisheria katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo, ili wananchi wapate uelewa wa masuala ya kisheria na kupata matokeo yatakayoonekana.

Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Kitaifa mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu:- “Msaada wa Kisheria kwa Maendeleo Endelevu”ambapo kilele cha maadhimisho haya kimeenda sambamba na uzinduzi wa Jarida la Msaada wa Kisheria, ambalo limezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) na viongozi wengine wakionesha nakala ya Jarida la Msaada wa Kisheria lililozinduliwa katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akiteta jambo na Msajili wa Taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Felistas Mushi, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa Katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa mkoa mkoa huo(hawapo pichani), katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani), katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jarida la msaada wa kisheria katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Baadhi ya wataalam wa sheria na watoa huduma za kisheria  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani), katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja  na baadhi ya viongozi wa Mkoa huo na wataalam wa Sheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na taasisi za watoa huduma za kisheria, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktioba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati walioketi) akiwa katika picha na baadhi ya viongozi wa Mkoa huo, wataalam wa Sheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na wawakilishi wa taasisi za watoa huduma za kisheria, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkurugenzi wa Taasisi inayotoa huduma ya msaada wa kisheria ya Mama’s Hope Organisation for Legal Assistant (MHOLA),Bw. Saulo Malauri (kulia) akipokea nakala ya Jarida la Msaada wa Kisheria kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi Msajili wa Taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Felistas Mushi, nakala ya Jarida la Msaada wa Kisheria, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani), katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, nakala ya Jarida la Msaada wa Kisheria, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera, nakala ya Jarida la Msaada wa Kisheria, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkurugenzi wa Taasisi inayotoa huduma ya msaada wa kisheria ya Mama’s Hope Organisation for Legal Assistant (MHOLA),Bw. Saulo Malauri (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) na viongozi wengine wakionesha nakala ya Jarida la Msaada wa Kisheria lililozinduliwa katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akitoa salamu za wilaya ya Bariadi, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mwakilishi wa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio akitoa taarifa katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, mhe. Tano Mwera akitoa salamu, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Msajili wa Taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Felistas Mushi, akitoa taarifa ya namna wananchi wa Mkoa wa Simiyu walivyohudumiwa katika masuala ya kisheria wakati wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria,  katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa Katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Baadhi ya viongozi na watoa msaada wa huduma ya kisheria wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani), katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Baadhi ya viongozi na watoa msaada wa huduma ya kisheria wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani), katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mwanasheria kutoka Wizara ya Mambo ya ndani, akipokea cheti cha pongezi kwa kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria yaliyoadhimishwa Kitaifa Katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019 cheti hicho kimekabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika kilele cha maadhimisho hayo Oktoba 25, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa  tatu kushoto) na viongozi wengine wakishuhudia burudani kutoka kwa Eliza Band wakati wa  Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Wasanii wa Eliza Band ya mkoani Simiyu, wakitoa burudani katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) na viongozi wengine wakisikiliza jambo kwa makini wakati wa  Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Afisa Uhusiano wa Shule ya Sheria Tanzania(LST), Bi. Scholastica Njozi akipokea cheti cha pongezi kwa kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria yaliyoadhimishwa Kitaifa Katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019 cheti hicho kimekabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika kilele cha maadhimisho hayo Oktoba 25, 2019.

Tuesday, October 22, 2019

MAVUNDE AWATAKA VIONGOZI KUWATUMIA WATOA MSAADA WA KISHERIA KUTATUA MATATIZO YA WANANCHI

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde amezindua rasmi Maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria ambayo yanafanyika Kitaifa
Mkoani Simiyu na kutoa wito kwa viongozi wa Serikali kuwatumia wasajili wasaidizi na watoa huduma za kisheria kutatua matatizo ya kisheria yanayowakabili wananchi.

Akizungumza na wananchi Oktoba 21, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi  Mkoani Simyu Mavunde amesema matatizo ya kisheria yanashughulikiwa kisheria na siyo kisiasa hivyo ni vema wakawashirikisha na wakaambatana nao hata katika ziara zao ili waweze kutoa msaada wa kisheria kila unapohitajika.

“Yapo mambo mengi sana ambayo ni ya kisheria wananchi mmekuwa mkikimbilia kwa viongozi wa kisiasa, siasa ina sehemu yake inakoma inabaki sheria, wiki ya msaada wa kisheria ni fursa ya kipekee kuelewa namna ya kushughulikia matatizo yenu na mnaendelea kujifunza kuwa sheria inabaki kuwa sheria na utatuzi wake unakuwa katika mfumo uliowekwa kisheria,” alisema Mavunde.

Awali akitoa taarifa ya wiki ya msaada wa kisheria  Msajii wa Taasisi za watoa huduma za kisheria, B. Felistas Mushi amesema lengo la kuwepo wa huduma ya msaada wa kisheria ni kuhakikisha haki inapatikana kwa wananchi wasioweza kumudu gharama za wawakili”tunaamini kuwa baada ya maadhimisho haya kutakuwa na mtazamo chanya katika kutatua matatizo ya wananchi kisheria.”

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka ametoa wito kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu wahakikishe katika ziara zao wanaambatana na wasajili wasaidizi na watoa huduma za kisheria walio katika maeneo yao ili waweze kutatua na kutoa ushauri wa namna ya kutatua matatizo yote kisheria.

Aidha, amewataka viongozi na wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya vijiji, kata na wilaya kuhakikisha kuwa wanatumia vizuri mafunzo wanayopewa na wakayatafsiri kwa vitendo katika utatuzi wa matatizo ya watu kwa haki na kushirikiana na viongozi wa Serikali, taasisi na vyombo vyote vya maamuzi.

Katika hatua nyingine Mtaka ameshauri kuwa ingekuwa vema pia kama masuala ya kisheria yakajumuishwa katika baadhi ya masomo kama vile somo la Uraia ili kuendelea kujenga uelewa wa pamoja juu ya namna ya kukabiliana na matatizo yote ya kisheria.

Kwa upande wake Mkuugenzi Mtendaji wa TANLAP, Bi. Christina Ruhinda ameiomba Serikali na taasisi zake kushirikiana na watoa huduma za kisheria ili huduma hizo ziwe endelevu na matatizo ya wananchi yaweze kufanyiwa kazi kwa haki.

Mkurugenzi wa Miradi Shirika la Legal Services Facility, Bi. Scholastica Jullu amesema shirika ilo litaendelea kufadhili mashirika yanayotoa msaada wa kisheria kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa kisheria mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu “Msaada wa Kisheria kwa Maendeleo Endelevu”, wakati yakiadhimishwa kitaifa mkoani SIMIYU yanapotarajiwa kuhitimishwa Oktoba 25, 2019 pia yanaadhimishwa katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Geita, Iringa, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro,Mbeya, Mtwara, Mwanza, Njombe, Ruvuma, Shinyanga, Tabora na Tanga.
MWISHO
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde (wa pili kulia) akimsikiliza mmoja wa wananchi wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu aliyefika katika banda  la Wizara ya Mambo ya Ndani kupata msaada wa kisheria, katika uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya Msaada wa kisheria Oktoba 21, 2019 yanayofanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde (aliyesimama) akishuhudia wanasheria kutoka Kituo cha Haki za Binadamu wakitoa huduma ya msaada wa kisheria  kwa mmoja wa wananchi wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, katika uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya Msaada wa kisheria Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akimuongoza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde na viongozi wengine kutembelea mabanda ya watoa huduma ya msaada wa kisheria, katika uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya Msaada wa kisheria Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.



Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde (kulia) akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, katika uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria uliofanyika  Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
Mtaalam kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS), akitoa  maelezo kwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde ( wa pili kulia) alipotembelea banda la Taasisi hiyo, katika uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria uliofanyika  Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
Msajili wa Taasisi za Watoa huduma ya msaada wa kisheria nchini, Bi. Felistas Mushi akiwasilisha taarifa ya maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria, katika uzinduzi wa maadhimisho hayo  Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
 Baadhi ya wananchi , Wenyeviti na Wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya Vijiji na kata mkoani Simiyu, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde (hayupo pichani ), katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019. 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde , akizungumza na baadhi ya wananchi , Wenyeviti na Wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya Vijiji na kata mkoani Simiyu,katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria  Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa kwanza mbele), Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde(mwenye suti mbele)  na viongozi wengine wakifurahia jambo mara  baada ya kutembelea mabanda ya watoa huduma ya msaada wa kisheria, katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
 Baadhi ya viongozi na watoa huduma ya msaada wa kisheria, wakifuatilia jambo katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019. 

 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde (katikati walioketi),  akiwa katika picha ya pamoja baadhi ya viongozi  wa Mkoa na watoa huduma ya msaada wa kisheria mara baada ya uzinduzi wa Maonesho ya Wiki ya Msaada wa kisheria, Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.


Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Lilian Kilembe akitoa maelezo mbele ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, alipotembelea banda la wizara katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria   Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.



Baadhi ya wananchi wakipata huduma ya msaada wa kisheria katika mabanda mbalimbali ya watoa huduma hiyo, katika Maadhimisho ya wiki ya Msaada wa kisheria, maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.

Mtaalam kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS), akitoa taarifa ya chama hicho katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria   Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.

 Mkurugenzi Mtendaji wa TANLAP, Bi. Christina Kamili Ruhimba akitoa taarifa ya taasisi hiyo katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria   Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
 Mshauri wa Masuala ya Kijinsia Bungeni, Bi Stella Manda kutoka UN WOMEN akiwasilisha taarifa ya Shirika hilo kwa niaba ya Mkurugenzi, katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria   Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019. 


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde (katikati walioketi),  akiwa katika picha ya pamoja baadhi ya viongozi  wa Mkoa na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na usalama Mkoa wa Simiyu, mara baada ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa kisheria, Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
Baadhi ya viongozi na watoa huduma ya msaada wa kisheria, wakifuatilia jambo katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
Baadhi ya viongozi na watoa huduma ya msaada wa kisheria, wakifuatilia jambo katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto) akimuongoza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde na viongozi wengine kutembelea mabanda ya watoa huduma ya msaada wa kisheria, katika uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya Msaada wa kisheria Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!