TAARIFA KWA UMMA
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka anawaalika wananchi na wadau wote wa
maendeleo katika Uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji mkoani Simiyu utakaofanyika
tarehe 15 Machi 2017, katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki Mjini Bariadi kuanzia
saa 3:00 asubuhi.
Mgeni
rasmi katika uzinduzi huo ni Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda
Mwongozo
wa uwekezaji Mkoani SIMIYU unabainisha fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo
Mkoani humo na utaongoza uandaaji na utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya
Mkoa na Halmashauri zake.
Aidha,
Mwongozo unakusudia kutekeleza azma ya Serikali ya Tanzania ya Viwanda kama ilivyofafanuliwa katika Mpango wa pili
wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano (2016/2017 – 2020/2021) na Dira ya
Maendeleo ya Taifa 2025.
Pamoja na mambo mengine mpango huu unabainisha taarifa
mahususi kwa makampuni na watu binafsi kutoka ndani na nje nchi, wenye nia ya
kuwekeza katika maeneo yenye rasilimali
nyingi ambazo hazijaanza kutumika (untapped resources) ili kukuza uwezo wa
uzalishaji katika sekta zote muhimu Mkoani Simiyu.
Mwongozo
huu ni matokeo ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na
Kijamii (ESRF) Januari - Februari 2017, katika Halmashauri zote za Mkoa wa
Simiyu (Bariadi Vijijini, Bariadi Mjini, Busega, Itilima,Maswa na Meatu) kwa
ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
Imetolewa na:
Stella
A. Kalinga
Afisa
Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Simiyu
13
Machi, 2017.
0 comments:
Post a Comment