Wednesday, May 1, 2019

RC MTAKA: SIMIYU TUTAENDELEA KUFANYA KAZI KWA KUHESHIMIANA NA KUSIKILIZANA

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema  Viongozi  Mkoani Simiyu wataendelea  kufanya kazi  na kuwahudumia wananchi  kwa kuzingatia utawala bora, utawala unaofuata sheria na uongozi wa kuheshimiana na kusikilizana.

Mtaka ameyasema hayo Mei Mosi, 2019 wakati alipokuwa akizungumza na wafanyakazi na wananchi mkoani humo katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Kimkoa, yaliyofanyika katika Uwanja wa Nguzonane Wilayani Maswa.

“Tungependa tujenge utumishi ambao ni wa kipekee sana kwenye mkoa na kila mtumishi aliye kwenye mkoa huu ajisikie fahari kufanya kazi Simiyu; ahadi yangu kwenu ni kwamba tutaendelea kufanya kazi kwa kuheshimiana,kusikilizana na kutiana moyo katikati ya changamoto ambazo watumishi wanazipitia” alisema

Aidha, amewashukuru wafanyakazi kwa namna walivyojitoa kwa hali na mali  kuhakikisha kwamba malengo ya Serikali ya kuwahudumia wananchi yanatekelezeka  na kusisitiza kuwa mkoa utaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na Vyama vyote vya wafanyakazi na kuwataka waajiri wote wathamini vipaji vya watumishi wao.
Kwa upande wake Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Mkoa wa Simiyu, Bw. Said Mselem ameomba Serikali kushughulikia suala la upandaji wa mishahara na madaraja kwa watumishi ili kuwaongezea ari na motisha katika kazi.
Katika hatua nyingine Mselem ameiomba Serikali kuu kuona uwezekano wa kuwabadilishia mfumo wa malipo ya mshahara watumishi wanaolipwa kupitia mapato ya ndani na kuanza kuwalipa kupitia HAZINA, ili wawe na uhakika wa kupata mishahara yao na michango yao ya mifuko ya hifadhi ya jamii iwasilishwe kwa wakati.
Nao baadhi ya wafanyakazi  kutoka vyama tofauti vya wafanyakazi wamesema Wafanyakazi Mkoani Simiyu wanapenda kazi zao na wanafanya kazi kwa uadilifu, hivyo wameiomba  Serikali iendelee kuboresha mazingira na kuwasaidia kutatua changamtozao ili waweze kufanya kazi wa uhuru na kujituma zaidi.
‘Watumishi tunapenda kazi zetu na tunafanya kwa bidii na uadilifu, tunajua wapo wachache wanaotuangusha lakini tunaendelea kuwahimiza wawajibike kutimiza azma ya kuwatumikia wananchi, ombi letu kwa Serikali itukumbuke kwenye kupanda madaraja wapo ambao hawajapanda toka mwaka 2015” alisema Mwenyekiti CWT Itilima Mwl. Rehema Shalali.
“Watumishi wanaolipwa kwa mapato ya ndani wanakutana na changamoto ya mafao yao wanapostaafu, mafao hayaendi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kuwa wakati maana hawalipwi mishahara kwa wakati tunamwomba Mhe. Rais aliangalie hili, ili watumishi hao nao waweze kulipwa na HAZINA moja kwa moja” alisema Sara Kiyuga Mjumbe wa Baraza Kuu TALGWU Taifa.
Maadhimisho ya Mei Mosi kwa mwaka 2019 yamebebwa na Kauli Mbiu “ TANZANIA YA UCHUMI WA KATI INAWEZEKANA, WAKATI WA MISHAHARA NA MASLAHI BORA KWA WAFANYAKAZI NI SASA”  ambapo yamefanyika kwa mara ya saba sasa Kimkoa tangu mkoa wa Simiyu kuanziswa mwezi Machi, 2012.
MWISHO

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(wa tatu kulia) akiimba wimbo wa mshikamano daima wa Wafanyakazi na baadhi ya viongozi wa Serikali na Vyama vya Wafanyakazi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani,  Mei Mosi yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akipokea Maandamano ya Wafanyakazi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Baadhi ya wafanyakazi mkoani Simiyu wakipita mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Baadhi ya wafanyakazi mkoani Simiyu wakipita mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Baadhi ya wafanyakazi mkoani Simiyu wakipita mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Baadhi ya wafanyakazi mkoani Simiyu wakiwa kwenye maandamano, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Baadhi ya wafanyakazi mkoani Simiyu wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani  Mei Mosi yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wafanyakazi wa mkoa huo Mei Mosi, 2019 katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Mkoa wa Simiyu, Bw. Said Mselem akitambulisha viongozi wa vyama vya wafanyakazi Mei Mosi, 2019 katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Mkoa wa Simiyu, Bw. Said Mselem akisoma risala ya wafanyakazi wa mkoa wa Simiyu kwa Mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Simiyu,, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) Mei Mosi, 2019 katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka aweze kuzungumza na wafanyakazi wa mkoa huo Mei Mosi, 2019 katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.



 Kwaya ya walimu wilayani Maswa wakitoa burudani ya wimbo katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2019 yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala wa Wilaya za Mkoa huo, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2019 yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslous Nyongo akiwasalimia wafanyakazi na wananchi kwa ujumla, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2019 yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2019 yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.


 Baadhi ya wafanyakazi mkoani Simiyu wakipita mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.


Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi zawadi ya Ufanyakazi hodari Dereva wake Bw.Viecent Mtebe, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2019 yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi zawadi ya Ufanyakazi hodari Mtunza Kumbukumbu wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega Bi. Laurencia katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2019 yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi zawadi ya Ufanyakazi hodari Mfamasia wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bw. Oscar Tenganamba katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2019 yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!