Thursday, October 17, 2019

MIFUKO YA UWEZESHAJI KIUCHUMI YATAKIWA KUWAWEZESHA WANANCHI MITAJI WAANZISHE VIWANDA


Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga ametoa wito kwa Mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kuangalia jinsi ya kuwezesha wananchi wengi zaidi kupata mitaji ya kuanzisha viwanda, ili uchumi wa nchi ukue na kupunguza changamoto zinazokabili jamii.

Kiswaga ameyasema wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika uzinduzi wa Maonesho ya tatu ya  mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

“Sote tunafahamu kwamba Tanzania inalenga kufikia uchumi wa katika ifikapo mwaka 2025 na viwanda ni nyenzo itakayowezesha nchi kufika huko; viwanda vina mchango mkubwa sana katika kukuza uchumi wa nchi  kwa kuwa vinanufaisha jamii kwa kutoa ajira, kulipa kodi, kununua malighafi kutoka kwa wakulima na mengine mengi,” alisema Kiswaga.

Aidha, Kiswaga alitoa wito kwa wananchi wa mikoa ya kanda ya ziwa na maeneo mbalimbali nchini kufika katika maonesho haya kupata maelezo kutoka kwa wawakilishi wa mifuko /programu za uwezeshaji za Serikali, kuonesha bidhaa, kunua bidhaa za wajasiriamali na kupata uelewa wa masuala ya uwezeshaji wananchi.

Naye Afisa Maendeleo ya Biashara wa Taasisi ya kusaidia sekta binafsi na Kilimo,  (PASS) Kanda ya Ziwa, Faustine Mungo amesema wameandaa mpango mkakati wa miaka mitano ambapo wanatarajia kutoa ajira 700,000 ambao unatarajia kuzifikia familia zaidi ya 200,000.

Kaimu Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji, Bi.Esther Mmbaga kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC), amesema malengo ya maonesho haya ni pamoja na kukuza uelewa wa wananchi  kuhusu uwepo, majukumu na vigezo katika kutoa huduma za mikopo na programu za uwezeshaji.

Bi. Mmbaga ameongeza kuwa malengo mengine ni kuhamasisha wananchi ili waweze kunufaika na fursa zilizopo katika mifuko na programu za uwezeshaji na kuhamasisha wananchi kujenga utamaduni wa kuweka akiba na kuwekeza katika miradi yenye tija.

Maonesho ya tatu ya  mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, yenye Kauli Mbiu “Mitaji ni Chachu ya Kujenga Uchumi wa Viwanda”ambayo yanaendelea katika uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi yanatarajiwa kufungwa rasmi Oktoba 20, 2019.
MWISHO
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka),  akizungumza na wananchi katika ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Baadhi ya wananchi wa Bariadi mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka),  katika ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.


 Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akimsikiliza Afisa kutoka Mamlaka ya Masoko ya  Mitaji na Dhamana, katika ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka),  akizungumza na wananchi katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi  na Watumishi wa BarazalaTaifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi   katika Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akimsikiliza mmoja wa wanufaika wa mikopo kutoka SIDO katika ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Afisa Uhusiano Mkuu wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC), Bw. Edward Kessy (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga wakati alipotembelea mabanda ya maonesho wakati ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.



Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga(mwenye suti nyeusi) akiangalia bidhaa za wajasiriamli kutoka mikoa ya Tabora na Dodoma wakati alipotembelea mabanda ya maonesho wakati ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Afisa Biashara wa Taasisi ya Private Agricultural Sector Support (PASS) Kanda ya Ziwa, Faustine Mungo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga alipotembelea mabanda ya maonesho wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Mahaza Gamitwe (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

Kaimu Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji , B. Esther Mmbaga kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC), akiwasilisha taarifa wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na watendaji kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC), wakifuatalia masuala mbalimbali wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga(mwenye suti nyeusi) akiangalia kukuwanaofugwa na  wajasiriamali wakati alipotembelea mabanda ya maonesho wakati ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akimsikiliza Afisa kutoka UTT, alipotembelea mabanda ya maonesho katika ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akimsikiliza Afisa kutoka mfuko wa kuhifadhi wanyamapori , alipotembelea mabanda ya maonesho katika ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Kikundi cha Ucheshi Cha mjini Bariadi kikiwaburudisha wananchi katika ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

Kikundi cha Ngoma BASEKI kutoka  mjini Bariadi kikiwaburudisha wananchi katika ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!