|
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka akizungumza na wananchi wa Bariadi (hawapo
pichani) wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa
Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi. |
|
Kutoka
kulia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka , Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Simiyu, ACP. Onesmo Lyanga na Afisa Usalama wa Taifa Mkoa wakipokea maandamano
wa wananchi (hawapo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya
Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi. |
|
Watoto
wa Kituo cha Watoto Yatima cha Home Of Peace cha Kanisa la K.K.K.T Bariadi wakiwa
katika maandamano wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga
Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi |
|
Baadhi ya wananchi wa
Bariadi wakiwa katika maandamano wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya
Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi.
Mkuu wa Dawati la
Jinsia na Watoto Mkoa wa Simiyu, ASP. Kajeng Muro akizungumza na wananchi wa
Bariadi (hawapo pichani) wakati wa
Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika
kimkoa Mjini Bariadi.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP. Onesmo Lyanga akizungumza na wananchi wa
Bariadi (hawapo pichani) wakati wa
Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika
kimkoa Mjini Bariadi
Watoto
wa Kituo cha Watoto Yatima cha Home Of Peace cha Kanisa la K.K.K.T Bariadi wakiwasilisha
ujumbe wao kwa njia ya ngonjera wakati
wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia
yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi.
Baadhi
ya waimbaji wa kwaya ya Kanisa la AICT Bariadi wakitoa burudani ya wimbo kwenye
Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika
kimkoa Mjini Bariadi.
Watoto wa Kituo cha
Watoto Yatima cha Home Of Peace cha Kanisa la K.K.K.T Bariadi wakiwasilisha
ujumbe wao kwa njia ya ngonjera wakati
wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia
yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi.
Baadhi
ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na wadau wa mapambano dhidi ya Ukatiliwa Kijinsia
wakisikiliza hotuba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha
Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi
Baadhi
ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na wadau wa mapambano dhidi ya Ukatiliwa Kijinsia
wakisikiliza hotuba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha
Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya
pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa, Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa na baadhi ya Maafisa
wa Dawati la Jinsia na Watoto, mara baada ya kufunga maadhimisho ya Kilele cha
Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi
la Polisi la Mkoa huo mara baada ya kufunga maadhimisho ya Kilele cha Siku 16
ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo mara baada ya kufunga maadhimisho ya Kilele
cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya
pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Vyama vya Siasa
na Watendaji wa Wilaya ya Bariadi mara baada ya kufunga maadhimisho ya Kilele
cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi |
Baadhi ya askari wa
Jeshi la Polisi( Kikosi cha kuzuia Ghasia) wakiwa katika maandamano wakati wa Maadhimisho
ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini
Bariadi.
|
|
Baadhi
ya wananchi wa Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
(hayupo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili
wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi.
|
Na Stella Kalinga |
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amewahimiza wananchi wa Mkoa huo kulitumia
vema Dawati la Jinsia na Watoto la Jeshi la Polisi katika kukabiliana na
vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mtaka
ameyasema hayo leo wakati alipozungumza na wananchi wa Bariadi katika Maadhimisho
ya Kilele cha Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Mkoani humo ambayo
yamefanyika katika kituo cha mabasi cha zamani Mjini Bariadi.
Mtaka
amesema Wananchi wanapaswa kutoa taarifa na malalamiko yao juu ya vitendo vya
ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na mashambulio ya kudhuru mwili, ubakaji,
ulawiti, mashambulio ya aibu, ndoa za utotoni na vitendo vingine vinavyofanywa katika
jamii ili wahalifu wanaojihusisha na vitendo hivyo waweze kuchukuliwa hatua.
Aidha,
Mtaka amesema pamoja na kulitumia Dawati la Jinsia lililopo katika vituo vya
Polisi, wananchi wazitumie Ofisi za Serikali zikiwepo Ofisi za Vijiji/Mitaa,
Kata, Wilaya na Mkoa katika kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili wa kijinsia
badala ya kwenda katika Mashirika yasiyo ya Kiserikali ambayo baadhi huwatoza fedha
katika kuwapa huduma hizo.
“Litumieni
dawati la jinsia kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto
wa kike na wanawake. Watumieni Maafisa Maendeleo ya jamii, Maafisa Ustawi wa
Jamii na maafisa wetu wengine wa Serikali mpewe huduma hizo bure, badala ya
kupeleka malalamiko yenu kwenye mashirika au asasi ambazo si za Serikali
zinazowatoza fedha” alisema Mtaka.
Akizungumza
katika Maadhimisho hayo Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Simiyu ASP. Kaneng Muro amesema
Serikali kupitia Vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Polisi
haitavumilia mtu yeyote atakayebainika kutenda vitendo vya kikatili na
imejipanga kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa kabisa katika jamii.
Naye
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu,ACP Onesmo Lyanga amesema wananchi waache
kujichukulia sheria mkononi ikiwa ni pamoja na mauaji ya vikongwe kwa imani za
kishirikina badala yake watoe taarifa za uhalifu katika vyombo vya dola ili vichukue
hatua dhidi ya wahalifu hao kwa mujibu wa sheria.
Wakati
huo huo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amelipongeza Jeshi la Polisi
Mkoani humo kwa kazi linayofanya ya kupambana na uhalifu na hivyo kufanya mkoa
kuwa salama.
Sanjari
na hilo Mkuu huyo wa Mkoa amesema Mkoa wa Simiyu unakabiliwa na tatizo la kuwaozesha watoto
katika umri mdogo hali ambayo imesababisha vifo wakati wa kujifungua kwa baadhi
ya watoto wa kike, msongo wa mawazo na kukosa maamuzi kwa kuwa wengi wao
wanaolewa na watu wazima.
Katika
kukabiliana na hilo Mtaka amesema wazazi wote wahakikishe watoto wao
wanapelekwa shule ifikapo Januari mwaka 2017 na wasiwakatize masomo na
kuwalazimisha kuolewa, ambapo alisema wale watakaokaidi watakuwa vibarua wa
kufanya usafi katika Ofisi za Taasisi za Umma.
“Kama
mtu anataka kuwa kibarua wa Serikali mwakani aache kumpeleka mtoto shule, atafanya
usafi polisi, shuleni, hospitali,vituo vya afya, zahanati, masoko na maeneo
mengine ya Umma. Hatuwezi kuwapa kazi askari wetu badala ya kulinda raia na
mali zao waje wakulazimishe wewe umpeleke mwanao shule; nasema hivi ili tutakapoanza
vitendo tusilaumiane” alisema Mtaka.
Mtaka
ameongeza kuwa Serikali itawachukulia hatua kali ikiwa ni pamoja na kifungo
baadhi ya watu wasio waadilifu ambao wamekuwa wakiwarubuni wanafunzi wa kike na
kukatiza masomo yao kwa kuwapa mimba, hali inayopelekea kuwa na ndoa za
utotoni.
Maadhimisho
ya Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia hufanyika kuanzia Novemba 25 hadi
Disemba 10 kila mwaka ambapo Kauli Mbiu yaMaadhimisho haya mwaka 2016 ni “FUNGUKA, PINGA UKATILI WA KIJINSIA, ELIMU
SALAMA KWA
WOTE”
0 comments:
Post a Comment