Wednesday, May 29, 2019

WANANCHI 17,084 KUNUFAIKA NA HUDUMA ZA VIPIMO IGALUKILO BUSEGA

Jumla ya Wananchi 17,084 wa kata ya Igalukilo na Vijiji jirani wilayani Busega wanatarajia kunufaika na huduma za vipimo mbalimbali vya afya na kupunguza umbali wa kupata huduma hiyo mara baada ya kukamilika kwa Jengo la Maabara linalojengwa katika Kituo cha Afya cha Igalukilo


Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Busega, Dkt. Godfrey Mbangali wakati akiwasilisha taarifa ya Ujenzi wa jengo hilo kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo hilo.

Pamoja na Jengo hilo Mwenge wa Uhuru umepitia miradi mbalimbali wilayani Busega ikiwa ni pamoja na Vyumba vitatu vya madarasa na matundu sita ya vyoo Shule ya Sekondari Ngasamo, ujenzi wa Jengo la Benki ya NMB na Ujenzi wa Kisima Kirefu cha Maji Kijiji cha Bukabile. 

Aidha, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 amekagua kazi zinazofanywa na vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu pamoja na kuzindua klabu ya Wapinga rushwa katika Shule ya Sekondari Kabita.

Baadhi ya wananchi wakishuhudia Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee  Mkongea Ali, akiweka jiwe la msingi Jengo la Maabara katika kituo cha Afya Igalukilo, wakati wa mbio za Mweng  wa uhuru wilayani Busega Mei 27, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga(kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera, kwa ajili ya kuanza mbio zake wilayani Busega Mei, 27, 2019.
 Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee  Mkongea Ali, akiweka jiwe la msingi Jengo la Benki ya NMB lililopo NYASHIMO, wakati wa mbio za Mweng  wa uhuru wilayani Busega Mei 27, 2019.


Jengo la Benki ya NMB lililopo NYASHIMO, lilowekewa jiwe la msingi wakati wa mbio za Mweng  wa uhuru wilayani Busega Mei 27, 2019.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee  Mkongea Ali (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi ambao ni wanachama wa klabu ya kupinga rushwa shule ya sekondari Kabita, walimu wao walezi,  Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni (mwenye shati la kijani) na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera(mwenye skafu na nguo ya kitenge), mara baada ya kuzindua klabu hiyo Mei 27, 2019.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee  Mkongea Ali, wakimbiza mwenge wa uhuru wengine  na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Busega wakieleka eneo la kutoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru, mara baada ya kukagua matundu sita ya vyoo, katika shule ya sekondari Ngasamo, wakati wa mbio za Mweng  wa uhuru wilayani Busega Mei 27, 2019.
Mbunge wa Busega Dkt. Raphael Chegeni (mwenye shati la kijani) akizungumza jambo na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee  Mkongea Ali, kabla ya kufungua mradi wa  Kirefu cha Maji Kijiji cha Bukabile, wakati wa mbio za Mweng  wa uhuru wilayani Busega Mei 27, 2019.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee  Mkongea Ali akipokea maelezo kutoka kwa kiongozi wa kikundi cha vijana wanaotengeneza bidhaa za ngozi wialayni Busega, wakati wa mbio za Mweng  wa uhuru wilayani Busega Mei 27, 2019.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!