Thursday, December 29, 2016

MKUU WA MKOA WA SIMIYU ATOA TAMKO LA MKOA KUHUSU ELIMU MWAKA 2017



Na Stella Kalinga
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka ametoa tamko la Mapinduzi ya Elimu na mwelekeo wa Elimu mwaka 2017 kama kipaumbele cha kwanza kwa mkoa huo.

 Mkuu huyo wa Mkoa ametoa tamko hilo katika kikao maalum cha viongozi na wadau mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili dira ya maendeleo ya Mkoa huo.

Tamko hilo linamtaka kila Mwalimu Mkuu, Mtendaji wa Kijiji, Mtendaji wa Kata kuhakikisha ifikapo tarehe 05 Januari, 2017 awe amebandika majina yote ya watoto wanaoanza awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza tarehe 09 Januari, 2017.

Mtaka amesema tangu Serikali ya awamu ya tano ilipotangaza elimu bila malipo Mkoa wa Simiyu umepokea takribani kiasi cha shilingi 2,841,356,000/= kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, hali iliyowapunguzia mzigo wazazi.

Mtaka amesema wajibu wa wazazi ni kuhakikisha kila mtoto anapelekwa shule tarehe 09 Januari, 2017 shule zitakapofunguliwa, ambapo amesema wazazi wote ambao hawatawapeleka watoto wao shule watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwa vibarua wa kudumu watakaofanya usafi katika Taasisi za Umma.

“Wazazi wote ambao hawatawapeleka watoto shule wajiandae kuwa vibarua wa kudumu wa Serikali, hao ndiyo watakaosafisha masoko, vituo vya polisi, hospitali, vituo vya afya wengine watadeki hata madarasa na maeneo mengine ya Serikali. Nimeamua kuongea mbele yenu viongozi ili ujumbe huu muwafikishie wananchi, lakini pia nimekuwa nikizungumza na wananchi kila ninapofanya mikutano ya hadhara”, amesema Mtaka.

Pamoja na tamko hilo ameelekeza mambo muhimu yaliyoamuriwa kupitia vikao ya kisheria na kimaamuzi kama Vikao vya Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC),Kamati za Ushauri za Wilaya(DCC), Mabaraza ya Madiwani, Vikao vya Maendeleo ya kata (WDC) na mikutano ya vijiji yatekelezwe ambayo ni kukamilisha madawati Desemba 2016,kukamilisha ujenzi wa madarasa ifikapo Januari 30, 2017.

Maelekezo mengine ni pamoja viongozi wote kugawana na kusimamia madarasa yote ya mtihani (darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili, kidato cha nne na kidato cha sita), Shule zote kutumia chaki za Maswa, Madarasa ya Mitihani kufanya mazoezi ya kila siku asubuhi  saa 1:30 2:00 asubuhi, na kuwepo kwa makambi ya kielimu kwa shule, kata, Wilaya na Mkoa katika siku za mwisho za juma, mapumziko ya kati na mwisho wa mihula.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu,Ndg.Jumanne Sagini amewataka Watendaji wote Serikali kuhakiksha kuwa wanafanyia kazi maelekezo yanayotolewa na viongozi wa mkoa huo ili kutekeleza dira ya maendeleo ya Mkoa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa amesema katika utekelezaji wa Kauli mbiu ya Mkoa huo ya “Wilaya Moja Bidhaa Moja”baada ya wilaya ya Maswa kuzalisha chaki, Wilaya ya Meatu kusindika maziwa Mkoa umejipanga kuanzisha kilimo cha Umwagiliaji wilayani Busega mwaka 2017.

Mtaka amesema Katibu Tawala Mkoa ameunda kikosi kazi cha Wahandisi wa kilimo watakaosaidiana na watalaam wa Busega kuandaa mpango kazi wa utekelezaji wa kilimo cha Umwagiliaji hususani kilimo cha mpunga  kwa misimu miwili au zaidi ili wananchi wa Busega wanufaike kwa kuwa na maji ya Ziwa Victoria.

Pamoja na kilimo cha umwagiliaji Mtaka amewataka wananchi wa Mkoa wa Simiyu kulima mazao yanayokomaa muda mfupi na yanayostahimili ukame kama mtama, muhogo na viazi kutokana na taarifa kuwa mwaka 2017 hautakuwa na mvua za kutosha.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Lamadi wilayani Busega, Mhe.Laurent Bija amesema ili wilaya hiyo iweze kuzalisha chakula cha kutosha mkoa mzima na ziada kwa ajili ya kuuza kupitia mradi wa  kilimo cha umwagiliaji,  mkoa unapaswa kuwa  na mpango mkakati wa kudumu kwa lengo la kuufanya mradi huo kuwa endelevu.

Naye Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Simiyu,Mhe.Gimbi Masaba ametoa wito kwa viongozi wa mkoa huo kuwajibika ipasavyo katika shughuli za maendeleo ya wananchi bila kujali tofauti zao za kisiasa.


Kikao cha Viongozi na Wadau wa Maendeleo Mkoani Simiyu kimewahusisha Viongozi wa Serikali Ngazi ya Mkoa, Wilaya,Wabunge, Madiwani, Watendaji wa Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri, Viongozi wa CCM ngazi ya Mkoa na wilaya,viongozi wa Vyama vingine vya siasa na wadau wengine.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) akizungumza na viongozi na wadau wa maendeleo wa Mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao cha kujadili dira ya maendeleo ya Mkoa mwaka 2017.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini (wa pili kushoto) akizungumza na viongozi na wadau wa maendeleo wa Mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao cha kujadili dira ya maendeleo ya Mkoa mwaka 2017.
Mkuu  wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akizungumza na viongozi na wadau wa maendeleo wa Mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao cha kujadili dira ya maendeleo ya Mkoa mwaka 2017.
Baadhi ya Viongozi na wadau wa Maendeleo wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika kikao kilichowahusisha wadau hao ambacho kilifanyika jana katika ukumbi wa Bariadi Alliance mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi na wadau wa Maendeleo wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika kikao kilichowahusisha wadau hao ambacho kilifanyika jana katika ukumbi wa Bariadi Alliance mjini Bariadi. 
Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Joyce Masunga (wa pili kulia) akizungumza katika kikao cha Viongozi na Wadau wa Maendeleo wa Mkoa huo kilichofanyika jana ukumbi wa Bariadi Alliance mjini Bariadi.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Bw. Paulo Faty akiwasilisha dhana ya Wilaya Moja,Bidhaa Moja (ODOP)  ambayo imeshaanza kutekelezwa Mkoani Simiyu mbele ya Viongozi na Wadau wa Maendeleo wa Mkoa huo katika kikao kilichofanyika jana ukumbi wa Bariadi Alliance mjini Bariadi.
Diwani wa Kata ya Lamadi, Mhe.Laurent Bija akichangia katika  kikao cha viongozi na wadau wa Maendeleo ya Mkoa wa Simiyu katika kikao kilichofanyika jana ukumbi wa Bariadi Alliance mjini Bariadi
Diwani wa Kata ya Zanzui na Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa,Mhe.Jermia Shigala akichangia hoja katika  kikao cha viongozi na wadau wa Maendeleo ya Mkoa wa Simiyu katika kikao kilichofanyika jana ukumbi wa Bariadi Alliance mjini Bariadi.
Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Itilima,Mhe. Benson Kilangi, Mkuu wa Wilaya ya Maswa,Mhe.Dkt.Seif Shekalaghe, Mkuu wa Wilaya ya Busega,Mhe.Tano Mwera na Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe.Dkt.Joseph Chilongani wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Wadau wa Maendeleo ya Mkoa huo, kilichofanyika jana ukumbi wa Bariadi Alliance mjini Bariadi.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Simiyu, Mhe.Gimbi Masaba akichangia hoja katika  kikao cha viongozi na wadau wa Maendeleo ya Mkoa wa Simiyu katika kikao kilichofanyika jana ukumbi wa Bariadi Alliance mjini Bariadi.
Diwani wa Kata ya Lingeka wilayani Meatu akichangia hoja katika  kikao cha viongozi na wadau wa Maendeleo ya Mkoa wa Simiyu katika kikao kilichofanyika jana ukumbi wa Bariadi Alliance mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe.Seif Shekalaghe akichangia hoja katika  kikao cha viongozi na wadau wa Maendeleo ya Mkoa wa Simiyu katika kikao kilichofanyika jana ukumbi wa Bariadi Alliance mjini Bariadi.

Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu walioshiriki kikao cha viongozi na wadau wa Maendeleo ya Mkoa huo kilichofanyika jana ukumbi wa Bariadi Alliance mjini Bariadi.
Diwani wa Viti Maalum kutoka wilaya ya Maswa, Mhe.Mercy Emmanuel akichangia hoja katika  kikao cha viongozi na wadau wa Maendeleo ya Mkoa wa Simiyu katika kikao kilichofanyika jana ukumbi wa Bariadi Alliance mjini Bariadi.


Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Joyce Masunga (wa pili kulia) akizungumza katika kikao cha Viongozi na Wadau wa Maendeleo wa Mkoa huo kilichofanyika jana ukumbi wa Bariadi Alliance mjini Bariadi.


Tuesday, December 27, 2016

MKUU WA MKOA WA SIMIYU AONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA SHULE KATA YA GAMBOSI

Na Stella Kalinga
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka ameongoza harambee ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Gambosi iliyopo Kata ya Gambosi wilayani Bariadi Mkoani humo.

Harambee hiyo imefanyika kufuatia azma ya Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) Tanzania, Ndg.Mark Malekana kutaka kuunga mkono juhudi za wananchi wa kata aliyozaliwa ya Gambosi katika ujenzi wa shule hiyo, kwa kuwa watoto wa kata hiyo wamekuwa wakisoma katika shule ya sekondari Miswaki kata ya jirani ya Mwasubuya.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi, Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Gambosi, Longino Nasari amesema Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kwa kushirikiana na wananchi wameanza kwa kujenga vyumba vitatu vya maabara, jengo la utawala na matundu 08 ya vyoo.

Askofu Malekana amewataka wananchi wa Gambosi kushirikiana na Serikali kujenga shule na miundombinu mingine ya Huduma za Jamii bila kujali tofauti zao za kiitikadi na dini ili kuitengeneza Gambosi mpya ya tofauti na jinsi inavyodhaniwa na watu kuwa ni mahali penye mambo ya kishirikina.

Aidha, Askofu Malekana ametoa wito kwa wananchi wa Gambosi hususani vijana kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo katika eneo hilo na kubadili fikra na mtazamo wa watu wengi juu ya eneo hilo.

“Maendeleo hayaji kwa muujiza wala hayaji kwa bahati mbaya, acheni hadithi za kusema kama Mungu kakupangia kufa maskini utakufa maskini, au kama ulipangiwa kuwa na tajiri utakuwa hivyo, hapana Mungu hakupanga hivyo. Muachane kabisa na fikra hizo potofu fanyeni kazi kwa bidii, mjenge Gambosi Mpya”

Pamoja na kuhimiza maendeleo Askofu Malekana amewataka wananchi wa Gambosi kudumisha amani na kuwatengenezea mazingira rafiki watumishi wanaopangwa kufanya kazi katika eneo  hilo ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba za kupangisha ili waone fahari kufanya kazi Gambosi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amewataka wananchi kuona umuhimu wa elimu na kuwapeleka shule watoto wote wanaopaswa kwenda shule mapema mwezi Januari, 2017 shule zitakapofunguliwa.

Wakati huo huo Mtaka amewataka wananchi kuvitumia vituo vya kutolea huduma za Afya pale wanapougua badala ya kwenda kwa waganga wa jadi ili kupunguza vifo visivyo vya lazima vinaivyoibua chuki  na visasi vitokanavyo na ramli chonganishi, ikiwa ni pamoja na ukataji wa mapanga kwa vikongwe kwa imani za kishirikina.

“Tumieni vituo vyetu vya huduma za Afya vilivyopo  ili mfanyiwe uchunguzi na kupewa tiba kwa gharama nafuu; wazee na watoto chini ya miaka mitano wanatibiwa bure. Pamoja na unafuu huo unasikia mtu anampeleka mtoto kwa mganga anachanjwa chale akifikishwa hospitali hana damu hana maji anakufa, akifa mnaanza kutafuta mchawi, hiyo tabia iachwe kabisa” amesema Mtaka

Katika Harambee hiyo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi mifuko 604 ya saruji, nondo 100, bati 20, misumari kilogramu 7, Madawati 80, Unga wa Ngano mfuko mmoja na mafuta ya kula katoni 1 kwa ajili ya chakula cha mafundi, vitabu 18 na fedha taslimu vilipatikana, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 21,761,050, ikiwa ni michango ya Askofu wa Kanisa la SDA Tanzania na wadau wake, Viongozi wa Serikali ya Mkoa na Wilaya, Wafanyabiashara wa Bariadi na wananchi wa Gambosi.


Mkuu wa Mkoa amehimiza fedha hizo zitumike kwa makusudi yaliyokusudiwa na ujenzi uendelee ili kufikia mwaka 2018 shule hiyo ifunguliwe.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kulia) akizungumza na wananchi wa Gambosi (hawapo pichani) wakati wa  Harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana katika kijiji cha Gambosi wilayani Bariadi.

Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA), Ndg.Mark Malekana akizungumza na  wananchi wa Gambosi(hawapo pichani)  wakati wa  Harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana katika kijiji cha Gambosi wilayani Bariadi.


Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa Gambosi (hawapo pichani) wakati wa  Harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana katika kijiji cha Gambosi wilayani Bariadi.

Kutoka kulia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) wakiwa na viongozi wengine wakati walipotembelea eneo la ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi kabla ya kufanya harambee ya ujenzi wa shule hiyo kijijini Gambosi (Bariadi).
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Gambosi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa  Harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana kijijini hapo wilayani Bariadi.
Diwani wa Kata ya Gambosi, Mhe.Bahame Kaliwa akizungumza na wananchi wa Gambosi (hawapo pichani)  wakati wa  Harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana katika kijiji cha Gambosi wilayani Bariadi.
Paroko wa Parokia ya Ngulyati wilayani Bariadi akizungumza na wananchi wa Gambosi (hawapo pichani) wakati wa  Harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana katika kijiji cha Gambosi wilayani Bariadi.
Mbunge wa Jimbo la Itilima ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu, Mhe.Njalu Silanga akizungumza na wananchi wa Gambosi (hawapo pichani) kabla ya kuchangia katika  Harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana katika kijiji cha Gambosi wilayani Bariadi.


Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe.Duka Mashaurimapya akipeana mkono na Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA), Ndg.Mark Malekana baada ya kuwasilisha mchango wa Halmashauri hiyo wakati wa  Harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana katika kijiji cha Gambosi.

):- Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu na Mbunge wa Itilima ,akipeana mkono na Diwani wa Kata ya Gambosi Mhe. Bahame Kaliwa, baada ya kuwasilisha mchango wake wakati wa  Harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana katika kijiji cha Gambosi.
Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA), Ndg.Mark Malekana akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka  risiti aliyopewa baada ya kununua mifuko 100 ya saruji  kwa ajili ya  kuchangia Ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Gambosi wakienda kuchangia wakati wa Harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana katika kijijini hapo

Sunday, December 25, 2016

SERIKALI MKOANI SIMIYU YATANGAZA KILIMO CHA UMWAGILIAJI KIPAUMBELE MWAKA 2017

Na Stella Kalinga
Serikali Mkoani Simiyu imetangaza Kilimo cha Umwagiliaji kuwa kipaumbele cha mwaka 2017 hususani kilimo cha Mpunga wilayani Busega.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka katika kikao maalum kilichofanyika jana kati ya uongozi wa mkoa huo, uongozi wa wilaya ya Busega, Maafisa Watendaji wa Kata pamoja na Maafisa Ugani wa Wilaya na wa Kata.

Mtaka amesema katika kutekeleza azma ya Kilimo cha umwagiliaji kuwa kipaumbele mwaka 2017 wilayani Busega , Serikali itawahahamasisha wananchi kulima mpunga na kuhakikisha kuwa maji na miundombinu ya umwagiliaji inawafikia katika mashamba yao kwa kadri ya utaratibu utakaowekwa. 

Mtaka ameongeza kuwa kufuatia kuwepo kwa taarifa ya kutokuwa na mvua za kutosha  mwaka 2017 wananchi wamepata hofu ya mazao yao kukauka , hivyo Serikali imekusudia kuwatoa wananchi hofu hiyo kwa kuwahakikishia kuwa itawawezesha kupata maji kutoka Ziwa Victoria kwa ajili ya kumwagilia mashamba yao.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amesema Wilaya ya Busega ni wilaya ambayo wananchi wake wanaweza kulima kwa kipindi cha mwaka mzima kwa kuwa ina uhakika wa maji, hivyo Serikali imekusudia wananchi walime mpunga kwa misimu isiyopungua miwili kwa mwaka.

“Niko tayari kufanya ziara kila kijini hapa Busega ili nizungumze na wananchi, niwatoe hofu ya waliyo nayo juu ya mazao yao kukauka kutokana na kukosa mvua, maana Serikali itawapelekea maji” amesema Mtaka.

Pamoja na kuwahakikishia wananchi upatikanaji wa maji Serikali ya Mkoa kwa kushiriakiana na Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi itawasaidia wananchi kupata mbegu bora ya mpunga ambayo itawawezesha kupata mavuno mengi na bora kuanzia gunia 35 hadi 40 za mpunga kwa heka moja.

Sambamba na hilo Mtaka amesema katika kutekeleza mkakati wa  Kilimo cha Umwagiliaji kama Kipaumbele; wananchi, serikali na wadau wengine wa kilimo kila mmoja atakuwa na wajibu na majukumu yake ili makakati huo utekelezwe kwa tija, ambapo amesema yapo majukumu yatakayofanywa na wananchi, mengine yatafanywa na Serikali (Halmashauri /Wizara ya Kilimo) , Viongozi na mengine yatatekelezwa na wadau.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa huo, Ndg.Jumanne Sagini amesema Serikali ya Mkoa itaunda kikosi kazi cha Wahandisi wa Kilimo na Umwagiliaji kutoka Halmashauri zote za Mkoa huo, ambao watapaswa kuandaa mpango kazi na wajibu wa kila mdau katika utekelezaji wa mradi huo, kabla ya Januari Mosi, 2017.

Sagini amesema Wataalam hao kwa kushirikiana na watalaam wa Wilaya ya Busega watapaswa kukaa pamoja na kuandaa mpango kazi utakaobainisha mipango ya muda mrefu na ya muda mfupi, ambayo itapelekea kutekelezwa kwa mradi wa kilimo cha umwagiliaji kwa tija  na matokeo chanya kwa wananchi.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Busega Mhe. Mickness Mahela akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti,  amesema madiwani wote wa wilaya hiyo watatoa ushirikiano na kuhakikisha mpango huo wa kilimo cha umwagiliaji unafanikiwa kwa kiasi kikubwa na kuwasaidia wananchi.


Mkuu wa Mkoa anatarajia kuanza ziara ya siku sita wilayani Busega kuanzia Januari 03 hadi Januari 09, 2017 kwa lengo la kuzungumza na wananchi juu ya kilimo cha umwagiliaji kupitia mikutano ya hadhara, ambapo ameagiza taarifa ya mikutano hiyo zitolewe katika nyumba za ibada, kwenye mbao za matangazo za Vijiji na kata na gari la matangazo litumike ili wananchi wote wapate taarifa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (wa pili kushoto) akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Halmashari ya Wilaya ya Busega (hawapo pichani) katika kikao maalum cha kujadili mkakati wa kilimo cha umwagiliaji wilayani humo, (wa tatu) Katibu Tawala Mkoa,Ndg. Jumanne Sagini.
Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Tano Mwera akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Halmashari ya Wilaya ya Busega (hawapo pichani) katika kikao maalum cha kujadili mkakati wa kilimo cha umwagiliaji wilayani humo.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Watendaji wa Wilaya ya Busega wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa, Mhe.Anthony Mtaka katika kikao maalum cha kujadili mkakati wa kilimo cha umwagiliaji wilayani Busega.

Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Huduma za Maji katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhandisi.Hatari Kapufi akichangia katika kikao maalum cha kujadili mkakati wa kilimo cha umwagiliaji wilayani Busega.

Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega akizungumza katika kikao maalum cha kujadili mkakati wa kilimo cha umwagiliaji wilayani humo kilichofanyika jana katika Ukumbi wa Silsosi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (wa pili kushoto)  akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Halmashari ya Wilaya ya Busega (hawapo pichani) katika kikao maalum cha kujadili mkakati wa kilimo cha umwagiliaji wilayani humo.

Thursday, December 22, 2016

RC SIMIYU AKUTANA NA VIONGOZI WA MKOA WA SHINYANGA KUJADILI MATUMIZI YA CHAKI ZA MASWA

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) akionesha pakti ya Chaki za Maswa kwa  Wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa Elimu wa Wilaya za Mkoa wa Shinyanga (hawapo pichani) walioshiriki kikao maalum cha kujadili matumizi ya Chaki hizo katika Mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (katikati) akizungumza na Wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa Elimu wa Wilaya za Mkoa wa Shinyanga (hawapo pichani) wakati wa kikao maalum cha kujadili matumizi ya Chaki zinazotengenezwa Maswa (Simiyu) katika Mkoa wa Shinyanga,(kushoto) Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Zainab Telack na Katibu Tawala Mkoa, Ndg.Albert Msovela.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Mkoani Shinyanga Ndg.Augostine Matomora akichangia katika kikao maalum cha kujadili matumizi ya Chaki zinazotengenezwa wilayani Maswa (Simiyu) katika Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama , Mkoani Shinyanga Ndg. Anderson Msumba akichangia katika kikao maalum cha kujadili matumizi ya Chaki zinazotengenezwa wilayani Maswa (Simiyu) katika Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi katoni ya Chaki za Maswa-Simiyu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Zainab Telack(kushoto) baada ya kikao maalum cha kujadili matumizi ya Chaki hizo Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akimkabidhi katoni ya Chaki za Maswa-Simiyu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Mkoani Shinyanga Ndg.Simon Berege baada ya kikao maalum cha kujadili matumizi ya Chaki hizo Mkoani humo.
Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kikao maalum cha kujadili matumizi ya Chaki zinazotengenezwa wilayani Maswa (Simiyu) katika Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.Dkt. Titus Kamani akizungumza na Wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa Elimu wa Wilaya za Mkoa wa Shinyanga (hawapo pichani) wakati wa kikao maalum cha kujadili matumizi ya Chaki zinazotengenezwa Maswa mkoani Simiyu, katika Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akimkabidhi katoni ya Chaki za Maswa-Simiyu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,baada ya kikao maalum cha kujadili matumizi ya Chaki hizo katika Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Mkoani Shinyanga Ndg. Simon Berege akichangia katika kikao maalum cha kujadili matumizi ya Chaki zinazotengenezwa wilayani Maswa (Simiyu) katika Mkoa wa Shinyanga.
: Baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa Elimu wa Wilaya za Mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) katika kikao maalum cha kujadili matumizi ya Chaki zinazotengenezwa Maswa Mkoani Simiyu katika Mkoa wa Shinyanga.

   Na Stella Kalinga
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amekutana na Uongozi wa Mkoa wa Shinyanga wakiogozwa na Mkuu wa Mkoa huo,Mhe.Zainab Telack, Katibu Tawala Mkoa na Wakurugenzi wa Halmashauri zote kujadili juu ya matumizi ya Chaki za Maswa mkoani Shinyanga.

Mtaka amesema Mkoa wake umefungua mlango wa biashara na ushirikiano katika bidhaa zinazozalishwa Mkoani Simiyu chini ya Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja, Bidhaa Moja” kila wilaya itazalisha bidhaa moja itakayoitambulisha(branding); ambapo Wilaya ya Maswa imeanza kwa kutengeneza Chaki (MASWA CHALKS) na Wilaya ya Meatu inasindika maziwa ya ng’ombe (MEATU MILK).

Mtaka ameongeza kuwa Watanzania wanapaswa kuthamini na kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na kubadili mtazamo wa kifikra kuwa bidhaa bora ni zile zinazozalishwa nje ya nchi, chini ya Kauli Mbiu “Buy Tanzania, Watanzania Tupende vya Kwetu”

Aidha, Mtaka amesema endapo viongozi hao wataridhia kutumia Chaki zinazotengenezwa na Vijana wa Maswa, wataokoa fedha nyingi zinazotolewa na Serikali kupitia Elimu bila malipo kwa kuwa zinauzwa kwa gharama nafuu ikilinganishwa na zile zinazotoka nje.

“Shule zetu zimekuwa zikinunua chaki kwa gharama kubwa kati ya shilingi 35,000 hadi 60,000 kwa katoni , lakini Vijana hawa wa Maswa watawauzia shilingi 25,000 kwa katoni.Chaki hizi zimethibitishwa na Shirika la Viwango nchini (TBS) na taratibu za TRA zimezingatiwa, vijana wanatoa risiti za EFD” alisema Mtaka.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Zainab Telack amesema ikiwa Wakurugenzi Halmashauri na Maafisa Elimu wa Wilaya za Mkoa huo wataridhia kutumia chaki za Maswa  katika shule zao uongozi wa Mkoa huo hautakuwa na kipingamizi.

Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu walikubaliana kwa pamoja na kuunga mkono jitihada za Serikali na Vijana wa Wilaya ya Maswa kukubali kununua chaki za Maswa ili zitumike katika shule zao.

Kiwanda cha chaki kinachoendeshwa na Vijana wa Wilaya ya Maswa kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kinaweza kuzalisha takribani katoni 200 kwa siku na wakati matumizi halisi ya Mkoa wa Simiyu pekee ni katoni 700 kwa mwezi hivyo kuna ziada ya kuuza nje ya mkoa huo.


Wednesday, December 21, 2016

MKAPA FOUNDATION YAKABIDHI NYUMBA 28, MAJENGO MAWILI YA UPASUAJI MKOANI SIMIYU

Na Stella Kalinga
Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation imekabidhi Serikali jumla ya Nyumba 28 kati ya 48 zinazotarajiwa kujengwa kwa ajili ya watumishi wa Idara ya Afya na Majengo Mawili ya Upasuaji kwa ajili ya huduma za akina mama wajawazito Mkoani Simiyu.

Akipokea na kufungua Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya cha Ngulyati Wilayani Bariadi na Nyumba za Watumishi katika Hospitali ya Mkula wilayani Busega, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto , Mhe.Ummy Mwalimu ameishukuru Taasisi hiyo kwa kuuunga mkono Serikali katika uboreshaji wa huduma za Afya, hasa katika ujenzi wa miundombinu ya Afya.

Mhe.Waziri amesema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuboresha huduma za Afya kwa kuongeza kiwango cha  upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, miundombinu ya Afya ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Hospitali, Vituo vya Afya, Zahanati na Majengo ya Upasuaji, hivyo upatikanaji wa majengo hayo utasaidia wananchi wa maeneo husika kupata huduma zinazotakiwa.

Mhe.Waziri ameongeza kuwa Serikali imeanza kwa kuboresha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa kuongeza bajeti, ambapo  kwa Mwaka 2015 zilitengwa jumla ya shilingi bilioni 31 na mwaka 2016 zimetengwa shilingi bilioni 51.

Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine imejipanga kujenga kiwanda cha kutengeneza dawa Mkoani Simiyu, hivyo pindi kiwanda hicho kitakapokamilika dawa za Vituo Mbalimbali vya kutolea huduma za Afya zitanunuliwa Simiyu.

Aidha, Mhe.Ummy Mwalimu ameutaka Uongozi wa Mkoa uhakikishe unasimamia ukusanyaji wa mapato katika Vituo vyote vya kutolea huduma za Afya,  ili sehemu ya mapato hayo itumike kununulia dawa na vifaa tiba kwa lengo la kuwahakikishia wananchi upatikanaji wa huduma bora za afya.

Katika kukabiliana na tatizo la vifo vya akina mama wajawazito na watoto wakati wa kujifungua, Mhe.Ummy Mwalimu amewataka akina mama wajawazito kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya, ikiwa ni pamoja na kituo cha Afya cha Ngulyati mahali ambapo Jengo la Upasuaji na wodi kwa ajili ya  akina mama wajawazito vimejengwa.

Sanjari na hilo Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza kwa nyakati tofauti na wakazi wa Ngulyati wilayani Bariadi na Mkula wilayani Busega, amewahakikishia kuwa Wizara yake italeta watumishi wa idara ya afya ili kukabiliana na upungufu uliopo na akazitaka Halmashauri zote mkoani Simiyu kutengeneza mazingira mazuri ambayo yatawapa motisha watumishi watakaoletwa na kuendelea kubaki Simiyu.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya nyumba za watumishi na majengo ya Upasuaji, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Dkt.Hellen Mkondya Senkoro amesema,  Taasisi hiyo imekamilisha majengo hayo yote na akaiomba Serikali kuweka miundombinu iliyosalia kama maji, vifaa vya kutolea huduma na watumishi ili wananchi waweze kunufaika na miradi hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  ameishukuru Taasisi ya Mkapa Foundation na akaahidi kuwa Serikali itajitahidi kuhakikisha changamoto zote zinatatuliwa katika miradi ya Benjamin Mkapa Foundation ili itekelezwe kwa tija na manufaa kwa wananchi.

Aidha,Mkuu huyo wa Mkoa amemshukuru Waziri wa Afya,Maendeleo yaJamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu kwa kutoa magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) nane(08) kwa Vituo vya Afya,Hospitali za Wilaya na Hosptali Teule ya Mkoa kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma.

Wakati huo huo Mbunge wa Busega,Mhe.Dkt.Raphael Chegeni amemshukuru Mhe Waziri kwa jitihada zinazoendelea kufanyika katika kuboresha huduma za Afya Mkoani Simiyu na akamuomba aupe kipaumbele Mkoa wa Simiyu, hususani Wilaya za Busega na Itilima ambazo ni mpya kila Wizara yake inapogawa rasilimali au miundombinu mingine ya Afya.


 Wilaya za Mkoa wa Simiyu zilizonufaika na Mradi wa Ujenzi wa Majengo ya Upasuaji sambamba na wodi ya wazazi Bariadi na Busega ambayo yamejengwa kwa thamani ya shilingi milioni 435, kwa upande wa Nyumba za Watumishi wilaya ya Busega (Nyumba 10),Itilima (Nyumba 10) na Bariadi ni Nyumba 08 ambazo zimegharimu jumla ya shilingi bilioni 1.47.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(wa tatu kulia) akikata utepe katika ufunguzi wa Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya Ngulyati lililokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (kushoto) akisoma Jiwe la ufunguzi wa Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya Ngulyati lililokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(wa pili kulia) akikagua baadhi ya vifaa tiba mara baada ufunguzi wa Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya Ngulyati lililokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(kulia) akiwa na baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa mara baada ufunguzi wa Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya Ngulyati lililokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akikagua baadhi ya vifaa tiba mara baada ufunguzi wa Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya Ngulyati lililokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(kushoto) akisaini vitabu vya wageni mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya  ufunguzi wa Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya Ngulyati lililokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, (kulia)Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation,Dkt.Hellen Mkondya Senkoro akiwasilisha taarifa ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya Ngulyati lililokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi hiyo.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Bariadi,Mkoa wa Simiyu na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation mara baada ufunguzi wa Jengo la Upasuaji (pichani) katika Kituo cha Afya.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(kushoto) akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngulyati wilayani Bariadi baada ya   ufunguzi wa Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya Ngulyati lililokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.

Baadhi wa wananchi wa Kata ya Ngulyati wakimsikiliza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(hayupo pichani) alipozungumza nao baada ya   ufunguzi wa Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya Ngulyati lililokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation,Dkt.Hellen Mkondya Senkoro (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(kulia) hati ya makabidhiano ya Jengo Upasuaji katika Kituo cha Afya Ngulyati

Mbunge wa Jimbo la Busega Mhe. Dkt. Raphael Chegeni (kushoto)akionesha hati ya makabidhiano ya Nyumba 10 za Watumishi wa Afya zilizokabidhiwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.

Kutoka kushoto,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe,Anthony Mtaka,Waziri wa Afya,Mhe.Ummy Mwalimu,Mbunge wa Busega,mhe.Dkt.Raphael Chegeni naMkuu wa Wilaya ya Busega,Mhe.Tano Mwera wakicheza wimbo wa Kisukuma na wananchi wa Kata ya Mkula wilayani Busega mara baada Mhe.Waziri kufungua Nyumba za Watumishi zilizokabidhiwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.

Mkuu wa Wilaya ya Busega,Mhe.Tano Mwera akizungumza na wananchi wa Mkula baada ya Nyumba za Watumishi zilizokabidhiwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation kufunguliwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt.Mageda Kihulya akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka(wa pili kushoto) wakizungumza jambo, mara baada ya ufunguzi wa nyumba za watumishi kata ya Mkula ilayani Busega.

Kutoka kushoto Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Bariadi,Mhe,Robert Lweyo,Mbunge wa Busega, Mhe.Dkt.Raphael Chegeni na Mbunge wa Itilima Mhe.Njalu Silanga wakizunguza jambo mara baada ya ufunguzi wa Jengo la Upasuaji Ngulyati Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,Mhe.Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngulyati mara baada ya ya ufunguzi wa Jengo la Upasuaji Ngulyati liliokabidhiwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu,Dkt.Titus Kamani akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngulyati mara baada ya ya ufunguzi wa Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya cha Ngulyati liliokabidhiwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi wa Kata ya Mkula wilayani Busega baada ya   ufunguzi wa Nyumba za Watumishi zilizokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation. 
Baadhi wa wananchi wa Kata ya Mkula wakimsikiliza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (hayupo pichani) alipozungumza nao baada ya   ufunguzi wa Nyumba za Watumishi wa Hospitali ya Mkula zilizokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Wananchi wa Ngulyati mara baada ya Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu kufungua Jengo la Upasuaji katika Kituo cha 
Afya Ngulyati lililokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu akiwatambulisha viongozi mbalimbali wa Mkoa huo (hawapo pichani) kwa wananchi wa Kata ya Mkula baada ya   ufunguzi wa Nyumba za Watumishi wa Hospitali ya Mkula zilizokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya ya Busega ,Mkoa wa Simiyu mbele ya moja ya Nyumba za Watumishi katika Hospitali ya Mkula (Busega) zilizokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!