Monday, October 21, 2019

WAZIRI MHAGAMA AZITAKA HALMASHURI KUHAKIKI TAASISI NDOGO ZA FEDHA KUBAINI TAASISI UCHWARA

Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Jenista  Mhagama , ameziagiza  halmashauri zote nchini kufanya uhikiki wa kina wa taasisi ndogo za kifedha zinazotoa mikopo  kwa wananchi na vikundi, ili kuzibaini  taasisi uchwara ambazo zimekuwa zikiwaibia watanzania badala ya kuwanufaisha kiuchumi..


Waziri Mhagama ametoa agizo hilo, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, yaliyofanyika Kitaifa katika  Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Oktoba 20, 2019.

“Ninajua baadhi ya taasisi ndogo za fedha badala ya kuwasaidia  wanachama zimekuwa ziifanya kazi ya kuiba fedha za wanachama  na kuwafanya wanachama warudi nyuma badala kusonga mbele, agizo hili Baraza la Taifa la Uwezesheshaji wananchi Kiuchumi mlifuatilie kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI,” alisema Mhagama.

Katika hatua nyingine ameitaka mifuko/programu za uwezeshaji wanachi kiuchumi kutoa mikopo kwa riba nafuu tofauti na taasisi nyingine za kifedha, ambapo amebainisha kuwa takribani wajasiriamali 1,237,984 wamenufaika na mikopo ya mifuko hiyo na hadi kufikia Juni 2019 jumla shilingi bilioni 388.4 zimetolewa.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga ametoa wito kwa Taasisi za kifedha kuhakikisha zinajibu changamoto za wananchi huku akiwataka wananchi (wajasiriamali) walioshiriki maonesho haya kutumia vema fursa walizoziona katika mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ili wakuze uchumi wao.

Baadhi ya wanufaika wa mikopo wilaya ya Bariadi na Busega mkoani Simiyu na Chato Mkoani Geita  wamezishukuru Taasisi za kifedha zilizowakopesha mitaji jambo ambalo limewasaidia kuimarsisha shughui zao za kiuchumi wanazofanya ikiwa ni pamoja na kilimo na ufugaji.

“Naishukuru Benki ya AZANIA na wadhamini wangu Taasisi ya PASS kwa kuniwezesha kupata mkopo wa shilingi milioni 20, kuanzia sasa nitalima kisasa na nitaenda kuongeza miundombinu ya maji kwenye shamba langu maana nilikuwa nalima ekari 10 kwa kumwagilia badala ya ekari 30 nilizo nazo,” alisema Elisha Malugu kutoka wilayani Busega.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC) Dkt. Festus Limbu amesema NEEC inaendelea kufuatilia agizo la Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa alilolitoa Juni 2019 la kila mkoa kuwa na kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi, lengo likiwa kuvifanya vituo hivyo kuwa kitovu cha uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi. Beng’ Issa amesema Maonesho haya yameshirikisha Taasisi 45, wajasiriamali zaidi ya 200 kutoka mikoa ya Simiyu, Mbeya, Pwani, Mwanza, Tabora, Kagera , Mara, Singida na Dar es Salaam na kutoka nchi jirani za Burundi na Kenya.

Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii chini ya Kauli Mbiu, “Mitaji ni Chachu ya Kujenga Uchumi wa Viwanda” yametanguliwa na maonesho ya kwanza yaliyofanyika Mbeya mwaka 2017, ambapo ya pili yalifanyika mwaka 2018  jijini Dodoma.
MWISHO



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama ( wa pili kulia) akimkabidhi Bi. Efrancia Kabuga kutoka Wilaya ya Kishapu mfano wa Hundi ya shilingi 50,000,000/=mkopo  kutoka benki ya CRDB , ambao amefadhiliwa na Taasisi ya PASS, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019  Mjini Baradi Mkoani Simiyu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama ( katikati) akikata utepe kama ishara ya kuzindua Mpango mkakati wa Baraza  la Taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC) kwa kipindi cha 2018/2019 mpaka 2022/2023, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019  Mjini Baradi Mkoani Simiyu(kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na kulia ni Mwenyekiti wa NEEC, Dkt. Festus Limbu
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akiwasikiliza baadhi ya wajasiriamali waliowezeshwa na Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo(SIDO), wakati alipotembelea mabanda ya maonesho,  katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019   Mjini Baradi Mkoani Simiyu.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza mwakilishi wa Kiwanda cha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa maelezo kuhusu asali inayozalshwa na kiongozi huyo  wakati alipotembelea mabanda ya maonesho,  katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019   Mjini Baradi Mkoani Simiyu.

Baadh ya viongozi na watendaji wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani), katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019   Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani), katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019   Mjini Baradi Mkoani Simiyu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (katikati walioketi), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Baraza  la Taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC) na wawakilishi wa mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019   Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akiangalia trekta alilokopeshwa, Bw. Donald Swai kutoka Bunamhala wilayani Bariadi , trekta hilo ni mkopo aliopewa kwa ufadhili wa Mfuko wa Pembejeo,trekta hilo ni mkopo kutoka Mfuko wa Pembejeo, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019   Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi kadi ya trekta Bw. Donald Swai kutoka Bunamhala wilayani Bariadi , trekta hilo ni mkopo aliopewa kwa ufadhili wa Mfuko wa Pembejeo, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019   Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (katikati walioketi), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya  Mkoa wa Simiyu, wakuu wa wilaya na baadhi ya viongozi wa Baraza  la Taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC), katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019   Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama ( wa pili kulia) akimkabidhi Nakala ya Mpango mkakati wa Baraza  la Taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC), kwa kipindi cha 2018/2019 mpaka 2022/2023Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019  Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama ( wa pili kulia) akimkabidhi Bw. Elisha Malugu  kutoka Wilaya ya Busega  mfano wa Hundi ya shilingi 20,000,000/=mkopo  kutoka kutoka AZANIA benki chini ya ufadhili wa Taasisi ya PASS, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019  Mjini Baradi Mkoani Simiyu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi cheti cha ushiriki Kaimu Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji,Bi. Esther Mmbaga katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019  Mjini Baradi Mkoani Simiyu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi cheti cha ushiriki Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019  Mjini Baradi Mkoani Simiyu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi cheti cha ushiriki Mwakilishi wa wafanyakazi wa Kiwanda cha Chaki Maswa, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019  Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akiwasilisha salamu za  Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa  Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019  Mjini Baradi Mkoani Simiyu.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Simiyu, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019  Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Simiyu, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019  Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akiwasikiliza baadhi ya watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) wakati alipotembelea mabanda ya maonesho,  katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019   Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na maafisa wa Taasisi ya PASS  wakati alipotembelea mabanda ya maonesho,  katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019   Mjini Baradi Mkoani Simiyu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akihoji jambo katika Banda la Mfuko wa Misitu ,  wakati alipotembelea mabanda ya maonesho  katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019   Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (wa sita kushoto) akicheza pamoja na Msanii Elizabeth Maliganya na viongozi wengine, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019   Mjini Baradi Mkoani Simiyu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (wa tatu kulia) akimsikiliza Afisa kutoka Shirika la Viwango nchini (TBS), wakati alipotembelea mabanda ya maonesho,  katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019   Mjini Baradi Mkoani Simiyu.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!