Friday, April 28, 2017

WAZIRI LUKUVI AWATAKA WAKAZI WA LAMADI KURASIMISHA MAKAZI YAO

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb) amewataka wakazi wa Lamadi wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, kurasimisha makazi yao katika kipindi hiki ambacho zoezi la urasimishaji makazi kwa gharama nafuu linaloendelea wilayani humo.

Waziri Lukuvi ametoa wito huo leo wakati wa zoezi la kuhamasisha urasimishaji makazi yalioendelezwa kiholela  na kukabidhi hati miliki 122  kwa wananchi wenye maeneo yaliyorasimishwa katika Kijiji cha Lamadi.

Lukuvi amesema Lamadi ni Mji wa Kibiashara  hivyo wakazi wake wanapaswa kujenga nyumba zao katika maeneo yaliyopimwa na kutolewa hati ili waishi katika makazi rasmi na salama.

“Mhe.Rais mpendwa wenu ametuagiza kuja Lamadi kurasimisha makazi yaliyokuwa holela ili yawe makazi salama na rasmi, huu ni upendeleo maalum ametoa kwamba waliojenga katika maeneo haya yanayoitwa makazi holela wengi ni maskini na siyo makosa yao, inawezekana wakati wanajenga hakukukwa na viwanja vilivyopangwa na kupimwa na Serikali” alisema

“Mhe.Rais ameagiza watu wote wanaotaka kushiriki zoezi hili wachangamkie fursa hii, ametoa ofa kuwa ninyi ambao mlijenga siku nyingi na mnataka kuongeza thamani ya nyumba zenu mtoke kwenye mtaji mfu na kufanya majengo yenu yatumike kama mtaji wa maendeleo” alisisitiza.

Lukuvi amesema wananchi watakaporasimisha maeneo yao watapata fursa ya kutumia hati miliki zao kupata dhamana ya mikopo katika benki mbalimbali kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi.

Aidha, amesema ofa hii ya kurasimisha maeneo ni ya muda tu,  hivyo akawataka wakazi zaidi ya 5000 waliopimiwa viwanja vyao kulipia kabla ya tarehe 30 Juni 2017 ili waweze kupewa hati miliki za maeneo yao na ambao bado hawajapimiwa waone umuhimu wa kupima na kulipia viwanja vyao pia kabla ya muda huo.

Amesema  wananchi wanapaswa kusaidiana na Uongozi wa Wilaya ya Busega  katika kufanikisha zoezi la urasimishaji kwa kuchangia gharama kidogo ili wapimiwe, warasimishiwe, wawekewe alama za mipaka, wapewe ramani na kupewa hatimiliki za maeneo yao na akawataka pia kurasimisha maeneo ya mashamba  na kuyatafutia hati.

Wakati huo huo Mhe.Lukuvi amewataka wananchi wote waliopata hati na wale watakaendelea kupewa kulipa kodi ya ardhi ya kila mwaka kwa Serikali na wale watakaokaidi kulipa kodi hiyo hati zao zitafutwa.

Akizungumza baada ya kupokea hati kutoka kwa Waziri Lukuvi, Mzee Musa Metusela Kole mkazi wa Lamadi, ameishukuru Serikali kwa kurasimisha maeneo yao kwa gharama nafuu na huduma nzuri kutoka kwa wataalam ambao waliwafuata wananchi katika maeneo yao na akatoa wito kwa wananchi wengine kurasimisha maeneo yao ya makazi na mashamba pia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Ndg.Anderson Njiginya amesema zoezi la urasimishaji ardhi kwa wakazi wa Lamadi limechangia kuongeza mapato yatokanayo na ardhi kwa Serikali, kupunguza migogoro ya ardhi baada ya kupima na kuweka mipaka ya kudumu katika viwanja na kuwawezesha wananchi kutumia hati za maeneo yao kwa shughuli zao za kiuchumi.


Zoezi la urasimishaji wa makazi katika Kituo cha Kibiashara Lamadi lilianza Mwezi Julai 2016 hadi sasa ambapo shughuli ya utambuzi wa miliki umekamilika kwa kupata viwanja 5223  na shughuli ya umilikishaji Viwanja ilianza Aprili 11, 2017 ambapo hadi sasa hati 138 zimeandaliwa kati ya hizo 122 zimekabidhiwa leo kwa wamiliki na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb).
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb) akimkabidhi hati miliki ya kiwanja Mzee Musa Metusela Kole mkazi wa Lamadi katika zoezi la kahamasisha urasimishaji makazi na kutoa hati miliki kwa baadhi ya wananchi lililofanyika leo katika Kituo cha Kibiashara Lamadi wilayani Busega.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb) akiwaonesha wananchi wa Lamadi moja ya hati miliki ya kiwanja, katika zoezi la kahamasisha urasimishaji makazi na kutoa hati miliki kwa baadhi ya wananchi lililofanyika leo katika Kituo hicho cha Kibiashara wilayani Busega.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb) akizungumza na wananchi wa Lamadi , katika zoezi la kahamasisha urasimishaji makazi na kutoa hati miliki kwa baadhi ya wananchi lililofanyika leo katika Kituo hicho cha Kibiashara wilayani Busega.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Busega ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe.Benson Kilangi akizungumza na wananchi wa Lamadi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb) , katika zoezi la kahamasisha urasimishaji makazi  na kutoa hati miliki kwa baadhi ya wananchi lililofanyika leo katika Kituo hicho cha Kibiashara wilayani Busega.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Ndg.Anderson Njiginya akiwasilisha taarifa ya Maendeleo ya Wilaya kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb)(wa kwanza kulia).
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb)(wa tatu kulia) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Mhe.Vumi Magoti (wa pili kulia) wakizungumza jambo katika zoezi la kahamasisha urasimishaji makazi na kutoa hati miliki kwa baadhi ya wananchi lililofanyika leo katika Kituo cha Kibiashara cha Lamadi wilayani Busega.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb) akimkabidhi hati miliki ya kiwanja Bibi. Elizabeth Manyuka Nyamagesi mkazi wa Lamadi katika zoezi la kahamasisha urasimishaji makazi  na kutoa hati miliki kwa baadhi ya wananchi lililofanyika leo katika Kituo cha Kibiashara Lamadi wilayani Busega.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb)(mwenye miwani) akicheza wimbo wa Kisukuma na wakazi wa Lamadi baada ya kukamilisha zoezi la kahamasisha urasimishaji makazi  na kutoa hati miliki kwa baadhi ya wananchi lililofanyika leo katika Kituo hicho cha Kibiashara wilayani Busega.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Ndg.Chele Ndaki akitambulisha baadhi ya viongozi ngazi ya Mkoa (hawapo pichani) walioshiriki katika ziara ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb) wilayani Busega.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb)(kushoto ) na Mwenyekiti wa Halmasahauri ya Wilaya ya Busega Mhe.Vumi Magoti (kulia) wakizungumza jambo baada ya zoezi la kahamasisha urasimishaji makazi na kutoa hati miliki kwa baadhi ya wananchi lililofanyika leo katika Kituo cha Kibiashara cha Lamadi wilayani Busega.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb)(kushoto ) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmasahauri ya Wilaya ya Busega Ndg.Anderson Njiginya (kulia) wakizungumza jambo baada ya zoezi la kahamasisha urasimishaji makazi na kutoa hati miliki kwa baadhi ya wananchi lililofanyika leo katika Kituo cha Kibiashara cha Lamadi wilayani Busega.

Thursday, April 27, 2017

RC MTAKA APONGEZA JESHI LA POLISI KUPUNGUZA MATUKIO YA UHALIFU

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoani humo kwa kupunguza matukio ya uhalifu hali iliyobadili taswira ya mkoa na kuufanya usikike katika masuala  maendeleo.

Mtaka ametoa pongezi hizo katika kikao chake na Viongozi na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani humo kilichofanyika leo  Mjini Bariadi.

Amesema askari wa Jeshi la Polisi wamefanya kazi kubwa katika kubadili taswira ya mkoa wa Simiyu ambapo kwa sasa viongozi na wananchi wamekuwa wakijadili masuala ya maendeleo ukiwemo Uchumi wa Viwanda kwa sababu ya amani na utulivu uliopo.

“Simiyu ya zamani ni tofauti kabisa na ya sasa,  zamani tulikuwa tukiangalia TV, tukisikiliza redio au kusoma magazeti habari zilikuwa ni mauaji ya vikongwe, kukatana mapanga na mauaji ya watu wenye ualbino.  Pamoja na viongozi wa Dini kuomba Mungu kwa ajili ya mkoa wetu lakini Jeshi la polisi pia limefanya kazi kwa nafasi yake pamoja na vyombo vya Ulinzi na Usalama ” alisema Mtaka.

 Aidha, amesema Serikali imedhamiria kuujenga Mkoa wa Simiyu kuwa Mkoa mpya wa kiuchumi jambo ambalo linapaswa kujulikana na wadau wote muhimu wa maendeleo wakiwemo viongozi na askari wa Jeshi la Polisi ambao aliwataka kuchangamkia fursa mbalimbali za uwekezaji na maendeleo mkoani humo.

“ Chini ya Falsafa ya Wilaya Moja Bidhaa Moja, Sasa hivi Maswa wanatengeneza chaki, Meatu wanasindika Maziwa na tunapanua kiwanda cha maziwa kwa kufanya uwekezaji mkubwa ambapo pia tutatengeneza maziwa ya unga kwa ajili ya watoto, tutaanza kilimo cha umwagiliaji Busega pamoja na kuanzisha kiwanda cha kutengeneza Tomato sauce; hapa kila wilaya ina jambo la kufanya, hizi zote ni fursa  ninyi askari na viongozi changamkieni fursa zilizopo” alisisitiza.

Ameongeza kuwa kipindi cha miaka mitatu ijayo, Mkoa wa Simiyu unatarajia kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje kwa asilimia 40%  kwa kuwa vitaanzishwa viwanda vya kuchakata mazao mbalimbali yanayopatikana hapa nchini katika kilimo, mifugo na uvuvi.

Wakati huo huo Mtaka amewataka askari wa jeshi la polisi kutekeleza majukumu kwa kuzingatia maadili ya kazi yao ikiwa ni pamoja na kupima nguvu ya kutumia kukabiliana na raia katika matukio mbalimbali na kuepuka fedheha ya kuwa watoa taarifa kwa wahalifu.

Vile vile amewataka askari wote kuwa waangalifu katika lugha wanayotumia wakati wakiwa wanatekeleza majukumu yao.

Wakati akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mkoa kwa nasaha mbalimbali alizotoa kwa Viongozi na Askari wa Jeshi la Polisi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Boniventure Mshongi amewataka viongozi na askari kufanya kazi zao kwa weledi huku wakizingatia maadili yao.

Katika kikao hicho viongozi na askari wa Jeshi la Polisi wamewasilisha maoni, mapendekezo na maombi mbalimbali kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ikiwa ni pamoja na kuomba Mamlaka za Serikali za Mitaa kupima na kuwauzia viwanja kwa bei nafuu ili wajenge na kuendeleza Mkoa huo.
Baadhi ya Askari Polisi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi na Askari wa Jeshi la Polisi wa Mkoa huo (hawapo pichani) katika  kikao kilichofanyika Mjini Bariadi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Boniventure Mshongi akizungumza katika kikao cha Viongozi na Askari wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi.
 Baadhi ya Viongozi wa Jeshi la Polisi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi. 
Baadhi ya Askari Polisi wakiimba Wimbo wa Maadili mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) kabla ya kikao kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Jeshi la Polisi wakiimba wimbo wa Maadili ya Polisi mbele ya  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) kabla ya kikao kilichofanyika Mjini Bariadi.
Stafu Jonas Mahanga Mmoja wa Viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu akichangia jambo katika kikao cha Mkuu wa Mkoa huo na Viongozi na Askari Polisi kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
WP Anna akichangia jambo katika kikao cha Mkuu wa Mkoa huo na Viongozi na Askari Polisi kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi wa Jeshi la Polisi wa Mkoa huo ( baadhi hawapo pichani) kabla ya kikao kilichofanyika Mjini Bariadi.
PC Simon kutoka Wilayani Busega  akichangia jambo katika kikao cha Mkuu wa Mkoa huo na Viongozi na Askari Polisi kilichofanyika leo Mjini Bariadi.



Saturday, April 22, 2017

KILICHOJIRI TAMASHA LA PASAKA SIMIYU: WANANCHI WAOMBA UTARATIBU WA MATAMASHA MIKOANI UWE ENDELEVU

Wananchi mkoani Simiyu kwa mara ya kwanza wameshuhudia Tamasha la Pasaka na kuomba Mwandaaji wa Matamasha ya Nyimbo za Injili kuendeleza utaratibu huu wa kufanya matamasha wakati wa sikukuu katika mikoa mbalimbali hususani Mkoa wa Simiyu.

Ombi hilo la wakazi wa Simiyu limetolewa wakati wa Tamasha la Pasaka mkoani  humo lililofanyika leo katika Uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi  na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi kutoka maeneo tofauti mkoani humo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamemshukuru Mwandaaji ya Tamasha hilo Mkurugenzi wa Msama Promotion Ndg.Alex Msama pamoja na viongozi wa Serikali Mkoani Simiyu kuona umuhimu wa kuandaa Tamasha hilo kwa kuwa nyimbo za injili zinazoimbwa na waimbaji mbalimbali wa Kitaifa na Kimataifa zinawafanya watu wasifu na kumwabudu Mungu na kuachana na mambo yasiyofaa.

“Tumelipokea kwa furaha sana tamasha hili na tunaomba leo isiwe mwisho kila mwaka liwepo; yaani kwetu ni kama zawadi maana tangu mkoa wetu uanze ni mara ya kwanza, hii ni dalili kuwa Mkoa wetu unatambulika na unapendwa,tunawashukuru viongozi wetu na tunamshukuru Msama kutuletea Tamasha la Pasaka” alisema Lilian Kagirwa mkazi wa Bariadi Mjini.

Naye, Daniford William mkazi wa Bariadi amesema wigo wa matamasha hayo utanuliwe na kuwawezesha wananchi katika mikoa yote nchini kupata ujumbe wa Neno la Mungu kupitia nyimbo za Injili katika nyakati tofauti kwa mwaka.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akitoa salamu za Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amesema Msama Promotion  afanye utaratibu wa kuandaa tamasha lingine kubwa mkoani Simiyu kwa kuwa wananchi hao wanampenda Mungu na wako tayari kumtukuza Mungu kupitia matamasha kama hayo.

“ Nichukue nafasi hii kuwakaribisha Msama Promotion na waimbaji wote wa nyimbo za injili mkoani Simiyu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, huu ni mkoa mpya lakini ni mkoa wenye kasi kubwa ya maendeleo na niombe wakati mwingine mtuletee tamasha kama hili  siku ya Sikukuu ya Krismasi au Pasaka ili watu wengi wapate nafasi ya kumtukuza Mungu kuzidi ilivyokuwa leo ”. alisema Kiswaga.


Aidha ,Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza wananchi kuendelea kuliombea Taifa na viongozi wote ili kudumisha amani, upendo na mshikamano wa nchi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Msama Promotion, Bwana Charles Mwakipesile amewashukuru na kuwapongeza wananchi wa Bariadi kwa mapokezi mazuri na akaahidi kuwa Kampuni hiyo itakuza vipaji vya baadhi ya waimbaji wa nyimbo za Injili walionekana kuwa na uwezo mzuri kufanya vizuri katika medani ya muziki wa injili.


Tamasha la Pasaka Mkoani Simiyu limehudhuriwa na Waimbaji wa Kitaifa na Kimataifa wakiwemo Upendo Nkone,Beatrice Mwaipaja,Upendo Kilahiro, Martha Mwaipaja, Jesca Honore, Sifael Mwabuka na  kwaya mbalimbali kutoka katika Makanisa ya Mjini Bariadi.
Mamia ya wananchi wa Bariadi Mkoani Simiyu wakimwabudu Mungu katika Tamasha la Pasaka lililofanyika leo katika Uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,Mhe.Festo Kiswaga akizungumzana wananchi wa Wilaya hiyo wakati wa Tamasha la Pasaka lililofanyika leo katika Uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,Mhe.Festo Kiswaga(wa pili kulia) naviongozi wngine wa Serikali na Dini wilayani humo wakishangilia jambo wakati wa Tamasha la Pasaka lililofanyika leo katika Uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Upendo Nkone kutoka jijini Dar es Salaam akimtukuza Mungu katika Tamasha la Pasaka lililofanyika leo katika Uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Upendo Kilahiro (mwenye gauni jeusi)  akiwa na waimbaji wengine kwa pamoja wakimtukuza Mungu katika Tamasha la Pasaka lililofanyika leo katika Uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi.
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Martha Mwaipaja kutoka jijini Dar es Salaam akimtukuza Mungu pamoja na baadhi ya wakazi wa Bariadi katika Tamasha la Pasaka lililofanyika leo katika Uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi.
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Upendo Kilahiro kutoka jijini Dar es Salaam (mwenye gauni jeusi) akimtukuza Mungu katika Tamasha la Pasaka lililofanyika leo katika Uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi.

Monday, April 17, 2017

SERIKALI MKOANI SIMIYU YAOMBA KIKUNDI CHA ULINZI CHA KIJESHI KUIMARISHA ULINZI, KUWEZESHA UFUGAJI WA SAMAKI ZIWA VICTORIA

Serikali mkoani Simiyu imeomba kuwepo kwa kikundi cha ulinzi cha kijeshi katika Wilaya ya Busega ili kusaidia mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu ikiwemo uvuvi haramu na kuwezesha ufugaji wa samaki ndani ya Ziwa Victoria kufanyika kwa usalama.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka wakati wa Hafla ya kumpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hapa nchini, Jenerali Venance Mabeyo iliyoandaliwa na ndugu zake kijijini kwao  Yitimwila ‘A’  katika Kata ya Kiloleri Wilayani Busega.

 “Tumepata changamoto nyingi sana kwenye ziwa, matukio mengi ya kihalifu liliwemo la uvuvi haramu , sisi kama mkoa tulikuja na wazo kwamba tungehitaji tupate ‘detouch’ moja eneo la Ziwa ili ukanda huu baada ya kufanya kazi kubwa ya kuchoma makokoro ya wananchi, tuwapeleke kwenye uvuvi wa kisasa hususani ufugaji wa samaki ziwani,  jambo ambalo Mheshimiwa Rais analipa kipaumbele sana; na namna  pekee ya kufanya ufugaji ule wa samaki ziwani, suala la ulinzi na usalama ni muhimu sana; ” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka amesema pamoja na kufanya ufugaji wa samaki  katika Ziwa Victoria, Serikali ya Mkoa imefanya makubaliano na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF kuwawezesha wananchi wa Busega kufanya kilimo cha Umwagiliaji kwa kutumia maji ya ziwa hilo ambayo ni ya uhakika.

“Tumeongea na NSSF kwa ajili ya kuanzisha mradi ambao hautazidi  bilioni moja, tutaleta mbegu za aina ya nyanya na pilipili zinazotakiwa ili wananchi wa Busega wazalishe kwa wingi. Hatutakuwa tayari kuona wananchi wanalima  nyanya na kuuza ndoo moja shilingi 500,  tumepanga  kuanzisha mradi wa kuzalisha ‘chill sauce’ na ‘tomato source’ .”alisema Mtaka.

Ameongeza kuwa Wataalam wa Wilaya na Mkoa kwa kushirikiana na Wataalam wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji , Kituo cha Utafiti wa Kilimo Ukiriguru wanafanya upembuzi yakinifu kuona namna miundombinu ya umwagiliaji itakavyojengwa ili kuwawezesha wananchi wa Busega kulima muda wote kupitia kilimo cha Umwagiliaji badala ya kutegemea mvua.

Mtaka amesema Serikali mkoani Simiyu imedhamiria kuhakikisha katika kipindi cha miaka mitatu ijayo Mkoa hauingizi bidhaa kutoka mikoa mingine na badala yake wananchi wake watazalisha na kutumia bidhaa zao wenyewe, hivyo ameomba Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuona namna ya kuweka vituo vya kuuza zana za kilimo katika maeneo ya kanda ya Ziwa ili wananchi wapate zana bora za kisasa zitakazowasaidia kulima kisasa.

Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hapa nchini, Jenerali Venance Mabeyo amewataka wananchi wa Busega kubadili mtazamo wao na kutumia maji ya ziwa Victoria kwa manufaa yao kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji ili wasikumbwe na tatizo la upungufu wa chakula kunapotokea ukame.

Kuhusu suala la ulinzi katika Ziwa Victoria amesema ombi  la Serikali ya Mkoa la kuwa na kikundi cha Ulinzi,  viongozi watalitafakari kuona namna ya kulishughulikia na akaeleza kuwa tayari Jeshi limeweka kikundi kidogo cha kiulinzi kutoka Jeshi la wanamaji,  lakini kutokana na ukubwa wa Ziwa Victoria kikundi hicho hakiwezi kuhimili kufanya doria maeneo yote na akaahidi kukiimarisha zaidi.

Jenerali Mabeyo pia amewaasa vijana wa Busega na mkoa wa Simiyu kwa ujumla kujiunga katika vikundi ili Serikali iwasaidie kutafuta mitaji ya kujishughulisha na Kilimo, uvuvi na ufugaji badala ya kukimbilia JKT tu,  japo amesema kwenda kwao JKT kunaweza kuwasaidia kupata stadi mbalimbali za maisha.

Naye Mwakilishi wa Baraza la Wazee wa Wilaya ya Busega, Bibi. Perazia Ndaki akisoma risala ya wazee kwa Mkuu wa majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo amemuomba Mkuu huyo wa majeshi kuona uwezekano wa kuanzisha Kambi ya jeshi la Kujenga Taifa(JKT) katika mikoa ya kanda ya Ziwa na hususani Mkoa wa Simiyu ili kuwasaidia vijana wengi kujiunga na kupata stadi mbalimbali zitakazowasaidia kujiajiri katika uvuvi, kilimo na ufugaji.

Mbunge wa Jimbo la Busega, Mhe.Raphael Chegeni amemuhakikishia Mkuu huyo wa majeshi kuwa endapo ombi la kuanzisha kambi katika Mkoa wa Simiyu litaridhiwa, Wilaya ya Busega itatoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kambi hiyo ambalo lipo tayari.


Sanjali na hilo viongozi mbalimbali wa dini walioshiriki katika hafla ya kumpongeza Mkuu huyo wa Majeshi, wamesisitiza wananchi kuwaombea yeye pamoja na viongozi wote wa Serikali wa ngazi zote ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo katika kuwatumikia wananchi.

Hafla ya kumpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hapa nchini, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo imefanyika kwa ajili ya ndugu zake kumpongeza kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli katika nafasi hiyo, ambapo  ilitanguliwa na ibada ya shukrani iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Ilumya Wilayani Busega, Jimbo la Shinyanga.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance  Mabeyo (katikati) akionesha siaha alizokabidhiwa na Wazee wa Busega kama ishara ya ushujaa kwake wakati wa hafla iliyoandaliwa na ndugu zake kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega kumpongeza kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli
 Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama hapa nchini, Jenerali Venance  Mabeyo na Mkewe wakishangilia jambo wakati wa hafla ya  kumpongeza Jenerali Mabeyo, kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega, kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa nafasi hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi na waalikwa katika hafla ya  kumpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali VenanceMabeyo, kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega, kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa nafasi hiyo.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo, akizungumza na viongozi na waalikwa mbalimbali kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega , katika hafla ya  kumpongeza kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa nafasi hiyo
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venanc Mabeyo, akimtambulisha Mke wake kwa viongozi na waalikwa mbalimbali kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega , katika hafla ya  kumpongeza kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa nafasi hiyo.
Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  hapa nchini, Jenerali Venance  Mabeyo na Mkewe wakizungumza jambo wakati wa hafla ya  kumpongeza Jenerali Mabeyo, kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa nafasi hiyo
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya ulinzi na Usalama wakifuatilia jambo wakati wa hafla ya  kumpongeza Jenerali Mabeyo, kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa nafasi hiyo.
Kutoka kulia Mkuu wa Wilaya ya Meatu,Mhe.Joseph Chilongani, Mkuu wa Wilaya ya Maswa. Dkt.Seif Shekalaghe, Mkuu wa Wilaya ya Itilima,Mhe. Benson Kilangi na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Mhe.Festo Kiswaga wakifuatilia jambo wakati wa hafla ya  kumpongeza Jenerali Mabeyo, kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa nafasi hiyo
Mbunge wa Jimbo la Busega Mhe.Raphael Chegeni viongozi na waalikwa katika hafla ya  kumpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo, kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega, kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa nafasi hiyo.
Mzee Salvatory Mabeyo baba wa Mkuu wa Majeshi Venance Mabeyo akitoa shukrani kwa viongozi na waalikwa mbalimbali walioshiriki hafla ya  kumpongeza Jenerali Mabeyo, kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa nafasi hiyo ambayo imefanyika kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega.
Katibu Tawala Mkoa Simiyu,Ndg.Jumanne Sagini(kushoto) akiwa na baaadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakifuatilia jambo wakati wa hafla ya  kumpongeza Jenerali Mabeyo, kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa nafasi hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Busega, mhe.Tano Mwera akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kuzungumza na hadharailiyoshiriki  hafla ya  kumpongeza Jenerali Mabeyo, kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa nafasi hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akipeana mkono na Mke wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hapa nchini, Jenerali Venance  Mabeyo mara baada ya kuzungumza na viongozi na waalikwa mbalimbali walioshiriki hafla ya kumpongeza Jenerali huyo kushika nafasi hiyo.
Katibu Tawala Mkoa Simiyu,Ndg.Jumanne Sagini(kulia)akimpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama hapa nchini, Jenerali Venance  Mabeyo mara baada ya kuvikwa vazi la kimila na wazee wa Busega.
Mke wa Jaji Mstaafu Thomas Mihayo (kulia) akimpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hapa nchini, Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya kuvikwa vazi la kimila na wazee wa Busega.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi , Jenerali Venance Mabeyo(wa nne kulia walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa Wilaya ya Busega hafla ya  kumpongeza Jenerali Mabeyo, kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa nafasi hiyo ambayo imefanyika kijijini kwao Yitimwila A wilayani humo.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Jenerali Venance  Mabeyo(wa nne kulia walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa Wilaya ya Busega hafla ya  kumpongeza Jenerali Mabeyo, kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa nafasi hiyo ambayo imefanyika kijijini kwao Yitimwila A wilayani humo.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama , Jenerali Venance Mabeyo(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wazazi na wakwe zake katika hafla ya  kumpongeza kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli ambayo imefanyika kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo(wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa kikundi cha ngoma cha Buyegu kutoka Jijini Mwanza katika hafla ya  kumpongeza kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa ambayo imefanyika kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega.
Jaji Msaafu Thomas Mihayo na Mke wake wakizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hapa nchini, Jenerali Venance Mabeyo kuzungumza na hadhara iliyoshiriki hafla ya  kumpongeza kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli ambayo imefanyika kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega.
Wasanii wa kikundi cha ngoma cha Buyegu kutoka Jijini Mwanza wakitoa Burudani kwa kucheza na nyoa aina ya chatu katika hafla ya  kumpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli ambayo imefanyika kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo(wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja viongozi mbalimbali wa mkoa, madhehebu ya dini na katika hafla ya  kumpongeza kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa ambayo imefanyika kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega.

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!