Wanufaika wa Mpango wa
kunusuru kaya maskini TASAF III wametakiwa kubuni miradi midogo midogo kwa
kutumia fedha wanazopata ili kujiongezea kipato.
Wito huo umetolewa na
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini wakati wa ziara yake wilayani
Itilima ya kukagua visima vya maji ambavyo ni miongoni mwa miradi ya kutoa ajira za muda kwa walengwa wa Mpango
wa kunusuru kaya Maskini TASAF III.
Sagini amesema wanufaika
wa TASAF ikiwa ni pamoja na waliopata ajira za muda katika uchimbaji wa Visima
na kulipwa ujira kidogo watumie fedha
hizo kujikimu na kuanzisha miradi midogo midogo ikiwemo ya biashara ndogo ndogo
na ufugaji wa kuku, bata, mbuzi na kondoo.
“ Mradi huu hautadumu
milele nawashauri katika kidogo mnachokipata mkitumie vizuri, anzisheni miradi midogo midogo itakayowasaidia
kuboresha kipato katika kaya zenu, wenye uwezo wa kufuga wafuge, wenye uwezo wa
kufanya biashara ndogo ndogo wafanye” alisema Sagini.
Mwenyekiti wa kijiji cha
Nanga Dismas Lyang’ombe amesema baadhi ya wanufaika wa mradi wa TASAF waliohusika
katika ujenzi wa visima vinne vilivyojengwa na Serikali kupitia Mradi wa TASAF
kwa kushirikiana na wananchi na kupewa ujira wa shilingi 2300 kwa siku, wameonesha
mabadiliko katika kaya zao tofauti na ilivyokuwa awali, ikiwa ni pamoja na
kufuga kuku, mbuzi na kuezeka nyumba zao kwa bati.
Aidha, Lyang’ombe ameishukuru Serikali kwa kujenga visima
hivyo kwa kuwa vimewasaidia wananchi wake kupata huduma ya maji katika umbali
mfupi
Kwa upande wao wananchi
wa vijiji vya Nguno, Nanga na Laini B vyote vya Wilaya ya Itilima alivyovitembelea
Katibu Tawala Mkoa Simiyu, wameomba Serikali hiyo kutibu maji yanayopatikana
katika visima hivyo ili wapate maji safi na salama.
Akijibu hoja hiyo,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Ndg. Mariano Mwanyigu
amesema Halmashauri yake itaandaa
utaratibu mzuri wa kitaalam kupitia
wahandisi wa maji kuhakikisha maji yanatibiwa na wananchi wanapata maji safi na
salama.
Miradi ya ajira za muda kwa wanufaika wa Mradi
wa TASAF hutekelezwa katika kipindi kigumu
kiuchumi ili kuwasiadia wanufaika hao na katika wilaya ya Itilima imeanza kutekelezwa
mwezi Disemba 2016 hadi Machi 2017.
Jumla ya miradi 161
imeibuliwa katika vijiji 65 vilivyo kwenye mpamgo, katika kipindi cha kwanza
cha utekelezaji wa miradi ya kutoa ujira ni visima 161 vinavyotakiwa kukamilishwa na visima 95 vimekamilika vinatoa maji, 66
viko katika hatua ya kufunikwa na vinatoa maji.
|
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini(wa
tatu kulia) akitoa maelekezo ya kuboresha eneo la kisima kwa Afisa Mtendaji wa
Kijiji cha Nanga, Juma Maiga (kushoto) wakati wa ziara yake wilayani Itilima, ya kukagua miradi ya ajira za muda kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru
kaya Maskini TASAF III
.Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini(wa
pili kushoto) akishuhudia mkazi wa kijiji cha Nguno wilayani Itilima akichota
maji katika Kisima kilichojengwa na Serikali kupitia mradi wa TASAF na wananchi (wanafaika wa mradi huo)
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini(wa tatu kulia) akitoa
maelekezo ya kuboresha ujenzi wa kisima
kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nguno (hayupo pichani) wakati wa ziara yake
wilayani Itilima, ya kukagua miradi ya ajira za muda kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru
kaya Maskini TASAF III.
Mratibu wa TASAF Mkoa wa Simiyu, Ndg. Nyasilu Ndulu (wa pili
kulia) akionesha eneo linalopaswa kuboreshwa katika ujenzi wa kisima Kijiji cha Nguno Itilima, kinachojengwa chini ya miradi ya ajira za muda kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru
kaya Maskini TASAF III.
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini (kulia) akizungumza na baadhi ya wakazi wa
kijiji cha Nguno wakati wa ziara yake wilayani Itilima, aliyoifanya kwa lengo la kukagua visima vilivyo katika miradi ya ajira za muda kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru
kaya Maskini TASAF III.
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya wakazi wa kijiji cha Nguno wakati wa
ziara yake wilayani Itilima, aliyoifanya
kwa lengo la kukagua visima vilivyo katika miradi ya ajira za muda kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru
kaya Maskini TASAF III.
Baadhi ya watumishi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Itilima wakimsilikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa
Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini(hayupo pichani) alipozungumza nao baada ya kumaliza
ziara yake wilayani humo aliyoifanya kwa lengo la kukagua visima vilivyo katika
miradi ya ajira za muda kwa walengwa wa
Mpango wa kunusuru kaya Maskini TASAF III.
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Itilima baada ya kumaliza ziara yake wilayani humo aliyoifanya kwa lengo
la kukagua visima vilivyo katika miradi ya
ajira za muda kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Maskini TASAF III,
(kushoto)n Mkurufgenzi mtandaji Mariano Mwanyigu(Katikati) Mkuu wa Wilaya, Mhe.
Benson Kilangi
Baadhi ya watumishi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Itilima wakimsilikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa
Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini(hayupo pichani) alipozungumza nao baada ya kumaliza
ziara yake wilayani humo aliyoifanya kwa lengo la kukagua visima vilivyo katika
miradi ya ajira za muda kwa walengwa wa
Mpango wa kunusuru kaya Maskini TASAF III.
|
0 comments:
Post a Comment