Wednesday, July 18, 2018

WAZIRI WA MIFUGO AONGOZA WAOMBOLEZAJI MEATU MAZISHI YA DIWANI SHUKIA ALIYEFARIKI KWA AJALI

Waziri wa mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina amewaongoza wakazi wa Wilaya ya Meatu na Mkoa wa Simiyu katika mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu Elias Shukia aliyefariki katika ajali ya gari Mkoani Singida akitokea Dodoma na kusababisha kifo chake na dereva na kusababisha watu wengine watano kujeruhiwa.
Ajali hiyo imetokea Julai 14 eneo la Mkiwa Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida ,baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina Toyota landcluser DFPA 0148 la Halmashauri ya Meatu kupasuka tairi na kupinduka mara tatu na kusababisha vifo hivyo viwili,huku majeruhi wa ajali hiyo Mkurugenzi Mtendaji, Mwenyekiti wa Halmashauri na Maafisa wa Halmashauri hiyo walipata majeruhi.
Mpina ametoa pole kwa familia, wananchi, Chama Cha Mapinduzi na Halmashauri ya Wilaya ya Meatu na kuwataka kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu kwa kuondokewa na madiwani watatu na dereva katika matukio mawili tofauti ya ajali na akawaomba wasifikiri kitu kingine tofauti juu ya kutokea kwa ajali hizo badala yake wajue kuwa ni mapenzi ya Mungu.
“ Kuna watu wanaweza wasiamini kuwa ajali zinaweza zikatokea Meatu kwa muda fupi hivi kama ilivyotokea kwetu, naomba ndugu zangu wananchi, viongozi tusiingie kwenye mtego huo tujue tu kuwa haya ni mapenzi ya Mungu kama walivyosema viongozi wetu wa dini kuwa Mungu ndiye anayejua hatma ya maisha yetu” alisema Mpina.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa pole kwa familia, chama na wananchi kwa msiba huo na  amewaagiza Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kuhakikisha stahili zote za marehemu zinalipwa kwa wakati kwa familia ya marehemu.
Aidha, amewaomba viongozi wa dini kufanya maombi kwa ajili ya  wilaya ya Meatu na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla kuomba Mwenyezi Mungu kuwaepusha viongozi na wananchi na mitihani ya ajali iliyotokea mfululizo.
“Wakati tunawaaga madiwani wetu wale wawili waliofariki kwenye ajali ya kwanza,  Mwenyekiti wa Halmashauri na madiwani wengine walikuwa kwenye matibabu , leo tunamuaga
Mhe. Shukia Mkurugezi na Mwenyekiti wako kwenye matibabu kwa sababu ya majeraha waliyoyapata katika ajali, sisi kama wanadamu tunaamini kwenye ulimwengu wa roho tuna nafasi ya kuomba, niwaombe viongozi wa dini tumwombe Mungu atuepushe na mitihani hii” alisema
Mbunge wa Jimbo la Meatu Salum Khamis amesema kifo cha mhe. Shukia  ni pigo kubwa kwa kata ya Mwanhuzi na Meatu kwa ujumla kwa kuwa marehemu Shukia enzi za uhai wake alikuwa mtetezi ndani ya Chama Cha Mapinduzi na wananchi katika shughuli za maendeleo.
Akitoa mahubiri wakati wa ibada ya Mazishi, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala aliwakumbusha waombolezaji wote kuishi wakimtegemea Mungu, kwa kuwa kila mtu hapa duniani anaishi kwa neema ya Mwenyezi Mungu, hivyo wanapaswa kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.
Marehemu Shukia ameacha mke na watoto wanne, BWANA ALITOA , BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE. AMINA!

MWISHO

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi,  baada ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.Enock Yakobo akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala akitoa sala wakati wa ibada ya mazishi aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi,  kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakiteta jambo kwenye msiba wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi ,kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Mbunge wa Meatu, Mhe. Salum Khamis akitoa salamu za rambirambi katika msiba wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo  yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Kutoka kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Mhe. Anthony Diallo,  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Meatu, Mhe.Juma Mwiburi wakiteta jambo jambo kwenye msiba wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Vijana wa CCM na Vijana wa KKKT Meatu wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi kuelekea kwenye mazishi yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.Enock Yakobo (kulia) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Mhe. Anthony Diallo wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi baada ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Mhe. Anthony Diallo akitoa salamu za rambirambi katika msiba wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Kutoka kushoto Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Meatu, Mhe.Juma Mwiburi, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Maswa, Mhe. Paul Jidayi na Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani,  wakiteta jambo jambo kwenye msiba wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Mhe. Anthony Diallo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakiteta jambo kwenye  msiba wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi,  kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Mama mzazi wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala akiongoza maombi ya kuuombea Mkoa wa Simiyu, wakati wa ibada ya mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali wakiwa katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu, ibada hiyo ilifanyika . Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Usharika wa Baraka Meatu.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala akiteta jambo na viongozi wengine wa Dayosisi hiyo kwenye ibada ya mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi,  kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali wakiungana na viongozi wa dini mkoa wa Simiyu, kuuombea Mkoa huo kabla ya mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi,  kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, baada ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani  akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, baada ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Mbunge wa Jimbo la Meatu Salum Khamis akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, baada ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Baadhi ya Viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania wakiwa katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kanisa la Kiinjili Kilutheri Tanzania  Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi,  kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi,  baada ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala akiongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, wakati wa  mazishi ya diwani huyo  yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala akizungumza na waombolezaji katika msiba wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Baadhi ya ndugu wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, wakisikiliza mahubiri ya viongozi wa dini  kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu..
Baadhi ya waombolezaji na ndugu wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, wakisikiliza mahubiri ya viongozi wa dini  kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala akiongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla ya  mazishi ya diwani huyo  yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Mjane wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mume wake, kabla ya mazishi yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,mhe.Anthony Mtaka akitoa salamu za rambirambi katika msiba wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla ya  mazishi ya diwani huyo  yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.


Tuesday, July 17, 2018

RC MTAKA AKUTANA NA KIONGOZI WA JUMUIYA YA WAISLAMU WA AHMADIYYA


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amekutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry .

Katika mazungumzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Jumuiya hiyo kwa namna ilivyowekeza katika miradi ya mbalimbali ikiwemo miradi ya maji hususani uchimbaji wa visima katika baadhi ya maeneo mkoani humo. 

Aidha, ameiomba Jumuiya hiyo kuona uwezekano wa kuwekeza kwenye sekta ya Afya hasa katika ujenzi wa Hospitali huku akiwahakikishia upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya ujenzi pindi watakapokuwa tayari.

Kwa upande wake Kiongozi Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry amesema atalichukua kama pendekezo kwa viongozi wenzake ili waweze kuona uwezekano wa kuwekeza katika ujenzi wa hospitali Mkoani Simiyu.

Wakati huo huo Kiongozi huyo amesema pamoja na kuchimba visima vya maji Jumuiya ya Ahmadiyya imewekeza katika  Elimu na Afya katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Naye Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Mkoa wa Simiyu, Shekh Abdulatif Yusuph Ngalombe amesema hadi sasa jumuiya hiyo imechimba visima 6 katika wilaya ya Itilima na kuboresha  visima 19 katika wilaya ya Itilima na Meatu kwa gharama ya shilingi 49,760,000 na kazi ikiwa bado inaendelea katika baadhi ya maeneo.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka (katikati) akisalimiana na Kiongozi wa Jumuiya wa Waislamu ya Ahmadiyya, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry mara baada ya kumaliza mazungumzo yao ofisini kwake Mjini Bariadi Julai 17, 2018.
Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka alipomtembelea Ofisini kwake Mjini Bariadi, Julai 17, 2018.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya, wakiongozwa na Kiongozi Mkuu Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry walipomtembelea ofisini kwake Mjini Bariadi, Julai 17, 2018.
Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka alipomtembelea Ofisini kwake Mjini Bariadi, Julai 17, 2018.
Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry akisaini Kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka alipotembelea kwa lengo la kufanya mazungumzo naye Mjini Bariadi, Julai 17,2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka (wa nne kushoto) akisalimiana na Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry mara baada ya kumaliza mazungumzo yao ofisini kwake Mjini Bariadi Julai 17, 2018

Saturday, July 14, 2018

WIZARA YA MADINI YAKABIDHI ENEO LA UJENZI WA KITUO CHA UMAHIRI SIMIYU


Wizara ya Madini kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) imekabidhi eneo la ujenzi wa Kituo cha Umahiri Bariadi Mkoani Simiyu kwa Mkandarasi wa ujenzi huo SUMA JKT ambao unaotarajiwa kuanza mwezi huu wa Julai 2018.

Makabidhiano hayo yamefanyika jana Mjini Bariadi Mkoani Simiyu na kushuhudiwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka, mara baada ya timu ya wataalam wa Wizara ya Madini na SUMA JKT kutembelea eneo la ujenzi lililopo Nyaumata Mjini Bariadi.

Akizungumzia kituo hicho Afisa Madini Mkoa wa Simiyu, Bw. Fabian Mshai amesema  “Kituo hiki ni Jengo la Ofisi ambalo litakuwa na kumbi  za kutolea mafunzo mbalimbali yahusianayo na uchimbaji wa madini unaozingatia kanuni za afya, usalama, uchambuzi wa madini na uhifadhi wa mazingira kwa wachimbaji wadogo ili uchimbaji uwe wenye tija”

Mshai ameongeza Kituo hiki cha Umahiri Bariadi kitajengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 1.3 na Kampuni ya Ujenzi ya SUMA JKT  na kusimamiwa na Kampuni ya Sky Actate Consultants.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Madini kwa kuamua kujenga Kituo hicho kwa kuwa mkoa huo ni mpya na unahitaji majengo mengi, hivyo amaesema ujenzi huo utajibu mahitaji ya mkoa katika kuwasaidia wachimbaji wadogo kuondokana na uchimbaji wa kienyeji na kwenda kwenye uchimbaji wa kisasa

"Wachimbaji wetu wadogo wamekuwa wakifanya shughuli zao kienyeji lakini uwepo wa kituo hiki utajibu mahitaji yao kwa sababu kitakuwa ni sehemu sahihi ya wao kupata elimu juu ya uchimbaji bora, wataalam wa madini watakuwa karibu kwa kuwa ukamilishaji wa kituo hiki utaenda sambamba na uwepo wa rasilimaliwatu" alisema Mtaka.

“ Sisi kama mkoa tuna faida ya uwepo wa rasilimali madini tuna nikeli, shaba, dhahabu, cobalt, tuna chumvi katika wilaya ya Meatu lakini pia tuna madini ya ujenzi kama kokoto, mchanga na mengine, hivyo uwepo wa kituo cha umahiri kutasaidia wachimbaji kufanya kazi zao katika utaalam ili uchimbaji ufanyike kwa ufanisi na uwe na tija” alisema.

Ameongeza kuwa uwepo wa kituo hicho pia utachangia kuboresha mazingira ya utendaji kazi ndani ya mkoa tofauti na ilivyo sasa, ambapo watumishi hao wanatumia majengo ya kukodi ambayo wakati mwingine hayakidhi mahitaji yao.

Amesema kuwepo kwa kituo hicho pia kutasaidia kufikia lengo la Serikali la kuhakikisha Sekta ya Madini inakuwa moja ya vyanzo vikubwa vya mapato kwa kuwekeza utaalam wa rasilimali watu, majengo, upimaji na utaalam mbalimbali wa kusaidia wachimbaji wadogo; hivyo akasisitiza SUMA JKT kukamilisha ujenzi wa kituo hicho kwa wakati.

Naye Luteni Kanali Petro Ngata Meneja wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka kuwa kazi ya ujenzi wa Kituo cha Umahiri Bariadi itafanyika kwa wakati.Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka (katikati) akishuhudia makabidhiano ya nyaraka za Ujenzi wa Kituo Mahiri cha Mkoa wa Simiyu kati ya Meneja wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa Luteni Kanali Petro Ngata na Meneja na Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), Bw. Andrew Erio  kutoka Wizara ya Madini, yaliyofanyika jana katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mara baada ya makabidhiano ya eneo la ujenzi wa kituo hicho Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa SUMA JKT na Wizara ya Madini wakikagua eneo la Ujenzi wa Kituo Mahiri Bariadi Mkoani Simiyu, kabla ya kufanya makabidhiano ya eneo hilo jana Mjini Bariadi.

Baadhi ya Viongozi wa SUMA JKT na Wizara ya Madini wakiangalia mchoro wa Jengo la Kituo cha Umahiri Bariadi Simiyu, katika  eneo la Ujenzi wa Kituo hicho kabla ya kufanya  makabidhiano ya eneo hilo jana Mjini Bariadi, kwa ajili ya kuanza taratibu za ujenzi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa sita kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa SUMA JKT baada ya kushuhudia makabidhiano ya nyaraka  za ujenzi wa Kituo cha Umahiri Bariadi kati ya Mkandarasi ambaye ni SUMA JKT na Wizara ya Madini yaliyofanyika jana katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya makabidhiano ya eneo la ujenzi wa kituo hicho Mjini Bariadi.Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa SUMA JKT baada ya kushuhudia makabidhiano ya nyaraka  za ujenzi wa Kituo cha Umahiri Bariadi kati ya Mkandarasi ambaye ni SUMA JKT na Wizara ya Madini yaliyofanyika jana katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya makabidhiano ya eneo la ujenzi wa kituo hicho Mjini Bariadi.

Friday, July 13, 2018

SERIKALI KUTOA SHILINGI BILIONI 1.5 UJENZI WA WODI YA MAMA NA MTOTO HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA SIMIYU


Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa SIMIYU.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu Julai 12, 2018, mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje(OPD)  la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, ambapo ameridhishwa na ujenzi wa jengo hilo.

Waziri Ummy amewahakikishia viongozi wa mkoa wa Simiyu kuwa Serikali imetenga shilingi Bilioni 1.5 na wadau wengine wameahidi kutoa shilingi bilioni 1.1 kwa ajili ya kukamilisha wodi ya mama na mtoto.

“Simiyu katika bajeti ya Serikali imetengewa shilingi bilioni 1.5 lakini tumepata pia shilingi bilioni 1.1 kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya ujenzi waWodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, lengo letu ni kukamilisha ujenzi haraka ili tuiwezeshe Halmashauri ya Mji wa Bariadi, kuchukua majengo ambayo yanatumika sasa hivi kama Hospitali Teule ya mkoa” alisema.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amesema baada ya kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Serikali ina mpango wa kujenga Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Mashariki Mkoani Simiyu, itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga  ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Rufaa ya Bugando ambayo inahudumia mikoa takribani minane.

Ameongeza kuwa pamoja na kuwa na mpango wa kujenga Hospitali ya hiyo Rufaa ya Kanda Simiyu, Serikali imekusudia kujenga Hospitali za Kanda tatu ambazo ni Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini ambayo imeanza kujengwa Mtwara, nyingine itajengwa Tabora Kanda ya Magharibi ili wananchi wapate matibabu ya kibingwa katika maeneo yao.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha za kujenga jengo hilo, ambazo zitasaidia kuboresha huduma za afya katika mkoa wa Simiyu .

Aidha, Mtaka amesema ardhi kwa ajili ya kujenga Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Mashariki itatolewa bure na akamhakikishia Waziri Ummy ushirikiano wa asilimia 100 kila watakapokuwa wakihitajika kwa namna moja au nyingine ili kufanikisha ujenzi wa hospitali hiyo.

Pamoja na Serikali kuahidi kutoa shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa SIMIYU,  pia Waziri Ummy amesema Serikali imetenga shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali yaWilaya ya Itilima.

MWISHOMeneja wa Wakala wa Majengo nchini(TBA) Mkoa wa Simiyu.Mhandisi.Likimaitare Naunga (wa pili kulia) akimuonesha Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(katikati) ramani ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, mara baada ya Waziri Ummy kutembelea na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali hiyo Mjini Bariadi, Julai12, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akimuongoza  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu , wakati alipotembelea  na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi, Julai 12, 2018.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wageni  wakati alipotembelea  na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi Julai 12, 2018.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipotembelea  na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi Julai 12, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea  na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi, Julai 12, 2018.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, mara baada ya kumaliza ziara yake ya kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi, Julai 12, 2018.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(katikati) akifurahia jambo na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipotembelea  na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi, Julai 12, 2018.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakitoka katika Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, mara baada Waziri Ummy  kutembelea na kuona maendeleo ya Ujenzi wa jengo hilo Mjini Bariadi, Julai 12, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Benjamin Mkapa Foundation, Dkt. Hellen Senkoro  wakati ziara ya Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alipotembelea  na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi Julai 12, 2018.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipotembelea  na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi, Julai 12, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akimuongoza  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu , wakati alipotembelea  na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi, Julai 12, 2018.

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!