Hatimaye suluhu ya mgogoro baina ya
mwekezaji wa kampuni ya MWIBA Holdings na wananchi wa vijiji saba
vinavyounda Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) ya Makao wilayani Meatu,
juu ya utata wa mkataba wa kumiliki ardhi, uanzishwaji wa ranchi
,mahusiano mabovu na kusogezwa kwa alama za mipaka katika makazi ya
wananchi imepatikana
Suluhu
hiyo imepatikana baada ya kufanyika kikao cha pamoja wilayani Meatu kati ya
Kamati ya Siasa ya CCM, Viongozi na Watendaji wa Serikali (Wilaya ya Meatu na
Mkoa wa Simiyu), Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Watendaji wa Kampuni ya MWIBA
Holdings na Viongozi wa Vijiji vinavyounda Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya
Makao, ambacho kimeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka
Pande zote mbili (Mwekezaji na
wananchi) zimekubaliana kuondoa kesi inayohusu mgogoro huo kwa Msuluhishi Jaji
Mstaafu Thomas Mihayo na kurejea tena katika meza ya maridhiano ili kujadili namna ya kuondoa
tofauti na dosari zote zilizoonekana awali.
Mtaka ameipongeza Kampuni ya MWIBA Holdings
kurejea katika meza ya mariadhiano na wananchi na ameagiza kufanyika
mabadiliko katika Menejimenti ya Kampuni hiyo kwa kuwa baadhi ya watendaji wametajwa kuwa chanzo
cha migogoro ambayo imekuwa ikiwanufaisha wao wenyewe huku ikichochea uhasama kati ya kampuni hiyo
na wananchi
“....Nawaeleza Wakurugenzi, baadhi ya
wasaidizi wenu wanawachafua sana, wanatengeneza migogoro na wananchi wetu kwa
manufaa yao wenyewe; mkitaka kufanya kazi na sisi chukueni hatua kwa watumishi
wenu, tunataka wawekezaji lakini hatuko tayari kuona wananchi wananyanyaswa kwa
namna yoyote ile” alisema Mtaka.
Naye Mbunge wa Jimbo la Meatu Salum Khamis
amesema nia yake ni kuona wananchi
hawabugudhiwi hivyo akatoa rai kuwa maridhiano yatakayofanyika kati ya pande
hizo mbili yafanyike kwa umakini sana ili makubaliano yatakayofikiwa yalinde
haki za wakazi wa Meatu na yasiwe chanzo cha migogoro.
Wakati huo huo baadhi ya wananchi
wamesema mipaka waliyoshiriki kuweka wakati wa uanzishwaji wa Jumuiya ya
Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) ya Makao, ilitolewa kinyemela na watumishi
wakiwemo viongozi wa Jumuiya hiyo kwa kushirikiana na mwekezaji huyo na
kusogeza nyuma alama hizo kwa kilomita 10 kutoka eneo la hifadhi kuelekea
eneo la makazi ya wananchi
Wananachi hao wamesema kuwa mipaka
ambayo imekuwa ikileta migogoro ni mpaka ulioko katika kijiji cha Bulongoja
kwenye bikoni namba 314, ambapo walisema kuwa bikoni hiyo iliondolewa na
kusogezwa nyuma zaidi ya kilometa 10 kutoka ndani ya hifadhi kuelekea kwenye makazi
yao.
Akitoa ufafanuzi wa suala hilo, Katibu
Tawala Mkoa, Ndg.Jumanne Sagini amesema atatuma timu ya wataalam Ngazi ya Mkoa
ambao watashirikiana na wataalam wa wilaya ya Meatu watakaokwenda kuhakiki
mipaka hiyo kwa kuzingatia ramani na kuirejesha
ilipokuwa, huku akisisitiza wataalam hao kuzingatia weledi.
Kwa upande wake Mkurugenzi kutoka Kampuni ya Mwiba Holdings Company Abdulkadir
Mohamed amekubali kumaliza mgogoro huo na kufanya mabadiliko ya
menejimenti yake ili waweze
kufanya uwekezaji wa utalii na mazingira kwa uhuru.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Dkt.Titus Kamani amewaasa viongozi na watendaji wa Serikali mkoani humo kutekeleza
wajibu wao katika kuwaletea wananchi maendeleo na wasiruhusu kwa namna yoyote
migogoro ikachukua nafasi kubwa kuliko maendeleo ya wananchi.
Jumuiya
Hifadhi ya wanyamapori (WMA) Makao inaundwa na vijji saba ambavyo ni Makao, Sapa,
Mwangudo, Mbushi, Iramba ndogo, Jinamo na Mwabagimu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony
Mtaka akizungumza na Kamati ya Siasa
ya CCM, Viongozi na Watendaji wa Serikali (Wilaya ya Meatu na Mkoa wa Simiyu),
Watendaji wa Mwekezaji Kampuni ya MWIBA Holdings na Viongozi wa Vijiji vinavyounda
Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao(hawapo pichani) katika kikao cha
kutafuta suluhu ya mgogoro wa mwekezaji huyo wananchi wilayani Meatu.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu,Mhe.Dkt.Joseph
Chilongani akifafanua jambo katika
kikao kilichofanyika wilayani humo kwa lengo la kutafuta suluhu ya mgogoro kati
ya Kampuni ya MWIBA Holdings na wananchi wa Makao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Meatu,Ndg. Fabian Manoza akifafanua jambo katika kikao
kilichofanyika wilayani humo kwa lengo
la kutafuta suluhu ya mgogoro kati ya Kampuni ya MWIBA Holdings na wananchi wa Makao
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Dkt. Titus Kamani akifafanua jambo katika kikao
kilichofanyika wilayani Meatu kwa lengo la kutafuta suluhu ya mgogoro kati ya
Kampuni ya MWIBA na wananchi wa Makao wilayani humo.
Mkurugenzi kutoka Kampuni ya MWIBA
Holding, Ndg. Abdulkadir Mohamed akifafanua jambo katika kikao
kilichofanyika wilayani humo kwa lengo la kutafuta suluhu ya mgogoro kati ya
Kampuni hiyo na wananchi wa Makao-Meatu.
): Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Joyce
Masunga akifafanua jambo katika
kikao kilichofanyika wilayani Meatu kwa lengo la kutafuta suluhu ya mgogoro
kati ya Kampuni ya MWIBA na wananchi wa Makao wilayani humo, (kulia) Mwenyekiti
wa CCM Meatu, Mhe.Juma Mwibuli.
Katibu wa Jumuiya ya Hifadhi ya
Wanyamapori ya Makao, Robert Simon akiwasilsha taarfa ya Jumuiya hiyo katika
kilichofanyika wilayani Meatu kwa lengo la kutafuta suluhu ya mgogoro kati ya
Kampuni hiyo na wananchi wa Makao-Meatu.
Baadhi ya wananchi wakitoa maelezo ya kusogezwa
kinyemela kwa mipaka ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao tofauti na
ile ya awali walioshuhudia ikiwekwa wakati wa uanzishwaji wa jumuiya hiyo,
katika kikao ilichofanyika kwa lengo la kutafuta suluhu ya mgogoro kati ya
Kampuni hiyo na wananchi wa Makao-Meatu.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais (Mazingira) na Mbunge wa Jimbo la Kisesa wilaya ya Meatu akichangia jambo katika kikao
kilichofanyika wilayani humo kwa lengo la kutafuta suluhu ya mgogoro kati ya
Kampuni ya MWIBA na wananchi wa Makao wilayani humo.
0 comments:
Post a Comment