|
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) akionesha pakti ya Chaki za
Maswa kwa Wakurugenzi wa Halmashauri na
Maafisa Elimu wa Wilaya za Mkoa wa Shinyanga (hawapo pichani) walioshiriki
kikao maalum cha kujadili matumizi ya Chaki hizo katika Mkoa wa Shinyanga |
|
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka (katikati) akizungumza na Wakurugenzi wa Halmashauri na
Maafisa Elimu wa Wilaya za Mkoa wa Shinyanga (hawapo pichani) wakati wa kikao
maalum cha kujadili matumizi ya Chaki zinazotengenezwa Maswa (Simiyu) katika
Mkoa wa Shinyanga,(kushoto) Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Zainab Telack na Katibu
Tawala Mkoa, Ndg.Albert Msovela.
|
|
Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Mkoani Shinyanga Ndg.Augostine Matomora akichangia
katika kikao maalum cha kujadili matumizi ya Chaki zinazotengenezwa wilayani
Maswa (Simiyu) katika Mkoa wa Shinyanga.
|
|
Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji wa Kahama , Mkoani Shinyanga Ndg. Anderson Msumba akichangia
katika kikao maalum cha kujadili matumizi ya Chaki zinazotengenezwa wilayani
Maswa (Simiyu) katika Mkoa wa Shinyanga.
|
|
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi katoni ya Chaki za Maswa-Simiyu Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Zainab Telack(kushoto) baada ya kikao maalum cha
kujadili matumizi ya Chaki hizo Mkoani humo.
|
|
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony
Mtaka akimkabidhi katoni ya Chaki za Maswa-Simiyu Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Msalala, Mkoani Shinyanga Ndg.Simon Berege baada ya kikao maalum cha
kujadili matumizi ya Chaki hizo Mkoani humo.
|
|
Viongozi wa Mkoa wa
Simiyu na Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kikao maalum
cha kujadili matumizi ya Chaki zinazotengenezwa wilayani Maswa (Simiyu) katika
Mkoa wa Shinyanga.
|
|
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.Dkt. Titus Kamani akizungumza na Wakurugenzi wa
Halmashauri na Maafisa Elimu wa Wilaya za Mkoa wa Shinyanga (hawapo pichani)
wakati wa kikao maalum cha kujadili matumizi ya Chaki zinazotengenezwa Maswa
mkoani Simiyu, katika Mkoa wa Shinyanga. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony
Mtaka akimkabidhi katoni ya Chaki za Maswa-Simiyu Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga,baada ya kikao maalum cha kujadili matumizi ya Chaki hizo
katika Mkoa wa Shinyanga.
|
|
Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Mkoani Shinyanga Ndg. Simon Berege akichangia
katika kikao maalum cha kujadili matumizi ya Chaki zinazotengenezwa wilayani
Maswa (Simiyu) katika Mkoa wa Shinyanga.
|
|
: Baadhi ya Wakurugenzi
wa Halmashauri na Maafisa Elimu wa Wilaya za Mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) katika kikao maalum cha kujadili
matumizi ya Chaki zinazotengenezwa Maswa Mkoani Simiyu katika Mkoa wa
Shinyanga.
|
Na
Stella Kalinga
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka amekutana na Uongozi wa Mkoa wa Shinyanga wakiogozwa na Mkuu
wa Mkoa huo,Mhe.Zainab Telack, Katibu Tawala Mkoa na Wakurugenzi wa Halmashauri
zote kujadili juu ya matumizi ya Chaki za Maswa mkoani Shinyanga.
Mtaka amesema Mkoa wake
umefungua mlango wa biashara na ushirikiano katika bidhaa zinazozalishwa Mkoani
Simiyu chini ya Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja, Bidhaa Moja” kila
wilaya itazalisha bidhaa moja itakayoitambulisha(branding); ambapo Wilaya ya Maswa
imeanza kwa kutengeneza Chaki (MASWA CHALKS) na Wilaya ya Meatu inasindika
maziwa ya ng’ombe (MEATU MILK).
Mtaka ameongeza kuwa
Watanzania wanapaswa kuthamini na kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na
kubadili mtazamo wa kifikra kuwa bidhaa bora ni zile zinazozalishwa nje ya nchi,
chini ya Kauli Mbiu “Buy Tanzania, Watanzania Tupende vya Kwetu”
Aidha, Mtaka amesema
endapo viongozi hao wataridhia kutumia Chaki zinazotengenezwa na Vijana wa
Maswa, wataokoa fedha nyingi zinazotolewa na Serikali kupitia Elimu bila malipo
kwa kuwa zinauzwa kwa gharama nafuu ikilinganishwa na zile zinazotoka nje.
“Shule zetu zimekuwa
zikinunua chaki kwa gharama kubwa kati ya shilingi 35,000 hadi 60,000 kwa
katoni , lakini Vijana hawa wa Maswa watawauzia shilingi 25,000 kwa
katoni.Chaki hizi zimethibitishwa na Shirika la Viwango nchini (TBS) na
taratibu za TRA zimezingatiwa, vijana wanatoa risiti za EFD” alisema Mtaka.
Kwa upande wake Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga Mhe.Zainab Telack amesema ikiwa Wakurugenzi Halmashauri na
Maafisa Elimu wa Wilaya za Mkoa huo wataridhia kutumia chaki za Maswa katika shule zao uongozi wa Mkoa huo
hautakuwa na kipingamizi.
Wakurugenzi wa
Halmashauri za Mkoa wa Simiyu walikubaliana kwa pamoja na kuunga mkono jitihada
za Serikali na Vijana wa Wilaya ya Maswa kukubali kununua chaki za Maswa ili
zitumike katika shule zao.
Kiwanda cha chaki
kinachoendeshwa na Vijana wa Wilaya ya Maswa kwa kushirikiana na Halmashauri ya
Wilaya ya Maswa kinaweza kuzalisha takribani katoni 200 kwa siku na wakati
matumizi halisi ya Mkoa wa Simiyu pekee ni katoni 700 kwa mwezi hivyo kuna
ziada ya kuuza nje ya mkoa huo.
0 comments:
Post a Comment