Tuesday, October 15, 2019

MAONESHO YA MIFUKO YA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI KUFUNGULIWA RASMI KESHO OKTOBA 16 SIMIYU

Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii  yanatarajiwa kufunguliwa rasmi kesho  Oktoba 16, 2019 na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka Mjini Bariadi Mkoani hapa, ambapo washiriki kutoka taasisi za Umma na binafsi zaidi ya 100, mifuko ya uwezeshaji zaidi ya 40 na vikundi vya kijamii (VICOBA) wanatarajiwa kushiriki.

Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 15, 2019 Mjini Bariadi Afisa Uhusiano Mkuu wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC), Bw. Edward Kessy  ambao ndiyo waandaaji amesema maonesho haya ni fursa kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa kujifunza huduma za mifuko ya uwezeshaji, taasisi za fedha na programu mbalimbali.

“Maonesho haya yameanza Oktoba 14, 2019 na yatafunguliwa rasmi Oktoba 16, 2019 na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na yatahitimishwa tarehe 20 Oktoba, 2019 na Mhe. Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, nitoe wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili waje wajionee huduma mbalimbali za mifuko, taasisi na vikundi vya kijamii,” alisema Kessy.

Afisa Biashara wa Taasisi ya Private Agricultural Sector Support (PASS) Kanda ya Ziwa, Faustine Mungo ametoa wito kwa wananchi kutembelea banda lao kujua huduma zao, huku akibainisha kuwa Taasisi hiyo kupitia mpango mkakati wa miaka mitano ulioanza mwaka 2018 inatarajia kuzifikia familia 235,000 kwa kudhamini mikopo kiasi cha shilingi bilioni 210.6 .

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya Posta Tanzania tawi la Bariadi, Bw. Shadrack Daudi amesema benki hiyo kwa kushirikiana na NEEC na PASS imetoa mikopo ya vikundi mbalimbali vya kijamii, vikundi rasmi na visivyo rasmi, wafanyabiashara, hivyo ni vema wananchi wafike kwa wingi kujionea fursa hizo ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Naye mnufaika wa mikopo ya mifuko ya uwezeshaji, Bw. Emmanuel Nyambi Katibu wa Chama cha Ushirika cha Msingi kutoka Kahama, ametoa wito kwa wananchi kufika katika maonesho hayo ili waweze kuona fursa za upatikanaji wa mikopo kupitia mifuko, programu na taasisi mbalimbali za kifedha huku akieleza kuwa hakuna urasimu katika utoaji wa mikopo.

“Natoa wito kwa wajasiriamali wadogo au vyama mbalimbali, wafike kwenye maonesho haya waje wajifunze namna ya kupata mikopo ya kuendeshea shughuli za kiuchumi, niwahakikishie hakuna urasimu kwenye mikopo, tunaipata kwa wakati na Benki Kuu inadhamini kikubwa ni kuwa waaminifu kurejesha mikopo,” alisema Nyambi.

Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii  mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu: “Mitaji ni Chachu ya Kujenga Tanzania ya Viwanda”.
Afisa Biashara wa Taasisi ya Private Agricultural Sector Support (PASS) Kanda ya Ziwa, Faustine Mungo (wa tatu kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) uliofanywa kwa lengo la kutoa taarifa rasmi ya maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii  yanayoendelea ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Afisa Uhusiano wa wa Baraza laTaifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC), Bw. Edward Kessy (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) uliofanyika leo Oktoba 15, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kutoa taarifa rasmi ya katika maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii  yanayoendelea ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Bariadi, Bw. Shadrack Daudi (wa pili kushoto) akizungumza akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) uliofanyika leo Oktoba 15, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kutoa taarifa rasmi ya maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii  yanayoendelea ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Afisa kutoka Benki ya Tanzania (BOT), Bi. Edista Njau (kushoto) akizungumza akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) uliofanyika leo Oktoba 15, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kutoa taarifa rasmi ya maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii  yanayoendelea ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wanufaika wa mikopo ya mitaji kutoka katika mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi wakitoa ushuhuda kwa waandishi wa habari namna mifuko hiyo ilivyowasaidia kupata mitaji, wanufaika hao wamehojiwa katika banda la Benki Kuu ya Tanzania, katika maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii  yanayoendelea ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu wakitembelea baadhi ya mabanda katika maonesho ya tatu ya mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayoendelea katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wataalamu kutoka Mfuko wa Misitu nchini (TFS) wakiendelea na maandalizi ya banda lao kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii  yanayoendelea katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

Baadhi ya wajasiriamali wakionesha bidhaa zao katika maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii  yanayoendelea katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya zana za kilimo zinazopatikana katika maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii  yanayoendelea katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya waoneshaji wakiwa katika maandalizi ya mabanda yao kwa ajili ya maandalizi rasmi ya ufunguzi wa maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii  yanayoendelea katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!