Tuesday, July 17, 2018

RC MTAKA AKUTANA NA KIONGOZI WA JUMUIYA YA WAISLAMU WA AHMADIYYA


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amekutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry .

Katika mazungumzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Jumuiya hiyo kwa namna ilivyowekeza katika miradi ya mbalimbali ikiwemo miradi ya maji hususani uchimbaji wa visima katika baadhi ya maeneo mkoani humo. 

Aidha, ameiomba Jumuiya hiyo kuona uwezekano wa kuwekeza kwenye sekta ya Afya hasa katika ujenzi wa Hospitali huku akiwahakikishia upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya ujenzi pindi watakapokuwa tayari.

Kwa upande wake Kiongozi Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry amesema atalichukua kama pendekezo kwa viongozi wenzake ili waweze kuona uwezekano wa kuwekeza katika ujenzi wa hospitali Mkoani Simiyu.

Wakati huo huo Kiongozi huyo amesema pamoja na kuchimba visima vya maji Jumuiya ya Ahmadiyya imewekeza katika  Elimu na Afya katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Naye Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Mkoa wa Simiyu, Shekh Abdulatif Yusuph Ngalombe amesema hadi sasa jumuiya hiyo imechimba visima 6 katika wilaya ya Itilima na kuboresha  visima 19 katika wilaya ya Itilima na Meatu kwa gharama ya shilingi 49,760,000 na kazi ikiwa bado inaendelea katika baadhi ya maeneo.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka (katikati) akisalimiana na Kiongozi wa Jumuiya wa Waislamu ya Ahmadiyya, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry mara baada ya kumaliza mazungumzo yao ofisini kwake Mjini Bariadi Julai 17, 2018.
Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka alipomtembelea Ofisini kwake Mjini Bariadi, Julai 17, 2018.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya, wakiongozwa na Kiongozi Mkuu Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry walipomtembelea ofisini kwake Mjini Bariadi, Julai 17, 2018.
Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka alipomtembelea Ofisini kwake Mjini Bariadi, Julai 17, 2018.
Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry akisaini Kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka alipotembelea kwa lengo la kufanya mazungumzo naye Mjini Bariadi, Julai 17,2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka (wa nne kushoto) akisalimiana na Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry mara baada ya kumaliza mazungumzo yao ofisini kwake Mjini Bariadi Julai 17, 2018

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!