Saturday, November 28, 2020

WANANCHI SIMIYU WATAKIWA KUSHIRIKI MICHEZO KUIMARISHA AFYA

 

Mkuu wa Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, Mhe. Benson Kilangi ametoa wito kwa wananchi na viongozi mkoani hapa kuona umuhimu wa kushiriki michezo kwa ajili ya kuimarisha afya. 

Kilangi ameyasema hayo Novemba 28, 2020 katika Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, likihusisha mashindano ya baiskeli, mbio fupi , ngoma za asili na mashindano ya taaluma kwa wanafunzi wa shule za sekondari; alipokuwa akitoa salamu za Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka. 

"Hii michezo tunayoifanya pamoja na kwamba ni burudani tunapaswa kuelewa kwamba michezo ni afya; ni wajibu wetu kila mmoja kwa nafasi yake ahakikishe anashiriki michezo, siyo lazima iwe kama hii tu, hata nyumbani tunaweza kufanya mazoezi madogo madogo kama kukimbia, kuruka kamba na mengine kwa afya," alisema Kilangi. 

Aidha, Kilangi aliongeza kuwa michezo ni ajira kwakuwa wapo watu wanajipatia vipato kupitia michezo na vile vile michezo ni biashara na inasaidia  kujenga mahusiano na undugu katika jamii. 

Akizungumzia Kauli Mbiu ya Tamasha la Simiyu Jambo Festival mwaka 2020 inayosema, “WAWEZESHE WANAWAKE NA WATOTO WA KIKE ILI KUWA NA DUNIA BORA” Kilangi amesema ni vema watoto wa kike na wanawake wakawezeshwa kwa kuwa ni wakombozi wa familia na ndiyo wanaorudisha maendeleo nyumbani kwa asilimia kubwa ikilinganishwa na wanaume.

 

Katika hatua nyingine Kilangi ametoa rai kwa wadau wakashirikiana na mkoa wa Simiyu kuona namna ya kuwa na matamasha yanayohusu michezo, sanaa na utamaduni kuanzia ngazi ya wilaya, ili kuendelea kuujenga Mkoa wa Simiyu katika nyanja mbalimbali.

 

Katibu Tawala wa  Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga amesema  kwa sasa Tamasha hilo limekuwa likishirikisha washiriki kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini, huku akibainisha kuwa nia ya Mkoa ni kupata washiriki wa ndani na nje ya nchi ili litumike pia katika kutangaza na kukuza fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo Simiyu. 

Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani ( UNFPA) ambao ndiyo wadhamini wakuu, Dkt. Amir Batenga amesema  Shirika hilo litaendelea kushirikiana na mkoa wa Simiyu katika masuala mbalimbali ya kuwawezesha watoto wa kike na wanawake katika nyanja mbalimbali kama kauli mbiu ya tamasha la Simiyu Jambo Festival mwaka 2020 inavyosema. 

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum (Vijana), Mhe. Lucy Sabo ameupongeza uongozi wa Mkoa kwa maandalizi mazuri na kutoa rai kuwa Tamasha la Simiyu Jambo Festival liwe endelevu kwa ajili ya kuinua vipaji kwa vijana na kuwahamasisha kushiriki katika utamaduni, sanaa na michezo. 

Baadhi ya washiriki wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival ambalo linafanyika kwa mara ya tatu mkoani Simiyu, wamewashukuru waandaji kwa maandalizi mazuri na ambapo wamebainisha kuwa mwaka huu ulinzi umeimarishwa zaidi. 

"Tunawapongeza waandaaji mwaka huu mashindano ni mazuri, Ulinzi umeimarika sana kuanzia tulipoanza, njiani kote mpaka tulipofika eneo la kumalizia,  kwa hali ilivyokuwa hakuna  ambaye angeweza kubebwa kwa namna yoyote ile ili kutafutiwa ushindi," alisema Paul Michael mshindi wa kwanza mbio za baiskeli wanaume kilomita 140. 

Katika mashindano ya baiskeli washiriki kutoka mikoa ya Mwanza na Shinyanga wameonekana kung'ara zaidi ambapo Paul Michael  kutoka Shinyanga ameibuka mshindi na kujinyakulia kitita cha shilingi 800,000/= na  Laurencia Luzuba ameongoza upande wa wanawake na kujinyakulia shilingi 600,000/= , upande wa walemavu Emmanuel John kutoka Simiyu ameibuka kidedea na kujipatia kitita cha shilingi 200,000/=

MWISHO.

Baadhi ya waendesha baiskeli wanawake wakiondoka eneo la  kuanzia mashindano ya baiskeli kilomita 80 Salunda Mjini Bariadi, Mashindano yaliyofanyika wakati wa tamasha la Simiyu Jambo Festival liliofanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Paul Michael kutoka mkoani Shinyanga akishengilia baada ya kuibuka mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kilomita 140 wanaume katika Tmasha la Simiyu Jambo Festival liliofanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akimkabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi 600,000/= mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kilomita 80 wanawake, Bi. Laurencia Luzuba kutoka mkoani Mwanza , katika Tamasha la Simiyu Jambo Festival liliofanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washindi nane wa kwanza katika mashindano ya mbio za baiskeli kilomita 80 wanawake, wakati wa  Tamasha la Simiyu Jambo Festival liliofanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.


Baadhi ya viongozi, watumishi na wananchi wa mkoa wa Simiyu wakikimbia mbio fupi za kilomita tano katika ufunguzi wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival liliofanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani (UNFPA) Dkt. Amir Batenga  akimkabidhi Emmanuel John  zawadi ya fedha taslimu shilingi 200,000/= baada ya kuibuka  mshindi wa kwanza katika mbio za baiskeli kilomita tano (kwa watu wenye ulemavu), wakati wa  Tamasha la Simiyu Jambo Festival liliofanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi (katikati walioketi) ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo(kushoto), Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga na washindi nane wa mbio za baiskeli kilometa 140 wanaume, wakati wa  Tamasha la Simiyu Jambo Festival liliofanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Kwiyeya Buluba mwanafunzi wa Kidato cha kwanza kutoka shule ya sekondari Simiyu, akipokea zawadi ya fedha taslimu kutoka kwa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi (aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ), mara baada ya kuibuka mshindi wa tatu katika uandishi wa isha, wakati wa  Tamasha la Simiyu Jambo Festival liliofanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Ngoma za asili kutoka kundi la Wagalu wakitoa burudani wakati wa  Tamasha la Simiyu Jambo Festival liliofanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Baadhi ya viongozi na watumishi wa mkoa wa Simiyu wakiburudika na ngoma za asili zilizokuwa zikitoa burudani wakati wa  Tamasha la Simiyu Jambo Festival liliofanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Baadhi ya washiriki wa mashindano ya mbio fupi kilomita 10 wanawake wakiondoka eneo la  kuanzia mashindano  hayo Salunda Mjini Bariadi, ambayo yamefanyika wakati wa tamasha la Simiyu Jambo Festival liliofanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP. Richard Abwao akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa mbio fupi kilometa 10 wavulana, wakati wa tamasha la Simiyu Jambo Festival liliofanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.


Baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja na washindi watano wa mashindano ya baiskeli kilometa tano walemavu, wakati wa tamasha la Simiyu Jambo Festival liliofanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mbunge wa Viti maalum Vijana, Mhe. Lucy Sabo akizungumza na wananchi wa mkoa wa Simiyu, wakati wa tamasha la Simiyu Jambo Festival liliofanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

TAZAMA PICHA MBALIMBALI ZA TUKIO LA SIMIYU JAMBO FESTIVAL

















 

Thursday, November 26, 2020

ZAIDI YA WATU 300 KUSHIRIKI MASHINDANO YA BAISKELI, MBIO FUPI NA NGOMA ZA ASILI SIMIYU

 

Zaidi ya wanamichezo 300 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wanatarajia kushiriki Tamasha la Simiyu Jambo Festival ambalo litahusisha mashindano ya mbio za baiskeli, ngoma za asili(wagika na wagalu), mbio fupi (kilometa kumi) pamoja na mashindano ya kitaaluma kwa wanafunzi wa shule za sekondari. 

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival Bi. Zena Mchujuko wakati akizungumza na waandishi wa habari Mjini Bariadi  leo Novemba 26, 2020 juu ya tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi. 

“Zawadi zitatolewa kwa mshindi wa kwanza mpaka wa kumi wanawake na wanaume (mbio za baiskeli), walemavu zitatolewa kwa mshindi wa kwanza mpaka wa tano; mbio fupi tutatoa kwa mshindi wa kwanza mpaka wa tatu,” alisema Bibi. Mchujuko.

Afisa Miradi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani (UNFPA) ambalo ndiyo mdhamini Mkuu wa Simiyu Jambo Festival,  Bw. Dennis Swai amesema shirika hilo limeamua kudhamini tamasha hilo kwa kuwa ni fursa mojawapo ya kuiweza jamii kutambua haki za watoto wa kike na wanawake katika kufikia malengo yao,  huku akiahidi kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali kama wadau wa maendeleo.

Kaimu Katibu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Simiyu, Bw. Mbezi Ally amesema chama hicho kimeandaa washiriki ambao ni wazuri katika mbio,  ambapo amebainisha kuwa baadhi yao wameshiriki mbio ndefu (kilomita 21 na Kilomita 42) ikiwemo Serengeti Safari Marathon na kutoa wito kwa washiriki kutoka maeneo yote ndani na nje ya mkoa kushiriki mashindano haya.

Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Mbio za Baiskeli Mkoa wa Simiyu, Bw. Buyaga George amesema pamoja na washiriki kutoka mkoa wa Simiyu, washiriki kutoka mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Tabora na Arusha wamethibitisha kushiriki mashindano ya mbio za baiskeli kwa wanaume (Kilomita 140) ,wanawake (kilomita 80) na walemavu (kilomita tano).

Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga amesema mkoa wa Simiyu ni maarufu kwa kutumia baiskeli kama nyenzo ya usafiri hivyo mkoa umeona haja ya kuwaendeleza wana Simiyu kwa utamaduni wao wa kutumia baiskeli ili waitumie fursa hiyo kuingia katika mashindano yanayoweza kuwafanya wawe waendeshaji bora wa baiskeli.

Aidha, Mmbaga ametoa wito kwa wadau na wafanyabiashara mkoani hapa kushiriki katika tamasha hili kwa namna mbalimbali ikiwa ni pamoja na kulitumia kutangaza huduma na bidhaa zinazopatikana Simiyu.

Tamasha hili la Simiyu Festival linafanyika kwa mara ya tatu sasa likiwa na Kauli Mbiu, “WAWEZESHE WANAWAKE NA WATOTO WA KIKE ILI KUWA NA DUNIA BORA” chini ya udhamini wa UNFPA, Jambo Food Products, Alliance Ginnery Ltd, Busega Mazao na SweetDreams Hotel,  Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

MWISHO

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga( wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi  leo Novemba 26, 2020 juu ya Tamasha la Simiyu Jambo Festival linalotarajiwa kufanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mratibu wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival , Bibi Zena Mchujuko (wa tatu kushoto) akitoa taarifa ya hali ya maandalizi ya tamasha hilo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi  leo Novemba 26, 2020  linalotarajiwa kufanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Afisa Miradi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani (UNFPA) mkoa wa Simiyu ambalo ndiyo mdhamini Mkuu wa Simiyu Jambo Festival,   Bw. Dennis Swai (wa pili kulia) akizungumza kwenye Mkutano na  waandishi wa habari katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi  leo Novemba 26, 2020 juu ya Tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Mbio za Baiskeli Mkoa wa Simiyu, Bw. Buyaga George(wa pili kushoto)  akizungumza kwenye Mkutano na  waandishi wa habari katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi  leo Novemba 26, 2020 juu ya mashindano ya mbio za baiskeli katika Tamasha la Simiyu Jambo Festival linalotarajiwa kufanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mratibu wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival , Bibi Zena Mchujuko (wa pili kushoto) akitoa taarifa ya hali ya maandalizi ya tamasha hilo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi  leo Novemba 26, 2020  linalotarajiwa kufanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Kaimu Katibu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Simiyu, Bw. Mbezi Ally (wa pili kushoto) akizungumza kwenye Mkutano na  waandishi wa habari(hawapo pichani)  katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi  leo Novemba 26, 2020 juu ya mashindano ya mbio fupi katika Tamasha la Simiyu Jambo Festival linalotarajiwa kufanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Bango lenye taarifa muhimu za Tamasha la Simiyu Jambo Festival

 

Wednesday, November 25, 2020

VIJANA 664 MKOANI SIMIYU KUNUFAIKA NA AJIRA ZA MUDA MSIMU MPYA WA KILIMO

Takribani vijana 664 mkoani Simiyu wanatarajia kunufaika  na ajira za muda katika msimu huu  ,baada ya  kupata mafunzo ya  matumizi sahihi  ya viuatilifu kwa ajili ya kukabiliana na wadudu wasumbufu wa zao la Pamba.

 

Hayo yamebainishwa jana Novemba 24, 2020 wakati wa kufunga mafunzo ya matumizi sahihi ya viuatilifu kwa wapuliziaji sumu katika zao la pamba yaliyotolewa na Gatsby Africa kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti na Udhibiti wa Viuatilifu (TPRI) katika Halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu ambayo yalihitimishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga.

 

Vijana hao wamebainisha mafunzo waliyoyapata pamoja na kuwasaidia kupata ajira yatawawezesha kuongeza tija katika uzalishaji wa pamba kwa kuwa wamefahamu matumizi sahihi ya viuatilifu ilinganishwa na awali walipokuwa wakifanya kazi hiyo kienyeji.

 

“Tulikuwa tunafanya kienyeji lakini kwa sasa tumepata ujuzi mfano tumejifunza ni dawa ipi inatumika kuua aina gani ya wadudu kwa wakati gani; lakini pia tumejifunza ni kwa namna gani tunaweza kutumia viuatilifu pasipo kuathiri mazingira yetu,” alisema Samwel Salum mpuliziaji viuatilifu vya zao la pamba Meatu.

 

“Mafunzo haya kwangu yana umuhimu mkubwa sana maana nitakuwa nikipulizia viuatilifu kwenye mashamba ya wakulima napata hela, lakini pia nitatumia mbinu nilizojifunza kupulizia kwenye mashamba yangu na nitaongeza uzalishaji,” alisema Mayunga Mlyaza mpuliziaji viuatilifu vya zao la pamba Meatu.

 

Afisa Kilimo wa Kata ya Sakasaka Wilayani Meatu, Sylvester Mholi amesema mafunzo hayo yamewaongezea uwezo wa kujiamini katika kutambua viuatilifu ambavyo vinasambazwa na wasambazaji kwa kuzingatia sheria na miongozo mbalimbali inayohitajika.

 

Mwakilishi wa Gatsby Africa shirika lililoshirikiana na Mkoa kuandaa mkakati wa mapinduzi kilimo cha pamba (2019-2024) katika mafunzo hayo Bw.Michael  Kahindi amesema wakulima waliofikiwa na wapuliziaji hawa wa viuatilifu katika msimu uliopita wamefanikiwa kuongeza tija katika Uzalishaji wa pamba kutoka kilo 250 mpaka kufikia kilo 600 kwa hekali.

 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga amesisitiza uadilifu wakati wa utekelezaji zoezi la upuliziaji dawa katika  mashamba ya  wakulima “tusifanye udanganyifu kwa wakulima, ukimdanganya mteja wako kesho hatarudi tena kwako; sisi kama mkoa tunaona fahari kuwa tunao vijana 664 ambao tumewaongezea thamani kwenye kazi walizonazo.”

 

Mtafiti wa kudhibiti visumbufu vya mazao/mimea kutoka Taasisi ya Utafiti wa viuatilifu nchini(TPRI), Bw. Ramadhan Kilewa amesema matarajio ya TPRI ni kuwa vijana hao wataenda kufanya kazi nzuri baada ya mafunzo hayo kwa kuwa awali baadhi yao walieleza kuwa walikuwa wakifanya kazi hiyo tofauti na maelekezo ya matumizi sahihi ya viuatilifu.

 

Kwa uapnde wake kaimu Katibu Tawala Msaidizi-Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji, Bibi. Kija Kayenze amesema “Lengo ni kuongeza tija hivyo tunatarajia tija itaongezeka sana kwa sababu wakulima wengi watakauwa wameshapata elimu sahihi ya matumizi ya viuatilifu

MWISHO

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akizungumza na baadhi ya vijana wanaotarajiwa kupata ajira za muda za  upuliziaji wa viuatilifu katika zao la pamba wakati akifunga mafunzo hayo Novemba 24, 2020 Mjini Mwanhuzi wilayani Meatu.
Baadhi ya vijana waliopewa mafunzo ya upuliziaji wa viuatilifu katika zao la pamba wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga wakati  akifunga mafunzo hayo Novemba 24, 2020 Mjini Mwanhuzi wilayani Meatu
.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Meatu, Bw. Albert Rutaihwa akizungumza na baadhi ya vijana wanaotarajiwa kupata ajira za muda upuliziaji wa viuatilifu katika zao la pamba wakati Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akifunga mafunzo hayo Novemba 24, 2020 Mjini Mwanhuzi wilayani Meatu.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga(wa tatu kulia walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wanaotarajiwa kupata ajira za muda  za upuliziaji wa viuatilifu katika zao la pamba mara baada ya kufunga mafunzo hayo Novemba 24, 2020 Mjini Mwanhuzi wilayani Meatu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga(wa tatu kulia walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wanaotarajiwa kupata ajira za muda  za upuliziaji wa viuatilifu katika zao la pamba mara baada ya kufunga mafunzo hayo Novemba 24, 2020 Mjini Mwanhuzi wilayani Meatu.

Baadhi ya vijana waliopewa mafunzo ya upuliziaji wa viuatilifu katika zao la pamba wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga wakati  akifunga mafunzo hayo Novemba 24, 2020 Mjini Mwanhuzi wilayani Meatu.

Baadhi ya vijana waliopewa mafunzo ya upuliziaji wa viuatilifu katika zao la pamba wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga wakati  akifunga mafunzo hayo Novemba 24, 2020 Mjini Mwanhuzi wilayani Meatu.




Tuesday, November 24, 2020

SERIKALI YAWAHAKIKISHIA WACHIMBAJI WADOGO WA DHAHABU BARIADI KUPEWA LESENI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila amewahakikishia wachimbaji wadogo katika mgodi wa dhahabu wa Bulumbaka uliopo katika kijijj cha Gasuma wilayani Bariadi mkoani hapa kuwa watapata leseni za uchimbaji na kusisitiza kuwa kamwe hawataondolewa katika mgodi huo. 


Prof. Msanjila ameyasema hayo jana Novemba 23, 2020 wakati akizungumza katika kikao chake na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi na baadhi ya wachimbaji wadogo, katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi. 


"Muombe leseni mtapewa, leseni haiwezi kutolewa kwa mtu kutoka huko aliko halafu hawa vijana ambao wanachimba sasa hivi wakaondolewa hapana; najua kuna maombi nayaonaona kwenye mitandao lakini msiwe na wasiwasi hayawezi kutoka," alisema Prof. Msanjila. 


Aidha, Prof. Msanjila ameeleza utaratibu wa fidia kwa wenye mashamba "tusiichukulie kwamba kwa kuwa na shamba unakuwa na haki ya kuchimba, hapana; ila ni kwamba wale wanaochimba hawana fedha ya kukufidia, sasa  tumeweka utaratibu kwamba fidia yako uipate taratibu kwenye mgao na naamini huwa ni nyingi kuliko fidia nyingine.”

 

Katika hatua nyingine Prof. Msanjila amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga kuanzisha upya mchakato wa kumpata msimamizi wa mgodi wa Bulambaka ambaye atahakikisha ulinzi unaimarishwa, mazingira yanaboreshwa ikiwa ni pamoja na uchimbaji wa vyoo pamoja na kuimarisha uhusiano mzuri miongoni mwa wachimbaji.


Awali baadhi ya wachimbaji wadogo na wamiliki wa mashamba walisilisha changamoto mbalimbali zinazowakabili katika mgodi huo ikiwa ni pamoja na kuomba uboreshaji wa miundombinu na upatikanaji wa huduma muhimu, ambapo Msanjila amebainisha kwamba Serikali inazifanyia kazi na baadhi zitatatuliwa na msimamizi wa mgodi huo baada ya kukamilika kwa mchakato wa kumpata ambao utaanzishwa Mkuu wa Wilaya. 


“Wachimbaji tumewekeza gharama kubwa sana, tunaomba serikali isaidie kuimarisha ulinzi na usimamizi wa mali tunazochimba na kuendelea kuboresha miundombinu ili tuweze kusafirisha mali tunazochimba hapa kwa urahisi,” alisema mchimbaji mdogo Wibelo Kihalata. 


“Wenye Maeneo tuliomba leseni ili na sisi tuweze kufanya kazi na Watanzania wenzetu, tunashukuru kwa kuwa mmetueleza kuwa hata sisi tukijiunga tunaweza kupata leseni tukachimba na siyo wenye hela peke yao tu,” alisema Masuke Sahani Mwenyekiti wa Kikundi cha Umoja Bulumbaka Bariadi. 


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema  atahakikisha mchakato wa kumpata msimamizi wa mgodi linafanyika kwa uwazi na kusimamia uendeshaji wa mgodi huo kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo  kutoka wizara ya Madini.

 

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga amesema Serikali ya mkoa wakati wowote itahakikisha inasimamia Serikali ya wilaya katika kuhakikisha shughuli zote zinazofanyika zinafuata sheria, kanuni na taratibu.

MWISHO 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila akizungumza baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka  Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.
Baadhi ya wananchi wakimsikilza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila katika kikao chake na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka  Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.
Mkuu wa Wilay ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza katika kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka  Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akizungumza katika kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka  Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akizungumza katika kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka  Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.
Bw. Samwel Chegeni mmoja wa wamili wa mashamba akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Dkt. Simon Msanjila na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka  Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.

 

Mchimbaji mdogo, Bw. Wibelo Kihalata akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Dkt. Simon Msanjila na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka  Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.

Baadhi ya wananchi wakimsikilza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila katika kikao chake na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka  Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.

Afisa Madini Mkazi wa mkoa wa Simiyu, akiwasilisha taarifa katika kikao cha ndani cha   Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, kwa lengo la kujadili uendeshaji wa machimbo madogo ya  Bulumbaka  Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.

 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akiagana na baadhi ya wananchi baada ya kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Dkt. Simon Msanjila na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka  Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi

Baadhi ya wananchi wakimsikilza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila katika kikao chake na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka  Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.

Afisa Madini Mkazi wa mkoa wa Simiyu, akiwasilisha taarifa katika kikao cha ndani cha   Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, kwa lengo la kujadili uendeshaji wa machimbo madogo ya  Bulumbaka  Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akiagana na baadhi ya wananchi baada ya kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Dkt. Simon Msanjila na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka  Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.

Baadhi ya wananchi wakimsikilza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila katika kikao chake na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka  Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.

Baadhi ya viongozi wakifuatilia kikao  cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Dkt. Simon Msanjila na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka  Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila akizungumza na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu katika kikao cha ndani kwa lengo la kujadili uendeshaji wa machimbo madogo ya  Bulumbaka  Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!